Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 29: Mimi Naweza Kusema Pole


Somo la 29

Mimi Naweza Kusema Pole

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba tunapofanya makosa, tunapaswa kusema pole na kuendelea kurekebisha makosa tuliyofanya.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mosia 27:8–37.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Kitabu cha Mormoni.

    2. Mwanasesere mdogo anayeweza kutosha kuingia mfukoni.

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Watoto wanapoingia chumbani au wanapokusanyika kwa ajili ya somo, kwa makusudi kufanya makosa fulani katika kupanga darasa au kuandaa somo. Unaweza—

  • Kuangusha kitu sakafuni.

  • Kuweka kiti kinyume.

  • Weka picha ikiwa juu chini.

  • Andika kitu fulani ubaoni au kwenye kipande cha karatasi na kisha ukifute au ukikate.

Baada ya kila kosa sema “Pole; nimekosea.” Kisha rekebisha kosa.

Waulize watoto kama waliona makosa yote uliyofanya. Sema kwamba kila mtu hufanya makosa.

Wakati mwingine tunafanya mambo ambayo ni makosa

Elezea kwamba tulipokuwa tunakua na kujifundisha kuchagua kilicho sahihi, wakati mwingine tunafanya chaguzi ambazo ni makosa. Haya si makosa kama vile kuweka picha juu chini; kuna nyakati tunapofanya kosa, kitu ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu na wazazi wetu hawataki sisi tufanye. Kwa kufanya chaguzi za makosa, zinaweza kutufanya sisi wenyewe na watu wengine kukosa kuwa na furaha.

Hadithi

Simulia hadithi ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe, ukitumia mwanasesere mdogo kuionyesha:

Travis na Matt walikuwa wanacheza kwa furaha nyumbani kwa kina Matt. Travis aliwapenda wanasesere wa Matt na alitamani wawe wake. Travis aliamua kuchukua baadhi ya wanasesere, na akawaweka mfukoni mwake bila kumwomba Matt.

Wakati Travis alipocheza na wanasesere nyumbani, haikufurahisha. Mama yake alimuuliza kwa nini hakuwa na furaha. Travis alimwambia mama yake kwamba alichukua wanasesere wa Matt bila kumwomba na sasa alikuwa anajisikia vibaya kwa sababu hiyo.

Mama ya Travis alimwambia kwamba ilikuwa ni kosa kuchukua kitu ambacho ni cha mtu mwingine. Alimwambia Travis anapaswa kurekebisha kosa lake la uchaguzi mbaya. Travis alikuwa anataka kurudisha wanasesere, lakini aliogopa kwamba pengine Matt angemkasirikia. Mama ya Travis alisema kwamba hata kama Matt anaweza kukasirika, kurudisha wamasesere ilikuwa jambo sahihi kufanya. Alimwambia Travis kwamba kwa kumwambia Matt samahani kungesaidia kuondoa hisia mbaya alizokuwa nazo kwa kufanya kosa.

Travis alirudisha wanasesere kwa Matt. Alisema samahani kwa kuchukua wanasesere bila kuomba na akaahidi kutofanya hivyo tena. Matt alikuwa na furaha kwamba Travis alirudisha wanasesere. Travis akawa na furaha kwa kuwa alisema ukweli na kurekebisha mambo (Imetoholewa kutoka kwa Pat Graham, “Travis Parents,” Friend, Mar. 1987, uk. 40–41).

  • Ni kitu gani Travis alikifanya kilichokuwa makosa?

  • Travis alijihisi vipi alipochukua wanasesere wa Matt?

Elezea kuwa tunapofanya kosa, tunajisikia vibaya moyoni. Hii ni njia mojawapo Baba wa Mbinguni hutusaidia kujua tumefanya makosa.

  • Travis alifanya nini kuondoa hisia mbaya?

  • Travis alijisikia vipi wakati aliporudisha wanasesere wa Matt na kusema samahani?

Tunapaswa kusema samahani

  • Unahisi vipi unapokuwa umefanya kosa?

  • Unaweza kufanya nini ili kufanya hisia mbaya ziondoke?

Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunapofanya kosa, tunahitaji kukiri. Kisha tunahitaji kusema “samahani.” Sisi pia tunahitaji kurekebisaha kosa tulilofanya na kuwaahidi kwamba hatutafanya hivyo tena.

Shughuli

Acha watoto wasimame na kufanya vitendo vya mstari ufuatao wa shughuli:

Ninapofanya kosa (chezesha vidole upande upande).

“Samahani,” Mimi nitasema.

Ninajisikia vibaya (vuta midomo chini kwa vidole, nuna

Kwa kile nilichofanya leo.

Nitafanya vyema (weka mikono kiunoni na uitikie kwa kichwa);

Nitajaribu kwa nguvu zangu zote.

Nitakuwa mwenye furaha. (tabasamu)

Kama nitafanya kile kilicho sahihi (kuja mikonona uitikie kwa kichwa).

Tunapaswa kufanya kila tuwezavyo ili kurekebisha kosa

Hadithi

Waonyeshe watoto Kitabu cha Mormoni. Waambie kwamba Kitabu cha Mormoni kinaelezea kuhusu mtu aliyefanya kosa.

Fungua Kitabu cha Mormoni na usimulie hadithi ya Alma, kama inavyopatikana katika Mosia 27:8-37. Elezea kwamba Alma hamkumsikiliza baba yake. Alimkaidi Baba wa Mbinguni na Yesu. Alifanya mambo mengi yaliyokuwa mabaya. Aliwaambia watu mambo ambayo hayakuwa ya kweli kuhusu Kanisa. Watu wengi waliamini maneno yake na hawakuweza kuwasiliza viongozi wa Kanisa.

Elezea kwamba Alma alibadilika kutoka katika kufanya makosa na akafanya mambo yaliyo sahihi. Alijaribu kurekebisha makosa aliyokuwa amefanya kwa kuwafundisha watu ukweli.

  • Je, unafikiri Alma alijisikia vipi wakati alipogundua alikuwa anafanya makosa? (Ona Mosia 27:29.)

  • Ni kwa namna gani Alma alijaribu kurekebisha makosa ambayo alikuwa amefanya? (Ona Mosia 27:32, 35–36.)

  • Unafikiri Alma alijisikia vipi wakati alipoanza kuwafundisha watu ukweli?

  • Tunapofanya makosa, kwa nini tunapaswa kujaribu kuyarekebisha?

Elezea tukio binafsi rahisi wakati ambapo ulimwambia mtu samahani. Waambie watoto jinsi ulivyojisikia na jinsi ulivyojaribu kurekebisha kosa ulilofanya.

Rejea mambo ambayo tunahitaji kufanya tunapogundua tumefanya makosa.

  1. Kiri umefanya kosa.

  2. Sema “Samahani.”

  3. Ahidi hautafanya hivyo tena.

  4. Tufanye tuwezavyo kurekebisha makosa yetu.

Elezea kwamba hizi hatua zote zinaitwa toba. Baba wa Mbinguni na Yesu wanafurahia tunapotubu makosa tuliyofanya.

Acha watoto wajadili jinsi wanavyoweza kufuata hatua hizi za toba katika hali zifuatazo:

  • Unapaswa kufanya nini kama umechukua kitu ambacho sio mali yao?

  • Unapaswa kufanya nini kama ulisema kitu kibaya kwa mtu fulani?

  • Unapaswa kufanya nini kama haukusema ukweli kwa wazazi wako?

  • Unapaswa kufanya nini kama ukimwangusha mtu?

Ushuhuda

Toa ushuhuda kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatupenda hata kama tumefanya makosa. Waambie watoto kwamba unajua watakuwa na furaha wanaposema samahani kwa makosa waliyoyafanya na wanapojaribu kutofanya tena makosa.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.

  1. Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “Repentance” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 98). Elezea kwamba kutubu humaanisha kusema samahani, na kuahidi kutofanya kosa hilo tena, kujaribu kurekebisha kosa.

  2. Mpatie kila mtoto kipande cha udongo au donge la udongo. Waonyeshe watoto jinsi ya kufinyanga udongo au donge la udongo ili kuwa mpira na kisha kulisukuma kuwa bapa. Wasadie kutengeneza uso wa tabasamu kwenye udongo au donge la udongo ili kuwakumbusha kwamba wanaposema “samahani” watajisikia vyema. (Viungo vya donge la udongo vinaweza kupatikana katika ukurasa xv wa kitabu hiki cha kiada.

  3. Mpe kila mtoto kipande cha karatasi na krayoni au penseli. Acha kila mtoto achore picha ya uso wa tabasamu. Andika picha Mimi naweza kuwa na furaha ninaposema samahani.

  4. Imbeni au semeni maneno ya “I Want to Live the Gospel” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk, 148).

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. “Kwa bahati mbaya” angausha sanduku la krayoni au vifaa vingine vidogo sakafuni. Waambie watoto samahani kwa kuangusha krayoni, na uwaulize kile wanachopaswa kufanya hali iwe nzuri. Mnaposafisha, waambie watoto kwamba unajisikia vyema sakafu inapokuwa nadhifu na safi tena. Waalike watoto wakusaidie kusafisha.

    Elezea kwamba wakati mwingine tunafanya mambo ambayo hutufanya sisi au wengine kuhisi huzuni. Wakati hili linapotokea, tunapaswa kusema “samahani” na kujaribu kurekebisha mambo. Washukuru watoto kwa kukusaidia kusafisha, na uwakumbushe wao kwamba watajisikia vyema wanapowasidia wengine.

  2. Imbeni au semeni maneno ya “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 61).

  3. Acha watoto waseme neno refu kama vile chamshakinywa. Waambie kwamba wakati mwingine ni vigumu kusema maneno fulani. Elezea kwamba inaweza kuwa vigumu kusema “samahani” tunapofanya makosa. Elezea kwamba hata kama neno “samahani” ni gumu kusema, linaweza kubadili hisia za huzuni kuwa hisia nzuri.

  4. Wasimulie watoto hadithi kuhusu watoto wawili ambao walikuwa wanacheza pamoja. Wakati mmoja wa watoto anapomsukuma mwingine, mtoto wa kwanza anasema , “samahani” na anajaribu kumsaidia aliyeumia ili ajisikie vyema. Jumuisha wazo la kugeuza hisia mbaya kuwa za furaha. Ukitaka unaweza kutumia mchoro wa Sura ya Tabasamu/Sura ya Kununa kutoka somo la 21. Acha mtoto ainue mchoro na kuugeuza ili kuonyesha hisia za watoto hawa katika hadithi.