Somo la 2
Baba wa Mbinguni Ana Mwili
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni ni mtu halisi, ana mwili kamili wa nyama na mifupa, na kwamba tumeumbwa kwa mfano Wake.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Yohana 14:9; Mafundisho na Maagano 130:22; Musa 2:27; na Joseph Smith—Historia 1:14–17. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 1.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia na Lulu ya Thamani Kuu.
-
Karatasi na krayoni kwa kilia mtoto.
-
Kioo kidogo.
-
Picha 1-3, Yesu Kristo (Picha za Sanaa za Injili 240; 62572); picha 1-4, Ono la Kwanza (Picha za Sanaa za Injili 403; 62470);
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Yesu Kristo yu kama Baba wa Mbinguni
Waulize watoto kama mtu yeyote amekwisha waambia kuwa wanafanana na wazazi wao. Onyesha picha1-3, Yesu ndiye Kristo, na uelezee kwamba Yesu ni Mwana wa Baba wa Mbinguni. Maandiko yanatuambia kwamba Yesu anafanana na Baba wa Mbinguni. Fungua Biblia na uelezee Yohana 14:9 kwa watoto.
-
Yesu anafanana na nani?
Sisi tunafanana na Baba wa Mbinguni na Yesu
Elezea kwamba kwa sababu sisi ni watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni, pia tunafanana naye. Tuna mwili kama wake. Elezea Musa 2:27 kwa watoto. Elezea kwamba kuumbwa katika mfano wa Baba wa Mbinguni humaanisha kwamba tunafanana naye.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.
-
Acha watoto wasimame na kusema mstari wa shughuli mara kadhaa, wakitumia vitendo vilivyoelezwa
Mimi Nina Mwili wa Ajabu
Mimi nina mwili wa ajabu (gusisha mikono kwenye kufua)
Baba wa Mbinguni aliupanga kwa ajili yangu.
Yeye alinipa masikio ili niweze kusikia (kunja kiganja sikioni)
Na macho ili niweze kuona (onyesha macho).
Mimi nina mikono miwili ambayo naweza kupiga makofi (piga makofi),
Miguu miwili ambayo inaweza kugeuka (geuka).
Nikitaka, naweza kugusa.
Vidole chini sakafuni (inama kugusa visole).
Ninapofikira kuhusu mwili wangu (weka kidole kichwani),
Sehemu yake bora ni (keti chini pole pole)
Baba wa Mbinguni aliipanga kwa ajili yangu.
Uweze kufanana sana na wake.
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno ya “I Have Two Ears” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 269) au “Head, Shoulders, Knees, and Toes” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.275). Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni alitupatia miili kama yake na kwamba miili hii ya ajabu inaweza kufanya mambo mengi.
-
Acha watoto wafanye zamu kutumia picha 1-4, Ono la Kwanza, ili wasimulie hadithi ya Ono la Kwanza kwa darasa lote.
-
Waambie watoto kuhusu upendo wako kwa watu wa familia yako.
Baba ya Marc alifariki Marc alipokuwa mtoto mchanga. Marc mara nyingi alishangaa baba yake alifananaje ? Yeye na mama yake walikuwa wanaenda kwenye shughuli ya familia ambapo angekutana na shangazi zake na wajomba zake ambao walimjua baba yake vyema.
Walipowasili, Mjomba Joe akaja kuwasamilia. Akamtazama Marc na kusema, “Mimi naweza kukutambua po pote. Una macho ya baba yako. “Shangazi Elizabeth alisema, “Unajua kitu Marc, una pua kama tu ya baba yako.” Shangazi Mary alisema, “Marc tabasamu lako linanikumbusha tabasamu la baba yako.”
Walipokuwa wakirudi nyumbani, Marc alimwambia mama yake, “Leo nimefurahi kweli! Nimejifunza mambo wengi kuhusu baba yangu leo. Nimejifunza kwamba mimi ninafanana naye, na hiyo inanifanya niwe na furaha! Sasa ninapotazama katika kioo, nitakumbuka yeye anafananaje, na sitamsahau.” Mama ya Marc akamjongelea, akaupiga mkono wa Marc kikofi, na kusema, “Wewe ukiwepo, mimi pia sitamsahau.”
Waambie watoto kama vile tu Marc alivyojua kwamba alifanana na baba yake ingawa hakuweza kumwona, tunajua kwamba sisi tunafanana na Baba yetu wa Mbinguni japo kuwa hatuwezi kumwona.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Onyesha picha 1-4, Ono la Kwanza. Simulia aina rahisi ya hadithi ya Ono la Kwanza. Sisitiza kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni watu halisi na wao husikia maombi yetu.
-
Onyesha picha 1-4, Ono la Kwanza, na uonyeshe jinsi miili yetu inavyofanana na ya Baba wa Mbinguni na Yesu. Unapoonyesha kila sehemu ya mwili katika picha, acha watoto waonyeshe sehemu inayolingana kwenye miili yao wenyewe. Kwa mfano, kama ukionyesha mkono wa Baba wa Mbinguni, watoto wanapaswa kuonyesha mikono yao.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari wa shughuli ufuatao unaposema maneno:
Joseph alipiga magoti mitini (piga magoti na ukunje mikono)
Na akasema maombi maalum (gusisha ncha za vidole kwenye midomo).
Yeye alimwona Baba na Mwana (tazama juu, upanguse macho kwa mikono)
Na hapo aliwasikiliza (kunja kiganja sikioni).
-
Onyesha mdomo wako na useme , “Huu ni mdomo wangu.” Kisha uliza “Unaweza kunionyesha mdomo wako?” na wasaidie watoto kuonyesha midomo yao wenyewe. Uliza, “Je, Baba wa Mbinguni ana mdomo?” Rudia macho, pua, masikio, mikono, na miguu. Kisha onyesha kila sehemu ya mwili bila kusema jina lake na uwaache watoto waitaje.