Somo la 24
Mimi Nawapenda Kaka na Dada Zangu
Madhumuni
Ni kumtia moyo kila mtoto kuonyesha upendo kwa kaka na dada zake.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Kutoka 1:22–2:10.
-
Kwa idhini ya Rais wako wa Msingi, mwalike mama amlete mtoto wake mchanga darasani. Muombe aelezee namna gani yeye humtunza mtoto mchanga, ikijumuisha kile ambacho yeye na familia yake hufanya kumtunza mtoto kwa usalama. Mtie moyo yeye aelezee kuhusu upendo anaohisi kwa mtoto wake. Kama hakuna mama mwenye mtoto mchanga, unaweza kumwalika mama kuja na picha ya mtoto wake alipokuwa mchanga.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Mwanasesere Mtoto Mchanga
-
Picha 1-2, Musa katika Kisafina cha Manyasi (Picha za Sanaa za Injili 106; 62063); picha 1-13, Joseph Smith (Picha za Sanaa za Injili 400; 62449);
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Taarifa kwa mwalimu: Unapofundisha somo hili, uwe na usikivu kwa hisia za watoto katika darasa lako ambao hawana kaka au dada yoyote.
Shughuli za Kujifunza
Mwaalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Tunaweza kuwapenda kaka na dada zetu
-
Je, kuna yeyote kati yenu aliye na kaka au dada mchanga?
Acha watoto ambao wana na kaka au dada mchanga kuzungumza kuhusu mtoto mchanga na kuelezea jinsi familia yao ilivyojianda kwa ajili mtoto mchanga mpya.
-
Je, kuna ye yote kati yenu aliye na kaka au dada mkubwa?
Acha watoto wazungumze kwa dakika chache kuhusu kaka na dada zao. Wakumbushe watoto kwamba uliongea katika somo lilopita kuhusu namna gani familia zote ni tofauti. Baadhi ya watu wana kaka na dada wengi, na baadhi wana wachache tu au hawana kabisa. Bila kujali tuna kaka na dada wangapi, tunapaswa kuwapenda na kuwa wakarimu kwao.
Tunaweza kuwasaidia kaka na dada zetu
-
Unawezaje kuwasaida kaka na dada zako?
-
Kaka na dada zako wanakusaidiaje wewe ?
Tunaweza kusaidia kuwatunza kaka na dada zetu wachanga
Elezea kwamba wakati mwingine inakuwa vigumu wakati mtoto mchanga mpya anapozaliwa katika familia kwa sababu mtoto huchukua muda na usikivu mwingi wa wazazi. Wasaidie watoto kuelewa ingawa wazazi wanaweza kuwa na shughuli nyingi na mtoto mchanga mpya, bado wanawapenda wale watoto wao wengine wote. Wakumbushe watoto kwamba mtoto mchanga anahitaji karibu kila kitu, hali watoto wakubwa (kama wale walio katika darasa lako) wanaweza kufanya mambo mengi wenyewe na kwa kaka na dada yao mchanga.
-
Je, ungewezaje kuwasidia wazazi kutunza kaka au dada mchanga.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Wape watoto krayoni au penseli, na waache wachore picha ya kaka au dada zao. Acha watoto wachukue zamu kuonyesha picha zao na kuzungumza kuhusu kaka na dada zao. Watie moyo watoto wazungumze kuhusu mambo ambayo wanaweza kufanya pamoja na kaka na dada zao.
-
Tafuta picha ya mtoto mchanga ya kila mtoto, kisha acha watoto wabahatishe kila mtoto ni nani. (Hakikisha unarudisha picha ya kila mtoto kwa wazazi ikiwa haijaharibiwa.) Wakumbushe watoto ambao wana kaka na dada wakubwa kwamba kaka na dada zao walisaidia katika kuwatunza walipokuwa watoto wachanga.
-
Imbeni au mseme maneno ya “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 253), mkitumia vishazi kama vile “Kuliwaza mtoto ni furaha” au “Kumsaidia dada yangu ni furaha.” Buni vitendo kama inavyopendekezwa na maneno.
-
Imbeni au semeni maneno ya mstari wa kwanza wa “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 198) ukibadilisha dada au kaka, na mama, au imbeni mstari wa pili wa “A Happy Family” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 198).
-
Lete picha ya familia yako mwenyewe na waambie watoto kuhusu kaka na dada zako. Unaweza kuwasimulia watoto baadhi ya matukio ya furaha ambayo mliyoyapata pamoja.
-
Ukitumia viwakilishi kama vile mwanasesere mchanga, kijikapu au kijisanduku, na skafu, wasaidie watoto kuigiza hadithi ya Miriamu na mtoto Musa katika kijisafina cha manyasi.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Weka kitu kidogo cha mtoto mchanga kinachotambulika kwa urahisi katika mfuko au soksi kubwa. Acha watoto waingize mkono ndani bila kuangalia na wajaribu kubahatisha kitu hicho ni nini kwa kukigusa.
-
Imbeni au semeni maneno ya “A Happy Family” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 198). Hali mkiimba, shikaneni mikono na mtembee katika duara pamoja na watoto, au buni vitendo rahisi vinavyoendana na wimbo.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari wa shughuli ufuatao huku ukisema maneno:
Hivi ndivyo mtoto mchanga hufanya
Makofi - makofi - makofi - makofi (pigeni makofi),
Hivi ndivyo mtoto mchanga hufanya
Pikebuu, nakuona (cheza pikebuu kwa mikono)!
Hivi ndivyo mtoto mchanga hufanya
Nyata - nyata - nyata - nyata (fanya kwa vidole “kutembea” hewani).
Hivi ndivyo mtoto mchanga hufanya
Lala - lala - lala - lala (laza shavu kwenye mikono iliyokunjwa).
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari wa shughuli huku wakisema maneno:
Musa Mtoto Mchanga
Musa Mtoto Mchanga alikuwa na mashua kama kitanda (kunja mkono na uweke kidole kwenye ule mkono mwingine).
Dada yake mwenye upendo akimtunza katika manyasi pale alipomficha (chungulia katika vidole lkilichoweka machono).
Siku moja binti malikia akamwona (inama ukiangalia chini) na kumchukua katika mikono yake (jifanye kama kumwinua mtoto);
Alisema, “Mimi nitamchukua mtoto huyu na kumlinda dhidi ya hatari zote” (jifanye kumliwaza mtoto mikononi).
(Kutoka Fascinating Finger Fun na Eleanor Doan. © 1951. Imetumika kwa Idhini.)