Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 16: Mimi nina Mwili


Somo la 16

Mimi nina Mwili

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuthamini na kuheshimu mwili wake.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Danieli 1 na Mafundisho na Maagano 89. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 29.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia, na nakala ya Mafundisho na Maagano.

    2. Picha 1-5, Familia na Mtoto (62307); picha 1-37, Danieli Akikataa Nyama na Mvinyo wa Mfalme; picha 1-16 (Sanaa za Picha za Injili 114; 62094); picha 1-38, Mtoto Akicheza na Mpira.

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Taarifa kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, wala siyo ulemavu wao.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Acha watoto wasimame. Wasaidie kuimba na kufanya vitendo vya “Head, Shoulders, Knees, and Toes” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 275). Imba wimbo pole pole vya kutosha ili kugusa au kutingisha sehemu za mwili zinapotajwa. Kwa mfano, ishara ya kichwa, inua mabega yako, kunja magoti yako, na simama kwa ncha za vidole.

Kichwa, mabega, magoti, na vidole, magoti na vidole magoti na vidole,

Kichwa, mabega, magoti, na vidole, macho, masikio, na pua,

Waelezee watoto kwamba wametumia miili yao kuwasaidia kuimba wimbo huu.

Baba wa Mbinguni alipanga kila mmoja wetu awe na mwili

Rejea pamoja na watoto kwamba tulipokuwa tunaishi mbinguni pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, hatukuwa na miili ya nyama na mifupa. Tulikuwa roho. Tulihitaji kuja duniani ili kupata miili ya nyama na mifupa. Baba wa Mbinguni alipanga sisi kuzaliwa duniani na kuwa na wazazi wa kidunia ili watutunze.

Onyesha picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga.

  • Ni kina nani walio katika picha hii?

  • Ni nani aliyepanga tuje duniani kupata miili na kuwa na familia?

Shughuli

Acha watoto wasimame na waigize vitendo vyako unapoelezea kwamba miili yetu ni kutoka juu ya vichwa vyetu (gusa kichwa) hadi ncha za vidole vyetu (gusa vidole). Nyuso zetu (tabasamu) na vidole vyetu (chezesha vidole) vyote ni sehemu za miili yetu. Acha watoto wageuke mara moja na kuketi chini.

Elezea kwamba miili yetu inaweza kufanya mambo mengi. Kila sehemu ya mwili wetu ina kazi muhimu ya kufanya.

  • Unaweza kufanya nini na macho yako?

  • Unaweza kufanya nini na masikio yako?

  • Unaweza kufanya nini na mdomo wako?

  • Unaweza kufanya nini na mikono yako?

  • Unaweza kufanya nini na miguu yako?

Shughuli

Acha watoto wasimame na kufanya mstari wa kitendo ufuatao:

Mimi Nina Mwili wa Ajabu

Mimi nina mwili wa ajabu (gusisha mikono kwenye kufua)

Baba wa Mbinguni aliupanga kwa ajili yangu.

Yeye alinipa masikio ili niweze kusikia (kunja kiganja sikioni)

Na macho ili niweze kuona (onyesha macho).

Mimi nina mikono miwili ambayo naweza kupiga makofi (piga makofi),

Miguu miwili ambayo inaweza kugeuka (geuka).

Kama nikitaka, naweza kugusa.

Vidole chini sakafuni (inama kugusa visole).

Ninapofikira kuhusu mwili wangu (weka kidole kichwani),

Sehemu yake bora ni (keti chini kimya kimya)

Baba wa Mbinguni aliipanga kwa ajili yangu.

Ili ufanane sana na wake.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuitunze miili yetu

Elezea kwamba kwa sababu miili yetu ni muhimu sana, Baba wa mbinguni na Yesu wametupatia sheria za kutusaidia kuitunza miili yetu na kuiweka iwe na nguvu na afya. Sheria hizi zinaitwa Neno la Hekima. Onyesha nakala ya Mafundisho na Maagano (au onyesha ukurasa wa jina wa Mafundisho na Maagano katika utatu wa maandiko) Elezea kwamba Neno la Hekima limeandikwa katika kitabu hiki cha maandiko.

Jadili aina ya vyakula ambavyo Neno la Hekima hutuambia vitasaidia kuiweka miili yetu kuwa na afya, kama vile matunda, mboga, na nafaka. Kisha jadili vitu ambavyo Baba wa Mbinguni na Yesu wametuambia tusitumie, kama vile tumbaku, vileo, na kahawa. Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunapotii Neno la Hekima na kula vyakula sahihi, Baba wa Mbinguni na Yesu wanafurahishwa nasi na watatubariki.

Hadithi

Simulia hadithi iliyo katika Danieli 1 kuhusu jinsi Danieli alivyokula chakula ambacho Baba wa Mbinguni alimtaka ale. Onyesha picha 1-37, Danieli Anakataa Chakula na Mvinyo wa Mfalme, katika wakati ufaao.

  • Danieli alifanya nini mfalme alipomwambia ale chakula ambacho hakikuwa kizuri kwake? (Ona Danieli 1:8, 12–13.)

  • Ni kwa namna gani Danieli na marafiki zake walibarikiwa kwa kufuata sheria za Baba wa Mbinguni kuhusu nini cha kula? (Ona Danieli 1:15, 17, 20.)

  • Ni vyakula gani vyenye kukupa afya unavyokula wewe?

  • Ni kwa nini unapaswa kula vyakula vya kukupa afya wewe?

  • Je, unajisikiaje wewe unapokula vyakula ambavyo ni vizuri kwako?

Elezea kwamba sisi pia tunahitaji kufanya mambo mengine ambayo yatafanya miili yetu kuwa na afya bora na nguvu.

Onyesha picha 1-48, Watoto Wakicheza na Mpira.

  • Watoto hawa wanafanya nini?

  • Kwa nini ni muhimu kuifanyisha miili yetu mazoezi?

  • Ni zipi baadhi ya njia nyingine tunazoweza kufanya mazoezi ya miili yetu?

Weka mikono yako pamoja juu ya upande mmoja wa uso wako na ufunge macho kana kwamba unalala.

  • Mimi ninajifanya nini?

  • Kwa nini ni muhimu kupata usingizi wa kutosha?

Jifanye unanawa mikono yako.

  • Mimi ninajifanya ninafanya nini?

  • Ni wakati gani tunapaswa kunawa mikono yetu?

  • Ni wakati gani tunapaswa kuoga?

  • Ni wakati gani tunapaswa kupiga mswaki meno yetu?

  • Kwa nini tunahitaji kuwa wasafi?

Jadili kanuni nyingine muhimu za afya, kama kuvaa ipasavyo kwa kila hali ya hewa, kudumisha tabia nzuri za kiusalama, na kupata hewa safi.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuilinde miili yetu.

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka tuilinde miili yetu kutokana na madhara na majeraha. Waulize watoto kuhusu hatari wanazoweza kukumbana nazo, ukitumia maswali yafuatayo au ubuni yako mwenyewe.

  • Ni nini kinaweza kutokea kama utachezea kiberiti?

  • Ni nini kinaweza kutokea kama utacheza mtaani au karibu na magari?

  • Ni nini kinaweza kutokea kama wewe si makini na vitu ambavyo vina ncha kali kama vile visu na mikasi?

  • Kwa nini tunajifunga mkanda tunaposafiri ndani ya gari?

Elezea kwamba sisi tunahitaji kuilinda miili yetu. Hatupaswi kufanya mambo ambayo ni hatari kwa miili yetu na yanaweza kuidhuru. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tujisikie kuwa tuko salama na wenye furaha. Wanatutaka tuitunze miili yetu ili tuwe na afya nzuri.

Ushuhuda

Toa hisia zako za shukrani kwa ajili ya mwili wako wa nyama na mifupa. Onyesha shukrani zako kwamba watoto wanaitunza miili yao ili waweze kuwa na afya nzuri na nguvu.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Imba ”Do As I’m |Doing” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 276), au “Hinges” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 277) na kufanya vitendo kama inavyopedekezwa na maneno. Waambie watoto jinsi ulivyo na shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya mwili ambao unaweza kufanya mambo mengi.

  2. Lete picha ya vitu aina mbali mbali vya kuliwa na kunywa. Acha watoto waamue kama kitu ni kizuri au kibaya kwa miili yao. Elezea kwamba baadhi ya vitu ni vizuri, lakini si vizuri tukivitumia kwa wingi. Kwa mfano, peremende ni tamu, lakini zikitumiwa kwa wingi zitatufanya tuumwe. Onyesha picha za vitu vizuri kwa watoto ili wavione.

  3. Katika mfuko au sanduku, lete vitu fulani ambavyo hutusaidia kutunza miili yetu. Jumuisha kitu ambacho hutusaidia kuwa wasafi, kama vile sabuni, kitambaa cha kuogea, au taulo ndogo, au mswaki. Jumuisha kitu kizuri cha kuliwa, blangeti ndogo kuwasilisha kulala, na kitu cha kuwasilisha mazoezi, kama vile mpira mdogo. Wape watoto vidokezo kuhusu kitu kimoja na uwaache wabahatishe ni kitu gani. Waonyeshe kitu hicho wanapobahatisha kwa usahihi. Endelea mpaka kila kitu kimefichuliwa.

  4. Waambie watoto wasimame na kufanya igizo la kuweka miili yao safi na nadhifu. Acha wajifanye wananawa mikono, kupiga mswaki, na kuchana nywele zao. Kisha uwaache wafanye igizo la njia waipendayo ya kufanya mazoezi, kama vile kuruka kichura, kurukaruka, kuruka kamba, au kurusha mpira.

  5. Zungumza na watoto kuhusu jinsi baadhi ya watu wanavyofanya mambo mabaya na miili yao. Hatupaswi kuwakejeli watu hawa, kuwanyoshea vidole au kuwacheka. Zungumza kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea watu walio na ulemavu wa kimwili (kuzungumza nao, kufanya urafiki nao, kuwachukulia kawaida, kuwasaidia kama wanahitaji msaada).

  6. Acha kila mtoto achore picha yake mwenyewe. Andika kila karatasi Nashukuru kwa ajili ya mwili wangu.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga, na uwaache watoto wazungumze kuihusu.

    • Je, wewe umewahi kuwa mtoto mchanga ?

    • Watoto wachanga wanaweza kutembea au kusema?

    Wakumbushe watoto kwamba wao wakati fulani walikuwa watoto wachanga, lakini sasa miili yao umekua na inaweza kufanya mambo mengi. Kadiri miili yao inavyozidi kukua, ndivyo watakavyoweza kufanya hata zaidi.

    Onyesha picha 1-16 Kuzaliwa kwa Yesu, na wakumbushe watoto kwamba hata Yesu alikuwa mtoto mchanga wakati mmoja.

  2. Onyesha kwa kidole mdomo wako na useme, “Huu ni mdomo wangu.” Kisha uliza “Je, unaweza kunionyesha mdomo wako?” na wasaidie watoto kuonyesha midomo yao. Rudia kwa ajili ya macho, pua, masikio, mikono, na miguu. Kisha onyesha kila sehemu ya mwili bila kusema jina lake na uwaache watoto waitaje. Ikiwa watoto wanaweza kutaja sehemu hizi zote, unaweza pia kuwauliza majina ya sehemu za mwili zisizojulikana sana na watoto, kama vile viwiko, magoti, vifundo na visigino.

  3. Buni hadithi rahisi kuhusu mtoto mdogo katika eneo lako. Elezea juu ya mtoto akiamka asubuhi, akivaa nguo, akila kifungua kinywa, na vinginevyo vya siku yote. Unapozungumza kuhusu kila shughuli, muulize mtoto ni sehemu gani za mwili mtoto anatumia.

  4. Acha watoto wasimame na kuimba maneno yafuatayo kwa tuni ya “Once There Was a Snowman” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 249). Tumia vitendo vya kuchuchumaa kwa mstari wa kwanza na vitendo vya kujinyoosha kwa mstari wa pili.

    Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mchanga, mchanga,

    Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mdogo, mdogo, mdogo.

    Sasa ninakuwa mkubwa, mkubwa, mkubwa,

    Sasa ninakuwa mkubwa, mrefu, mrefu, mrefu!