Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 11: Ninashukuru kwa ajili ya Samaki


Somo la 11

Ninashukuru kwa ajili ya Samaki

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuhisi shukrani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa ajili ya samaki na wanyama wa majini.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:20–23; Yona 1–3; na Mathayo 14:15–21; na Luka 5:1–11.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Samaki wa karatasi (ona mpangilio huko mwisho wa somo).

    3. “Ufito wa kuvua samaki”—fimbo iliyo na uzi uliofungwa na kilipu ya karatasi, kipande cha mshipi wa gundi, au sumaku aliyoungwa huko mwisho wa uzi. (Hifadhi fito hii kwa matumizi katika masomo yafuatayo.)

    4. Chombo cha kuwekea samaki wa karatasi.

    5. Kama inawezekana, tutafuta picha za samaki au wanyama wengine ambao huishi majini.

    6. Mkato 1-5, samaki, (mkato unaofanana na hiyo pia unaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha za Watoto wa Msingi seti ya 4).

    7. Picha 1-1, Ulimwengu (62196); picha 1-24, Yesu na Wavuvi (Picha za Sanaa za Injili 210; 62128); picha 1-25, Samaki; picha 1-26, Chura; picha 1-27, Kasa.

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Acha watoto wajifanye wamesimama darajani wakitazama mtoni au ziwani.

  • Unaona nini unapotazama ndani ya maji?

Acha watoto wasimame na kujifanya wanaogelea ndani ya maji kama samaki.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo waliumba samaki na wanyama wengine wa majini

Onyesha picha 1-1, Ulimwengu, na rejea baadhi ya vitu ambavyo Baba wa Mbinguni alimwomba Yesu aumbe vile vilivyozungumzwa katika masomo yaliyopita. Waambie watoto kwamba pia Yesu Kristo iliumba samaki (ona Mwanzo 1:20–23). Samaki ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwa dunia. Onyesha picha 1-25, Samaki na uzungumzie kuhusu pale samaki anapoishi.

  • Je, umeshawahi kuwaona samaki?

Acha watoto waelezee kuhusu samaki ambao wameshaona.

Onyesha mkato 1-5 na picha yoyote ya samaki uliyopata. Zungumza kuhusu aina mbali mbali za samaki, kama vile samaki kidhahabu, trauti, jodari, papa, au samaki yeyote anayefahamika na watoto darasani.

  • Ni wanyama gani wengine waoishi majini licha ya samaki?

Onyesha picha 1-26, Chura, na picha 1-27, Kasa. Zungumza kuhusu vyura na kasa na pale wanapoishi. Pia zungumza kuhusu nyangumi, kaa, sili, na wanyama wengine wa majini. Elezea kwamba baadhi ya wanyama wa majini huishi baharini, wengine katika maziwa, na wengine katika mito.

Shughuli

Msaidie kila mtoto kufikiria juu ya mnyama wa majini na ajifanye anatembea, kuruka, au kuogelea anavyoogelea.

Hadithi

Inua Biblia, na ueleze kwamba tunaweza kusoma kuhusu samaki katika maandiko. Simulia hadithi ya Yona, kama inavyopatikana katika Yona 1–3. Elezea kwamba Yesu aliandaa samaki mkubwa ili amumeze Yoha ili Yona asizame majini. Yesu alikuwa na kazi ya kufanywa na Yona. Unaweza kutaka kusoma kwa sauti mstari mmoja au miwili, kama vile Yona 1:17 au Yoha 2:1, na usimilie hadithi hii. (Kama unasoma mstari kwa sauti elezea kwamba Yesu wakati mwingine anaitwa “Bwana.”

  • Ni nani alimtuma Samaki amumeza Yona? (Ona Yona 1:27.)

  • Yona alifanya nini alipomezwa na samaki? (Ona Yona 2:1).

  • Yona alifanya nini alipotoka tumboni mwa samaki? (Ona Yona 3:1-3.)

  • Je, watu walimwamini Yona na kutubu? (Ona Yona 3:5, 10.)

Waambie watoto kwamba baadhi ya samaki ni wakubwa sana, kama yule samaki aliyemmeza Yona, na wengine ni wadogo sana na wanaweza kuishi katika bakuli.

Shughuli

Wasaidie watoto kufanya mchezo wa vidole ufuatao:

Samaki Kidhahabu

Kipenzi changu samaki kidhahabu kidogo hakina vidole (gusa vidole).

Yeye huogelea bila sauti na kugonga pua yenye njaa (onyesha pua).

Yeye hawezi kutoka nje nikacheza naye wala siwezi kuingia ndani kuogelea (fanya vitendo vya kuogelea).

Na ninaposema, “Toka nje tucheze,”

Yeye anaonekana kusema, “Njoo ndani,” (kitendo cha “njoo ndani” kwa mkono).

Hadithi

Onyesha Biblia tena unaposimulia hadithi ya Simioni Petro, kama inavyopatikana katika Luka 5:1–11.

Onyesha picha 1-24 Yesu na Wavuvi, katika wakati ufaao.

  • Kwa nini Yesu aliingia katika mashua ya Simioni Petro? (Ona Luka 5:3.)

  • Yesu alimwambia Simioni Petro afanye nini? (Ona Luka 5:4.)

  • Simioni Petro alivua nini katika wavu wake? (Ona Luka 5:6.)

Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo aumbe samaki na wanyama wa majini kwa matumizi yetu

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu aumbe samaki na wanyama wa majini kwa matumizi yetu ya chakula na madhumuni mengine.

Hadithi

Ukirejea Biblia tena, simulia hadithi inayopatikana katika Mathayo 14:15–21. Ukitaka unaweza kusoma kwa sauti mstari mmoja au miwili, kama vile Mathayo 14:16–17, unaposimulia hadithi.

Shughuli

Onyesha darasa ule ufito wa kuvulia samaki uliouandaa, mwalike mmoja wa watoto aje mbele na kuvua samaki. Weka mkato wa samaki kwenye chombo, na wakati mtoto anaponing’iniza uzi kwenye chombo, unga samaki kwa klipu, gundi, au sumaku na uache mtoto avute nje. Acha kila mtoto apate zamu ya kuvua samaki.

Acha watoto waongee kuhusu uzoefu wa wakati walipoenda kuvua samaki au wa kula samaki.

Ushuhuda

Elezea shukrani zako kwa ajili ya samaki na wanyama wa majini.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.

  1. Acha watoto wapake rangi samaki wa karatasi waliyemvua katika shughuli ya kuvua samaki (rudia shughuli hii kama unapenda). Andika Ninashukuru kwa ajili ya Samaki kwenye nyuma ya samaki wa kila mtoto.

  2. Acha watoto wasimame katika nusu duara. Weka samaki waliopakwa rangi na watoto kwenye sakafu mbele yao. Semeni mstari ufuatao pamoja:

    Samaki mdogo kwenye kijito,

    Ninaweza kukushika bila ndoana.

    Taja mtoto mmoja na acha mtoto huyo achague samaki wake kwa kutumia ufito wa kuvua samaki au kwa kumuonyesha samaki. Mtoto aseme, “Nimevua Mmoja, akisema rangi ya samaki. Kisha mtoto anamchukuwa yule samaki na ampeleke nyumbani. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu moja.

  3. Imbeni au semeni maneno ya “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 20).

  4. Wasaidie watoto kufanya mchezo wa vidole ufuatao: Elezea kwamba minoo ni samaki mdogo sana.

    Kasa Mdogo

    Mimi nina kasa mdogo.

    Anaishi katika sanduku (kunja mikono).

    Anaogelea mtoni (fanya vitendo vya kuogelea),

    Hupanda juu ya miamba (tembeza vidole juu mwendo wa kupanda juu).

    Aling’wafua minoo (piga makofi)

    Aling’wafua kiroboto (piga makofi),

    Aling’wafua mbu (piga makofi),

    Na alining’wafua mimi (piga makofi)!

    Alimshika minoo (piga makofi);

    Alimshika kiroboto (piga makofi);

    Alimshika mbu (piga makofi),

    Lakini hakunishika mimi!

    (Vachel Lindsay, kutoka Collected Poems of Vachel Lindsay. © 1920 na Macmillan Publishing Co., Inc., renewed 1948 na Elizabeth C. Lindsay. Imetumika kwa Idhini.)

  5. Wasaidie watoto kusema maneno ya shuguli ifuatayo: Elezea kwamba kijito ni mto mdogo na daka ni sehemu mafichoni.

    Samaki Watano Wadogo

    Acha watoto watano wasimame mbele ya darasa, kila mmoja akishikilia samaki wa karatasi.

    Samaki watano walikuwa wanaogelea katika kijito.

    Mmoja akaogelea mbali kwenye daka la siri (mtoto mmoja “anaogelea’ kurudi kwenye kiti chake).

    Samaki wadogo, samaki wadogo, wanafurahia kucheza,

    Samaki wadogo, samaki wadogo, wanaogelea siki nzima.

    Imba mstari mwingine na samaki wanne, kisha watatu, kisha wawili. Mtoto mmoja anaogelea mbali kila mstari. Wakati mtoto mmoja anapobakia, tumia mstari ufuatao:

    Samaki mmoja mdogo alikuwa anaogelea katika kijito;

    Akaogelea mbali kwenye daka la siri.

    Samaki wadogo, samaki wadogo, wanafurahia kucheza,

    Samaki wadogo, samaki wadogo, wanaogelea siku nzima.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Onyesha picha 1-25, Samaki; picha 1-26, Chura; na picha 1-27, Kasa. Kwa maneno yako mwenyewe, simulia hadithi ya uumbaji wa samaki na wanyama wa majini (ona Mwanzo 1:20–23). Elezea shukrani zako kwa ajili ya samaki na wanyama wa majini.

  2. Waambie watoto kwamba wanyama wengi wanaishi majini au karibu na maji. Acha wao wabahatishe ni mnyama gani unayemfikiria unapowapa vidokezo:

    1. Ngozi yangu ni kijani na laini na telezi. Mimi huruka. Mimi huishi karibu na maziwa, vijitoni, au vidimbwini. Unaweza kubahatisha mimi ni nani?

      (Watoto wanapokuwa wamebahatisha ni “chura,” onyesha picha 1-26, Chura, au chora chura ubaoni.)

    1. Mimi ni mwenda pole pole sana. Hubeba gamba gumu mgongoni mwangu. Ninapotishiwa, huvuta kichwa changu, mikono, na miguu yangu ndani ya gamba langu. Mimi ni nani?”

      (Watoto wanapokuwa wamebahatisha ni “kasa,” onyesha picha 1-27, Kasa, au chora kasa ubaoni.)

    Baada ya watoto kubahatisha wanyama wote wawili, acha wao waruke kama vyura; kisha acha watambae pole pole kama kasa.

  3. Imba pamoja na watoto “Oh, What Do You Do in the Summertime?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk, 245).

Chapisha