Somo la 12
Ninashukuru kwa ajili ya Wanyama
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuwa na shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya wanyama.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:24–25 na Mwanzo 6:5–8; 19.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Mikato 1-6 hadi 1-19 (mikato inayofanana na hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha vya Msingi seti ya 4, na 5).
-
Picha 1-28, Uumbaji—Viumbe Hai (Picha za Sanaa za Injili 100; 62483); picha 1-29, Kujenga Safina (Picha za Sanaa za Injili 102; 62053);picha 1-30, Nuhu na Safina Ikiwa na Wanyama (Picha za Sanaa za Injili 103; 62305);
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuwaumba wanyama
Rejea pamoja na watoto kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuumba ulimwengu wetu maridadi, ikijumuisha mchana na usiku, bahari na nchi kavu, na mimea na miti. Onyesha Biblia na uwakumbushe watoto kwamba tunaweza kusoma kuhusu Uumbaji katika kitabu hiki. Elezea kwamba Biblia inatuambia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu waliumba wanyama wote na kuwaweka ulimwenguni.
Onyesha picha 1-28, Uumbaji—Viumbe Hai.
-
Ni nani aliumba vitu unavyoona katika picha hii?
-
Majina ya wanyama walioko katika picha ni gani?
Eleza kwamba Yesu Kristo aliumba wanyama wa kila aina ili wawe ulimwenguni. Baadhi ya wanyama huishi shambani, wengine nyumbani mwetu. Wanyama wengine huishi msituni, wengine milimani, na wengine jangwani. Wanyama wengine huishi katika sehemu za baridi duniani na wengine wanaishi katika sehemu za joto,
-
Ni wanyama gani waishio shambani?
-
Ni wanyama gani wanaoishi msituni, milimani, au jangwani?
-
Unapendelea mnyama gani?
Wanyama hutusaidia
Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu waliwaweka wanyama duniani ili watusaidie. Tunatumia baadhi ya wanyama kama chakula, wengine hutufanyia kazi, na wengine ni wakupendeza kuwatazama au kucheza nao.
-
Je, wanyama hutusaidia vipi?
-
Ni kutoka kwa wanyama gani tunapata chakula, kama vile maziwa, mayai, au nyama?
-
Ni kutoka kwa wanyama gani tunapata bidhaa za nguo?
-
Ni wanyama gani wanapendeza kwa kufugwa?
-
Ni wanyama gani waweza kuendeshwa?
Acha watoto waongee kuhusu uzoefu waliopata kutokana na aina tofauti za wanyama.
Wanyama waliokolewa kutokana na gharika
Simulia hadithi ya Nuhu na Safina, kama inavyopatikana katika Mwanzo 6:5–8:19. Onyesha picha 1-29, Kujenga Safina, na picha 1-30, Nuhu na Safina iliyo na Wanyama. Unaweza pia kutumia maumbo ya mikato kuelezea hadithi.
-
Ni kwa namna gani Nuhu na familia yake walibarikiwa kwa kumtii Yesu?
-
Ni kwa namna gani wanyama waliokolewa?
-
Tunapoona upinde wa mvua, unatukumbusha nini?
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Cheza mchezo “Mnyama, Mnyama, Wewe ni Nani? Acha watoto watengeneze duara. Acha mtoto mmoja asimame katika ya duara na kujifanya kuwa mnyama. Watoto wengine wainue mikono yao ili kubahatisha ni mnyama gani huyu mtoto aliye katikati anamwigiza. Mtoto apobahatisha sahihi, anaingia katika duara na kumwigiza mnyama mwingine. Unaweza kutaka kila mtoto kwanza ukunong’onezee jina la mnyama ataigiza ili kuhakikisha mtoto anawelewa vyema akilini.
-
Cheza mchezo wa “Huyu ni Mnyama Gani? Waache watoto watoe vidokezo kuhusu mnyama fulani. Vidokezo vinaweza kuashiria pale mnyama anapoishi, jinsi alivyo mkubwa, sauti anayotoa, rangi yake, na jinsi huwasaidia watu. Waambie watoto wainue mikono yao wanapofikiria wanajua ni mnyama gani unayemwongelelea. Rudia kwa wanyama tofauti mara nyingi kama upendavyo kufanya.
-
Pamoja na watoto Imbeni au semeni maneno ya “The World Is So Big” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto , 235). Fanya vitendo kama inavyoonyeshwa chini:
Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),
Na ndani yake viumbe vya Mungu hupatikana;
Milima (weka kwa umbo la mlima juu ya kichwa)
Mabonde (weka viganja mbele ya mwili)
Na miti mirefu (nyoosha mikono kwa urefu)
Wanyama wakubwa (ishara ukubwa)
Na wanyama wadogo (ishara ya udogo)
Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),
Mungu anatupenda sisi wote; baraka zetu ni nyingi (kunja mikono na ujikumbatie).
-
Waache watoto waongee kuhusu wanyama wao wa kufugwa walio nao au wale ambao wangependa kuwa nao. Jadili na watoto jinsi tunavyopaswa kuwatendea na kuwatunza wanyama wa kufugwa.
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi na krayoni au penseli. Acha kila mtoto achore picha ya mnyama ampendaye. Andika kwenye kila picha Ninashukuru kwa ajili ya wanyama.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Onyesha picha 1-28, Uumbaji—Viumbe Hai. Kwa maneno yako mwenyewe, simulia hadithi ya uumbaji wa wanyama (ona Mwanzo 1:24–25). Elezea shukrani zako kwa ajili ya wanyama.
-
Chagua wanyama wachache ambao watoto wanawafahamu. Acha watoto wajifanye kuwa kila mnyama. Jadili jinsi wanyama hawa wanavyoonekana na sauti zao zinavyosikika na matumizi yao.
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “All Things Bright and Beautiful (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 231).