Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 42: Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho


Somo la 42

Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba yeye ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Marko 1:9–11; Mafundisho na Maagano 115:4; and Joseph Smith—Historia 1:5, 10–19. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 17.

  2. Kata kipande kikubwa cha karatasi au bango katika vipande vikubwa vya mchezo-fumbo kulingana na idadi ya watu darasani (watoto na mwalimu). Andika jina la kila mshiriki wa darasa kwenye kipande cha mchezo-fumbo.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Maandiko.

    2. Picha 1-4, Ono la Kwanza (Sanaa ya Picha za Injili 403; 62470); picha 1-8, Kupitisha Sakramenti (Sanaa ya Picha za Injili 102; 62021); picha 1-12, Msichana Akithibitishwa ( 62020); picha 1-18, Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu (Sanaa ya Picha za Injili 208; 62133); picha 1-39, Mtoto Mchanga Akibarikiwa; picha 1-40, Kuhudumia Wagonjwa (62342); picha ya nabii aliye hai.

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote zenye Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Inua juu kipande cha mchezo-fumbo kilicho na jina lako. Waambie watoto kwamba hii ni sehemu ya mchezo-fumbo. Gawa vipande vingine na uwasaidie watoto kupanga mchezo-fumbo. Onyesha kila jina katika mchezo-fumbo na ilisome kwa watoto. Elezea kwamba kama vile kila kipande cha mchezo-fumbo ni cha mchezo-fumbo huu, kila mmoja wao ni wa darasa hili. Elezea kwamba kuwa ni wa kitu fulani humaanisha kuwa ni sehemu ya kitu hicho.

  • Wewe ni wa kikundi gani kingine?

Eleza kwamba sisi ni wa makundi mengine, kama vile familia au jamii. Sisi pia ni wa Kanisa la Yesu.

Onyesha picha 1-39, Mtoto Mchanga Akibarikiwa.

  • Ni nini kinafanyika katika picha hili?

Waelezee watoto kwamba wengi wao walipokea jina na baraka walipokuwa watoto wachanga. Kwa sababu ya kupewa jina na kubarikiwa, majina yao yaliwekwa katika kumbukumbu za Kanisa na wanaweza kusema “Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Wasaidie watoto kusema “Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Shughuli

Fanya shughuli ya mstari “Mimi Nafurahi Nimekuja Kanisani Leo” pamoja na watoto.

Mimi Nafurahi Nimekuja Kanisani Leo (piga makofi na ujenge mnara wa kanisa kwa kuweka vidole vya mbele pamoja).

Mimi napenda kusikiliza (kunja kiganja sikioni).

Na kusali (kunja mikono na uinamishe kichwa).

Najifunza juu ya Yesu aliye juu (onyesha juu);

Ninafikiria juu ya Kristo na upendo Wake (jikumbatie mweyewe).

Elezea kwa watoto kwamba sisi tunakuja kwenye mikutano ya kanisa kujifundisha zaidi kuhusu Yesu na kile ambacho Yeye anataka tufanye. Waambie watoto kwamba katika somo hili watajifunza kuhusu baadhi ya mambo muhimu ambayo ni sehemu ya kanisa la Yesu.

Kanisa la Yesu lina ukuhani

Picha 1-8, Kupitisha Sakramenti (62021); picha 1-12 Msichana Akithibitishwa; na picha 1-40, Kuhudumia Wagonjwa. Acha watoto waseme kile wanachojua kuhusu kile kinachotendeka katika kila picha. Eleza kwamba ukuhani unahitajika kwa kila moja ya mambo haya. Ukuhani ni uwezo ambao Baba wa Mbinguni na Yesu wanao. Wao huutoa uwezo huu kwa wanaume waaminifu ili kwamba wanaume hawa waweze kusaidia kufanya kazi ya Baba wa Mbinguni na Yesu ulimwenguni. Onyesha wenye ukuhani katika kila picha. Acha watoto waseme neno ukuhani mara kadhaa.

  • Unamjua nani ambaye ana ukuhani?

Wasaidie watoto kuelewa kwamba wanaume ambao wana ukuhani wanaweza kubariki na kupitisha sakramenti, kubatiza, na kutoa baraka kwa watu, na kufanya mambo mengine muhimu. Onyesha picha 1-39, Mtoto Mchanga Akibarikiwa; tena na uwaambie watoto kwamba watoto wachanga hubarikiwa na wanaume wenye ukuhani.

Hadithi

Onyesha picha 1-18, Yohana Mbatizaji Anambatiza Yesu. Waache watoto waseme kile wanachokumbuka kuhusu picha hii. Kwa kifupi rejea hadithi, kama inavyopatikana katika Marko 1:9–11.

  • Ni nani anambatiza Yesu? (Ona Marko 1:19.)

  • Ni uwezo gani Yohana alihitaji ili kumbatiza Yesu? (Ukuhani.)

Elezea kwamba kubatizwa na mtu aliye na ukuhani ni sehemu muhimu ya kuwa sehemu ya kanisa la Yesu. Waambie watoto kwamba wanapofika umri wa miaka minane, wanaweza kubatizwa kuwa waumini wa kanisa la Yesu.

Kanisa la Yesu lina nabii

Hadithi

Onyesha picha 1-4, Ono la Kwanza, na wasimulie hadithi ya Joseph Smith na Ono la Kwanza, kama inavyopatikana katika Joseph Smith-Historia 1:5, 10–19.

Elezea kwamba kwa sababu Baba wa Mbinguni na Yesu waliongea na Joseph Smith, tunamwita Joseph Smith nabii. Nabii hutuambia kile ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka tujue.

  • Nabii ni nini? (Mtu ambaye ana wito maalumu wa kuongea na Baba wa Mbinguni na Yesu na kutuambia kile ambacho wao wanataka tujue.)

Onyesha picha ya nabii aliye hai. Waambie watoto juu ya yake. Elezea kwamba kanisa la Yesu daima limekuwa na nabii aliye hai ili atufundishe kile ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka sisi tujue na kufanya.

Wimbo

Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 110). Elezea kwamba kupotoka humaanisha kufanya makosa. Kila mtoto na ashikilie picha ya nabii aliye hai wakati mkiimba.

Mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, hautapotoka.

Mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, yeye anajua njia.

Kanisa la Yesu lina maandiko

Inua maandiko.

  • Nimeshika nini?”

Waache watoto waseme kile wanachojua kuhusu maandiko. Wakumbushe watoto kwamba maandiko yana mafundisho ya Baba wa Mbinguni na Yesu. Maandiko yana hadithi nyingi za kweli juu ya Yesu, manabii, na watu wengine. Maandiko ni sehemu muhimu ya kanisa la Yesu.

Sisi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

  • Tunapaswa kuwa wa kanisa la nani?

  • Je, jina la Kanisa ambalo sisi tuko linaitwaje?

Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 115:4 . Elezea kwamba jina hii humaanisha kwamba hili ni kanisa la Yesu katika nyakati ambazo sisi tunaishi sasa. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuna watu wengi ulimwenguni kote ambao ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Unaweza ukipenda kuelezea kwamba kuna makanisa mengine ulimwenguni leo ambayo yanafundisha kuhusu Yesu na kuwafundisha watu kuishi maisha mema, lakini hayana ukuhani, nabii aliye hai, au maandiko yote.

Shughuli

Omba kila mtu ambaye ni wa kanisa la Yesu asimame. Wakumbushe watoto kwamba wao wote wanapaswa kusimama. Acha watoto warudie “Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Kwa kifupi rejea, ukitumia picha na maandiko, kwamba nabii aliye hai, na maadiko ni sehemu muhimu za kanisa la Yesu.

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako wa ukweli wa injili. Wasaidie watoto kuhisi jinsi ilivyo muhimu na ajabu kuwa muumini wa kanisa la Yesu.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Tengeneza beji ambayo inasema Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa kila mtoto ili akavae nyumbani. Waache watoto wachore beji zao.

  2. Cheza mchezo ufuatao wa vidole pamoja na watoto:

    Hili ni Kanisa

    Hili ni Kanisa (piga makofi vidole vikishikana kwa ndani),

    Huu ni mnara (panua vidole vya mbele na weka incha pamoja).

    Fungua milango (fungua viganja, ukiweka vidole pamoja).

    Na waone watu (fukukuta vidole).

    Funga milango na usikie wao wakiomba (funga mikono vidole vikiwa ndani; ulete mikono kwenye sikio moja).

    Fungua milango na wote wanaenda zao (fungua

  3. Simulia hadithi ya mtoto ambaye ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Jumuisha shughuli ambazo watoto katika darasa lako wanaweza kushiriki, kama vile kuketi pamoja na familia zao katika mkutano wa sakramenti, kupokea sakramenti, kuketi kwa staha katika Msingi, kusali, na kuimba.

    Pia unaweza kuwaacha watoto wafikirie mawazo haya kwa kuuliza maswali kama vile “”Ni nini watoto wa Kanisa wanapaswa kufanya Jumapili?” “Ni nini wanapaswa kufanya katika mkutano wa Sakramenti? Katika Msingi?” “Ni nini wanapaswa kufanya nyumbani Jumapili?” “Ni nini wanapaswa kufanya wakati wa jioni ya familia nyumbani?” “Ni kwa jinsi gani wanapaswa kuwatendea wana familia na marafiki zao?” Wasaidie watoto kuelewa kile wavulana na wasichana ambao ni wa kanisa la Yesu wanapaswa kufanya.

  4. Waache watoto wafikirie juu ya makundi tofauti wanayohusika nayo, kama vile familia au darasa la Msingi. Waalike watoto waseme kile wanapenda kuhusu kila kikundi. Hitimisha mazungumzo na kile wao (na wewe) mnapenda kuhusu kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

  5. Imbeni au semeni maneno ya “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 77).

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Kabla ya darasa, chora picha nne rahisi—jicho, mkono, sikio, na mdomo—kwenye vipande tofauti vya karatasi.

    Waambie watoto kwamba kuna vitu vingi tunaweza kufanya kanisani. (Bandika picha ya jicho.) Tunaweza kusoma hadithi za maandiko. (Bandika picha ya mkono.) Tunaweza kuwa wakarimu kwa marafiki zetu. (Banika picha ya sikio.) Tunaweza kuwasikiliza kwa makini walimu wetu. (Bandika picha ya mdomo.) Tunaweza kusema kwa sauti za chini tukiwa kanisani. Acha kila mtoto aje na kuonyesha mojawapo wa picha. Picha inapoonyeshwa, waambie watoto tena kile inasimamia.

  2. Wasaidie watoto kuimba ”Book of Mormon Stories” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.118), mkitumia kitendo kinachopendekezwa na maneno. Au acha watoto watembee chumbani huku wakiimba.