Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 35: Naweza Kuwa na Huruma kwa Wanyama


Somo la 35

Naweza Kuwa na Huruma kwa Wanyama

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa umuhimu wa kuwa na huruma kwa wanyama.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mwanzo 2:19–20; 6–8.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Picha 1-28, Uumbaji—Viumbe Hai (Picha za Sanaa za Injili 100; 62483); picha 1-30, Nuhu na Safina Ikiwa na Wanyama (Picha za Sanaa za Injili 103; 62305);

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwaalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Jifanye kuwa mnyama ambaye anajulikana na watoto. Acha watoto wengine wabahatishe wewe ni mnyama gani. Acha kila mtoto achukue zamu kujifanya ni mnyama hali watoto wengine wakibahatisha yeye ni mnyama gani.

Adamu alimpa kila mnyama jina

Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni ndiye aliyepanga na Yesu akaumba wanyama, samaki, ndege, na wadudu duniani. Onyesha Biblia na uwaelezee watoto kwamba maandiko yanatuambia kwamba Adamu aliwapa wanyama wote majina (ona Kutoka 2:19–20). Onyesha picha 1-28, Uumbaji—Viumbe Hai.

  • Taja majina ya wanyama walioko katika picha hii? (Acha watoto wachuke zamu kuonyesha mnyama katika picha na kutaja jina lake.)

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuwe na huruma kwa wanyama

Hadithi

Onyesha picha 1-30, Nuhu na Safina Ikiwa na Wanyama, urejee hadithi ya Nuhu na Safina, kama inavyopatikana katika Mwanzo 6–8. Sisitiza kwamba angalao wanyama wawili wa kila aina waliokolewa wasizame. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawapenda wanyama na wanataka wawepo duniani.

  • Kwa nini Nuhu aliwaweka wanyama kwenye safina?

  • Ni wanyama gani unashukuru kwamba Nuhu aliwaweka kwenye safina?

  • Je, unafikiria Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuwatendee vipi wanyama?

Hadithi

Kwa maneno yako mwenyewe, simulia hadithi ya Rais Spencer W. Kimball, Rais wa kumi na mbili wa Kanisa.

Wakati Spencer W. Kimball alipokuwa mvulana, kazi yake ilikuwa ni kuwapeleka ng’ombe malishoni umbali wa maili moja kutoka nyumbani kwao. Siku moja alitengeneza kombeo, chombo ambacho angeweza kumtumia kutupia mawe kwenye vigingi vya ua na mashina ya miti. Akawa mweledi sana na angeweza kupiga mti au kigingi cha ua ambacho kilikuwa mbali.

Miti mirefu ilikua kando mwa barabara pale alipokuwa akilisha ng’ombe. Spencer aliona kwamba kulikuwa na ndege wengi wadogo kwenye hiyo miti. Wakati alipowaona wale ndege, alipatwa na majaribu ya kuwapiga kuonyesha jinsi alivyokuwa na shabaha. Basi lakini akakumbuka wimbo ambao alikuwa akiuimba katika Msingi. Unasema, “Usiue ndege wadogo. … Ulimwengu ni shamba la Mungu, na huwapa chakula wadogo kwa wakubwa.” Spencer alifikiria juu ya maneno yale aliyoyaimba. Akaamua kwamba wale ndege walikuwa muhimu kwa Baba wa Mbinguni, haikuwa vyema kuwaua. Kwa hivyo daima alikuwa makini sana kutupa mawe kwa kombeo lake pale hasingewapiga ndege wo wote (ona Conference Report, Apr. 1978, p. 71; au Ensign, May 1978, p. 47).

  • Spencer W. Kimball alionyesha vipi huruma wa wale ndege.

Waambie watoto kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka tuwe na huruma kwa wanyama wote.

Wimbo

Imbeni au semeni maneno ya “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 145).

Nataka kuwa mkarimu kwa kila mtu.

Kwani hivyo ni vyema, unaona.

Kwa hivyo najisemea mwenyewe, “Kumbuka hili.

Ukarimu unaanza nami.

  • Unao wanyama wa kufuga?

Shughuli

Waalike watoto wazungumze kuhusu wanyama wao wa kufuga na jinsi wanavyowatunza. Soma kauli ifuatayo na uwaache watoto wainue vidole gumba vyao juu kama kauli hiyo ni njia bora ya kuwatendea wanyama wa kufuga. Acha waweke vidole gumba vyao chini kama njia hiyo si ya ukarimu kuwatendea wanyama wa kufuga.

  • Walishe chakula kizuri kila siku.

  • Sahau kuwalisha.

  • Sahau kuwapa maji.

  • Kuwa na maji safi ya wao kunywa.

  • Andaa mahali salama na pazuri pa wao kulala.

  • Wafungie ndani katika sehemu yenye joto siku nzima.

  • Wape upendo na usikivu.

Ushuhuda

Wakumbushe watoto kwamba wanyama waliumbwa na Yesu na ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tuwe na huruma kwa wanyama. Elezea unavyojisikia kuhusu mnyama wa kufugwa au kuhusu wanyama.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Tengeneza nakala ya sungura iliyo mwisho wa somo hili kwa kila mtoto, na uache watoto wawapake rangi sungura wao. Gandisha mpira wa pamba kwenye mkia wa kila sungura ili aonekane kunenepa.

  2. Imbeni au semeni maneno ya “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 228).

  3. Ukitumia ufito wa kuvua samaki kutoka somo la 11 na mikato ya wanyama ambayo uja na kitabu hiki cha kiada, waache watoto wachukue zamu kuvua mnyama. Wakati kila mtoto anaposhika mnyama, acha watoto wachukue zamu kuonyesha wanyama wao na kueleza kile wanajua kuwahusu.

  4. Tengeneza beji ambayo inasema Mimi nitakuwa na huruma kwa wanyama kwa kila mtoto ili aivae nyumbani.

  5. Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mchezo wa vidole ufuatao:

    Paka Mdogo

    Paka wangu mdogo kakimbilia mtini (”tembeza vidole ya mkono wa kulia kwenye ule wa kushoto)

    Kajikalia kitako akinitazama mimi (acha mkono wa kulia kwenye bega la kushoto).

    Mimi nikasema, “Njoo, nyau,” akateremka akikimbia (tembeza vidole vikirudi chini ya mkono)

    Na akala chakula chote nilichomwekea katika bakuli yake (kunja mkono; jifanye mkono wako wa kulia ni mtoto wa paka akila chakula).

  6. Acha watoto wasimame na kufanya vitendo unapokariri mstari ufuatao:

    Nuhu

    Nuhu alijenga safina kubwa (nyoosha mikono kama umeipanua);

    Yeye alijua cha kufanya (weka kidole upande wa uso).

    Alipigilia, akakata, na akapima (fanya mwenendo kama ilivyosema)

    Kama alivyokuwa ameamriwa kufanya (Itikia kwa kichwa).

    Na Nuhu aliita familia yake (ashiria kwa mkono)

    Watembee kungia ndani ya mashua (tembea kwa utulivu)—

    Na wanyama, wawili kwa wawili (inua vidole viwili juu).

    Wakaingia ndani kuelea (fanya ishara kuelea kwa mikono).

    Mawingu mazito yakatanda (weka mikono juuu ya kichwa),

    Mvua ikanyesha (viringa vidole ukiigiza mvua)—

    Na ulimwengu wote ukafinikwa (fanya ishara ya kufagia kwa mikono),

    Hapakuwepo na nchi kavu kabisa (geuza kichwa upande na upande),

    Safina ilielea salama (fanya ishara kuelea kwa mikono)

    Siku nyingi usiku na mchana (weka mikono upande mmoja wa uso),

    Hatimaye jua lilichomoza tena (weka mikono daura juu ya kichwa)

    Na likaangaza vyema na kung’aa.

    Na maji yote nyakauka kabisa (weka mikono kufuani);

    Nchi kavu ikatokeza (mikono ilifunguka na ikielekea juu).

    Familia na Nuhu ikashukuru (inamisha kichwa na ukunje mikono)

    Kwamba Mungu daima yu karibu.

    (Imetoholewa kutoka kwenye mstari wa Beverly Spencer.)

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Waache watoto waongee kuhusu wanyama wao wa kufuga walio nao au wale wangependa kuwa nao. Jadili na watoto jinsi tunapaswa kuwatendea na kuwatunza wanyama wa kufuga.

  2. Imbeni au semeni maneno ya “The World Is So Big” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto , 235). Fanya vitendo kama inavyoashiriwa:

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Na ndani yake viumbe vya Mungu hupatikana.

    Milima (weka kwa umbo la mlima juu ya kichwa)

    Mabonde (weka viganja mbele ya mwili)

    Na miti mirefu (nyoosha mikono kwa urefu)

    Wanyama wakubwa (ishara ukubwa)

    Na wanyama wadogo (ishara ya udogo)

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Mungu anatupenda sisi wote; baraka zetu ni nyingi (kunja mikono na ujikumbatie).

  3. Onyesha mikato ya wanyama michache, moja kwa wakati, na uwaache watoto wakuambie kile wanachojua kuhusu kila mnyama na pale anapoishi, na mlio wake, na kile wanachopenda juu yake.