Halo kutoka Kiribati Rafiki, Jan. 2023, 18–19.
Halo kutoka Kiribati!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Kiribati (kee-ruh-bas) ni nchi ya kisiwa katika Bahari ya Pasifiki. Takribani watu 120,000 wanaishi huko.
visiwa 33
Kiribati ni visiwa vidogo vidogo vilivyo enea kwenye zaidi ya maili za mraba milioni 1.4 (kilometa 3.52) za bahari! Mahali pake kwenye sayari ya dunia inaiweka katika zoni ya kwanza ya wakati yenye kuona mwangaza wa jua la kila siku.
Fuko Nzuri za Bahari
Kiribati imejaa fuko zenye mchanga mwingi na miti ya minazi. Ni hali ya joto mwaka mzima.
Mifano Mizuri
Takribani asilimia 20 ya watu ni waumini wa Kanisa. Wao ni mfano mzuri kwa wengine wanaoishi kisiwani humo.
Kwenda Kuvua Samaki!
Kwa vile bahari imewazunguka pande zote, watu huko Kiribati wanakula vyakula vingi vya baharini. Nazi, wali na maboga pia ni maarufu
Hekalu Lipo Njiani
Mwaka 2020, Rais Russell M. Nelson alitangaza kwamba hekalu litajengwa huko Kiribati! Hivi ndivyo litakavyoonekana.