Mkato 1-26, baba; mkato 1-27, mama; mkato 1-28, msichana mdogo; mkato 1-29, mvulana umri wa mmisionari (mikato kama hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha ya Msingi seti 1).
Picha 1-10, Maombi ya Familia (62275); picha 1-15, Kubariki Chakula; picha 1-44, Yesu Akifundisha katika Ulimwengu wa Magharibi (Picha za Sanaa za Injili 316; 62380).
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuombe pamoja na familia zetu
Tunaweza kuwa na maombi ya familia kila siku
Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka tuombe pamoja na familia zetu kila asubuhi na kila usiku. Kwa kawaida baba au mtu aliye na majukumu ya familia anaweza kumchagua mtu yeyote aombe. Mtu yeyote katika familia anaweza kutoa maombi ya familia.
Tunaweza kuomba na familia zetu wakati gani?
Ni nani anayeweza kuomba?
Tunapokea baraka nyingi kwa kuomba pamoja kama familia
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
Fanya mstari wa shughuli ufuatao pamoja na watoto:
Huyu ni mama yangu, ambaye hunisaidia kucheza (inua kidole cha kwanza);
Huyu ni baba yangu, ambaye hufanya kazi siku nzima (Inua kidole cha pili).
Huyu ni kaka yangu, mwenye nguvu na mrefu (inua kidole cha tatu);
Huyu ni dada yangu, ambaye anapenda kucheza mpira (inua kidole cha nne).
Na huyu ni mimi; nina furaha kusema (onyesha kidole gumba)
Kwa Pamoja familia yetu hupiga magoti kuomba (funga ngumi).
Rusha au peana kitu laini kama vile kijifuko cha maharagwe au mpira kwa watoto, mmoja mmoja. Baada ya watoto kishika chombo, waulize wataje jina la kitu wanachoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili yake wakati wanapoomba maombi ya familia. Baada ya kila mtoto kupata zamu, rudia shughuli hii, watoto wakitaja mambo wanayoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili yake wanapoomba maombi ya familia.
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi na krayoni au penseli. Acha watoto wachore picha inayoonyesha familia yao ikiomba. Andika kila picha Nina furaha familia yangu inapoomba pamoja.
Imbeni au semeni maneno ya “A Song of Thanks” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20) au “A Prayer Song” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk.22).
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
Wasaidie watoto kurudia aya hii, mstari kwa mstari:
Tunampenda Baba wa Mbinguni.
Tunamshukuru tunapoomba.
Baba wa Mbinguni anatupenda;
Yeye husikia maneno tunayosema.
Simulia hadithi ya familia ikiomba pamoja na kupokea msaada uliohitajika. Kwa mfano, familia inaweza kupotea njia na kisha wakaipata; wanaweza kupoteza kitu fulani na kisha kukipata; mtu fulani katika familia anaweza kuwa anaumwa na kisha kujisikia vyema. Pendekeza kwamba hata zaidi ya kuomba kwa ajili ya msaada, familia zinapaswa kutoa maombi ya shukrani baada ya kupokea msaada waliohitaji. Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu hufurahia tunapowashukuru kwa ajili ya baraka wanazotupa.
Imbeni au semeni maneno ya aya ya kwanza na ya tatu ya “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20).