2023
Andika Mfano
Machi 2023


“Andika Mfano,” Rafiki, Machi. 2023, 8.

Kitu cha kuburudisha

Andika Mfano

Picha
mapishi ya mkate

Fikiria kitu fulani katika injili unachotaka kuwafundisha wengine. Ni kitu gani au mfano gani ungeweza kutumia ili kufundisha? Kichore au kiandike hapa.

Mfano: Imani ni kama mbegu kwa sababu inaweza kukua kidogo kidogo kwa wakati.

Tengeneza Mkate Wako

Unaweza kutumia mapishi haya kwa ajili ya shughuli kwenye ukurasa wa 11.

Maji ya uvuguvugu kikombe 1

Hamira vijiko 2 1/4 vya chai

Sukari nyeupe vijiko 2 vya mezani

Vikombe 3 vya unga

Chumvi kijiko 1 cha chai

1/4 kikombe cha mafuta ya mboga

  1. Changanya maji, hamira na sukari katika bakuli. Subiri dakika 5 kwa hamira kuumuka.

  2. Ichanganye kwenye unga, chumvi na mafuta.

  3. Kanda kinyunya kwa dakika 10. Weka kwenye kikaango kilichopakwa mafuta. Funika na acha uumuke kwa muda wa saa moja.

  4. Pigapiga kinyunya na ukiache kiumuke kwa dakika 10 zaidi Oka katika nyuzi 350°F (175°C) kwa dakika 30-40.

Chapisha