Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 43: Tuna Nabii Aliye Hai


Somo la 43

Tuna Nabii Aliye Hai

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba sisi tunabarikiwa tunapomfuata nabii.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze 1 Samweli 3:1–10, 19–20 Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 9.

  2. Orodhesha kwenye vipande vya karatasi binafsi mafundisho kadhaa ya nabii aliye hai kutoka kwenye hutoba za mkutano mkuu au maandishi katika magazeti ya Kanisa. Andaa angalao vipande vya karatasi vingi kadiri iwezekanavyo kulingana na idadi ya watoto darasani. Kunja vipande hivyo vya karatasi na uviweka katika bakuli au kikapu. Mafundisho yanaweza kujumuisha—

    • Jifunze kutoka katika maandiko kila siku.

    • Kuishika kitakatifu siku ya Sabato.

    • Kusali kila siku.

    • Nenda katika mkutano wa sakramenti na Msingi.

    • Kuwa mwaaminifu.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Picha 1-4, Ono la Kwanza (Sanaa ya Picha za Injili 403; 62470); picha 1-29, Kujengwa kwa Safina (Sanaa ya Picha za Injili 102; 62053); picha 1-42, Mvulana Samweli Aliyeitwa na Bwana (Sanaa ya Picha za Injili 111; 62498); picha 1-66, Musa na Kichaka Kinachoteketea kwa Moto (Sanaa ya Picha za Injili 107; 62239); picha ya nabii aliye hai.

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote zenye Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwaalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Moja kwa wakati, onyesha picha ya Nuhu (picha 1-29), Musa (picha 1-66), na Joseph Smith (picha 1-4). Waalike watoto waseme kile wanachojua kuhusu kile kinachotendeka katika kila picha.

Baada ya kujadili kile watoto wanachojua kuhusu picha hizi, kwa ufupi elezea kwamba Yesu alimwambia Nuhu ajenge safina ili familia yake iokolewe kutokana na gharika. Yesu alimwambia Musa akawatoe Waisraeli utumwani. Yesu alimwambia Joseph asijiunge na kanisa lo lote wakati huo duniani.

Manabii huzungumza na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Elezea kwamba Nuhu, Musa, na Joseph Smith wote walikuwa manabii. Nabii ni mtu ambaye huongea na Baba wa Mbinguni na Yesu. Kwa vile Baba wa Mbinguni na Yesu hawapo ulimwenguni kutufundisha, wana manabii wa kuwasaidia. Baba wa Mbinguni na Yesu humfundisha nabii, na nabii hutufundisha sisi kile tunachopaswa kufanya ili kwamba tuweze kubarikiwa na kuwa wenye furaha.

Hadithi

Onyesha picha 1-42, Mvulana Samweli Aliyeitwa na Bwana, na usimulie hadithi ya Samweli akiitwa kuwa nabii, kama ilivyopatikana katika 1 Samweli 3:1–10, 19–20. Soma 1 Samweli 3:10 kwa darasa.

Elezea kwamba Samweli alikuwa mvulana mdogo wakati Yesu alipoongea naye kwa mara ya kwanza. Alipokuwa amekua, aliwafundisha watu wake nini Baba wa Mbinguni na Yesu walitaka wao wafanye.

Shughuli

Waombe watoto watatu wajifanye kuwa wao ni Samweli. Eli, na Yesu na waigize hadithi hiyo. Rudia na watoto wengine katika nafasi hizi, kama inahitajika.

Tunaye nabii duniani leo

Onyesha picha ya nabii aliye hai. Waambie watoto kitu fulani unachojua kuhusu nabii.

Acha watoto wasimame na kusema, “(Jina la nabii aliye hai) ni nabii wa Mungu.”

  • Kwa nini tunamhitaji nabii aliye hai? (Ili tuweze kujua kile Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanye.

Elezea kwamba nabii hutufundisha sisi kwa kuongea katika mikutano mikuu. Mikutano na mikusanyiko mikubwa inayohudhuriwa na watu wengi. Tunaweza kumsikiliza nabii kwenye runinga, redio, au sauti na video iliyorekodiwa. Maneno yake pia yanaandikwa katika magazeti ya Kanisa ambayo wazazi wetu au watu wengine wanaweza kutusomea.

Shughuli

Acha kila mtoto achague kipande cha karatasi kutoka kwenye bakuli au kikapu ulichoandaa. Soma ujumbe ulioko kwenye kila kipande cha karatasi na jadili na watoto kwa kifupi. Waambie watoto kwamba ujumbe huu ni mambo yote ambayo nabii aliye hai ametuagiza tufanye.

Shughuli

Waulize watoto wafikirie njia wanazoweza kumfuata nabii. Rusha au toa kijifuko cha maharagwe au kitu laini kwa kila mtoto na sema, “Nitamfuata nabii wetu kwa .” Acha kila mtoto akamilishe sentensi hiyo na njia anayoweza kumfuata nabii.

Tunabarikiwa tunapomfuata nabii

Rejea tena picha za Nuhu, Musa, Joseph Smith, na nabii aliye hai. Elezea kwamba kwa sababu familia ya Nuhu ilimfuata, iliokolewa kutokana na gharika. Kwa sababu Waisraeli walimfuata Musa, walikombolewa kutoka Misri na kuingia katika nchi bora. Kwa sababu watu walimfuata Joseph Smith, walikuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Elezea kwamba watu hawa walibarikiwa kwa sababu walimfuata nabii? Sisi pia tutabarikiwa tunapomfuata nabii.

Wimbo

Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 110). Elezea kwamba kupotoka humaanisha kufanya makosa. Acha kila mtoto ashikile picha ya nabii aliye hai wakati mkiimba.

Mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, hautapotoka.

Mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, mfuate nabii, yeye anajua njia.

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako wa nabii aliye hai. Waambie watoto kwamba unajua kwamba tunapomfuata nabii, tutabarikiwa na kuwa na furaha.

Shughuli zenye Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Pata kanda ya sauti au kanda ya video ya nabii aliye hai ili uwachezee au waonyeshe watoto video hiyo au picha zake katika magazeti ya Kanisa.

  2. Imba au sema maneno “We Thank Thee, O God, for a Prophet,” (Hymns, no.19) kwa watoto.

  3. Simulia tena hadithi ya ono la Rais Lorenzo Snow la Mwokozi (ona somo la 26). Elezea kwamba Yesu alimtokea Rais Snow na kumwambia jinsi ya kuongoza Kanisa. Yesu alimwambia Rais Snow kile atakachowafundisha waumini wa Kanisa?

  4. Fikiria juu ya hali fulani ambapo watoto wangeweza kufuata mafundisho ya nabii. Elezea kila hali kwa darasa, na waache watoto wasimilie au waigize kile watafanya katika kila hali ili kumfuata nabii. Kwa mfano: “Unaona hela jikoni. Ungependa kuzichukua, lakini unajua ni za mama yako. Utafanya nini kufuata mafundisho ya nabii ya kuwa mwaminifu?

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Onyesha picha ya nabii aliye hai wakati wa somo lote. Chukua muda kuwaelezea watoto yeye ni nani. Elezea kwamba yeye anawapenda na anataka kuwasaidia wao kurudi kwa Baba wa Mbinguni na Yesu. Rudia haya mara mbili au tatu wakati wa darasa.

  2. Cheza “Fuata Kiongozi” pamoja na watoto. Acha watoto wasimame katika mstari. Mtoto wa kwanza katika mstari akimbie, aruke, aruke kamba, au afanye kitendo upande mwingine wa chumba. Watoto wengine mwafuate mtoto wa kwanza, kwa kufanya kile anachofanya. Kisha mtoto wa kwanza aende mwisho wa mstari, na mtoto anayefuata anakuwa kiongozi mpya. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu ya kuwa kiongozi.

    Baada ya mchezo wakumbushe watoto kwamba nabii ndiye kiongozi wa Kanisa. Kama tutafuata mambo anayotuambia tufanye, atatuongoza sisi kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

Chapisha