Somo la 46
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismasi)
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuhisi shukrani kwa ajili ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mathayo 2:1–12 na Luka 1:26–35; 2:1–20.
-
Tafuta utondoti rahisi mchache juu ya kuzaliwa kwa watoto walio katika darasa lako, kama vile walizaliwa wapi, walikuwa na nywele za rangi gani, na waliishi wapi wiki ya kwanza ya maisha yao. Uwe mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote walioasiliwa.
-
Kata papi za karatasi (takribani 8” urefu na 11/2” upana) kwa ajili ya kutengeneza minyororo ya Krismasi. Kata papi za kutosha kutengeneza mnyororo mfupi kwa kila mtoto.
-
Andika taarifa fupi ukielezea kuhusu mnyororo wa Krismasi (tazama somo) kwa wazazi wa kila mtoto, ili wamhimize mtoto wao kufanya matendo ya ukarimu.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Mandhari madogo ya kuzaliwa kwa Yesu. Ukitaka waweza kutumia mwanasesere aliyefunikwa kwa blangeti, akiwa amelala kwenye kisanduku kidogo. Kata nyota kutoka kwenye karatasi na uitundike kwenye mandhari ya kuzaliwa kwa Yesu. Kama mandhari hayawezi kupatikana, tumia picha 1‑75, Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 200; 62116).
-
Krayoni rangi na gundi.
-
Picha 1‑75, Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Sanaa za Picha za Injili 200; 62116); picha 1‑76, Hamna Chumba katika Nyumba ya Wageni (62115); picha 1‑77 Matangazo ya Kuzaliwa kwa Kristo kwa Machungaji (Sanaa za Picha za Injili 202; 62117); picha 1‑78, Mamajusi (Sanaa za Picha za Injili 203; 62120).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwaalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Tunasherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo wakati wa Krisimasi
Elezea kwamba kwa vile huu msimu wa Krismasi, tunasherekea kuzaliwa kwa mtu ambaye sisi wote tunampenda.
-
Ni kuzaliwa kwa nani ambako sisi tunasherekea?
Zawadi yetu kwa Yesu ni kuwa kama Yeye
Elezea kwamba kila Krismasi tunaposherekea kuzaliwa kwa Yesu, tunaweza kumpa zawadi. Hatuwezi kutoa dhahabu, uvumba, na manemane kama mamajusi, lakini tunaweza kutoa aina nyingine ya zawadi. Tunampatia Yesu zawadi wakati tunapojaribu kuwa kama Yeye. Tunakuwa kama Yesu wakati tunapokuwa wakarimu kwa familia na marafiki zetu.
Shughuli zenye Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Simulie tena hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu wakati watoto wakiigiza sehemu za Yusufu, Mariamu, Mwenye nyumba ya wageni, wachungaji, na mamajusi. Tumia viwakilishi kama vile mtoto mwanasesere, blangeti dogo, na mtandio, kama vinaweza kupatikana. Mpe kila mtoto nafasi ya kushiriki. Ukitaka unaweza kurudia shughuli hii, kwa kuwaruhusu watoto wachukue nafasi tofauti.
-
Wasaidie watoto kukata au kuchora mapambo ya nyota rahisi. Acha watoto wapake rangi mapambo yao, na kuunga kwa uzi kila nyota ili mtoto aweze kutundika mahali fulani nyumbani mwao.
-
Jadili baadhi ya maandalizi ya kibiashara kwa ajili ya Krismasi ambayo watoto wameyaona. Wasaidie kuelewa kwamba vitu kama vile zawadi na karamu hufurahisha, lakini Krismasi hasa ni juu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo na umuhimu wa kulenga juu yake Yeye na maisha Yake.
-
Jadili desturi za kawaida katika eneo lenu ambazo Kristo - ndiye kitovu chake ambazo wewe unapendelea au unazifahamu. Waalike watoto wazungumze kuhusu tamaduni ambazo Kristo -ndiye kitovu chake ambazo familia zao hufurahia wakati wa Krismasi.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Acha watoto wajifanye kuwa wachungaji wanaopumzika malishoni. Wasadie kuigiza wakionyesha hofu ambayo wachungaji waliona wakati walipomwona malaika, kisha furaha waliojisikia wakati walipoelewa taarifa hizo. Wasaidie kufikiria kuwasikia malaika wakiimba na kulitazama anga maridadi la usiku na kuiona nyota ile. Wakitembea pamoja chumbani wakimtafuta mtoto. Wakipiga magoti mbele za mtoto Yesu katika hori, na kuimba wimbo wa sifa.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mstari ufuatao unaposema maneno haya:
Mtoto katika hori (pembeza mikono kama vile kumbembeleza mtoto),
Mama mwenye upendo karibu (mikono ya kupokea),
Nyota iking’aa mbinguni (hali ya kushangaza angani),
Mwana wa Mungu yu hapa (kupiga makofi ya shangwe)!
-
Imba au mseme maneno “Little Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 39, au ”Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 61). Wakumbushe watoto kwamba sisi husherekea kuzaliwa kwa Yesu wakati wa Krismasi.
-
Tengeneza karatasi za kukata za Yesu Kristo kama amefunikwa nguo. Kusanya nyasi kavu, au majani makavu na uyalete kwa watoto ili wayagundishe kuwa “hori” (karatasi ya mraba) Acha watoto wagundishe karatasi ya kukata ya mtoto Yesu juu ya kitanda cha nyasi au majani makavu.