2023
Kumfuata Yesu huko Kiribati
Machi 2023


“Kumfuta Yesu Kristo huko Kiribati,” Rafiki, Machi. 2023, 16–17.

Kumfuata Yesu huko Kiribati

Kutana na Scott!

Kuhusu Scott

Picha
Picha ya uso wa mvulana akitabasamu

Umri: miaka 8

Kutoka: Tarawa, Kiribati

Lugha: Kiribati na Kiingereza

Malengo na ndoto: Kuwa daktari

Familia: Mama na Scott

Jinsi Gani Scott Anamfuata Yesu

Picha
Mvulana akimshikilia mvulana mwingine mgongoni ndani ya bahari

Scott ni mtiifu na mkarimu. Anapenda kuwa mfano mzuri, hasa kwa binamu yake mdogo. Yeye ni rafiki mwema sana kwa binamu yake kiasi kwamba siku zote anamwita mdogo wake. Scott anasali kila usiku na kila asubuhi. Kila siku anapenda kwenda kwenye shughuli za Kanisa, na anapenda jioni ya nyumbani. Yeye anapenda kuwasaidia wengine pia. Anataka kuwasaidia wengine kwa sababu anahisi vizuri anapofanya hivyo. “Kuwasaidia watu wengine kunanifanya niwe na furaha,” anasema.

Mapendeleo ya Scott

Picha
Nyumba juu ya nguzo, brokoli na matufaha, vitu vinavyojulikana na wimbi la bahari

Hadithi ya Maandiko: Wakati Yesu Kristo alipozaliwa

Mahali: Kwenye nyumba ya mababu zake

Tunda na mboga: Matufaha, brokoli

Somo shuleni: Kiingereza

Rangi: Bluu

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Amanda Yoshida

Chapisha