Somo la 6
Baba wa Mbinguni na Yesu Wananipenda Mimi
Madhumuni
Ni kumsidia kila mtoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanampenda kila mmoja wetu.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Marko 10:13–16; na Yohana 3:18; na 3 Nefi 17:11–12, 21-24.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia na Kitabu cha Mormoni
-
Kioo kidogo.
-
Picha 1-1, Ulimwengu (62196);Picha 1-3, Yesu Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 240; 62572); picha 1-4, Ono la Kwanza (Sanaa ya Picha za Injili 403; 62470);Picha 1-19, Kristo na Watoto (Sanaa ya Picha za Injili 216; 62467); picha 1-20, Yesu Akiwabariki Watoto Wakinefi.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo hutupatia baraka
Wakumbushe watoto kwamba kabla ya kuja duniani, tuliishi pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wao walipanga sisi tuje duniani ili tuweze kujifunza na kukua. Wanatujua na wanatujali.
Onyesha picha 1-1, Ulimwengu.
-
Baba wa Mbinguni alimwomba Yesu aumbe nini kwa ajili yetu?
Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu waliumba dunia na kila kitu kilichopo ndani yake. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu walipanga vitu vyote tunavyohitaji ili tuishi na kuwa na furaha. Vitu hivi vinatukumbusha sisi juu ya upendo wao kwetu.
-
Ni vitu gani vinakukumbusha wewe juu ya upendo wa Baba wa Mbinguni kwako? (Majibu yanaweza kujumuisha vitu kama vile familia, marafiki, Kanisa, mimea, na wanyama.)
Yesu alionyesha upendo wake kwa watoto
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanampenda kila mmoja wetu
Wasaidie watoto kuelewa jinsi kila mmoja wao alivyo muhimu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanampenda kila mmoja wetu na wanatujua kwa jina.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.
-
Imbeni au semeni maneno ya “Jesus Is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 58). Mpe kila mtoto nakala za kitini cha “Jesus is Our Loving Friend,” kama inayopatikana (mwishoni wa somo) na acha watoto wapake rangi vitini vyao.
-
Imbeni ua semeni maneno ya “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 5) au “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.74).
-
Onyesha picha za vitu ambavyo Baba wa Mbinguni na Yesu wametupatia, kama vile hekalu, wanyama, maua, familia, chakula, nyumba, majumba ya mikutano, au maandiko. (Picha zinaweza kupatikana kutoka maktaba ya jumba la mikutano, Sanaa ya Picha za injili, au magazeti ya Kanisa. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wametupatia vitu hivi kwa sababu wanatupenda.
-
Leta kitu, kama vile chupa ya kinywaji tupu, ambayo inaweza kuzunguka kama mshale. Wakalishe watoto chini katika duara na uweke chupa katikati ya duara. Zungusha chupa sakafuni. Wakati inamlenga mtoto, mtoto yule anapaswa kusema kitu ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu wametupa ambacho kinaonesha upendo wao kwetu. Msaidie kila mtoto kufikiria jibu inapofika zamu yake. Baada ya mtoto kujibu, acha azungushe chupa ili imlenge mtoto mwingine.
-
Andaa sanduku au mfuko ambao una vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kwetu ili kuishi duniani, kama vile chakula, maji, au nguo. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu waliipanga dunia hii kwa ajili ya sisi kuishi ndani yake. Elezea kwamba sanduku au mfuko una baadhi ya vitu ambavyo tunavihitaji ili kuishi duniani. Wape watoto vidokezo kuhusu kitu kimoja na mpaka wabahatishe ni nini. Wanapobahatisha ni nini, kitoe kutoka kwenye sanduku au mfuko. Endelea na mchezo mpaka watoto wabahatishe vitu vyote.
-
Tengeneza beji ambayo inasema Baba wa Mbinguni na Yesu Wananipenda kwa kila mtoto ili avalie au achukue nyumbani. Unaweza kunganisha beji kwa mtoto au kuunga kamba kwenye beji na kumvisha mtoto shingoni. Unaweza kuzificha beji chini ya viti vya watoto kabla ya darasa na kuwaacha watoto wazitafute.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wasaidie watoto kusema maneno na kufanya vitendo vya mstari ufuatao.
Kama wewe ni mrefu, mrefu sana (jinyoshe na mikono juu sana)
Kuna nafasi kanisani kwa ajili yako.
Kama wewe ni mdogo, mdogo sana (chuchumaa chini),
Kuna nafasi kanisani kwa ajili yako.
Mrefu (jinyoshe)
Mdogo (chuchumaa)
Mrefu (jinyoshe)
Mdogo (chuchumaa)
Baba wa Mbinguni na Yesu Wanatupenda wote.
-
Semeni mstari ufuatao na wasaidie watoto kufanya vitendo vinavyoelezwa:
Baba wa Mbinguni Ananijua
Baba wa Mbinguni ananijua (jiote mwenyewe)
Na kile mimi ninapenda kufanya.
Yeye anajua jina langu na pale ninapoishi (tengeneza paa kwa kugusanisha vidole vya mikono yote).
Mimi najua ananipenda, pia (pitisha mikono na uweke mikono nyuma ya mabega kama kumbatio).
Yeye anajua kile kinachonifanya kuwa na furaha (weka vidole kwenye mdomo unao tabasamu).
Yeye anajua kile kinachonifanya kuwa na huzuni. (weka vidole kwenye mdomo uliogueza kwenda chini).
Mimi najua anataka kunisaidia (jionyeshe mweyewe);
Na hiyo inanifanya nisikie furaha!