Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 40: Sakramenti Hunisaidia Kumfikiria Yesu


Somo la 40

Sakramenti Hunisaidia Kufikiria juu ya Yesu

Madhumuni

Ni kumtia moyo kila mtoto kufikiria juu ya Yesu Kristo wakati wa sakramenti.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Luka 22:19–20 na 3 Nefi 8:1–11. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 23.

  2. Kwa idhini ya rais wa Msingi, muombe askofu aandae mshiriki wa akidi ya makuhani aje kwenye darasa lako kwa dakika chache mwanzoni mwa somo. Mshiriki wa akidi ya makuhani anapaswa kujiandaa kuwaambia watoto kuhusu majukumu yake katika kuhudumia sakramenti na hisia zake kuhusu ibada hii takatifu.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia na Kitabu cha Mormoni

    2. Picha za matukio kutoka katika maisha ya Yesu kama vile 1-16, Kuzaliwa kwa Yesu (Sanaa ya Picha za Injili 201; 62495); picha 1-17, Mvulana Yesu Hekaluni (Sanaa ya Picha za Injili 205; 62500); picha 1-19, Kristo na Watoto (Sanaa ya Picha za Injili 216; 62467); picha 1-43, Yesu Akimponya Kipofu (Sanaa ya Picha za Injili 213; 62145); na nyinginezo zo zote unazotaka kutumia.

    3. Picha 1-3, Yesu Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 240; 62572); picha 1-8, Kupitishwa kwa Sakramenti (62021); picha 1-44, Yesu Akifundusha katika Dunia ya Magharibi (Sanaa ya Picha za Injili 316; 62380); picha 1-70, Karamu ya Mwisho (Sanaa ya Picha za Injili 225; 62174).

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Onyesha picha 1-8, Kupitisha Sakramenti. Waambie watoto kwamba mkutano wa Jumapili ambapo tunakutana pamoja kama familia unaitwa mkutano wa sakramenti.

  • Kwa nini tunaita mkutano huu mkutano wa sakramenti?

Mtambulishe mshiriki wa akidi ya makuhani kwa watoto. Acha yeye awaambie kuhusu majukumu ya wenye Ukuhani wa Haruni juu ya sakramenti. Acha yeye aelezee hisia zake kuhusu wajibu wake katika ibada hii takatifu. Mshukuru kwa ajili ya kuja kwake na umruhusu arudi kwenye mkutano wake wa akidi au darasa la Shule ya Jumapili.

Yesu alitupa sakramenti ili kutusaidia sisi kumkumbuka Yeye

Onyesha picha 1-3, Yesu Kristo Wakumbushe watoto kwamba Yesu ni mwana wa Baba wa Mbinguni. Kwa sababu Yesu anatupenda sana, alikuja ulimwenguni kuwa Mwokozi wetu. Yeye aliwaponya wagonjwa, akafundisha injili, na kuonyesha njia sahihi ya kuishi. Kisha alikufa kwa ajili yetu.

Hadithi

Onyesha picha 1-70, Karamu ya Mwisho. Simulia hadithi ya Karamu ya Mwisho, kama inavyopatikana katika Luka 22:19–20. Soma kwa sauti kutoka kwenye Biblia kifungu cha mwisho cha mstari wa 19: “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Elezea kwamba Yesu aliwaambia Mitume Wake kuwa wakutane pamoja kila siku ya Sabato na kumkumbuka yeye kwa kupokea sakramenti.

Onyesha picha 1-44, Yesu Anafundisha katika Nchi za Magharibi. Elezea kuwa Yesu alipowatembelea Wanefi, aliwaambia wakutane pamoja siku ya Sabato na kumkumbuka yeye kwa kupokea sakramenti (ona 3 Nefi 18:1–11).

  • Mitume walitakiwa kumfikiria nani walipokuwa wanapokea sakramenti?

  • Wanefi walikuwa wanatakiwa kumfikiria nani wakati wanapokea sakramenti?

  • Ni nani sisi tunapaswa kumfikiria tunapopokea sakramenti?

  • Tunapokea sakramenti lini?

Shughuli

Fanya shughuli mstari ifuatayo pamoja na watoto:

Mimi Nafurahi Nimekuja Kanisani Leo

Mimi Nafurahi Nimekuja Kanisani Leo (piga makofi na ujenge mnara wa kanisa kwa kuweka vidole vya mbele pamoja).

Mimi napenda kusikiliza (kunjia kiganja sikioni).

Na kusali (kuja mikono na uinamishe kichwa).

Najifunza kuhusu Yesu aliye huko juu (ota juu);

Ninafikiria kuhusu Kristo na upendo wake (jikumbatie mweyewe).

Hadithi

Onyesha picha za maisha ya Yesu moja baada ya nyingine. Ikiwa watoto wanatambua picha, acha wasimulie hadithi hiyo. Kama hawajui hadithi hiyo, waelezee kwa ufupi. Acha watoto wengi kadiri iwezekanavyo washiriki katika kusimulia hadithi.

  • Ni hadithi gani za Yesu unazoweza kufikiria juu yake wakati wa sakramenti?

Waache watoto wasimulie hadithi kuhusu Yesu ambazo wanaweza kufikiria juu yake wakati wa sakramenti. Kama hawawezi kufikiria yo yote, wasimulie hadithi moja ua mbili juu ya Yesu ambazo wewe unapendelea kufikiria juu yake wakati wa sakramenti.

Tunaweza kuwa na staha wakati wa sakramenti

Shughuli

Wasaidie watoto kusema mstari ufuatao, wakitumia vitendo vilivyoelezwa:

Mimi Nitakunja Mikono Yangu (kunja mikono),

Mimi nitainamisha kichwa changu (inamisha kichwa),

Na kimya, kimya niwe (nong’ona mstari huu).

Wakati sakramenti inapobarikiwa,

Nitakukumbuka Wewe.

Elezea kwamba kwa sababu Yesu alitupa sakramenti ili kutusaidia kumkumbuka Yeye, ni muhimu sisi kufikiria juu ya Yesu na kuwasaidia wengine kufikiria juu yake Yeye pia. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuwa na staha wakati wa sakramenti.

Shughuli

Nong’ona mojawapo ya kauli zifuatazo kwa mtoto na muache yeye airudie kwa sauti kwa darasa. Endelea na kauli zingine na kwa watoto wengine.

  1. Tunajitayarisha kwa ajili ya sakramenti kwa kuimba wimbo wa staha ambao unatukumbusha juu ya Yesu.

  2. Tunasikiliza kwa makini sala ya kubariki mkate inaposemwa.

  3. Mkate unapopitisha kwetu, tunachukua kipande kimoja tu.

  4. Tunasikiliza kwa makini sala ya kubariki maji inaposemwa.

  5. Kwa staha tunakunywa maji na kuweka kikombe kwenye trei.

  6. Kamwe hatuchezi na mkate au vikombe vya sakramenti.

Elezea kwamba kufanya mambo haya huonyesha sisi tuna staha wakati tunapopokea sakramenti.

  • Tunawezaje kuwa na staha wakati wa sakramenti?

Shughuli

Acha watoto wasikilize kwa makini vitendo unavyoelezea. Waambie watoto wasimame kama unasema kitu fulani wanachopaswa kufanya au kukifikiria wakati wa sakramenti. Waambie waketi chini kama unasema kitu wasichopaswa kufanya ua kukifikiria wakati wa sakramenti. Tumia mifano ifuatayo au yako mwenyewe.

  • Sikiliza kwa makini wakati sala za sakramenti zinaposemwa.

  • Kumbuka kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatupenda.

  • Fikiria kuhusu kwenda pikiniki

  • Kumbuka kwamba Yesu aliwaponya watu wagonjwa.

  • Zungumza na kaka au dada yako.

  • Jichezeshe chezeshe

  • Fikiria juu ya Yesu akiwabariki Watoto

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako kuhusu jinsi unavyoshukuru kupokea sakramenti ili kumkumbuka Yesu Kristo na lile ambalo ametufanyia sisi. Elezea kwamba wewe unashukuru sana hususani wakati kila mtu anapokuwa na staha wakati wa sakramenti ili uweze kuzingatia katika kufikiria juu ya Yesu.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Imba au sema maneno “Before I Take the Sacrament” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 73) au ”To Think about Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 71).

  2. Acha mtoto achore picha yake mwenyewe akipokea sakramenti. Andika kila picha Mimi ninaweza kumfikiria Yesu wakati nikipokea sakramenti.

  3. Lete darasani trei tupu za mkate na maji. Acha watoto wachukue zamu kutazama na kushika trei hizo. Acha watoto waelezee kile kinachotendeka wakati wa huduma ya sakramenti katika mkutano wa sakramenti.

  4. Acha watoto waigize baadhi ya hadithi wazipendazo kutoka katika maisha ya Yesu.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Elezea kwamba sakramenti ni njia iliyorahisishwa: Onyesha picha ya Yesu na uwaambie watoto kuna muda siku ya Jumapili ambao sisi tunamkukmbuka Yesu kwa njia maalumu. Huu ni wakati tunakula kipande cha mkate na kunywa kikombe kidogo cha maji wakati wa mkutano wa Sakramenti. Elezea kwamba wakati wa sakramenti tunakumbuka ni kiasi gani Yesu anavyotupenda na kufikiria kuhusu mambo mengi ambayo ametufanyia ili kutusaidia kuwa na furaha.

  2. Imba au sema maneno “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 57, au ”Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 60).

  3. Wasaidie watoto kufanya matendo ya mstari wa shughuli huku wakisema maneno:

    Uumbaji

    Yesu alisema jua liangaze (fanya duara kubwa juu ya kichwa kwa mikono),

    Mvua inyeshe (teremsha mikono chini mbele ya mwili wako ukichezesha chezesha vidole),

    Maua yakue (kunja mikono, viganja vikielekea juu).

    Yesu alisema ndege na waimbe (fungua na ufungue vidole na gumbu mfano wa mdomo wa ndege.

    Na ikawa hivyo, ikawa hivyo (kunja mikono).

    (Johnie B. Wood, katika Sing, Look, Do, Action Songs for Children, ed. Dorothy M. Peterson [Cincinnati: Standard Publishing Co., 1965].)

    Wakumbushe watoto kwamba Yesu alitupa vitu vingi ili kutufanya tuwe na furaha. Wakati wa sakramenti tunaweza kuonyesha kuwa tunashukuru kwa kufikiria juu ya Yesu.

Chapisha