Somo la 3
Mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu
Madhumuni
Ni kuwasaidia watoto kuelewa kwamba tuliishi na Baba wa Mbinguni kama watoto wa kiroho kabla ya kuja duniani na kwamba tunaweza kuishi pamoja naye tena baada ya maisha haya.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Ibrahimu 3:22–27. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 2.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Maandiko.
-
Mwanasesere au umbo la karatasi.
-
Picha 1-6, Ulimwengu (62521); picha 1-7, Yesu Kristo (Sanaa za Picha za Injili 240; 62572); picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga (62307); picha 1-6 Jioni ya Familia Nyumbani (62521); picha 17, Familia yenye Upendo; picha 1-8, Kupitisha Sakramenti (62021); picha 1-9, Sala ya Asubuhi (62310); picha 1-10, Sala ya Familia (62275); picha 1-11, Mvulana Akibatizwa (62018); picha 1-12, Msichana Akithibitishwa (62020); picha 1-13, Joseph Smith (Sanaa ya Picha za Injili 400; 625449).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Sisi tu watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni
Rejea pamoja na watoto jinsi tulivyoishi na Baba wa Mbinguni kama watoto wake wa kiroho kabla ya kuzaliwa kwetu duniani. Tuliona furaha, na tulipenda kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni. Hatukuwa na miili ya nyama na mifupa kama tulivyo sasa, lakini tulikuwa na roho. Elezea kwamba roho hufanana na mwili lakini haina nyama na mifupa.
-
Uliishi wapi kabla ya kuzaliwa duniani?
Baba wa Mbinguni alitutuma sisi kuja kuishi hapa duniani
Onyesha picha 1-1, Ulimwengu. Elezea kwamba dunia ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Chini ya maelekezo ya Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo aliumba dunia kwa ajili yetu. Tulitumwa kuja kuzaliwa hapa na kupokea mwili.
Onyesha picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga. Waache watoto waseme kuhusu picha hii. Waambie kwamba tulichangamkia kuja duniani ili kujifunza na kukua, Tulikuja duniani kama watoto wachanga katika familia ambazo zingetupenda na kutulea.
Waambie watoto kwamba tulikuja duniani, tulipatiwa miili ya kimwili kama ngozi, misuli, damu, na mifupa Acha watoto waguse mikono yao wenyewe.
-
Je, unahisi mfupa ndani ya mkono wako?
-
Unaweza kuona na kuhisi ngozi yako?
-
Unaweza kuhisi misuli yako?
Wakumbushe watoto kwamba roho zetu ndani ya miili yetu hutupatia uhai, lakini hatuwezi kuziona au kugusa roho zetu. Miili yetu inaweza kuonekana na kuguswa. Waambie watoto kwamba hii ni baraka kubwa kuwa na mwili.
Baba wa Mbinguni anataka turudi kwake siku moja
Onyesha upendo wako kwa Baba wa Mbinguni. Waambie watoto kwamba siku moja unataka kurudi kwa Baba wa Mbinguni ili uweze kumwona na kuwa pamoja naye tena. Elezea kwamba hii ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Yeye anataka kila mmoja wetu kurudi kuishi pamoja naye wakati maisha ya duniani yatakapoisha. Anataka sisi, wazazi wetu, na familia zetu zote ziwe pamoja naye tena.
Elezea kwamba ili kuishi na Baba wa Mbinguni na Yesu tena, sharti sisi tubatizwe na kutii amri zake zote. Onyesha maandiko. Elezea kwamba maandiko yanatufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu na kile ambacho wanataka sisi tufanye.
Ukitumia picha zilizoorodheshwa katika sehemu ya “Maandalizi.” zungumza kuhusu kile ambacho Baba wa Mbinguni anataka sisi tujifunze na kufanya hapa duniani. Anataka sisi tuzipende familia zetu, tusiwe wachoyo, twende kanisani, tupokee sakramenti, kuomba asubuhi na usiku, kuwa na maombi ya familia na jioni ya familia nyumbani, kubatizwa, kuthibitishwa na kumpokea Roho Mtakatifu, ndoa ya hekaluni, kujifunza kuhusu manabii, na kuwa kama Baba wa Mbinguni na Yesu.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilichoandikwa Mimi ni moto wa Mungu, na uache kila mtoto achore picha yake yeye mwenyewe. Acha watoto waonyeshe picha zao kwa wengine walio darasani. Himiza kila mtoto aseme kitu fulani kizuri kuhusu yeye mwenyewe huku akionyesha picha hii.
-
Wasaidie watoto kusema mstari ufuatao na wafanye vitendo vinavyoelezwa:
Uumbaji wa Mungu
Mungu aliumba mwezi (fanya duara kwa mikono).
Na nyota za kumetameta (fungua na ufunge mikono)
Na uziweke hewani (fikia juu)
Aliumba jua (tengeneza duara kubwa juu ya kichwa)
Na miti (nyoosha mikono kwa urefu)
Na maua (weka mikono kama bakuli)
Na ndege wadogo ambao huruka (punga mikono).
(Kutoka Fascinating Finger Fun na Eleanor Doan. © 1951. Imetumika kwa Idhini.)
-
Andika maswali yafuatayo kwenye kipande tofauti cha karatasi. Rejea somo hili kwa kumwaachia kila mtoto achague kipande cha karatasi. Soma kila swali na umuache mtoto mmoja alijibu. Rudia kama inavyohitajika ili kumpa kila mtoto nafasi.
-
Mtoto wa Mungu ni nani? (Mimi, kila mtu.)
-
Tuliishi wapi kabla ya kuzaliwa kwetu hapa duniani? (Mbinguni pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu.)
-
Kwa nini Baba wa Mbinguni alimwambia Yesu aumbe dunia kwa ajili yetu? (Ili tuweze kupata miili na kujifunza kile tunachohitaji kufanya ili tuishi pamoja Baba wa Mbinguni na Yesu tena.)
-
Je, tunahitaji kufanya nini ili tuishi tena na Baba wa Mbinguni na Yesu? (Kutii amri, tusiwe wachoyo, tubatizwe, twende hekaluni na vinginevyo. Acha watoto waonyeshe picha ifaayo wanapojibu swali hili.)
-
Tunaweza kuishi na kina nani baada ya kumaliza maisha hapa duniani? (Baba wa Mbinguni na Yesu na familia zetu.)
-
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Kwa idhini ya Rais wako wa Msingi, mwalike baba amlete mtoto wake mchanga darasani. Zungumza kuhusu kina baba na jinsi wanavyowapenda watoto wao. Waambie watoto kwamba wana baba wawili ambao wanawapenda: baba yao wa hapa duniani na baba yao wa mbinguni. Kabla watoto wachanga kuzaliwa duniani, waliishi mbinguni na Baba wa Mbinguni. (Fahamu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako, ambao baadhi yao yawezekana kuwa hawana baba katika nyumba zao.)
-
Lete jozi moja au mbili za “Viatu vya Baba” darasani. Zungumzia kuhusu ni nani huvaa viatu hivi vikubwa. Acha watoto walinganishe saizi ya viatu vyao wenyewe au miguu na viatu vikubwa. Acha kila mtoto achukue zamu kutembea na “Viatu vya Baba.”
-
Imbeni au semeni mstari miwili ya kwanza ya “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 4).
Nliishi mbinguni kwa muda mrefu, ni kweli;
Niliishi huko na nilipenda huko pamoja na watu niwajuao. Vivyo hivyo nawe.
(© 1987 by Janice Kapp Perry. Imetumika kwa Idhini.)
-
Tuliishi na nani mbinguni? (Baba wa Mbinguni na Yesu na kila mtu.)
-
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwenye mstari wa shughuli ufuatao huku ukisema maneno: Rudia mara nyingi kama ungependa kufanya hivyo.
Fanya duara kila mtu akisimama na kushikana mikono. Shikaneni mikono wakati wote wa shughuli.
Sisi wote tuliishi pamoja na Baba wa Mbinguni (kila mtu aje karibu pamoja, na kuleta mikono katikati ya duara).
Alitutuma hapa duniani ili tuishi (fungueni duara kubwa).
Alitupatia familia za kutupenda na kutufundisha (njooni karibu pamoja tena).
Familia zetu zitatusaidia kuishi pamoja naye tena (fungueni duara kubwa).