Somo la 26
Familia Zinaweza Kuwa Pamoja Milele
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba mahekalu ni sehemu takatifu, ambapo familia zinaweza kuuganishwa pamoja milele, na kumhimiza kila mtoto kujiaanda kuingia hekaluni.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mafundisho na Maagano 97:15–17 na 124:37–41. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 36, na “Hekalu” katika Kamusi ya Biblia
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Nakala ya Mafundisho na Maagano.
-
Picha 1-5, Familia na Mtoto (62307); picha 1-7, Familia yenye Upendo; picha 1-54 Hekalu la Salt Lake (Sanaa za picha za injili 502; 62433); picha za mahekalu zinazopatikana (Sanaa za picha za injili 505; 62434–62448, 62566–62569, 62583–62601, 62613–62619); ukurasa wa michoro mwishoni wa somo.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Hekalu ni mahali patakatifu
Elezea kwamba hekalu ni mahali patakatifu (ona M&M 97:15–17). Waombe watoto warudie neno takatifu. Hii humaanisha kwamba hekalu ni mahali maalum sana ambapo kila kitu kinatukumbusha Baba wa Mbinguni na Yesu.
Waambie watoto kwamba kama wanashika amri za Baba wa Mbinguni, wanaweza kwenda hekaluni watakapokuwa watu wakubwa. Elezea kwamba katika hekalu tunafanya ahadi maalum na Baba wa Mbinguni na Yesu za kutii amri zake. Pia tunaweza kuoana katika hekalu, na tunaweza kubatizwa kwa niaba ya watu ambao hawakubatizwa walipokuwa hai walipokuwa duniani.
Acha watoto wainue vidole vitatu na urudie vitu vitatu wanavyoweza kufanya katika hekalu watakapokuwa watu wakubwa:
“Katika hekalu tunaweza kufanya ahadi maalum na Baba wa Mbinguni.”
“Katika hekalu tunaweza kuoana.”
“Katika hekalu tunaweza kubatizwa kwa niaba ya wengine.”
Mahekalu husaidia familia kuwa pamoja milele
Picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga, na picha 1-7, Familia yenye Upendo. Elezea kwamba mahekalu yanaweza kusaidia familia kuwa pamoja milele. Wakati mwanaume na mwanamke wanapooana katika hekalu na kutii amri, Baba wa Mbinguni huwaahidi wao kwamba wanaweza kuwa pamoja na watoto wao wote milele. Tunaita hii kuunganishwa kama familia?
-
Ni watu gani walio katika familia yako?
-
Unahisi vipi unapokuwa pamoja na familia yako?
-
Ni kwa namna gani familia zinaweza kuwa pamoja milele?
Waambie watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanaipenda kila familia na wanataka kila familia kuunganishwa pamoja milele. Elezea kwamba familia ambazo hazijaunganishwa hekaluni zinaweza kujiandaa kwa kutii amri za Baba wa Mbinguni. Kisha zinaweza kwenda hekaluni kuunganishwa kama familia.
Ninaweza kujiandaa kwenda hekaluni
Wakumbushe watoto kwamba kila mtu ambaye hutii amri za Baba wa Mbinguni anaweza kwenda hekaluni. Onyesha ukurasa wa michoro uliyojumuishwa mwisho wa somo na acha watoto wajadili amri zilizoonyeshwa hapo. Elezea kwamba kutii amri hizi kutawasaidia watoto kuwa wenye kustahili kwenda hekaluni wanapokuwa wakubwa.
-
Omba.
-
Tii wazazi.
-
Pendaneni.
-
Nenda kanisani
-
Kulipa zaka.
-
Kula vyakula vizuri (kutii Neno la Hekima).
-
Kuwa mwaaminifu.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Wasaidie watoto kuelewa kwamba milele ni muda mrefu. Unaweza kuwaambia kwamba ni muda mrefu sana kuliko ule wanaongojea siku yao ya kuzaliwa au sikukuu inayofuata; ni muda mrefu mtu mzee wanayemjua amekuwa hai; ni muda mrefu kuliko sasa hadi nyakati Adamu na Hawa walipokuwa hai. Elezea kwamba milele humaanisha kitu kisicho na mwisho.
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mstari ufuatao unaposema maneno haya:
Milele ni Muda Gani?
Milele ni muda gani (onyesha kichwa na kidole, kana vile unafikiria)?
Ni muda mrefu kushinda mwaka (weka ngumi kidevuni, na uweke kiwiko juu ya ule mkono mwingine).
Ni muda mrefu kushinda wakati inachukua (weka ile ngumi ingine kidevuni, na uweke kiwiko juu ya ule mkono mwingine).
Kwa Krismasi kufika.
Milele ni muda gani (onyesha kichwa na kidole, kana vile unafikiria)?
Sio muda mrefu kuishi (tikisa kidole)
Na familia ambayo unaipenda (jikumbatie [mwenyewe).
Kwani kamwe, haitaisha!
-
Kwa idhini ya rais wako wa Msingi, waalike wazazi wa mtoto wa darasa lako waje kuelezea hisia zao kuhusu umuhimu wa kuunganishwa pamoja.
-
Tengeneza nakala ya ukurasa wa michoro uliopo mwisho wa somo kwa kila mtoto. Waache watoto wapake rangi michoro hii.
-
Kwa idhini ya rais wako wa Msingi, alika familia katika kata yako ambayo hivi karibuni ilienda hekaluni kuunganishwa kusimulia darasa kuhusu tukio hilo.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari ufuatao huku ukisema maneno:
Mimi Ni Msaidizi
Sasa kwamba mimi ni mkubwa na mrefu (simama kwa vidole na ukinyoosha mikono juu sana).
Nitakuwa msaidizi mzuri.
Msaidizi wa baba (inua kidole cha kwanza juu).
Ambaye ni mkarimu na ni mwema;
Nitamfanyia mama yangu hivyo (inua kidole cha pili juu).
Mambo ambayo ninapaswa.
Msaidizi wa dada (inua kidole cha tatu juu).
Na kaka pia (inua kidole cha nne juu).
Msaidizi wa marafiki zangu wote wakweli (inua kidole gumba juu)
Msaidizi wa Mungu nitajaribu kuwa.
Kwa kuwapenda wengine jinsi anavyonipenda (kunja mikono).
Nataka kuwa msaidizi wa wote (nyoosha mikono kabisa),
Sasa kwamba mimi ni mkubwa na mrefu (simama vidole na ukinyoosha mikono juu sana).
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mstari wa shughuli ufuatao huku ukisema maneno: Rudia mara nyingi kama unavyotaka.
Fanya duara kila mtu akisimama na ukishikana mikono. Shikaneni mikono wakati wote wa shughuli.
Sisi wote tuliishi pamoja na Baba wa Mbinguni (kila mtu aje karibu pamoja, na kuleta mikono katikati ya duara).
Alitutuma hapa duniani ili tuishi (fungueni duara kubwa).
Alitupatia familia za kutupenda na kufundisha (njooni karibu pamoja tena).
Familia zetu zitatusaidia kuishi pamoja naye tena (fungueni duara kubwa).
-
Tengeneza mchoro rahisi wa hekalu kwenye karatasi ili watoto wapake rangi.