2023
Lengo Langu la Kitabu cha Mormoni
Machi 2023


“Lengo Langu la Kitabu cha Mormoni,” Rafiki, Machi. 2023, 31.

Watoto na Vijana

Lengo Langu la Kitabu cha Mormoni

Picha
Msichana akisoma maandiko akiwa amevaa spika za kichwani

Kielelezo na Rachel Hoffman-Bayles

Niliweka lengo langu la kumaliza kusoma Kitabu cha Mormoni kabla ya ubatizo wangu, kama kaka na dada yangu wakubwa walivyofanya. Lakini COVID ilipotokea, nilikosa sana shule, na kusoma ikawa vigumu zaidi kwangu. Kitabu cha Mormoni kina maneno mengi magumu, nami nilihitaji msaada.

Wazazi wangu na mimi tukapata wazo. Nilitumia aplikesheni ya Gospel Library kwenye simu ya mama yangu kusikiliza Kitabu cha Mormoni. Tuliishusha sauti pole pole ili niweze kusoma na kufuatisha kwa urahisi zaidi. Pia nilisimama njiani na kuangalia video zilizounganishwa katika aplikesheni hiyo. Kila mara niliposoma, niliweka alama kwenye chati. Nilizungumza na mama kuhusu kile nilichokuwa ninasoma. Ilikuwa ni vizuri!

Nilikuwa nafanya vizuri katika kusoma, lakini sikufikiria kama ningeweza kumaliza kabla ya ubatizo wangu. Hivyo nikajisemea badala ya kumaliza kabla ya ubatizo wangu, ningemaliza kabla ya mwisho wa mwaka (ambao ulikuwa mwezi mmoja baadae). Niliendelea kusoma. Nyakati zingine mama yangu au dada yangu walisoma pamoja na mimi.

Desemba 31, nilimaliza Kitabu cha Mormoni. Familia yangu yote ilishangilia. Kisha niliingia chumbani kwangu na kusema sala. Niliuliza kama Kitabu cha Mormoni kilikuwa cha kweli.

Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anasikiliza ninaposali. Najua wazazi wangu wa mbinguni wananipenda. Ninajua kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu, na Yesu Kristo anatupenda.

Chapisha