Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 10: Ninashukuru kwa ajili ya Miti, Mimea, na Maua


Somo la 10

Ninashukuru kwa ajili ya Miti, Mimea, na Maua

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuhisi shukrani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu kwa ajili ya miti, mimea, na maua.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:11–13.

  2. Weka tunda, mboga, au tawi dogo katika mfuko wa nguo au karatasi.

  3. Andaa sampuli kidogo ya tunda, mboga, au mkate. Zungumza na wazazi wa watoto ili kuhakikisha hakuna mtoto yoyote anayeweza kudhuriwa na chakula unacholeta.

  4. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Kama inawezekana. Lete picha za miti, mimea, na maua ya eneo lako, na ulete vyombo vidogo vichache vya mbao, kama penseli, kijiko, au bakuli, kutoka nyumbani kwako.

    3. Mkato 1-5, maua, (mikato inayofanana na hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha za Watoto wa Msingi seti ya 3).

    4. Picha 1-22, Mti Uliochanua Maua Mengi; picha 1-23, Kiota na Makinda wa Ndege

  5. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Pitisha mfuko ulio na tunda, mboga, au tawi ndani yake, funga ili watoto wasione kilichoko ndani. Acha watoto waguse mfuko na kubahatisha kitu kilicho ndani yake. Waambie wasiseme kwa sauti jibu lao mpaka kila mtu amepata nafasi ya kugusa mfuko. Baada ya kila mtu kuwa ameshagusa mfuko, na uwaache watoto waseme kile wanachofikiria kiko ndani ya mfuko huo. Toa kitu hicho kutoka ndani ya mfuko, na uzungumze kuhusu mwonekano wake na umuhimu wake.

Miti, mimea, na maua hufanya dunia kuwa mahali maridadi pa kuishi

Wakumbushe watoto kwamba kila kitu katika dunia kiliumbwa kulingana na mpango wa Baba wa Mbinguni. Katika siku ya tatu ya uumbaji, Yesu aliumba miti, mimea, na maua (ona Mwanzo 1:11–13). Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu walitaka kuifanya dunia kuwa maridadi kwa miti, mimea, na maua.

Onyesha mkato wa maua na picha zo zote za miti, mimea, au maua ulizopata. Acha watoto waongee kuhusu uzoefu wowote walio nao juu ya miti, mimea, au maua.

Hadithi

Simulia hadithi ambayo inawafundisha watoto kwamba miti, mimea, na maua hufanya dunia kuwa mahali maridadi pa kuishi. Zungumzia kuhusu mimea maridadi ambayo inakua pale unapoishi. Kama hutumika katika eneo lako, ukitaka unaweza kutumia picha 1-22, Mti Uliochanua Maua Mengi, na mawazo yafuatayo:

Kelly ana mti aupendao ambapo yeye ucheza chini yake. Asubuhi moja mama alimwamsha na kusema kwamba alikuwa na kitu cha kumstajabisha Kelly akikiona. Mti alioupenda Kelly ulikuwa umechanua maua meupe maridadi ambayo yalionekana kama bisi. Kelly aliuliza bisi zimefikaje kwenye mti aupendao, na mama yake anaelezea umuhimu wa kuchanua kwa maua.

Wimbo

Acha watoto waimbe ”Popcorn Popping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk.242), wakitumia vitendo vinavyopendekezwa na maneno. Elezea kwamba msimu wa kuchipua kwa mti wa mwaprikoti huonekana kama bisi.

Nilitazama nje dirishani, na niliona nini?

Bisi zikichanuka kwenye mti wa mwaprikoti!

Msimu wa kuchipua huniletea mshangao wa ajabu.

Maua yalichanua mbele ya macho yangu.

Ningeweza kutwaa bakuli na kuwa na karamu,

Kidonge cha bisi ambacho kingenukia utamu sana.

Lakini haikuwa hivyo, lakini ilionekana hivyo.

Bisi zikichanua juu ya mti wa mwaprikoti.

Elezea kwamba maua hukua kwenye miti, mengine hukua kwenye vichaka na mashamba ya mizabibu, na mengine hukua mahali popote ardhini. Waalike waelezee kuhusu maua ambayo wameshayaona.

  • Tunawezaje kutumia maua ili kuufanya ulimwengu wetu kuwa maridadi? (Tunayapanda katika bustani za maua, kutengeneza mashada ya maua, na kuyaweka kwenye nywele zetu au nguoni.

  • Kwa nini sisi humpa mtu maua? (Kwa matukio maalumu na kufanya watu wawe na furaha.)

Mimea na miti ni muhimu kwa maisha yetu

Hadithi

Elezea kwamba mimea na miti ni muhimu kwa maisha yetu. Onyesha picha 1-22, Mti Uliochanua Maua Mengi, na usimulie hadithi kuhusu matumizi mengi ya miti. Tumia mawazo yafuatayo au zungumza kuhusu njia zingine ambazo watu katika eneo lako hutumia miti.

Kwanza ndege hutumia mti kama makazi yao. Kwa makini hujenga kiota, na mama ndege utaga mayai ndani yake. (Onyesha picha 1-23, Kiota na Makinda wa Ndege.) Wakati vifaranga vinapoanguliwa kutoka kwenye mayai, mti huwa makazi mazuri kwao. Huwakinga dhidi ya jua kali, dhidi ya mvua, na dhidi ya wanyama huko ardhini ambao wangewadhuru. Mti pia hutoa matunda kwa familia ambayo inaishi karibu. Watoto hucheza chini ya kivuli cha mti na kujenga bembea kwenye matawi makubwa. Wakati sehemu za mti zinapokufa, familia huukatilia chini na kuutumia kama kuni za kuotea moto nyumbani.

  • Kwa nini miti ni muhimu kwetu? (Hutupa chakula, mbao, kivuli, na mahali pa kucheza.)

Onyesha baadhi ya vitu kutoka nyumbani kwako au darasani ambavyo vimetengenezwa kwa mbao, na uzungumzie kuhusu matumizi mengi ya mbao.

  • Ni vitu gani vingine unavyojua vimetengenezwa kwa mbao?

Elezea kwamba pia tunaweza kutumia mimea katika njia nyingi. Mojawapo ya vitu muhimu zaidi ambavyo mimea hutupa sisi ni chakula.

  • Ni aina gani ya mimea ambayo sisi hutumia?

Kama zo zote kati ya picha zako ulizopata zinaonyesha mimea ambayo hutumika kama chakula, waonyeshe sasa.

Shughuli

Zungumza na watoto kuhusu nafaka, matunda, na mboga zinazokuzwa hapo kwenu. Elezea kwamba nafaka mara nyingi hutengenezwa mkate au chakula cha nafaka. Muulize kila mtoto ataje chakula akipendacho ambacho hutokana na mmea. Acha watoto waonje sampuli ya matunda, mboga, au mkate ambao umenunua. Waambie kuhusu mmea au mti ambao chakula hicho kinatoka kwake.

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu waliumba mimea mingi tofauti na miti ili tuweze kuwa na vitu vizuri vya kula.

  • Tunawezaje kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili chakula chetu? (Kwa kukumbuka kuombea chakula kabla ya sisi kula.)

Ushuhuda

Toa ushuhuda wa upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu walio nao kwa kila mmoja wetu. Wakumbushe watoto kukumbuka upendo huo kila siku wanapoona mti, mimea na maua maridadi.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.

  1. Lete mbegu kiasi (kama vile mbegu za maua, maharagwe, na ngano) na kikombe cha karatasi kilichojaa mchanga kwa kila mtoto achukue nyumbani. Waonyeshe watoto jinsi ya kupanda mbegu zao, na wakukumbushe kwamba watahitajika kuinyunyiza maji na kuipa mwangaza kwa ajili ya mbegu kuota.

  2. Acha watoto warudie nyuma yako maneno ya wimbo “Little Seeds Lie Fast Asleep (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 243). Kisha acha wajifanye kuwa mbegu ndogo wakiamka na kujinyoosha huku wakimba au kusema maneno hayo tena.

  3. Kata petali, majani, na vikonyo kutoka kwa karatasi ya rangi na uache kila mtoto abandike baadhi yake katika umbo la ua kwenye kipande kingine cha karatasi. Andika kila karatasi Nashukuru kwa ajili ya maua maridadi.

  4. Lete tunda au mboga ikiwa na mbegu ndani yake. Waambie watoto kwamba kuna kitu cha kushangaza humo ndani. Kata tunda au mboga ili watoto waweze kuona mbegu. Elezea kwamba wakati mbegu zilizopandwa na kunyunyizwa na maji na kupata mwangaza, zitakua na kuzaa mtunda mengi na mboga.

  5. Wapeleke watoto matembezi ya nje ili waone aina tofauti za mimea. Kama hali ya hairuhusu kwenda nje, watoto wanaweza kutazama nje dirishani na kuchukua zamu kuelezea ile mimea wanaweza kuona. Kama inavyofaa, elezea mabadiliko ya misimu ambayo uathiri mimea na miti.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Onyesha picha 1-22, Mti Uliochaua Maua Mengi. Waambie watoto kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuumba mimea na miti (ona Mwanzo 1:11–13). Elezea kwamba hutupa mbao na matunda. Mimea hutupa matunda na mboga.

  2. Lete mmea au sehemu ya mmea (kama vile maua au majani fulani ili watoto wapate kuona, kugusa, na kunusa). Mpe kila mtoto nafasi ya kugusa au kushika mmea. Sema rangi yake, harufu, au urembo wake. Elezea shukrani zako kwa ajili mimea, maua, na miti.

  3. Kariri mstari ufuatao, na uonyeshe kwa vitendo. Kisha acha watoto wafanye vitendo pamoja na wewe huku ukikariri mstari ufuatao.

    Mimi Nalima

    Mimi nalima, lima, lima (fanya vitendo vya kulima),

    Na kisha napanda mbegu kiasi (inama na ijifanye kupanda mbegu).

    Mimi napalilia, palilia, palilia (fanya vitendo vya kupalilia),

    Na kisha mimi nang’oa magugu (inama chini na ufanye vitendo vya kung’oa).

    Jua hung’aa sana na kwa joto (weka mikono juu ya kicha na ufanya duara).

    Mvua inaanguka, na hivi (lete mikono chini, uiviringe).

    Hapa mbele ya macho yangu,

    Mbegu zinaanza kuota (weka vidole vya mkono wa kushoto katikati ya vidole vya mkono wa kulia).

  4. Imba “In the Leafy Treetops” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 240), pamoja na watoto.

Chapisha