Somo la 19
Ninashukuru kwa ajili ya Macho Yangu
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuthamini macho yake na kile yanachoweza kufanya.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Yohana 9:1–7 na 3 Nefi 11:1-17.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia na Kitabu cha Mormoni
-
Kigurudumu cha uzi chenye tundu kubwa na kamba ya kiatu au kipande cha kamba. (Kama una darasa kubwa, ukipenda unaweza kuwaletea zaidi ya kitu kimoja ya vitu hivi.)
-
Shali au kitambaa cha kufunga ili mtu asione.
-
Picha 1-43, Yesu Akimponya Kipofu (Picha za Sanaa za Injili 213; 62145); picha 1-44, Yesu Akifundisha katika Nchi za Magharibi (Picha za Sanaa za Injili 316; 62380);
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Taarifa kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, wali si ulemavu wao.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Macho yetu ni baraka kwetu
Elezea kwamba tuna macho ili tuweze kusoma na kujifunza, kufanya kazi na kucheza, na kuona dunia maridadi.
Jadili na watoto jinsi maisha yao yangekuwa tofauti kama hawengeweza kuona.
-
Ungewezaje kula chakula?
-
Ungewezaje kujua ni nguo gani za kuvaa?
-
Ungewezaje kujua njia zako hapo nyumbani?
Ninamshukuru Baba wa mbinguni kwa ajili ya macho yangu
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Waalike watoto watazamane kwa makini machoni, kope, mifuniko ya macho, nyusi na kope. Elezea kwamba vifuniko, nyusi na kope zetu husaidia kuzuia uchafu, vumbi na jasho kuingia machoni mwetu.
-
Kabla ya darasa, tumia chombo chenye ncha kama pini kutoboa mashimo katika kipande cha karatasi cha duara na mraba. Darasani, wafunge watoto kitambaa usoni mmoja kwa wakati na uwaulize wao waguse matundu kwenye karatasi na waseme ni maumbo gani. Elezea kwamba hii ni kama breli, ambayo ndivyo wasomavyo watu vipofu.
-
Ukitumia mifuko ya karatasi, tengeneza macho ambayo yanafunguka na kufumba kwa kila mtoto (ona kielelezo hapo chini). Andika kila mfuko wa karatasi nashukuru kwa ajili ya macho yangu. Acha watoto wapake rangi macho yao na wachore nywele kwenye mifuko yao ya karatasi. Ukitumia macho ya mfuko wa karatasi, igiza pamoja na watoto nyakati ambapo tunafunga na kufumbua macho yetu, kama vile tunapoamka, au tunapolala, tunapoomba, na tunaposhtuka.
-
Kama inawezakana wapeleke watoto kwa matembezi ya asili huko nje. Waambie wakunje mikono yao na wawe kimya sana wanapotembea, ili weweze kuzingatia kutumia macho yao. Wanaporudi darasani, waombe wachukue zamu kuelezea kile walichokiona.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Imbeni au semeni maneno ya “Popcorn Popping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 242). Ekezea kwamba kuchanua kwa mwaprikoti huonekana kama bisi.
-
Kama mkitazama nje kupitia dirishani, kama isemwavyo katika wimbo, mtaweza kuona bisi zikitokeza kwenye mwapricoti. Unatakiwa kufanya nini ukitazama nje dirishani?
Acha watoto watazame nje dirishani, au watembeze nje kwa dakika chache. Rudini darasani na warejee kile walichokiona.
-
Je, mlitumia nini kuona vitu hivi? (Macho.)
Elezea kwamba tunapswa kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya macho yetu.
-
-
Wasaidie watoto wasimame na kusema maneno yafuatayo, wakitumia vitendo kama inavyooneshwa na maneno:
Gusa macho yako,
Gusa pua lako,
Gusa masikio yako,
Gusa vidole vyako,
Nyosha mikono yako,
Juu juu sana,
Hata juu sana,
Kuelekea angani,
Weka mikono yako,
Kwenye nywele zako;
Keti chini kimya kimya,
Kwenye kiti chako.
-
Waonyeshe watoto chombo kidogo. Elezea kwamba utakiweka mahali fulani chumbani, na watatumia macho yao kukitafuta. Waombe watoto wafunge macho yao, na uweke chombo hicho mahali kinapoonekana lakini pasipo wazi. Acha watoto wafungue macho yao na watafute chombo hicho bila kutembea au kufanya kelele. Waambie wakunje mikono yao wanapokipata chombo hicho. Wakumbushe watoto kuwa sharti watulie na kuwaacha wale wengine watafute chombo hicho kwa macho yao. Rudia mara nyingi kama inavyohitajika.