Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 45: Ufufuko wa Yesu Kristo (Pasaka)


Somo la 45

Ufufuko wa Yesu Kristo (Pasaka)

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba Yesu Kristo alifufuka.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Luka 23:33–24:12, 36–40, 51. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 12.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Picha 1-3, Yesu Kristo (Picha za Sanaa za Injili 240; 62572); picha 1-16, Kuzaliwa kwa Yesu (Picha za Sanaa za Injili 201; 62495); picha 1-55, Mahubiri Mlimani (Picha za Sanaa za Injili 212; 62166); picha 1-59, Kusulubiwa (Picha za Sanaa za Injili 230; 62505); picha 1-72, Yesu Akiomba Gethsemane (Picha za Sanaa za Injili 227; 62175); picha 1-73, Kuzikwa kwa Yesu (Picha za Sanaa za Injili 231; 62180); picha 1-74, Yesu Anaonyesha Makovu Yake (Picha za Sanaa za Injili 234; 62503)

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Shika picha 1-3, Yesu Kristo, ikitazama chini kwenye paja lako. Waambie watoto kwamba utazungumzia kuhusu mtu ambaye ni muhimu sana. Waombe watoto wabahatishe mtu huyu ni nani baada ya wewe kuwapa vidokezo:

  1. Mtu huyu anampenda kila mtu sana.

  2. Aliishi duniani zamani sana na kuanzisha Kanisa Lake.

  3. Alitufundisha jinsi ya kuishi na kuwa na furaha.

  4. Aliwabariki watu na kuwaambia wawe wakarimu na wenye upendo.

Wakati wanafunzi wameshabahatisha (au wewe umewaambia) kwamba mtu huyu ni Yesu, onyesha picha hiyo.

Yesu anatupenda

Wakumbushe watoto kwamba Yesu ni mwana wa Baba wa Mbinguni. Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu duniani kwa madhumuni muhimu.

Hadithi

Onyesha picha 1-16, Kuzaliwa kwa Yesu. Kwa ufupi simulia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Pengine ungependa watoto wakusaidie kusimulia hadithi hii. Wakumbushe kwamba Yesu alikuwa mtoto maalum sana.

Onyesha picha 1-55, Mahubiri Mlimani. Elezea kwamba wakati Yesu alipokomaa, alianzisha kanisa Lake na kuwafundisha watu jinsi ya kuishi na kupendana.

Wimbo

Acha watoto waimbe au waseme maneno ya “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 61), wakitumia vitendo:

Yesu alisema mpende kila mtu (panua mikono wazi kabisa);

Watendee kwa ukarimu, pia (ishara ya kichwa ya kukubali),

Wakati moyo wako umejawa na upendo (weka mkono juu moyo),

Wengine watakupenda (jikumbatie mwenyewe).

Onyesha picha 1-72, Yesu Akiomba huko Gethsemane.

  • Je! Yesu anafanya nini katika picha hii?

Elezea kwamba kabla ya Yesu kufariki, alienda kuomba katika sehemu iliyoitwa Bustani ya Gethsemane. Yesu aliteseka hapa kwa ajili ya dhambi zetu ili tuweze kutubu na kusamehewa makosa ambayo tumefanya. Yesu alikuwa mtu wa pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa ajili yetu. Alifanya hivyo kwa sababu anatupenda sana.

Yesu alfufuka

Elezea kwamba watu wengi ambao waliishi wakati wa Yesu ulimwenguni walimpenda. Hata hivyo, baadhi ya watu hawakumpenda Yesu. Hawakuamini Yeye alikuwa mwana wa Baba wa mbinguni.

Hadithi

Onyesha picha 1-59, Usulubisho. Elezea kwa urahisi neno Usulubisho, kama ilivyoelezewa katika Luka 23:33–46. Elezea kwamba watu ambao hawakumpenda Yesu walikuwa wakatili sana kwake. Askari walipigilia misumari katika mikono na miguu ya Yesu na kutundika kwenye msalaba. Walimwacha Yesu Kristo msalabani mpaka akafariki. (Uwe makini katika kusumulia hadithi hii katika shughuli iliyopo chini. Baadhi ya watoto wanaweza kuwa wepesi kudhuriwa na wazo la watu kumuumiza Yesu.)

Elezea kwamba wakati Yesu akifariki, roho yake aliuacha mwili wake na kwenda mbinguni. Wakumbushe watoto kwamba kila mmoja wetu ana roho. Roho zetu haziwezi kuonekana, lakini ndizo zinatufanya tuwe hai.

Onyesha picha 1-73, Mazishi ya Yesu. Elezea kwamba watu ambao walimpenda Yesu waliutwaa mwili wake na kuuzinga makini kwa vitambaa. Wakaumbeba mwili wa Yesu hadi kaburini (sehemu kama pango ambapo watu walizikwa) na pole pole wakauweka mwili wake chini (ona Luka 23:50–56).

Onyesha picha 1-74, Yesu Anaonyesha Makovu Yake. Elezea kwamba siku tatu baada ya Yeye kufa, Yesu alifufuka. Alikuwa hai tena. Wakati Yesu alifariki, roho yake iliuacha mwili wake. Wakati yeye alifufuka, mwili wake ulirudi tena kwenye mwili wake. Yesu Kristo alikuwa ndiye mtu wa kwanza kufufuka.

Elezea kwamba watu wengi walimwona Yesu baada ya yeye kufufuka (ona Luka 24). Yesu aliwafundisha marafiki zake na kuwaonyesha mwili wake uliofufuka (ona Luka 24:36). Aliwaacha marafiki zake kumgusa ili wajue kwamba mwili wake uliofufuka ulikuwa wa nyama na mifupa (ona Luka 24:39–40). Baada ya kuwafundisha watu, Yesu alienda kuishi tena na Baba wa Mbinguni (ona Luka 24:51).

Elezea kwamba siku ile Yesu alifufuka ilikuwa Pasaka ya kwanza. Tunasherekea Pasaka kila mwaka: ili kutusaidia kukumbuka kwamba Yesu alifufuka.

Shughuli

Acha watoto wasimame na kufanya vitendo vya msitari ufuatao:

Yesu Akawa Hai Tena

Siku tatu baada ya Yesu kufariki (inua vidole vitatu juu).

Kulikuwa na makovu kawenye mikono na miguu yake (onyesha viganja vya mikono na miguu).

Na kovu la mkuki katika ubavu wake (onyesha ubavu).

Yesu alikuja na akatufundisha sote (panua mikono kabisa).

Kuishi Injili ya kweli (kunja mikono).

Kwa sababu Yesu alifufuka.

Sisi pia tutafufuka (ishara ya kichwa ya kukubali).

Sisi tutafufulka

Wasaidie watoto kuelewa kwamba Yesu alirudi tena kuwa hai baada ya kufakariki. Yesu yu hai sasa hivi mbinguni, na kamwe hatafariki tena. Elezea kwamba Yesu alifanya iwezekane kwetu kufufuka kama yeye. Hii inamaaisha kuwa kila mmoja wetu ataishi baada ya sisi kufa

  • Je! Unamjua mtu yeyote ambaye alifariki?

Eleza kuwa watu wanapofariki, roho zao bado huwa hai. Siku moja watafufuka, ambako humaanisha miili yao na roho zao zitaungana tena kama Yesu alivyofanya. Ukipenda unaweza kuwaelezea watoto kwamba tunaweza tusifufuke baada ya siku tatu, kama Yesu, lakini sisi wote tutafufuka siku moja.

Acha watoto warudie neno kufufuka mara kadhaa na uwaambie inamaanisha nini.

Eleza jinsi ilivyo ajabu sana kujua kwamba watu wote wanaowajua na kuwapenda—wazazi wetu, kaka, dada, babu na bibi, na marafiki—kuwa watafufuka. Sisi wote tutaishi baada ya kufariki. Yesu ndiye aliyefanya hili liwezekane.

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako kwamba Yesu anampenda kila mmoja wetu. Kwa sababu ya upendo wake mkuu kwetu, aliteseka na kufa na kufufuka ili kwamba kila mmoja wetu pia afufuke siku moja.

Shughuli zenye Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Kwa ufupi jadili baadhi ya matukio ya Pasaka na desturi ambazo watoto wanazifahamu. Kiri kwamba desturi za kilimwengu za Pasaka zinafurahisha, lakini wasaidie watoto kutenganisha mawazo hayo na maana halisi ya Pasaka.

  2. Waonyeshe watoto glovu ama glovu ya kiganja. Linganisha miili yetu ya duniani na mkono iliovikwa glovu. Onyesha jinsi mkono (roho) huifanya glovu (mwili) kutenda. Toa glovu na elezea kwamba hii kama kifo kimwili. Roho na mwili zimetangaishwa, na mwili hauwezi kutenda. Vika glovu tena katika mkono na uelezee kwamba hii kama kufufuliwa. Sasa roho na mwili vimeunganishwa. Wakumbushe watoto kwamba Yesu alifufuka, watu wote watafufuliwa siku moja.

  3. Tengeneza nakala za kitini za “Yesu Kristo ni Rafiki Yetu Mpendwa,” inayopatikana mwishoni wa somo la 6, na acha watoto waipake rangi.

  4. Rusha ama mpe mtoto kijifuko cha maharagwe au kitu laini kwa mtoto na muache ajibu mojawapo ya maswali yaliyopo hapo chini (ama swali kama hilo) kabla ya kukirusha au kukupa kijifuko cha maharagwe. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu ya kujibu swali.

    • Kwa nini tunasherehekea Pasaka?

    • Nani alikuwa mtu wa kwanza kufufuka?

    • Inamaanisha nini kufufuka?

    • Mwili wa Yesu ulikuwa wapi baada ya yeye kufariki?

    • Baada ya Yesu kufufuka, watu wengi walimwona Yesu?

    • Kwa nini Yesu aliwaambia watu waguse mwili wake uliofufuliwa?

    • Ni kina nani ambao watafufuliwa kwa sababu Yesu alifufuka?

  5. Acha watoto waimbe au waseme maneno ya “ “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 64) au “Jesus Has Risen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 70).

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Wasaidie watoto kufanya matendo mstari wa shughuli ufuatao unaposema maneno:

    Yesu Amefufuka!

    Hapa ndipo mahali ambapo Yesu alikuwa amelala (onyesha)

    Ona, jiwe limeviringishwa mbali!

    Inama chini; tazama ndani :inama chini na tumia mkono kukinga macho)

    Hayupo hapa (simama)!

    Yesu Amefufuka! Jipeni moyo (pigeni makofi)!

    (Dana Eynon, katika Bible Story Finger Plays and Action Rhymes [Cincinnati, Ohio: Standard Publishing Co., 1964], uk. 29.)

  2. Elezea kwamba Yesu alikufa na kufufuka msimu wa majani kuchipuka. Msimu wa majani kuchipuka ni wakati wa maisha mapya. Miti na maua huanza kukua tena. Wanyama wengi huzaliwa msimu wa majani kuchipuka. Kila mtoto na achore picha inayoonyesha ya maua au wanyama mchanga. Onyesha picha1-3, Yesu ndiye Kristo, na uelezee kwamba kwa sababu Yesu alifufuka, sisi wote tutaishi tena baada ya kufariki.

  3. Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno ya “Jesus Loved the Little Children” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 59) au “Jesus Is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.58). Wakumbushe watoto kwamba tunasherekea Pasaka ili kumkumbuka Yesu na ufufuko Wake.