Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Kutohoa Kitabu cha Kiada kwa Matumizi ya Chekechea


Kutohoa Kitabu cha Kiada kwa Matumizi ya Chekechea

Darasa la Chekechea

Ni nani anayehudhuria.

Watoto ambao wana angalao miezi 18 lakini hawajafika umri wa miaka 3 ifikapo Januari 1 wanaweza kuhudhuria chekechea kwa ridhaa ya wazazi wao. Angalao walimu wawili wanapaswa kuitwa kwa kila darasa la chekechea. Kama walimu si mume na mkewe, wanapaswa wawe wa jinsia moja. Walimu wote wanapaswa kuwa katika darasa wakati wote wa muda wa darasa la Msingi.

Madhumuni

Mudhumuni ya darasa la chekechea ni kuandaa mahali pa upendo, salama, na mahali palipoandaliwa ili watoto wadogo waweze kuongeza uelewa na upendo wao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, kupata uzoefu chanya katika mazingira ya Kanisa, na kukua katika hisia za kujithamini. Darasa la chekechea ndiyo uzoefu wa kwanza wa Kanisa ambapo watoto wadogo sana wanaweza kufundishwa injili na kufahamiana na watoto wengine na watu wazima.

Mazingira Asili

Chumba cha chekechea kinapaswa kuwa kisafi, maridadi, chenye kuvutia na kiwe karibu na msalani kama inawezekana. Chumba cha chekechea kinaweza kugawanywa katika sehemu tofauti tofauti za kuchezea (kwenye zulia au mkeka, kama inawezekana), ya kusomea, au ya shughuli, na ya kufundishia. Wanasesere wanapaswa kuwa safi, salama, na katika hali nzuri. Vyombo vya kupandwa havipaswi kutumika.

Ratiba ya Muda

Chekechea kwa kawaida huchukua saa 1 na dakika 40. Muda unapaswa kugawanywa katika vipindi kadhaa tofauti, kila kimoja kiimarishe madhumuni ya somo.

Jaribu kupanga masomo ambayo yanafuata muundo sawa wiki hata wiki. Watoto hujiona salama wakati kuna ratiba ya kawaida na mabadiliko yanayofahamika kutoka shughuli moja hadi nyingine. Muundo ufuatao uliopendekezwa unaweza kugeuzwa kulingana na mahitaji ya eneo.

Karibu

Muda wa kucheza:

Dakika 35

Muda wa Kukusanyika:

Dakika 10

Muda wa Muziki:

Dakika 10

Muda wa Vitafunwa:

Dakika 10

Muda wa Somo:

Dakika 10

Muda wa Shughuli:

Dakika 15

Kufunga

Dakika 10

Watoto wa chekechea hawaendi kwenye muda wa kushirikiana au mazoezi ya kufungua na kufunga.

Karibu: Watoto wanapokuja katika darasa la chekechea, msalimie kila mmoja kwa jina lake. Msaidie kila mtoto kuelewa kuuona upendo wako na upendo wa Baba wa Mbinguni. Muziki laini unaweza kuleta utulivu, na mazingira yenye kualika. Nyimbo zilizorekodiwa kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto zinapatikana katika kanda ya kaseti (52428) na diski (50428).

Muda wa kucheza: Waruhusu watoto wacheze kwa uhuru na wanasesere, ubao wa mafumbo, picha, au vitabu. Mhimize kila mtoto achague kitu kimoja tu cha kucheza nacho kwa wakati mmoja na akirudishe mahali pekee kabla ya kuchukua kitu kingine. Usimlazimishe mtoto kushiriki kama yeye hajisikii kufanya hivyo. Watoto wengi wa umri huu hawajawa tayari kihisia au kijamii kushiriki. Uwepo wako ni muhimu kwa watoto, lakini usiwaingilie sana katika mchezo wao. Mwisho wa muda wa kucheza, wasaidie watoto kurudisha wanasesere.

Shughuli maalum zinaweza kuendeshwa wakati wa muda huu (ona “Shughuli na Michezo ya Chekechea,” xiv–xvii), lakini watoto hawapaswi kuhitajika kushiriki.

Muda wa Kukusanyika: Wakusanye watoto ili kuimba wimbo na kujiandaa kuomba. Orodha ya zinazowezekana kuwa nyimbo za maombi iko kwenye ukurasa wa 310 wa Kitabu cha Nyimbo za Watoto. Mwalike mtoto atoe maombi ya kufunga. Wafundishe watoto kutoa maombi mafupi na rahisi. Wasaidie kama inahitajika. Baada ya maombi, waalike watoto kuzungumza na kuwa mwinginliano na mwalimu na wengine katika mazingira yasiyo rasmi. Onyesha upendo, ukunjufu na heshima kwa maneno na matendo yako. Kuwa msikivu na aliye tayari kubadilika.` Jadili mahitaji na upendeleo wa watoto. Mada zifaazo kwa majadiliano zinaweza kuwa—

  • Matukio ya hivi karibuni katika maisha ya watoto, kama vile mtoto mpya nyumbani au matembezi ya familia.

  • Sikukuu Maalum.

  • Hali ya hewa.

  • Kuangalia mambo ya asili.

  • Ujuzi wa kijamii kama vile kusikiliza, kushiriki, au kutumia tabia njema.

  • Vitendo vya ukarimu.

Mistari ya michezo, mazoezi ya kujikunja na kujinyoosha, nyimbo pia zinaweza kutumika wakati huu ili kuwasaidia watoto kushinda ukosefu wa utulivu.

Muda wa Muziki: Muziki unaweza kutumiwa wakati wote wa darasa la chekechea ili kuleta mazingira ya furaha na kuvutia; kufundisha ujumbe wa injili; na kuwaruhusu watoto kuwa na mabadiliko ya mwendo (ona Muziki katika Darasa la Chekechea,” xvii–xix). Watoto hufurahia kuimba nyimbo zile zile wiki hadi wiki. Viongozi na walimu wa chekechea wanapaswa kuwa na nakala ya Kitabu cha Nyimbo za Watoto Wengine wanaweza kualikwa kusaidia kwa muziki katika chekechea.

Muda wa Vitafunwa: Panga muda wa vitafunwa kulingana na mahitaji ya watoto. Hela kwa ajili ya vitafunwa hutoka kwenye bajeti ya watoto wa darasa la Msingi. Kwa sababu watoto hupata vitafunwa kila wiki katika chekechea, walimu wanapaswa kuwauliza wazazi kama kuna vyakula vyo vyote ambavyo hawataki watoto wao wale (ona Church Handbook of Instructions, Book 2: Priesthood and Auxiliary Leaders 1998], 239). Kabla ya kugawa vitafunwa, msaidie mtoto kuombea chakula.

Muda wa Somo: Masomo katika kitabu cha kiada hiki yaliandikwa kwa kiwango cha watoto wa umri wa miaka mitatu, lakini shughuli nyingi katika masomo na shughuli zenye kuboresha zinafaa kwa watoto wadogo. Kila somo pia lina sehemu ya Shughuli za Ziada kwa Watoto Wadogo.” (Fahamu kwamba vifaa na maandalizi yanayohitajika kwa shughuli za ziada hazijaorodheshwa katika sehemu ya “Maandalizi” ya kila somo. Kwa uangalifu soma maelezo ya kila shughuli unayotaka kutumia ili kuhakikisha una kila kitu unachohitaji.)

Mifano ya jinsi masomo katika kitabu hiki cha kiada yanavyoweza kutoholewa kwa darasa la chekechea inapatikana katika ukurasa wa xix–xx. Unapotohoa masomo, kumbuka kwa maombi kufikiria uelewa wa watoto na mambo yanayopendwa na watoto. Shughuli zinapaswa kuwa fupi na aina tofauti tofauti kwa sababu watoto wa umri huu wana usikivu mfupi sana. Watoto hujifunza vyema kwa kurudia rudia, kwa hivyo ukitaka unaweza kurudia shughuli wakati wa somo au masomo yajayo. Kwa msaada wa ziada wa kufundisha watoto wadogo, tazama “Kuandaa Masomo,” “Kufundisha Masomo,” ”Muziki Darasani,” na “Vifaa vya Picha” ukurasa vi–viii.

Muda wa Shughuli: Chagua shughuli kama vile za kupaka rangi, kutengeneza vitu na donge la plastiki, kuigiza, michezo, na vinginevyo (ona “Shughuli na Michezo ya Chekechea,” xiv–xvii) ambazo zinaimarisha ujumbe wa injili, zikiruhusu kushiriki, na kuleta uzoefu wa ubunifu. Usiwe na wasi wasi kama watoto wadogo hawataki kurudi kucheza tena.

Muda wa Kufunga: Wasaidie watoto kurudisha wanasesere na vifaa; kisha kwa kifupi rejea na ufanye muhtasari wa ujumbe wa injili uliofundishwa katika somo hili. Mwalike mtoto atoe maombi ya kufunga.

Kuwaandaa Watoto kwa ajili ya Chekechea

Wiki chache kabla ya mtoto kuingia chekechea, mshauri wa kwanza katika urais wa Msingi anapaswa kuwapa wazazi wa mtoto nakala ya orodha iliyopo kwenye ukurasa wa xi na apange mkutano kati wazazi na walimu wa chekechea.

Orodha ya Kupimia ya Wazazi

Mtoto anaweza kuanza muda wake wa kwanza katika chekechea kwa shauku, au hofu, tabasamu au machozi. Wazazi wanaweza kufanya mengi ili kufanya tukio la mtoto wa chekechea kuwa la kufurahia kwa kumuandaa mtoto mapema. Watoto wanapojua kule wanakoenda na kile wanachokitarajia, kwa kawaida wanakuwa na hamu ya kuhudhuria. Wale wanaokuja na maelezo kidogo au bila maelezo yo yote wanaweza kuogopa na kukataa kukaa. Mwandae mtoto wako kuja chekechea kwa kufanya vitu vingi kati ya vitu hivi kama iwezekanavyo.

  1. Mfundishe mtoto wako kuhusu chekechea angalau wiki mbili kabla ya yeye kuhudhuria kwa mara ya kwanza .

  2. Fanya mpango kwa mtoto wako kukutana na walimu wa chekechea wiki moja au mbili kabla ya mara yake ya kwanza ya kuhudhuria chekechea.

  3. Fanya mpango mtoto wako kukutana na wachache kati ya watoto wengine wa chekechea.

  4. Wakati wa wiki kabla ya mtoto wako kuingia chekechea, zungumza mambo chanya kuhusu chekechea.

  5. Mpekele mtoto wako kuona chumba cha chekechea wakati hakuna watu huko.

  6. Siku moja kabla, mkumbushe mtoto wako kwamba chekechea itaanza kesho.

  7. Katika siku ya kwanza ya chekechea, mpe mtoto wako muda kiasi wa kujiandaa kuja kanisani. Usimharakishe.

  8. Waache wanasesere wa mtoto wako huko nyumbani.

  9. Mshughulikie mtoto wako kwa mahitaji yake ya kwenda msalani na kula kabla ya kumpeleka katika chekechea. Mtoto ambaye anahitaji kubadilishwa nepi atapelekwa kwa mzazi.

  10. Fika haraka katika chekechea.

  11. Mhakikishie mtoto wako kwamba utakuja baadaye. Mara moja uje kumchukua mtoto wako mwisho wa kipindi cha chekechea.

  12. Kama mtoto wako anaogopa, bakia katika chekechea pamoja naye kwa mara chache za mwanzoni.

  13. Waambie walimu wa chekechea ni madarasa gani wewe utahudhuria wakati wa muda wa chekechea ili waweze kumleta mtoto wako kwako kama kuna shida.

  14. Waarifu walimu wa chekechea kama mtoto wako ana shida za kipekee, kama vile kudhurika na chakula.

  15. Elezea uzoefu wako wa chekechea kwa mtoto katika njia chanya na kwa ukarimu. Hakikisha unasema mambo mazuri kuhusu darasa na walimu wa chekechea wa mtoto wako.

  16. Kumbuka kwa upendo na subira zitaleta uzoefu mzuri wa chekechea kwa mtoto wako.

Tafadhali usimpeleke mtoto wako katika chekechea kama ana dalili zo zote kati ya hizi zifuatazo.

  • Homa

  • Mafua

  • Kikohozi

  • Usumbufu au kukasirika

  • Kutapika

  • Kuharisha

  • Vipele

  • Kutokwa na matongotongo machoni

  • Chawa kichwani

  • Ugonjwa au maradhi yaliyotibiwa na antibiotiki ndani ya saa 48.

  • Ugonjwa wa watoto ulio wazi katika kipindi cha maambukizi:

    tetekuwanga (siku saba)

    surua (mpaka vipele viishe)

    homa ya vipele vyekundu (mpaka vipele viishe)

    matumbwitumbwi. ( mpaka uvimbe uishe, kwa kawaida siku saba)

    upele ambukizi wa malengelenge

Ikiwa mtoto wako amedhurika na kitu ambacho kinasababisha kutokwa na kamasi, kukokoa, au vipele, tafadhali waambie walimu wa chekechea kuwa dalili za mtoto wako si ya kuambukiza.

Tabia za Watoto Wadogo

Kujifunza tabia zifuatazo za watoto wadogo inaweza kukusaidia kuelewa vyema kwa nini watoto wa darasa lako wanafanya vile wanavyofanya. Tumia ujuzi huu katika kuandaa na kufundisha masomo na katika kufahamiana na watoto. Kumbuka kwamba hii ni miongozo ya jumla; watoto hawakui kwa kiwango sawa au kutenda kwa njia sawa wakiwa wa umri mmoja. Kwa maelezo zaidi juu ya tabia za watoto ona Teaching, No Greater Call (110–11)

Tabia za Kiakili za Mtoto Mdogo

  • Hufikiria kwa urahisi na uhalisi. Haelewi mawazo ya kinadharia.

  • Ana usikivu wa muda mfupi (dakika moja hadi tatu).

  • Kila mara huuliza maswali au kusema maneno ambayo hayapo katika mada.

  • Ana udadisi na upekuzi.

  • Kwa kawaida husisimka kujifunza na kujaribu kitu kipya.

  • Hufurahia kurudia rudia.

  • Anaweza kufanya maamuzi rahisi

Tabia za kimwili za Mtoto Mdogo

  • Kwa kawaida ni mchangamfu sana.

  • Anakuza uwezo wa kutembea, kuruka, na kupiga makofi.

  • Kwa urahisi hukosa utulivu, hukasirika, na kuchoka haraka.

  • Ni rahisi kutengua na kubomoa kuliko kujenga upya.

Tabia za Kijamii za Mtoto mdogo

  • Ni mwaminifu.

  • Kwa kawaida anafurahia kucheza peke yake.

  • Kila mara ni mchoyo na mbinafsi.

  • Ni mgumu kushirikiana na kufanya kwa zamu.

  • Kila mara anabishana kwa ajili wanasesere.

Tabia za Kimhemko za Mtoto Mdogo

  • Kwa kawaida ana hamu ya kupenda na kupendwa.

  • Ana milipuko ya kimhemko ya mara kwa mara.

  • Hulia kwa urahisi.

  • Hubadilika mara kwa mara.

Tabia za Kiroho za Mtoto Mdogo

  • Anatamani kuomba lakini atahitaji msaada.

  • Anaweza kuanza kujifunza maana ya staha.

  • Ni msikivu kwa Roho Mtakatifu.

  • Huelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatupenda.

  • Huelewa mawazo ya msingi ya kiroho.

Matatizo na Suluhisho Zinazoweza kuwepo katika Chekechea

Hata katika chekechea bora, watoto wakati mwingine huwa na tabia mbaya. Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya kawaida ya kitabia na mapendekezo ya kuyasuluhisha.

Shida

Suluhu Inayowezekana

Mzazi anakwambia mtoto hataki kuja katika chekechea. Mtoto anapiga kelele wakati mzazi anapojaribu kuondoka.

Wahimize wazazi kuwaandaa watoto wao kwa ajili ya chekechea mapema (ona Kuwaandaa Watoto kwa ajili ya Chekechea,: ukurasa x–xi). Mwalike mzazi kukaa mpaka mtoto atulie na kujisikia vizuri. Inaweza kusaidia kuwaalika watu wazima wengine ili kumshika mtoto anayelia mpaka anapojisikia yu salama.

Mtoto anaonekana kukuogopa au kuwaogopa watoto wengine, anatanga tanga bure katika chekechea, na hataki kusema na mtu yeyote.

Kuwa na subira, usimilamishe mtoto chochote. Mpe muda wa kukujua wewe, watoto wengine, na mazingira. Mara kwa mara mhakikishie mtoto na kupendekezea ajaribu shughuli moja au mbili. Wasaidie watoto kupata uzoefu wa ufanisi wa aina fulani.

Wakati wote wa kipindi cha chekechea, mtoto anashikilia mguu wako au anajaribu kuketi kwenye paja lako.

Watoto wadogo wanahitaji ukunjufu na usikivu. Dakika ya kumshika na kuongea na mtoto mara kwa mara kawaida umridhisha. Kisha mhimize mtoto kujihusisha na shughuli za chekechea.

Wakati wa muda wa somo, watoto kadhaa wanasimama na kuondoka kabla ya shughuli kumalizika.

Kuwa macho na uwe mwepesi kutambua mahitaji, mambo wayapendayo, na muda wa usikivu wa kila mtoto. Angalia ishara za kuchoka au usumbufu ili wewe uweze kugeuza shughuli ili kuendana na mapenzi ya watoto. Usimlaizmishe mtoto kushiriki katika shughuli yoyote. Ikiwa baadhi ya watoto wanataka kurudi kucheza na wanasesere, waache wafanye hivyo.

Mtoto hawezi kuketi kimya na kusikiliza. Yeye husukuma na kuwavuruta watoto walio keti karibu naye.

Mwalimu wa pili anaweza kuelekeza usikivu wa watoto kwenye shughuli inayoendeshwa na mwalimu wa kwanza. Mpe mtoto kitu cha kushikilia ili kwa ukamilifu aweze kuhusika katika somo au shughuli.

Watoto kadhaa wanaanza kupigana kwa sababu ya mwanasesere. Mtoto mmoja anarusha mateke, kupigana, au kuuma kwa meno ili amiliki mwanasesere.

Watoto wakati mwingine wanaweza kutatua kutokubaliana kwao wao wenyewe, lakini unapaswa kuingilia kati kama inahitajika kuzuia kuumizana au kuharibu vitu. Unaweza kupendekeza njia za watoto za kusuluisha matatizo yao.

Mtoto anaanza kucheza vibaya,—akimrusha mwanasesere, kugonganisha, au kumtupatupa. Kisha anakimbia kimbia hadi sehemu zingine za chumba.

Unahitaji kusimamamisha tabia hii. Mwelezee mtoto kwa nini hapaswi kufanya hivyo; kisha mwelekeze mtoto kwenye shughuli ingine.

Mtoto anachukua mwanasesere mmoja baada ya mwingine kutoka kabatini, na anakataa kumrudisha mwanasesere yeyote.

Kwa upole lakini kwa uthabiti mwelezee tabia unayotarajia. Mwonyeshe mtoto jinsi ya kurudisha wanasesere. Mhimize mtoto kurudisha kila mwanasesere kabla ya kumchukua mwingine.

Mtoto anaaza kunung’unika na kulia. Wakati unapojaribu kumfariji, yeye anasema, “Mimi sikupendi,” na kujiondoa.

Watoto wadogo kawaida ni rahisi kugeuzwa. Mwonyeshe mtoto mwanasesere maalum na upendekeze kwamba inaweza kuwa furaha kucheza naye. Kama hii haifui dafu, jaribu hadithi au kitabu. Kumpangusa mtoto machozi wakati mwingine humsaidia kuacha kulia. Kama mtoto anaendelea kulia, mpeleke kwa mzazi.

Mtoto akiuliza, “Mama yangu atakuja saa ngapi? Ninaweza kwenda nyumbani saa ngapi?

Mhakikishie mtoto kwamba wazazi wao watakuja. Zungumza kuhusu baadhi ya mambo ambayo yatafanyika kabla ya muda wa kwenda nyumbani.

Shughuli na Michezo kwa Chekechea

Tumia shughuli katika sehemu hii kwa hiari yako wakati wa muda wa chekechea au muda wa shughuli. Unaweza pia kutumia shughuli yoyote katika sehemu hii ambayo inalingana na somo husika wakati wa muda somo la chekechea, na shughuli kutoka somo linaloweza kutumiwa wakati wa muda wa kucheza. Acha shughuli ziwepo kwa watoto wakati wa muda wa kucheza, lakini usiwahitaji watoto kushiriki. Watoto wengine wanaweza kupendelea kucheza na wanasesere wakati wote wa muda wa kucheza.

Shughuli za Sanaa

Tukio la kufanya sanaa linaweza kuwa la kufurahisha na linaweza kuwasaidia watoto kukuza kujiamini, ubunifu, umahiri wa mwili, uratibu wa macho na mikono, na kutambua hisi zao. Sanaa pia zinaweza kuwa njia ya kuridhisha ya kujieleza kibinafsi. Unaweza kutumia ubunifu na usanifu katika kupanga miradi ya sanaa ifaayo kwa darasa lako.

Miongozo hii inaweza kukusadia kupanga miradi ya ubunifu wa sanaa.

  • Fanya miradi rahisi.

  • Jiandae. Kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika na jua jinsi ya kufanya mradi wewe mwenyewe.

  • Kuwa Mwenye Kunyumbulika. Ukiwa unaweza kumnyumbulika, hautasumbuka wakati mradi utaenda jinsi usiyotarajia. Kumbuka kwamba watoto kila mara wanapendelea sana kujaribu na vifaa unavyowapa kushinda kumaliza mradi.

  • Uwe chanya na uwe mwenye kupenda kile wafanyacho watoto, na uwape pongezi ya dhati.

  • Tumia fofauti fofauti. Panga miradi ambayo inawawezesha watoto kutumia vifaa na mbinu tofauti tofauti wiki hadi wiki.

  • Uwe na busara. Watoto wadogo daima hawajaribu kuwasilisha chochote katika sanaa yao. Wao wanafurahia kufanya majaribio na vifaa walivyopatiwa. Kama unataka kusema kitu juu ya kazi ya mtoto, sema, “Niambie kuhusu picha yako” badala ya kuuliza, “Hii ni nini?”

  • Toa msaada mdogo kabisa. Saidia inapohitajika lakini waruhusu watoto wafanye kazi zao wenyewe.

Kupaka rangi hadi muziki.

Vifaa vinavyohitajika: Muziki uliorekodiwa au muziki wa vyombo, karatasi, na krayoni au penseli za rangi.

Cheza muziki watoto wakipaka rangi. Acha wapake rangi kulingana na vile muziki unavyowafanya wajisikie.

Kolaji

Kolaji ni picha iliyotengenezwa kwa kugundisha pamoja vipande vya karatasi, picha, au vifaa vingine.

Vifaa vinavyohitajika: Karibu kifaa chochote kinaweza kutumiwa katika kolaji, kama vile karatasi ya kufunga zawadi, tishu, sampuli za karatasi ya ukutani, majani, mchanga na bidhaa za makaroni. Utahitaji gamu au gundi na kipande cha karatasi au chombo fulani kingine ambacho kina bapa (kuwa kama kitako cha kolaji) kwa kila mtoto.

Acha watoto wachague vifaa vya kugundisha kwenye kitako cha kolaji. Acha wao watengeneze usanifu wo wote wanaotaka.

Kutunga Makaroni

Vifaa vinavyohitajika: Makaroni kubwa ambayo haijapikwa (au vipande vya majani au vifaa vingine ambavyo vitakuwa rahisi kutunga), kipande kikubwa cha uzi au kitani kwa kila mtoto, na gundi au nta.

Tengeneza mwisho mmoja wa kila kipande cha uzi au kitani kuwa mgumu kwa kuchovya kwenye gundi au nta. Baada ya kukauka, itakuwa ngumu vya kutosha kuruhusu kutunga. Funga fundo kwenye ule mwisho mwingine wa uzi ili makaroni yasidondoke. Acha kila mtoto atunge makaroni, na kisha kuifunga miisho ya kila uzi wakati watoto wamemaliza.

Donge la Kuchezea Rahisi

Vifaa vinavyohitajika:

  • Vikombe 2 vya unga

  • Kikombe 1 cha chumvi

  • Mafuta ya mboga kijiko 1

  • Kikombe cha maji 3/4

  • Rangi ya chakula (kwa hiari)

Changanya unga na chumvi. Ongeza mafuta na maji ya kutosha kupata ugumu wa udongo. Ongeza maji kidogo kwa wakati mpaka mchamganyiko unakuwa rahisi kupindika lakini haunati. Changanya na uukande kiasi. (Ili kulipaka rangi donge la kuchezea, ongeza rangi ya chakula kwenye maji kabla ya kuongeza kwenye unga na chumvi.)

Tengeneza donge la kuchezea nyumbani kabla ya kulileta katika chekechea, na lihifadhi katika chombo kisicho na hewa, kama inawezekana. Leta karatasi (karatasi yenye nta huwa bora sana) kutandaza mezani pale ambapo watoto watatumia donge la kuchezea.

Mistari ya Michezo na Shughuli:

Watoto wanapenda kufanya mambo ambayo yanahusisha kutembea, kama vile michezo rahisi au vitendo vya mistari au nyimbo. Mistari mingi ya shughuli imejumuishwa katika masomo, na michezo fulani rahisi imeelezwa hapo chini. Watoto wanapoifurahia shughuli, shughuli hiyo inaweza kutumiwa mara nyingi mwaka mzima, sio tu katika somo pale ambapo limetajwa.

Miongozo hii inaweza kukusaidia kufundisha watoto mistari mipya ya shughuli:

  • Kariri mstari wa shughuli kabla ya darasa.

  • Sema maneno na ufanye vitendo kwa ajili ya watoto kwanza, ukiongezea chumvi vitendo. Kisha waalike watoto kuungana nawe.

  • Nenda pole pole ili watoto waelewe maneno na vitendo.

  • Tumia vifaa vya picha mara kwa mara ili kuwasilisha mstari wa shughuli. Watoto huwa wasikivu na kujifundisha vizuri wanapokuwa na kitu cha kutazama.

  • Fupisha mstari wa shughuli kama watoto wanakosa utulivu. Kama mstari wa shughuli ni mrefu, ukitaka unaweza kuwasaidia watoto kufanya vitendo huku ukiimba au kusema maneno peke yake.

Mstari ya Staha

Tumia mistari ifuatayo wakati watoto wanapokosa utulivu na wanahitaji msaada wa kuwa na staha. Kutumia mojawapo ya hizi wakati mmoja kila wiki unaweza kuwasaidia watoto kujua wakati wa maombi ya kufungua au kufunga. Wasaidie watoto kusema maneno na fanya ubunifu kama ilivyopendekezwa na maneno:

Ifungue, Ifunge [Mikono]

Ifungue, Ifunge;

Ifungue, Ifunge;

Piga makofi kidogo.

Ifungue, Ifunge;

Ifungue, Ifunge;

Iweke kwenye mapaja yako.

Mimi Natikisa Mikono Yangu

Mimi natikisa mikono yangu.

Mimi nazungusha mikono yangu.

Mimi napiga makofi.

Mimi nanyosha mikono yangu,

Kisha naishusha chini.

Na naikunja mapajani.

Mimi natuliza mguu wangu.

Mimi napumzisha mguu wangu.

Mimi naketi wima kwenye kiti.

Mimi nainamisha kichwa changu.

Mimi nafunga macho yangu.

Mimi ni tayari kuomba.

Wakati mwingine mimi ni Mrefu, na Wakati Mwingine Mimi ni Mfupi

Tumia mstari ufuatao wa kujikunja na kujinyoosha wakati watoto wameketi na wanahitaji kutembea tembea. Rudia kama ukipenda.

Wakati mwingine mimi ni Mrefu—mrefu sana, sana (simama, kisha kwa vidole).

Wakati mwingine Mimi ni Mfupi—mfupi sana, sana (chutama, kisha chini zaidi).

Wakati mwingine mrefu, wakati mwingine mfupi (simama, kisha chutama).

Mimi sasa ni? (simama au chutama; acha watoto waseme kama wao ni warefu au wafupi)

Mbegu Ndogo

Waambie watoto jinsi mbegu hupandwa ardhini, na wasaidie kujifanya wao ni mbegu zinazokua. Sema, “Acha tujifanye sisi ni mbegu ndogo” (chutama au ujikunje kama mpira, na ufunge macho). “Jua lilichomoza na kufanya mbegu kuwa na joto. Kisha mvua ikanyesha na ikasema, ‘Amkeni, mbegu ndogo’” (fungueni macho na muanze kujinyosha). “Chomozeni ardhini, mbegu ndogo, ili muweze kukua” (simameni na mnyooshe mikono yenu juu ya kichwa). “Mbegu ndogo, mmekua kuwa maua maridadi [au miti mirefu].”

Acha Twende Nyumbani kwa Bibi [au Babu].

Sema, “Acha tujifanya tunaenda nyumbani kwa Bibi [au Babu]. Kwanza lazima tuvae makoti yetu [au magauni]” (jifanyeni kuvaa makoti au magauni). “Acha tuingie garini [au basini]” (jifanyeni kufungua mlango na kwenda na gari). “Ee, barabara hii ina mabonde sana” (fanya mwendo wa kuvuka mabonde). “Tazama, acha tumpungie mkono afisa wa polisi” (fanya kama kupunga mkono). “Tumekaribia huko. Haya Bibi [au Babu] anakuja sasa. Acha tumpe yeye kumbatio kubwa sana” (jifanye kumkubatia Bibi au Babu).

Kuwasaidia Wazazi Wetu

Waelekeze watoto kufanya vitendo ambavyo vinaashiria kuwasaidia wazazi wao. Unaweza kusema, “acha tujifanye tunafagia sakafu.” Watoto wajifanya kufagia sakafu. Unaweza kuendelea na kutandika vitanda, kuosha madirisha, kuzoa taka, kulima shamba, kuosha gari, au shughuli zingine zinazofaa katika eneo lako.

Mchezo wa Kubingirisha Mpira

Vifaa vinavyohitajika; Mpira.

Acha watoto waketi katika nusu duara. Wewe keti mbele yao na bingirisha mpira hadi kwa mtoto mmoja, huku ukiita jina la mtoto huyo au ukiuliza swali linalohusiana na somo hilo. Mtoto yule anabingirisha mpira kwako tena na anasema jina lako au kujibu swali. Hakikisha kila mtoto anapata angalao zamu moja. Unaweza pia kucheza mchezo huu kama mmesimama, mkitupiana mpira.

Kulinganisha Maumbo

Vifaa vinavyohitajika; Karatasi za rangi, mkasi.

Tumia karatasi za rangi kutengeneza mkato mmoja mkubwa na mkato mmoja mdogo kwa kila mojawapo ya maumbo, mraba, duara, pembetatu, moyo, pembenane, na yai. Tandaza maumbo sakafuni. Acha kila mtoto achukue zamu kuweka umbo dogo juu ya umbo kubwa linalofanana nalo. Kwa mageuzi, tengeneza maumbo hayo hayo kwenye karatasi za rangi tofauti, na uwaache watoto waoanishe kwa kutumia rangi badala ya umbo.

Maumbo ya Muziki

Vifaa vinavyohitajika: Duara za rangi tofauti zilizo katwa kutokana na karatasi za rangi au vitambaa, muziki uliorekodiwa au wa vyombo, gundi ya kanda (hiari).

Gundisha au weka duara sakafuni katika duara kubwa. Acha watoto watembee nje ya duara kubwa wakati muziki unapopigwa. Muziki unaposimama, kila mtoto anataja jina la rangi ya duara iliyo karibu na yeye. Kwa mageuzi, tumia maumbo tofauti na uwaache watoto wataje rangi na umbo.

Kurusha Kijifuko cha Maharagwe

Vifaa vinavyohitajika: Vijifuko vya maharagwe; sanduku, kikapu, au dango (tengeneza kwa kukata mashimo katika picha iliyotundikwa kwenye kifaa kigumu).

Acha watoto warushe vijifuko vya maharagwe katika sanduku, kikapu, au dango. (Unaweza kutengeneza vijifuko vya maharagwe au dango kufanana na sikukuu au somo.) Watoto wanaweza pia kurusha vijifuko vya maharagwe kwenye vibao au masanduku ambayo yamewekwa moja juu ya lingine.

Sanamu

Vifaa vinavyohitajika: Muziki uliorekodiwa au wa vyombo.

Au acha watoto watembee chumbani huku muziki hukicheza. Muziki unaposimama, watoto wanasimama tuli kabisa kama sanamu. Watoto wanaweza kutembea tena muziki unapoanza, lakini lazima wasimame tuli unaposimama.

Muziki katika Darasa la Chekechea

Muziki katika darasa la chekechea uleta mazingira ya ukunjufu na upendo, kufanya Msingi kuwa mahali pa furaha. Watoto wa umri wa chekechea wako tayari kujifunza juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, wao wenyewe, na ulimwengu huu maridadi. Njia muhimu kwao ya kujifundisha ni kupitia muziki. Watoto wanaweza kufurahia muziki katika njia nyingi tofauti. Wanaweza kuimba, kupiga vyombo vya muziki, kucheza muziki, na kusikiliza muziki. Tazama “Muziki Darasani,” ukurasa vii, kwa maelezo ya ziada juu ya kutumia muziki kwa ajili ya kufundisha watoto wadogo.

Kuimba

Watoto wadogo wanaweza kuwa hawataki kuimba pamoja nawe (watoto wadogo sana wanaweza kuwa hawawezi kuimba pamoja nawe), lakini wanafurahia kukusikiliza wewe ukiimba na mara nyingi wanajifunza kanuni muhimu kupitia nyimbo. Wahimize watoto kuimba, lakini usjiali kama hawatafanya hivyo. Watoto wale ambao hawawezi kuimba wanaweza kufurahia kufanya vitendo vingine rahisi huku wewe ukiimba.

Ukitaka unaweza kutumia nyimbo zile zile kila wiki unapoanza kila shughuli kwa njia tofauti. Watoto wanaposikia tuni waijuayo, watajua ni shughuli gani ambayo inaanza. Unaweza pia kubadilisha maneno ya wimbo ili kuendana na hali ya watoto au shughuli. Imba nyimbo zipendwazo na watoto mara nyingi mwaka mzima.

Nyimbo zifuatazo kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto zinafaa hasa kwa matumizi katika chekechea. Yaliyojumuishwa ni baadhi ya mapendekezo ya njia unavyoweza kutohoa maneno. Unaweza kuwa na mawazo mengine kwa ajili ya njia za kutohoa nyimbo hizi au zingine katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto ili ziweze kufaa kwa ajili ya chekechea.

  • “A Happy Family” (p. 198) (© 1975 Pioneer Music Press, Inc.). Buni mstari kuhusu chekechea au darasa lako la Msingi la watoto wenye furaha. Tumia kama maamkizi: “Namuona Suzi; naye ananiona. …”

  • “Fanya Ninavyofanya” (uk. 276). Tumia kwa kuonyesha maelekezo: “Safisha chekechea; nifuate, nifuate mimi! …” au “Kusanyikeni tuimbe. …”

  • “Yafurahisha Kutenda” (uk. 253).

  • “Haya Tuko Pamoja” (uk.261).

  • “Mimi Nachezesha chezesha” (uk. 271)

  • “Kama Una Furaha” (uk.266).

  • Mikono Yangu” (uk. 273).

  • Once There Was a Snowman (© 1981 Pioneer Music Press, Inc.) Buni mistari kuhusu vitu vingine vya asili: Wakati mmoja kulikuwa na mti wa kijani kibichi … mrefu, mrefu, mrefu. Katika kivuli chake nikajituliza … kidogo, kidogo, kidogo.

  • “Mvua Inanyesha Kila Mahali” (uk.241).

  • “Kuimba Wimbo” (uk.253). Badilisha “Imba” na vitendo vya kawaida: Ruka Kamba, ruka kamba, ruka kamba, au Ruka, ruka, ruka.” Imba kuhusu nguo, rangi, au mwenyewe: Viatu, viatu, viatu; mimi napenda viatu vyangu. Mimi Huvivaa miguuni mwangu: viatu, viatu, viatu!”

  • “Tabasamu” (uk. 267).

  • “Bisi Zikikaangwa” (uk. 242).

Vyombo vya Muziki

Pata vyombo rahisi vya muziki kwa ajili ya watoto kucheza.

Zumari au tarumbeta: Toboa mashimo machache kwenye upande wa pembe ya karatasi ngumu (kama aina ya karatasi ya kufunga vitu, karatasi iliyo na nta, au karatasi za kupangusa mikono. Kwa ubora maalum, gandisha gundi ya kanda kwenye miisho yote. Cheza, vuma au imba katika neli hili.

Vibao vya Msasa: Kata vipande viwili ya mbao ya unene wa 1” na upana wa 2” kwa urefu wa 4.” Kata vipande viwili vidogo, vya 1” kwa 21/2” Piga msasa sehemu yo yote yenye ncha kali au kata kona yo yote ya vibao hivi. Weka vibao vidogo katikati ya vibao vikubwa na upigilie misumari. Weka kipande cha msasa chini ya kila kibao. Kucheza, gonganisha vibao pamoja au visugue vipande vya msasa kimoja dhidi ya kingine.

Njuga: Weka punje za mahindi au maharagwe yaliyokauka kwenye mkebe usio na sehemu zenye ncha kali, au katika chombo za karatasi. Acha watoto wavirembe vyombo hivi. Funga kwa gundi ya mkanda vizuri kuzuia watoto kula au kucheza na vilivyo ndani yake. Kucheza, tikisa tikisa.

Kengele: Tunga kengele katika mshipi wa kitambaa. Kucheza, tikisa tikisa.

Mwendo wa Muziki

Mwendo wa ubunifu kwa muziki huwasaidia watoto kutumia nguvu zao vyema na kukuza uwezo wao wa kutumia akili kwa ubunifu. Imba, cheza piano au chombo kingine, au tumia muziki uliorekodiwa ili watoto waendane nao.

Kujumuisha watoto katika mwendo wa muziki, unapaswa:

  • Kuwaelekeza watoto katika kukimbia, kurukaruka, kuinama, kuzunguka, kutembea kwa vidole, kutambaa, kuruka, au kujinyoosha ili kuendana na muziki. Acha watoto wachukue zamu kuongoza vitendo vya kundi.

  • Cheza au imba nyimbo zenye midundo tofauti na waache watoto wakimbie au watembee kwa kuendana na muziki.

  • Acha watoto wapunge skafu za rangi au tepe za karatasi wanapokwenda pamoja na muziki.

  • Tumia nyimbo za vitendo wakati watoto wanapohiitaji kubadilisha mwendo. Ikiwa watoto wamekaa kwa muda mrefu, wimbo wa vitendo ukitumia misuli mikubwa na mwendo mkubwa itakuwa inafaa. Ikiwa wamekuwa katika mwendo na wanahitaji kutulia, wimbo wa vitendo ukitumia misuli midogo wakati watoto wamekaa chini itafaa.

Kusikiliza

Kitabu hiki cha kiada kinaambatana na kanda za sauti ambazo zinaweza kutumiwa kwa shughuli za kusikiliza. Kanda ya sauti ina sehemu tano:

  1. “Muziki tulivu”—wa kuchezwa wakati watoto wakiingia chekechea au nyakati zingine wakati mazingira ya amani yakihitajika.

  2. “Muziki wa Utambuzi”—wa kuwasaidia watoto kutambua aina mbali mbali za sifa bainifu za kimuziki.

  3. “Kuendana na Muziki”—unapigwa kwa ajili ya watoto wanapofanya vitendo kama kuinama au kujinyoosha. Watoto wanaweza kutumia nguvu na kukuza ujuzi wa kimwili na kimdundo wanaposikiliza na kushiriki.

  4. “Maonyesho ya Kimuziki”—kuwahimiza watoto kusikiliza na kuendana kwa uhuru na muziki. Teuzi fupi kumi na mbili zimejumuishwa, pamoja na mapendekezo ambayo yanapendekeza njia za kuendana na muziki. Usitumie zaidi ya teuzi tatu katika kipindi cha darasa moja.

  5. “Hadithi za Kujifanya”—zinachezwa ili kuwapa watoto shughuli ya kufanya. Kwa kufuata maelekezo na kusikiliza hadithi kwa makini, watoto hujumuika katika maigizo na shughuli zingine za mwili. Hadithi zilizo na kichwa “Matembezi Msituni,” “Matembezi kwenye Bustani ya Wanyama,” na “Wanasesere katika Sanduku la Wanasesere.” Tumia hadithi moja tu katika kipindi cha darasa.

Unaweza pia kutumia Kitabu cha Nyimbo za Watoto kwenye kaseti za muziki (muziki tu, 52505; muziki na maneno, 52428) au diski (muziki tu 50505; muziki na maneno, 50428) kama zinapatikana.

Watoto wanaweza kuwa na wakati mgumu kuzingatia muziki kama wanasikiliza tu. Changanya kusikiliza pamoja na kuimba, kutembea, au shughuli zingine, kama katika mifano ifuatayo:

  • Acha watoto walale chini na kusikiliza aina tofauti za muziki. Zungumzia jinsi muziki unavyowafanya wao kujisikia. Kisha waache wao waonyeshe jinsi wanavyojisikia.

  • Cheza muziki wa kutembea na waache watoto watembee chumbani.

  • Au acha watoto wapige makofi kwa mdundo wa muziki wanaosikiliza

Sampuli ya Masomo Yaliyotoholewa

Ifuatayo ni mifano ya jinsi masomo mawili katika kitabu cha kiada hiki yanavyoweza kutoholewa kwa matumizi ya chekechea. Unaporejea sambuli, fahamu kwamba:

Kila kipande cha muda katika somo hili huzingatia ujumbe rahisi wa injili. Shughuli na muziki hupaswa kuwasaidia watoto kuanza kuelewa kanuni za msingi za injili na maneno.

Ni sehemu fulani tu kutoka somo la mwanzo zimechaguliwa. Hii husaidia kufanya darasa kuwa rahisi, hai, na la kufaa kwa watoto wa umri wa chekechea.

Shughuli zilizochaguliwa hazitumiwi kila mara katika mpangilio mmoja ambao unajitokeza katika somo la asili. Shughuli wakati wa somo zinapaswa kupangwa katika utaratibu ambao utawasaidia vyema watoto wa umri wa chekechea kuelewa ujumbe wa injili.

Somo la 6: Baba wa Mbinguni na Yesu Wananipenda

Karibu

Njia moja ya kuweka mazingira ya staha kwa chekechea ni kucheza muziki kutoka kwenye kanda za kaseti za sauti za Kitabu cha Nyimbo za Watoto. Kutanguliza ujumbe wa injili katika somo hili, unaweza kumpa kila mtoto beji ambayo inasema “Baba wa Mbinguni na Yesu Wananipenda Mimi” (ona shughuli ya kuboresha ya 6 uk. 17).

Muda wa kucheza

Dakika 35

Wakati wa muda wa kucheza, tafuta njia za kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kwa mfano, unaweza kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu hufurahia tunapokuwa wakarimu kwa kila mmoja na wanatupenda sana. Unaweza pia kuwasaidia watoto kukumbuka somo la wiki iliyopita kwa kuwauliza, “Mwana wa Baba wa Mbinguni ni nani?

Wakati wa Kukusanyika

Dakika 10

Wakati wa kukusanyika unaweza pia kutumiwa kuwaandaa watoto kwa ajili ya somo. Anza kwa kuimba wimbo wa maombi na msaidie mtoto kuomba. Kisha wasaidie watoto kujiandaa kwa ajili ya somo, kwa kuwauliza ni nani alitupatia dunia hii maridadi na injili na Kanisa (tazama shughuli ya usikivu, uk. 15).

Muda wa Muziki

Dakika 10

Muziki unaweza kufaa sana katika kuwasaidia watoto wa umri wa chekechea kujifunza ujumbe wa injili. Kwa mfano, katika somo hili unaweza kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu kwa kuimba “I Know My Father Lives” au “I Feel My Savior’s Love” shughuli ya kuboresha ya 2, uk.12). Kama muda unaruhusu, rejea nyimbo kutoka masomo yaliyopita au imbeni nyimbo zilizoteuliwa zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa xvii.

Muda wa Vitafunwa

Dakika 10

Ingawa hakuna shughuli inayotumika hapa ili kuimarisha ujumbe wa injili, unaweza kuwakumbusha watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatupenda na kwamba tunapaswa kuwashukuru kwa kila kitu, ikijumuisha chakula chetu. Mwalike mtoto atoe maombi ya baraka juu ya chakula.

Muda wa Somo

Dakika 10

Somo hili lina sehemu kadhaa ambazo zinaweza kutumiwa kuwasaidia watoto wa umri wa chekechea kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanawapenda. Kwa mfano, unaweza kutumia sehemu zifuatazo kutoka somo la 6:

Muda wa Shughuli

Dakika 15

Muda wa shughuli huwapatia watoto nafasi za kuwa wabunifu na kutumia nguvu zao. Inapowezekana, shughuli zinapaswa kusaidia kuimarisha ujumbe wa injili. Kwa mfano, unaweza kucheza mchezo wa kubiringisha mpira (uk. xvi), ukiuliza maswali ili kuimarisha ujumbe wa injili.

Muda wa Kufunga

Dakika 10

Tumia muda wa kufunga kuwakumbusha watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanampenda kila mmoja wao na wanawajua kwa majina. Elezea hisia zako za shukrani kwa ajili ya baraka ambazo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wametupatia. Kisha msaidie mtoto kutoa maombi ya kufunga.

Somo la 10; Ninashukuru kwa ajili ya Miti, Mimea, na Maua

Karibu

Msalimie kila mtoto kwa jina wanapoingia katika darasa la chekechea. Unapowasalimia, tanguliza mada ya somo kwa kuwaambia kwamba leo watajifunza kuhusu mimea, maua, na miti.

Muda wa kucheza

Dakika 35

Wakati wa muda wa kucheza, waandae watoto kwa somo hilo kwa kuwaambia kuhusu vitu vingi vizuri katika dunia hii ambavyo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo waliumba kwa ajili yetu ili tuifurahie.

Wakati wa Kukusanyika

Dakika 10

Imba wimbo wa maombi; kisha msaidie mtoto kuomba. Kwa somo hili, unaweza pia kuleta mimea ili watoto wapate kuona, kugusa, na kunusa. Kisha toa shukrani zako kwa ajili ya mimea, maua, na miti (ona shughuli ya ziada ya 2, ukurasa 30).

Muda wa Muziki

Dakika 10

Imba “Ndani ya Kilele cha Miti ya Majani Mengi” (ona shughuli ya ziada ya 2, ukurasa 30). Kufanya vitendo vya wimbo kutasaidia kujenga mazingira ya furaha na kuwapa watoto mabadiliko ya mwendo. Kama muda unaruhusu, unaweza pia kurejea nyimbo kutoka somo lililopita.

Muda wa Vitafunwa

Dakika 10

Inapowezekana, anza muda wa vitafunwa kwa shughuli rahisi ambayo inahusiana na ujumbe wa injili. Kwa mfano, katika somo hili kitafunwa kinaweza kuwa mkate na tunda. Waelezee watoto kwamba vitu hivi vinatoka kwa miti, mimea, na maua (ona shughuli iliyo ukurasa wa 29). Kisha msaidie mtoto kuomba baraka juu ya chakula.

Muda wa Somo

Dakika 10

Chagua sehemu kutoka kwa somo hili ambazo unahisi zitawasaidia watoto kuelewa ujumbe wa injili. Kwa mfano, unaweza kuwasaidia watoto kuelewa jinsi miti, mimea, na maua hukua kwa kupasua tunda ili watoto waweze kuona mbegu. Elezea kile ambacho lazima kitokee ili mbegu zikue na kuwa matunda mengi (ona shughuli ya kuboresha ya 4, ukurasa wa 30). Kisha wasaidie watoto kupanda mbegu katika vikombe vya karatasi vilivyojaa mchanga (ona shughuli ya kuboresha ya 1, ukurasa wa 29).

Muda wa Shughuli

Dakika 15

Baada ya somo, unaweza kucheza muziki laini huku watoto wakipaka rangi picha za miti, mimea, na maua. Shughuli zinaweza kuchaguliwa kutoka kwenye somo hili au kutoka katika yale ambayo yameorodheshwa kwenye ukurasa wa xiv–xvii. Watoto wengine wanaweza kupendelea kucheza na wanasesere wakati huu. Andaa shughuli, lakini usiwalazimishe watoto kushiriki.

Muda wa Kufunga

Dakika 10

Muda wa kufunga hutumiwa kufanya muhtasari ujumbe wa injili na kuwaandaa watoto kwa maombi. Katika somo hili, unaweza kuwaacha watoto warudie nyuma yako maneno ya wimbo “Mbegu Ndogo Zimelala Usingizi Manana” ili kuwakumbusha watoto kwamba tunashukuru kwa ajili ya miti, mimea, ana maua (ona shughuli ya kuboresha ya 2, ukurasa wa 29). Kisha msaidie mtoto kutoa maombi ya kufunga.

Chapisha