Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 31: Ninashukuru kwa ajili ya Nyumba Yangu


Somo la 31

Ninashukuru kwa ajili Nyumba Yangu

Madhumuni

Ni kumtia moyo kila mtoto ahisi shukrani kwa ajili ya nyumba yake na ili asaidie kuitunza.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze 1 Nefi 2:2–6na 17:7–8, 186; na 18:6.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Kitabu cha Mormoni

    2. Chombo cha maji, chombo cha mchanga, na tawi dogo. Kama ukipenda, lete picha za ziwa, mchanga, na mti.

    3. Karatasi, krayoni au penseli.

    4. Picha 1-60, Lehi na Watu Wake Wanawasili Nchi ya Ahadi (Picha za Sanaa za Injili 304; 62045); picha 1-61, Kutoka Nauvoo (Picha za Sanaa za Injili 410; 62493);

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Onyesha chombo au picha ya maji na uliza ni wanyama gani au wadudu gani hufanya makazi yao ndani ya maji. Wasaidie watoto wafikirie juu ya wengi kadiri iwezekanavyo. Onyesha mchanga na kisha tawi, na uwasaidie watoto kufikiria juu ya wanyama na wadudu ambao hufanya makazi yao kwenye ardhi na miti.

  • Unafikiri ingekuwaje kama kila makazi yako yangekuwa majini?

  • Ni nini kingetokea kama makazi yako yangekuwa mtini?

Kuna aina nyingi za makazi tofauti

Waambie watoto kwamba wanyama na wadudu wanaishi katika makazi ya aina nyingi tofauti. Watu wanaishi katika makazi aina nyingi tofauti.

Hadithi

Onyesha picha 1-60, Lehi na Watu Wake Wanawasili Nchi ya Ahadi, na uonyeshe Kitabu cha Mormoni huku ukisimulia kuhusu Lehi na familia yake na aina ya makazi waliyoishi (ona 1 Nefi 2:2–6; 1 Nefi 17:7–8; na 1 Nefi 18:6, 23). Familia ya Lehi ilikuwa na makazi mazuri huko Yerusalemu, lakini wakati Bwana alipowaambia waondoke Yerusalemu, walisafiri nyikani na kuishi katika mahema. Baada ya miaka mingi Bwana alimwamuru Nefi, mwana wa Lehi, ajenge mashua. Lehi na familia yake waliishi katika mashua walipokuwa wakisafiri hadi nchi ya ahadi, mahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu walikuwa wamewaandalia kuishi. Baada ya kuwasili katika nchi ya ahadi, Lehi na familia yake waliishi katika mahema mpaka walipoweza kujenga makazi ya kudumu.

  • Ni nyumba za aina gani tofauti Lehi na watu wake waiishi ndani yake?

Hadithi

Onyesha picha 1-61, Kutoka Nauvoo. Simulia kuhusu waumini wa Kanisa mwanzoni ambao waliishi katika mji ulioitwa Nauvoo. Walifanya kazi kwa bidii kujenga nyumba zao na hekalu maridadi. Lakini baadhi ya watu katika Nauvoo hawakuwapenda waumini wa Kanisa na waliwalazimisha kuondoka. Waumini wa Kanisa walisafiri na mizigo ile tu ambayo ingeweza kutosha katika magari ya mikokoteni iliyofunikwa. Kwa sababu magari ya mikokoteni iliyofunikwa yalikuwa madogo, watoto wengi iliwabidi waache nyuma wanasesere wao. Baadhi ya watu waliishi katika magari yao yaliyofunikwa na katika mahema kwa wakati mrefu.

  • Kwa nini ingekuwa vigumu kuishi katika gari lililofunikwa au hema?

Shughuli

Acha watoto wasimame na kufanya mstari ufuatao wa kitendo:

Watoto watangulizi walitembea na kuongea (tembea mahali pamoja);

Kisha wakacheza michezo na kururuka na kuruka kamba (rukaruka mahali pamoja).

Ilipokuwa usiku, nyota zikang’aa na kumetameta (funga na ufungue mikono);

Ndani ya magari ya kukokotwa walilala na kuota (funga macho, ulaze kichwa mikononi).

Nyumbani ni mahali ambapo tunapendwa

Elezea kwamba aina ya nyumba tunayoishi si muhimu. Tunaweza kuishi katika nyumba kubwa, nyumba ndogo, ghorofani, hema, au mashua. Kitu cha muhimu ni kwamba nyumba zetu ni mahali ambapo wanafamilia wanapendana. Niambie kuhusu nyumba yako mwenyewe na kile kinachoifanya iwe mahali pa upendo.

  • Kwa nini wewe unapenda kuwa nyumbani?”

  • Unajuaje kuwa familia yako inakupenda?

  • Je, wewe umeshalala mbali na nyumbani?

  • Ulilala wapi?

  • Ulijisikia vipi uliporudi nyumbani mwako mwenyewe?

Wakumbushe watoto jinsi ilivyo vizuri kurudi nyumbani mwenu wenyewe na kwenye vitanda vyenu.

Wimbo

Acha watoto wasimame na kusikiliza unapoimba au kusema maneno ya “Home” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 192). Waambie watoto wajikumbatie wenyewe wanaposikia neno nyumbani. Kama ukipenda, rudia mstari huu na uwaache watoto waimbe au waseme maneno pamoja nawe.

Nyumbani ni pale moyo ulipo.

Na joto na upendo uko tele.

Nyumbani ni pale mikono ya joto hukumbatia.

Hukumbatia kabisa.

(© 1975 by Sonos Music, Orem, Utah. Haki zote zimehifadhiwa. Umetumika kwa ruhusa.)

Tunaweza kusadia familia zetu kutunza nyumba zetu

Elezea kwamba tunahitaji kutunza nyumba zetu ili ziwe mahali pazuri pa kuishi. Kila mwana familia anapaswa kusaidia kudumisha usafi na umaridadi.

Shughuli

Acha watoto wafanye igizo la baadhi ya mambo wanayoweza kufanya ili kusaidia kudumuisha usafi na kusafisha nyumba, kama vile kuokota wanasesere, kufagia sakafu, kukunja nguo na kuziweka kabatini.

Waalike watoto waje mmoja kwa wakati na wasimame karibu nawe. Mwelezee kila mtoto hali ambayo kwayo anaweza kuwa msaidizi mwema nyumbani. Uliza mtoto anaweza kufanya nini ili kusaidia katika hali hiyo nyumbani. Tumia mifano ifuatayo au ubuni hali zako mwenyewe za kuendana na washiriki wa darasa.

  • Kwa bahati mbaya umemwaga glasi ya maji sakafuni bila kukusudia. Je, unapaswa kufanya nini?

  • Umecheza na vibao vyako vya mbao mchana wote. Sasa ni saa ya mlo. Unapaswa kufanya nini na vibao vyako hivyo?

  • Mama anaharakisha kupeleka chakula cha jioni mezani. Yeye anahitaji mtu wa kupanga meza ili familia iweze kula. Unaweza kufanya nini?

  • Nguo zako zimesafishwa na kukunjwa vizuri. Je, sasa unapaswa kuzifanya nini?

  • Umekuwa ukicheza nje na viatu vyako vikashika tope. Unatakiwa kufanya nini kabla ya kuingia ndani ya nyumba?

  • Kitanda chako kimevurugika unapoamka asubuhi. Unapaswa kufanya nini?

Watie moyo watoto wazungumze kuhusu mambo wanayoweza kufanya ili kudumisha usafi na kusafisha nyumba zao. Waambie watoto jinsi unavyofanya katika kudumisha usafi na kusafisha nyumba yako.

Shughuli

Wape watoto krayoni au penseli, na acha kila mtoto achore picha ya kitu alichofanya katikati ya wiki ili kusaidia nyumbani. Andika kila picha Nashukuru kwa ajili ya nyumba yetu.

Ushuhuda

Elezea hisia zako kuhusu nyumba yako na uonyeshe shukrani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa kukubariki wewe na pamoja na nyumba yenu.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Lete vyombo vya nyumbani vya kawaida kwenye mkoba (japo moja kwa kila mtoto). Acha mtoto achague chombo kutoka kwenye mkoba na aelezee jinsi anavyokitumia anaposaidia nyumbani. Kwa mfano, kitambaa cha kupangusa au kukaushia vyombo, kijiko kinachoweza kutumika wakati ukipanga meza kwa ajili ya mlo, na mwanasesere wanaweza kuweka mbali wakati wa kusafisha chumba.

  2. Imbeni au semeni maneno “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 253), mkitumia kifungu cha maneno “Kutandika kitanda changu ni furaha” au “Kupanga meza ni furaha” huku wakifanya igizo kwa vitendo.

  3. Chora mikono ya kila mtoto kwenye kipande cha karatasi ili apeleke nyumbani. Andika kila picha Nina mikono ya kusaidia. Zungumza kuhusu kile ambacho mikono ya watoto inavyoweza kufanya ili kusaidia.

  4. Acha watoto wajifanye kuwa viti vyao ni magari ya kukokotwa yaliyofunikwa. Acha watoto waburuze viti vyao katika duara kama watangulizi walivyofanya usiku ili kujilinda dhidi ya maadui na wanyama wakali. Acha waigize wakitengeneza moto wa kambi na kupika chakula cha jioni, wakiimba na kucheza dansi baada ya chakula, wakipanda kwenye magari yao ya kukokotwa (viti) ili kwenda kulala.

  5. Lete picha za aina tofauti za nyumba, au uzichore ubaoni au kwenye kipande cha karatasi. Jadili na watoto kile ambacho kila nyumba imejengwa nacho na namna ambavyo ingekuwa kuishi ndani yake. Unaweza kujumuisha hema, kasri, banda, na nyumba ya miti na udongo.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Imbeni au semeni maneno ya “When We’re Helping (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 198). Acha waigize mambo wanayoweza kufanya ili kusaidia nyumbani.

  2. Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mchezo wa vidole ufuatao:

    Vidole vidogo vyenye shughuli (kunja ngumi),

    Ni nani atatusaidia kutii?

    “Mimi.” “Mimi.” “Mimi.” “Mimi.” “Mimi” (nyosha kidole kwa kila “Mimi” mpaka vidole vyote vimefunguka),

    Vidole vidogo vyenye shughuli vinasema.