Somo la 28
Mimi Naweza Kuwa Mtiifu
Madhumuni
Ni kuimarisha hamu ya kila mtoto kumtii Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuwatii wazazi wake.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Yohana 14:15; na Waefeso 6:1. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 31.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Maandiko.
-
Picha 1-5, Familia na Mtoto (62307); picha 1-8, Kupitishwa kwa Sakramenti (62021); picha 1-9, Sala za Asubuhi (62310); picha 1-46, Watoto Wakimpa Mama Maua; picha 1-55, Mahubiri Mlimani (Sanaa ya Picha za Injili 212; 62166); picha 1-56 Watu Watatu Katika Tunuu Yenye Mto Mkali (Sanaa ya Picha za Injili 212; 62093).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuwatii wazazi wetu
Onyesha picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga.
-
Picha hii inaonyesha nini?
Mwonyeshe mtoto mchanga katika picha na uzungumze kuhusu jinsi kila mmoja wetu alivyokuja duniani kama mtoto mchanga. Wakumbushe watoto kwamba kwa sababu watoto wachanga ni wadogo sana na hawajiwezi wanahitaji mtu mzima na mkubwa wa kuwatunza.
-
Ni nani alikutunza ulipokuwa mtoto mchanga?
-
Ni nani anayekutunza sasa?
Waelezee watoto kwamba watu ambao wanatutunza, kama vile wazazi na wana familia wengine, wanawapenda na wanataka wao wawe salama na wenye furaha.
-
Wazazi wako walikufundisha usifanye nini?
Zungumza kuhusu mambo ambayo watoto wanataka kufanya ambayo yanaweza kuwaumiza au kuwafanya wasiwe na furaha, kama vile kucheza mtaani, kugusa jiko moto, kuchukua kisu chenye makali, kukimbia kwenye mteremko wa kilima kikali, kupigana na kaka na dada zako.
-
Kwa nini wazazi wako hawataki wewe ufanye mambo haya?
Zungumzia kuhusu mambo ambayo watoto wanaweza kufanya kwa usalama na furaha, kama vile kucheza na wanasesere, kutembelea sehemu na familia zao, na kuwa wakarimu kwa kaka na dada zao.
-
Kwa nini wazazi wenu wanawaacha mfanye mambo haya?
-
Kwa nini mnapaswa kuwatii wazazi wenu?
Elezea kwamba wazazi wetu wanatupenda na wataka tufanye mambo ambayo ni salama na ya furaha.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tutii amri
Onyesha picha 1-55, Mahubiri Mlimani.
-
Ni nani aliye katika picha hii?
Elezea kwamba Yesu alipokuwa duniani, aliwafundisha watu kile ambacho Baba wa Mbinguni alikuwa anataka tufanye. Mafundisho haya huitwa amri. Inua maandiko. Waambie watoto kwamba amri zimeandikwa katika maandiko.
Baba wa Mbinguni hutubariki tunapokuwa watiifu
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Imbeni au semeni maneno ya “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 146) au “I Have Two Little Hands” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 272).
-
Acha kila mtoto achukue zamu kuwapa darasa maelekezo fulani, kama vile “simama” na “weka mikono kichwani.” Acha watoto wengine watii maelekezo hayo.
-
Ukitumia ufito wa kuvulia samaki kutoka somo la 11 na uandae samaki fulani wa karatasi ambao juu yake umeandika maelekezo rahisi, kama vile “kunja mikono yako” “rudia ‘Yesu alisema, Kama unanipenda, zishike amri zangu,’” “tembea kwa utulivu chumbani humu,” “tabasamu kwa watoto wengine,” na “saidia darasa kuimba ‘I Am a Child of God.’” Mpe kila mtoto nafasi ya kushika samaki wa karatasi na atii maelekezo yaliyoandikwa kwenye samaki.
-
Rejea hadithi ya Nuhu, ukisisitiza kwamba Nuhu na familia yake waliokolewa kutokana na gharika kwa sababu walitii amri.
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilichochorwa uso wa furaha na kuandikwa na maneno Nina furaha ninapotii. Waache watoto wachore nyuso zao.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mchezo ufuatao wa vidole:
Vidole vidogo vyenye shughuli (kunja ngumi),
Ni nani atatusaidia kutii?
“Mimi nita.” “Mimi nita.” “Mimi nita.” “Mimi nita.” “Mimi nita” (nyosha kidole kwa kila “Mimi nita” mpaka vidole vyote vimefunguka),
Vidole vidogo vyenye shughuli vinasema.
-
Lete vitu kadhaa ambavyo vinatoa ulinzi, kama vile viatu, kofia, na glavu. Waulize watoto ni ulinzi wa aina gani kila kitu hutoa (kwa mfano, viatu hulinda miguu yetu, kofia hulinda vichwa vyetu kutokana na baridi au macho yetu kutokana na jua). Waambie watoto kwamba tunapowatii wazazi wetu, tutalindwa pia. Zungumza kuhusu baadhi ya sheria na jinsi zinavyoweza kutulinda.
-
Inua mikono yako na uwaonyeshe watoto jinsi ya kutembeza vidole. Acha watoto wainue mikono yao, watembeze vidole, na wafungue na kufunga mikono yao. Elezea kwamba tunaweza kutembeza mikono yetu na vidole vyetu wenyewe, wala si mtu mwingine. Elezea kwamba tunaweza kufanya mikono yetu itii mtu anapotuomba tufanya kitu fulani. Kufanya hivi hutufurahisha moyoni.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mstari wa shughuli huku ukisema maneno:
Mimi Napenda Mikono Yangu
Mimi napenda mikono yangu; ni yangu (nua mikono na uitazame).
Inashughulika na husaidia mpaka mwisho wa siku (fanya igizo la mikono ikifanya kazi.
Inaweza kujikunja kimya kimya (kunja mikono) au piga makofi kwa nguvu (makofi)!
Inapofanya kile kilicho sahihi, hunifurahisha!