Somo la 9
Ninashukuru kwa ajili ya Maji
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuwa na shukrani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa ajili ya maji.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:9–10; Kutoka 17:1-6; na Mathayo 3:13–17.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Kama inawezekana, tumia picha za aina mbalimbali ya maji, kama maziwa, mito, na bahari.
-
Picha 1-8, Kupitisha Sakramenti (62021); picha 1-11, Mvulana Akibatizwa (60018); picha 1-18 Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu (Sanaa za picha za Injili 208; 62133).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Maji ilikuwa sehemu ya Uumbaji
Soma kwa sauti na uelezee Mwanzo 1:9–10.
-
Kwa nini maji ni muhimu sana kwetu?
-
Tunapataje maji yetu?
Wasaidie watoto kuelewa kwamba maji hutoka katika vyanzo vingi, ikijumuisha maziwa, mito, bahari, mvua, na theluji. Elezea kwamba theluji na barafu ni maji yaliyoganda. Onyesha picha za maji ulizopata na uzungumze kuhusu mahali ambapo maji yanatoka katika eneo lako.
Waambie watoto kwamba wewe una shukrani kwamba maji ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni.
Tunahitaji maji kufanya mambo mengi
-
Kwa nini tunahitaji maji? Maji hutumiwa kwa ajili gani?
Elezea kwamba vitu vingi vyenye uhai, ikijumuisha watu, wanyama, mimea, vinahitaji maji ili kuishi. Kama inawezekana, mpe kila mtoto kikombe kidogo cha maji ya kunywa. Zungumza kuhusu jinsi miili yetu haiwezi kuishi bila maji.
-
Ni kwa namna gani wanyama na mimea hupata maji inayohitaji.
Elezea kwamba sisi pia tunahitaji maji kufanya mambo mengine, kama vile kuoshea na kupikia.
Yesu alimpa Musa na Waisraeli maji huko jangwani
Maji ni muhimu katika Kanisa
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Karirini mstari ufuatao pamoja na watoto mara kadhaa, mkifanya vitendo kama inavyoelezwa:
Matone ya Mvua
Wakati maua yana kiu.
Na majani yamekauka (fungua mikono na uinyoshe juu kabisa),
Matone madogo ya furaha
Yanatiririka kutoka angani (lete mikono chini, uiviringe).
Katika vyote hunyunyiza (chezesha vidole upande upande).
Katika siku zake za furaha,
Mpaka uangavu wa joto la jua (weka mikono juu ya kichwa na fanya duara).
Huyafukuzilie mbali (ficha vidole nyuma).
-
Wasaidie watoto kuimba ua kusema maneno ya “Rain Is Falling All Around” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 241) au “’Give,’ Said Little Children” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.236).
-
Acha mtoto achore picha ya maji, kama vile ziwa, mto, au matone. Andika kwenye karatasi ya kila mtoto Ninashukuru kwa ajili ya Maji.
-
Acha watoto waseme kuhusu au wafanye igizo la njia ambazo wanaweza kucheza na maji, kama vile kuogelea, kuteleza barafuni, kutegengeza mtu wa theluji, au kurukaruka ndani ya vidimbwi.
-
Wasaidie watoto kuelewa kwamba maji hutusaidia kusafisha vitu. Acha watoto wafanye igizo la shughuli za kusafisha wakitumia maji, kama vile kuosha nguo au kunawa mikono.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Fanya shughuli zote au baadhi ya zifuatazo ili kuwasaidia watoto kujifunza njia tofauti za kutumia maji:
-
Mpe kila mtoto kiasi kidogo cha maji ya kunywa. Watoto wanapokunywa maji, elezea kwamba maji ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ulimwengu. Tunaweza kunywa maji tunapokuwa na kiu.
-
Weka maji kidogo katika bakuli na umsaidie kila mtoto kunawa mikono yake. Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu walitupangia sisi tuwe na maji. Elezea kwamba tunaweza kutumia maji kuosha vitu.
-
Kama inawezakana wapeleke watoto nje na uache kila mmoja wao anyunyize mmea maji. Au lete mmea darasani na umruhusu kila mtoto kunyunyiza maji kidogo kwenye mmea. Elezea kwamba mimea pia inahitaji maji kukua.
-
-
Fanya vitendo vifuatavyo huku watoto wakijifanya kuwa mvua inanyesha—pole pole kwanza, na kisha kidogo kidogo ikinyesha sana.
-
Gusisha ncha za vidole pamoja.
-
Gusisha mikono pamoja.
-
Gusisha magoti, yakibadilishana na mikono.
-
Gonga gonga kwa miguu.
-