Somo la 32
Ninashukuru kwa Chakula na Mavazi
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuona na kuonyesha shukrani kwa ajili ya chakula na mavazi.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:11–12 na 1 Wafalme 17:8–16.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Matunda au mboga zikiwa na mbegu ndani yake.
-
Kijifuko cha maharagwe au kitu kingine laini.
-
Mkato 1-5, samaki; picha mkato 1-7, nguruwe; mkato 1-8, kondoo; makato 1-22, kuku (picha mikato kama hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha za Watoto wa Msingi seti 4); au tafuta picha za wanyama watoao chakula na mavazi katika eneo lako.
-
Picha 1-15, Kubariki Chakula; picha 1-50, Naweza Kujivika.
-
-
Fanya maandalizi yaliyo muhimu kwa ajili ya Shughuli yo yote yenye Kuboresha unayotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Tunatumia mimea na wanyama kwa chakula
-
Ni aina gani nyingine ya vyakula unavyopenda kula?
-
Tunapata wapi chakula chetu?
-
Ni nani aliumba mimea na wanyama ambao kwao tunapata chakula?
Zungumza juu ya baadhi ya vyakula unavyokula na pale vinakotoka. Elezea kwamba sisi tunapata vyakula vingi kutokana na mimea.
Mega au kata tunda au mboga uliyoleta na uonyeshe mbegu.
-
Hizi ni nini?
-
Kwa nini matunda yana mbegu?
Elezea kwamba Baba wa Mbinguni alipanga mimea iwe na mbegu ili mbegu ziweze kuota kuwa mimea mingi ili kutoa chakula kwa ajili yetu (ona Mwanzo 1:11–12). Unapopanda mmea kama vile tunda au mboga hukua, na mbegu zaidi hutokea.
Tunatumia mimea na wanyama kwa mavazi
Sema kwamba chakula sio kitu pekee tunachopata kutokana na mimea na wanyama. Onyesha picha 1-50, Naweza Kujivika.
-
Huyu mvulana anafanya nini?
-
Je, wewe unavaa nini wakati unapojivika?
Tunaweza kuwa na shukrani kwa ajili ya chakula na nguo
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilicho na mstari uliochorwa katikati kutoka juu kwa maneno Ninashukuru kwa ajili ya: ikiandikwa kutoka juu. Acha kila mtoto achore picha ya chakula upande mmoja wa mstari na aina ya vazi upande mwingine.
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno ya mistari miwili ya kwanza ya “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20).
-
Waache watoto wajifanye kuwa wao ni mbegu. Watoto hao wachutame kana vile wao wamepandwa ardhini, kisha wainuke pole pole jinsi jua linavyoangaza na mvua kuwanyeshea pole pole. Ukipenda unaweza kuwaacha watoto wachukue zamu kuwa jua na mvua.
-
Leta tunda au mboga na wape watoto kiasi kidogo kuonja. Elezea aina ya mbegu na mmea ule unaozaa tunda au mboga. (Zungumza na wazazi wa watoto ili kuhakikisha hakuna mtoto yo yote anayeweza kudhurika na chakula unacholeta.)
-
Elezea chakula kilicho maarufu kwa watoto bila kukitaja na uwaulize wabahatishe ni chakula gani unachoelezea. Kwa mfano, unaweza kusema, “Hiki chakula ni cheupe au hudhurungi kwa nje. Kina ganda. Kimelazwa kwenye kiota. Ni nini? (Yai.) Rudia mara nyingi kama upendavyo. Unaweza kuleta mfano wa kila chakula ambacho unaelezea.
-
Leta mavazi kama vile sweta, makoti, na kofia na uache watoto wajaribu wakati unapoongea kuhusu nguo ambazo watoto wanashukuru kuwa nazo.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno ya “A Song of Thanks” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20) au “For Health and Strength” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.21).
-
Acha watoto wafanye igizo la kuvaa mavazi unaposema maneno ya mstari wa shughuli ufuatao:
Watoto, vaeni suruali zenu, vaeni suruali, vaeni suruali.
Watoto, vaeni suruali zenu, moja, mbili, tatu.
Watoto, vaeni skati zenu, vaeni skati, vaeni skati.
Watoto, vaeni skati zenu, moja, mbili, tatu.
Watoto, vaeni shati zenu, vaeni shati, vaeni shati.
Watoto, vaeni shati zenu, moja, mbili, tatu.
Watoto, vaeni soksi zenu, vaeni soksi, vaeni soksi.
Watoto, vaeni soksi zenu, moja, mbili, tatu.
Watoto, vaeni viatu vyenu, vaeni viatu, vaeni viatu.
Watoto vaeni viatu vyenu, moja, mbili, tatu.
Watoto sasa vaeni nguo, vaeni nguo, vaeni nguo (pigeni makofi).
Watoto sasa vaeni nguo, acheni tucheze!