Somo la 5
Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kujua kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mathayo 3:13–17 na Luka 1:26–35; 2:1–7, 41–52. Tazama pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 3.
-
Kwa idhini ya rais wako wa Msingi, mwalike baba wa mmoja wa watoto aje darasani na kuzungumza kuhusu mtoto wake alipokuwa mtoto mchanga. Muombe alete picha na mwanasesere kipenzi, kama inawezekana. Mhimize yeye aelezee upendo wake kwa mtoto wake.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Picha 1-16, Kuzaliwa kwa Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 201; 62495); picha 1-17, Mvulana Yesu Hekaluni (Sanaa ya Picha za Injili 205; 62500); Picha 1-18, Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu; (Sanaa ya Picha za Injili 208; 62133).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Taarifa kwa mwalimu: Unapozungumza kuhusu akina baba katika somo hili, uwe mwangalifu kwa hisia za watoto katika darasa lako ambao hawana baba nyumbani mwao. Sisitiza kwamba sisi wote tuna Baba wa Mbinguni ambaye anatupenda. Ikiwa baadhi ya watoto katika darasa lako wana baba wa kambo, elezea kwamba baba wa kambo pia wanatupenda na wanatujali sisi.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Yesu Kristo ni mwana wa Baba wa Mbinguni
Waambie watoto kwamba kila mmoja wao ana baba wawili: baba wa duniani na Baba wa Mbinguni. Baba wa duniani ni baba wa miili yetu. Baba wa Mbinguni ni baba wa roho zilizo ndani ya miili yetu. Yesu ana baba mmoja tu, kwa sababu Baba wa Mbinguni ndiye baba wa roho, na wa mwili wake. Hiyo ndiyo sababu Yesu anaitwa Mwana wa Mungu.
Yesu anampenda Baba wa Mbinguni na anamtii yeye
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Weka picha tatu kutoka kwa somo hili, zikitazama chini kwenye paja lako au mezani. Mwalike mtoto achague mojawapo ya picha hizi, ionyeshe kwa darasa, na usimulie hadithi inayoonyeshwa katika picha hiyo. Fanya vivyo hivyo kwa zile picha zingine mbili.
-
Acha watoto waimbe au kusema maneno ya mstari wa kwanza wa “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 57).
-
Acha watoto wafanye igizo la hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu, mkitumia vitu rahisi kama vile mwansesere, shali, na skafu.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Onyesha picha 1-16, Kuzaliwa kwa Yesu, na waulize watoto huyu mtoto mchanga ni nani. Wasimulie kuhusu kuzaliwa kwa Yesu.
Elezea kwamba Yesu si mtoto mchanga bado. Sasa ni mtu mzima, na yeye ni msaidizi muhimu sana wa Baba wa Mbinguni. Onyesha picha1-3, Yesu ndiye Kristo, na uwaelezee watoto kwamba Yesu anatupenda na hutusaidia kwa njia nyingi.
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno yafuatayo kwa tuni ya “Once There Was a Snowman” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 249). Wakitumia vitendo vya kuchuchumaa kwa mstari wa kwanza na vitendo vya kujinyoosha kwa mstari wa pili.
Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mchanga, mchanga,
Wakati mmoja nilikuwa mtoto mchanga, mdogo, mdogo, mdogo.
Sasa ninakua mkubwa, mkubwa, mkubwa,
Sasa ninakuwa mkubwa, mrefu, mrefu, mrefu!
-
Zungumza na wazazi wa washiriki wa darasa lako mapema ili upate picha za washiriki wa darasa lako wakiwa watoto wachanga au wanasesere wadogo ambao walizoea kucheza nao. Onyesha vitu hivi kwa darasa. Mtambue mtoto mchanga katika kila picha au mmiliki wa kila mwanasesere. Elezea kwamba walipokuwa watoto wachanga walikuwa wanaonekana kama vile picha hizi na walicheza na wanasesere .