Somo la 22
Mimi Naweza Kufanya Mambo Mengi
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba kama watoto wa Baba wa Mbinguni kila mmoja sisi anaweza kufanya mambo mengi.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze 1 Samweli 17.
-
Wasiliana na wazazi wa kila mtoto katika darasa lako ili kujua kitu kimoja ambacho mtoto anaweza kufanya vyema au anajifunza kufanya.
-
Andaa vipande vya karatasi vilivyo na maelekezo rahisi, kama vile kupiga makofi, kuhesabu hadi tatu, kutembea chumbani, kuruka, kuchora duara (ubaoni au kwenye kipande cha karatasi) kusimama kwa mguu mmoja, kukunja mikono, au kuonyesha kitu ambacho ni rangi ya bluu. Andaa angalao vipande vingi vya karatasi kadiri iwezekanavyo kulingana na idadi ya watoto darasani. Chukua tahadhari juu ya watoto katika darasa lako ambao wana ulemavu, na hakikisha kwamba umewajumuisha katika mambo wanayoweza kufanya.
-
Andika jina la mtoto kwenye kipande tofauti cha karatasi tofauti.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Ufito mdogo wa kuvulia samaki (kwa hiari; ona somo la 11).
-
Chombo cha kuweka majina (kwa hiari).
-
Picha 1-5, Familia na Mtoto (62307); picha 1-10, Sala ya Familia (62275); picha 1-38, Watoto Wakicheza na Mpira; picha 1-50, Naweza Kujivisha Nguo; picha 1-51, Familia Ikifanya Kazi Pamoja (62313); picha 1-52, Daudi Anamuua Goliathi (Sanaa ya Picha za Injili 212; 62073).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Kwa taarifa ya mwalimu: Kuwa msikivu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, siyo ulemavu wao.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Miili yetu inaweza kufanya mambo mengi
Baba wa Mbinguni anaweza kutusaidia kufanya mambo mengi
Waambie watoto kwamba wakati mwingine tunaombwa kufanya mambo ambayo ni magumu.
-
Ni nini ambacho umeshajaribu kufanya ambacho ni kigumu?
-
Ni nani anaweza kutusadia kufanya mambo haya? (Wazazi, kaka na dada na walimu.)
-
Kwa nani tunaweza kuomba msaada tunapokuwa tunatakiwa kufanya jambo gumu? (Baba wa Mbinguni.)
Elezea kwamba Yesu Kristo anaweza kutusaidia wakati mambo yanapokuwa magumu.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Pamoja na watoto, imbeni ”Do As I’m Doing” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 276), au “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 253) na mkifanya vitendo viinavyofaa. Acha watoto wapendekeze vitendo kwa mistari ya nyongeza.
-
Wape watoto karatasi na krayoni, na uache kila mtoto achore picha ya kitu kimoja au vingi anavyoweza kufanya. Andika Mimi naweza kufanya mambo mengi kwenye kila karatasi la mtoto.
-
Wasadie watoto kuamua juu ya kitu wanachoweza kufanya nyumbani ili kumsaidia mtu fulani, kama vile kupanga meza, kufagia sakafu, au kulisha mnyama wa nyumbani. Wakumbushe wao kuwaambia wazazi wao juu ya hilo baada ya masomo ya darasa la Msingi ili wazazi wao waweze kuwasaidia kukumbuka kufanya.
-
Rudia baadhi ya shughuli zinazofaa katika somo la 16 hadi 20.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno yafuatayo kwa tuni ya “Once There Was a Snowman” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 249). Wakitumia vitendo vya kuchuchumaa kwa mstari wa kwanza na vitendo vya kujinyoosha kwa mstari wa pili.
Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mchanga, mchanga,
Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mdogo, mdogo, mdogo.
Sasa ninakua mkubwa, mkubwa, mkubwa,
Sasa ninakua mkubwa, mrefu, mrefu, mrefu!
Waache watoto waongee kuhusu mambo ambayo wamejifunza na kufanya tangu walipokuwa watoto wachanga.
-
Onyesha kwa kitendo kama vile kuruka, kupiga makofi, kurukaruka, na waombe watoto wataje kile ambacho wewe unafanya. Kisha acha watoto wafanye kitendo hicho hicho. Mpe kila mtoto nafasi ya kuonyesha kitendo. Waalike watoto wengine waseme ni kitendo gani na kisha wakiigize.