Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Nyimbo kwa ajili ya Chekechea kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto


Nyimbo kwa ajili ya Chekechea kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Nyimbo zifuatazo kutoka kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto zinazofaa hasa kwa matumizi katika chekechea. Yaliyojumuishwa ni baadhi ya mapendekezo ya njia unavyoweza kutohoa maneno. Unaweza kuwa na mawazo mengine kwa ajili ya njia za kutohoa nyimbo hizi au zingine katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto ili ziweze kufaa kwa ajili ya chekechea.

Kama nyongeza kwa nyimbo katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kutumia nyimbo za watoto kutoka kwenye tamaduni yako mwenyewe. Hakikisha nyimbo zinafikia kiwango kifuatacho:

  • Ni fupi na rahisi.

  • Zinatumia noti fupi (noti 5 hadi 8)

  • Maneno ni ya kurudiarudia (maneno yale yale yametumika mara kadhaa) na ni rahishi kujifunza.

  • Maneno yanaelezea vitu ambavyo watoto wanaweza kuviona, kusikia, kugusa, kunusa, au kuhisi.

  • Maneno yasiyo kinyume na mafundisho ya injili.

Chapisha