Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 1: Mimi ni Mtoto wa Mungu


Somo la 1

Mimi ni Mtoto wa Mungu

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba sisi ni watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni, ambaye anatujua na kutupenda sisi.

Maandalizi

  1. Jifunze kwa maombi Kutoka 2:1–10; Zaburi 82:6; Mafundisho na Maagano 138:55–56; na Musa 1:1–6. Ona pia Kanuni za Injili (31110), .sura ya 2.

  2. Tafuta sifa bainifu za kupendeza mbili au tatu za kila mtoto kwa kuzungumza na wazazi wake.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia na Lulu ya Thamani Kuu.

    2. Kijifuko cha maharagwe au kitu kingine laini.

    3. Picha 1-1, Ulimwengu (62196); picha 1-2, Musa katika Kijisafina cha Manyasi (Picha za Sanaa za Injili 106; 62063).

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Imba “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 2), pamoja na watoto.

Mimi ni mtoto wa Mungu,

Kanileta hapa,

Kanipa makao mema

Na wazazi wema

Niongoze, kaa nami,

Unifundishe

Unionyeshe njia

Ya kujia kwako.

Rusha kijifuko cha maharagwe au kitu laini kwa mtoto na useme, “Mimi namjua mtoto wa Mungu anayeitwa .” Acha mtoto aseme jina lake mwenyewe na kurusha kijifuko cha maharagwe kwako tena. Rudia shughuli hii mpaka kila mmoja apate zamu.

Sisi tu watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni

  • Baba wa Mbinguni ni nani? (Tumia majibu ya watoto kukupa mwelekeo katika kuelezea sehemu hii ya somo katika kiwango kinachofaa.)

Onyesha picha 1-1, Ulimwemgu. Elezea kwamba kabla ya kuzaliwa hapa duniani, tuliishi mbinguni na Baba yetu wa Mbinguni. Huko tulikuwa roho. Roho zetu haziwezi kuonekana, lakini ndizo zinazotufanya tuwe hai. Tulipokuwa roho, hatukuwa na nyama na mifupa kama miili yetu ilivyo sasa, lakini tulionekana hivi hivi.

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ni baba wa roho zetu, na sisi ni watoto wake wa kiroho. Hatuwezi kukumbuka kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani, lakini tunajua sisi ni watoto wake wa kiroho kwa sababu tunasoma hivyo katika maandiko.

Onyesha Biblia na usome Zaburi 82:6, ukielezea kwamba Aliye juu humaanisha Baba wa Mbinguni. Sisitiza kwamba kila mtu ulimwenguni ni mtoto wa Baba wa Mbinguni.

Wimbo

Imba “Mimi ni Mtoto wa Mungu” tena. Elezea kwamba Mungu ni jina lingine la Baba wa Mbinguni.

Baba wa Mbinguni anatujua na anatupenda

Eleza kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wetu sana kwa sababu sisi ni watoto wake. Yeye anajua majina yetu na yote yanayotuhusu sisi. Yeye anajua kile kinachotufanya kuwa na furaha na kile kinachotufanya tuwe na huzuni. Yeye anajua kilicho bora kwa kila mmoja wetu.

Shughuli

Sema mstari ufuatao mara kadhaa pamoja na watoto, wakitumia vitendo:

Baba wa Mbinguni Ananijua

Baba wa Mbinguni ananijua (jionyeshe mwenyewe)

Na kile mimi ninachopenda kufanya.

Yeye anajua jina langu na pale ninapoishi (tengeneza paa kwa kugusanisha vidole vya mikono yote).

Mimi najua ananipenda, pia (pitisha mikono na uweke mikono nyuma ya mabega kama kumbatio).

Yeye anajua kile kinanifanya kuwa na furaha (weka vidole kwenye mdomo wa tabasamu).

Yeye anajua kile kinachotufanya tuwe na huzuni. (weka vidole kwenye mdomo uliogueza kwenda chini).

Mimi najua anataka kunisaidia (jionyeshe mweyewe);

Na hiyo inanifanya nisikie furaha!

Mwambie mtoto aje mbele ya darasa. Ukutumia kile ulichojifunza kutoka kwa wazazi wa watoto, elezea kwamba Baba wa Mbinguni anajua kuhusu sifa bainifu za kupendeza za mtoto. Kwa mfano, unaweza kusema, “Baba wa Mbinguni anajua kwamba Emily ni binti mwenye upendo, humsaidia mama yake kumlea dada yake, na kawaida yeye ni mwenye furaha na tabasamu. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu moja.

Elezea kwamba tunapofanya mambo kwa ukarimu na upendo, tunakuwa kama Baba wa Mbinguni.

Tunaweza kuwa kama Baba wa Mbinguni

  • Mtoto wa mbwa anaitwaje?

  • Kitoto cha mbwa kikikua kitakuwa nini?

  • Mtoto wa kuku anaitwaje ?

  • Kifaranga kikikua kitakuwa nini?

Elezea kwamba kama vile wanyama wanakua na kuwa kama wazazi wao, sisi tutakua na kuwa kama wazazi wetu. Baba wa Mbinguni ni baba wa roho zetu, kwa hiyo tunaweza kuwa kama yeye. Baba wa Mbinguni ana upendo, ni mwema, na mkarimu, na anataka kutusaidia. Tunapokuwa wenye upendo, wema na wakarimu, tunakuwa kama Baba wa Mbinguni. Elezea kwamba tunapaswa kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni kila siku.

Baba wa Mbinguni ana kazi muhimu ya kufanywa na sisi

Hadithi

Onyesha picha 1-2, Musa katika Kijisafina cha Manyasi, na usimulie hadithi ya jinsi binti ya Farao alimwokoa Musa kutoka hatarini alipokuwa mtoto mchanga, kama inavyopatikana katika Kutoka 2:1-10.

Elezea kwamba Musa alikua na kuwa mmoja wa wasaidizi muhimu wa Baba wa Mbinguni, nabii. Baba wa Mbinguni alimwambia Musa kwamba Musa alikuwa mwanae (ona Musa 1:4, 6) na kwamba alikuwa na kazi muhimu kwa ajili ya Musa. Soma sehemu ya kwanza ya Musa 1:6 kwa watoto. Musa alifanya kazi hii wakati alipowatoa Waisraeli kutoka nchi ya Misri, mahali ambako walikuwa wanatendewa kwa ukatili sana, hadi nchi nyingine ambako Musa aliwafundisha amri za Baba wa Mbinguni.

Acha watoto waje mbele ya darasa moja baada ya mwingine, na msaidie kila mmoja kurudia sehemu ya kwanza ya mstari katika Musa 1:6, wakiweka badala yake majina yao wenyewe: “Mimi ninayo kazi ya kufanywa na wewe (jina la mtoto), mwanangu (binti yangu).”

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ama mambo muhimu kwetu ya kufanya wakati tunaishi ulimwenguni, kama vile kuwa mama au baba, mmisionari, mwalimu, msaidizi kanisani, au msaidizi katika jamii.

  • Ni kazi gani muhimu Baba wa Mbinguni angetaka sisi tufanye?

Shughuli

Acha watoto wafanye maigizo ya kile wao wanataka kuwa watakapokuwa watu wazima, kama vile mama au baba wakimshika mtoto mchanga, mmisionari akiieneza injili, au mwalimu akifundisha darasa.

Ushuhuda

Waambie watoto kwamba wanapaswa daima kukumbuka kwamba wao ni watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni na kwamba yeye anawajua wao na kuwapenda. Wasaidie wao kuelewa kwamba wanaweza kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na kwamba wana kazi muhimu ya kufanya hapa duniani. Unaweza kuwasimulia uzoefu wako binafsi ambao ulikusaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni anakujua wewe na anakupenda.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Onyesha picha za watu tofauti, au uzungumze kuhusu watu ambao watoto wanawajua, na uliza, “Je, huyu mtu ni mtoto wa Mungu?” Kwa mfano, “Je, Rais wa tawi ni mtoto wa Mungu?” “Je, askari polisi ni mtoto wa Mungu?” “Je, jirani yako ni mtoto wa Mungu” na kadhalika. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kila mtu ni mtoto wa Mungu.

  2. Ili kusisitiza kwamba Baba wa Mbinguni anamjua na kumjali kila mtoto, acha watoto wakamilishe sentensi zako, kama ilivyo katika mifano hii: “Baba wa Mbinguni anajua nina huzuni ninapo ,” “Baba wa Mbinguni anajua nina furaha ninapo ,’ ‘Baba wa Mbinguni anajua kitu ninachopendelea kufanya ,” “Baba wa Mbinguni anajua ninapenda kuja katika darasa la Msingi kwa sababu ,” “na kadhalika.

  3. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ni mfalme wa mbingu na ulimwengu. Kwa sababu sisi ni watoto Wake, sisi ni wana na mabinti wa mfalme. Tengeneza taji rahisi kwa kila mtoto na uandike maneno Mimi ni mtoto wa Mungu kwenye kila taji. Waache watoto wapake rangi mataji haya.

  4. Pamoja na watoto imbeni au semeni maneno ya mstari wa kwanza wa “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 4) au mistari yote “I Know My Father Lives” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 5).

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Waombe watoto kufikiria kitu wanachopenda (unaweza pia kupata habari hizi kutoka kwa wazazi wao mapema). Muulize kila mtoto kile anachopenda, na umwambie kwamba Baba wa Mbinguni anajua hilo, kama kwa mfano: “Baba wa Mbinguni anajua kwamba Leah anapenda mbwa.

  2. Wasaidie watoto kufanya vitendo vya shughuli ifuatayo:

    Kama wewe ni mrefu, mrefu sana (jinyoshe na mikono juu sana)

    Kuna nafasi kanisani kwa ajili yako.

    Kama wewe ni mdogo, mdogo sana (chutama chini),

    Kuna nafasi kanisani kwa ajili yako.

    Mrefu (jinyoshe)

    Mdogo (chutama)

    Mrefu (jinyoshe)

    Mdogo (chutama)

    Baba wa Mbinguni anatupenda wote.

  3. Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mstari ufuatao huku ukisema maneno:

    Musa Mtoto Mchanga

    Musa Mtoto Mchanga alikuwa na mashua kama kitanda (kunja mkono na uweke kidole kwenye ule mkono mwingine).

    Dada yake kipenzi alimchunga manyasini alipomficha (chungulia katikati ya vidole vya mkono machoni pako).

    Siku moja binti mfalme akampata (inama ukiangalia chini) na kumchukua katika mikono yake (jifanye kama kumwinua mtoto);

    Alisema, “Mimi nitamchukua mtoto huyu na kumlea asidhurike” (jifanye kumliwaza mtoto mikononi).

    (Kutoka Fascinating Finger Fun na Eleanor Doan. © 1951. Imetumika kwa Idhini.)

Chapisha