Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 41: Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo Wametupatia Maandiko


Somo la 41

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo Wametupatia Maandiko

Madhumuni

Ni kumsadia kila mtoto kuelewa kwamba maandiko yana maneno ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kwamba tunaweza kujifunza kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa kusoma maandiko.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Luka 22:19–20; 3 Nefi 18:21; Mafundisho na Maagano 59:6; Musa 7:11 Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 10.

  2. Jiandae kusimulia mojawapo ya hadithi unazozipenda kutoka kwenye maandiko, ukitumia picha kama inawezekana.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Seti ya maandiko (Biblia, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu).

    2. Kipande cha nguo cha kufunikia maandiko au kipande cha karatasi cha kujaradia.

    3. Picha 1-3, Yesu Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 240; 62572);Picha 1-18, Yohana Mbatizaji Akimbatiza Yesu (Sanaa ya Picha za Injili 208; 62133); picha 1-44, Yesu Akifundisha katika Ulimwengu wa Magharibi (Sanaa ya Picha za Injili 316; 62380);Picha 1-70, (Sanaa ya Picha za Injili 225; 62174).

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Kabla ya darasa, funika maandiko na kipande cha kitambaa au uyafunge na karatasi. Weka maandiko kwenye meza au kiti mahali ambapo wanafunzi wataweza kuona. Elezea kwamba umefunika kitu ambacho ni muhimu kwako na kwa kila mtu. Acha watoto wabahatishe kile ambacho umekifunika

Baada ya wachache kubahatisha, acha watoto wahisi kwa kugusa kitambaa au karatasi. Kama mtoto akibahatisha kwamba ni kitabu au vitabu, waambie watoto kwamba ni sahihi na uvifunue vitabu. Waambie watoto kwamba vitabu hivi vinaitwa maandiko. Acha watoto waseme neno maandiko mara kadhaa.

Maandiko ni vitabu vitakatifu

Elezea kwamba maandiko ni vitabu muhimu ambavyo ni tofauti na vitabu vingine. Ni vitabu vitakatifu. Wakumbushe watoto kwamba kitu ambacho ni kitakatifu hutusaida kufiiria kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu. Elezea kwamba maandiko yanatuambia kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu na jinsi wanavyotupenda. Yanatuambia kile Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanye ili tuweze kuwa na furaha.

Onyesha na utaje vitabu vinne vya maandiko, kimoja kimoja. Ikiwa baadhi vimeunganishwa kuwa kitabu kimoja, onyesha pembeni mwake ambapo vichwa vimeorodheshwa au nenda kwenye kurasa za jina la kila kitabu.

Shughuli

Waambie watoto kwamba tunapaswa kuyatunza vyema maandiko na kufungua kurasa zake kwa uangalifu. Acha watoto waje mbele ya darasa mmoja mmoja na kuonyesha jinsi wanavyoweza kushika maandiko na kufungua kurasa zake kwa uangalifu.

Elezea kwamba Maandiko yana hadithi ambazo ni za kweli. Hadithi hizi zinatusaidia kujua yale ambayo Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka tufanye. Hadithi katika maandiko zinatusaida katika maisha yetu.

Hadithi

Simulia mojawapo ya hadithi unazozipenda kutoka kwenye maandiko, ukitumia picha kama inawezekana. Sisitiza jinsi mambo yanayofundishwa katika hadithi za maandiko haya zinavyokusaidia wewe. Elezea jinsi unavyopenda kusoma hadithi katika maandiko.

Wimbo

Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 57). Wakumbushe watoto kwamba hadithi za maandiko wanazojifundisha katika darasa la Msingi ni za kweli.

Nisimulie hadithi za Yesu napenda kuzisikia.

Mambo ambayo ningetaka kumuuliza yeye aniambie kama angalikuwa hapa.

Mandhari za njiani, simulizi za baharini,

Hadithi za Yesu, nisimulie mimi.

Maandiko yana mafundisho ya Yesu

Elezea kwamba baadhi ya maandiko yanaandikwa na watu ambao walimjua Yesu na waliishi wakati wake. Walimwona Yesu na kumsikia Yeye akifundisha. Watu hao waliandika ili kwamba kila mtu aweze kujifunza kuhusu Yesu na mafundisho yake na kujua kwamba alikuwa mwana wa Baba wa Mbinguni.

Onyesha picha 1-70, Karamu ya Mwisho. Waache watoto waseme kile wanachokijua kuhusu picha hii. Onyesha Biblia na kisha watoto warudie jina lake. Fungua katika Biblia Luka 22. Elezea kwamba Yesu alifundisha katika Biblia kwamba tunapaswa kupokea sakramenti ili kumkumbuka yeye. Yesu alichukua mkate na kuwapa wanafunzi wake (wasaidizi). Alichukua kikombe na akawapa wanywe. Soma sehemu ya mstari wa 19 pale Yesu aliposema, “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Sema kwamba haya ni maneno ya Yesu.

Onyesha picha 1-44 Yesu akifundisha katika Nchi za Magharibi, na wakumbushe watoto kile kinachotendeka katika picha hii. Onyesha Kitabu cha Mormoni na uwaache watoto warudie jina lake. Fungua Kitabu cha Mormoni, 3 Nefi 18. Elezea kwamba Yesu aliwafundisha watu mambo mengi. Soma sehemu ya mstari wa 21 pale Yesu aliposema, “Ombeni katika familia zenu.”

  • Yesu anatuambia tufanye nini pamoja na familia zetu?

Onyesha picha 1-3, Yesu Kristo. Onyesha Mafundisho na Maagano na uwaache watoto warudie jina lake. Fungua Mafundisho na Maagano sehemu ya 59. Elezea kwamba mojawapo ya mambo ambayo Yesu alifundisha ilikuwa kwamba tunapaswa kumpenda kila mtu. Soma sehemu ya mstari wa 6 pale Yesu aliposema, “Mpende jirani yako.”

  • Yesu alisema tufanye nini?

  • Jirani yako ni nani?”

  • Je, unajisikia vipi unapokuwa mkarimu kwa wengine na kuonyesha upendo kwao?

Wimbo

Acha watoto waimbe au waseme maneno ya “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 61), wakitumia matendo yanayoelezwa hapa chini:

Yesu alisema mpende kila mtu (panua mikono wazi kabisa);

Watendee kwa ukarimu, pia (ishara ya kichwa ya kukubali),

Wakati moyo wako umejawa na upendo (weka mkono juu moyo),

Wengine watakupenda (jikumbatie mwenyewe).

Onyesha picha 1-18, Yohana Mbatizaji Anambatiza Yesu. Waache watoto waseme juu ya picha hii. Sisitiza kwamba Yesu alibatizwa na kwamba yeye anataka kila mtu abatizwe. Onyesha Lulu ya Thamani Kuu na uwaache watoto warudie jina lake. Fungua Lulu ya Thamani Kuu hadi Musa 7 na usimulie jinsi Yesu alivyomfundisha mtu aliyeitwa Enoki awaendee watu na kuwabatiza. Soma sehemu ya mstari wa 11 pale ambapo Yesu alisema, “Batiza katika jina la Baba, na la Mwana, … na la Roho Mtakatifu.”

Inua vitabu vinne vya maandiko. Sisitiza kwamba mafundisho ya Yesu yapo ndani ya hivi vyote

  • Hivi ni vitabu gani?

  • Ni mafundisho ya nani yanayopatikana ndani ya maandiko.

  • Kwa nini maandiko haya yaliandikwa?

  • Inakufanya ujisikie vipi kwa kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatupenda na wametupatia maandiko?

Ushuhuda

Elezea shukrani, na upendo wako kwa kuwa na maandiko. Toa ushuhuda kwamba maandiko ni maneno ya Baba wa Mbinguni na Yesu na kwamba kwa kujifunza maandiko tunaweza kujifunza nini Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka sisi tufanye.

Shughuli zenye Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Kunja vipande vya karatasi nusu na utengeneze mfano wa majalada ya vitabu vinne vya maandiko, seti moja kwa kila mtoto. Chapa majina ya vitabu vinne vya maandiko juu ya majalada. Toboa tundu pembeni mwa kila jalada na utumie kipande cha uzi au kamba ili kufunga pamoja majalada ya vitabu vyote vinne vya maandiko kwa ajili ya kila mtoto.

    Ndani ya kila jalada, andika kwa herufi kubwa maandiko ambayo yalifundishwa wakati wa somo.

    Biblia: Yesu alitufundisha juu ya sakramenti (Luka 22:19).

    Kitabu cha Mormoni: Yesu alitufundisha kusali katika familia zetu (3 Nefi 18:21).

    Mafundisho na Maagano: Yesu alitufundisha kuwapenda majirani zetu (M&M 59:6).

    Lulu ya Thamani Kuu: Yesu alitufundisha kubatizwa (Musa 7:11).

    Mpe kila mtoto seti ya majalada aende nayo nyumbani. Unavyofanya hivi, rejea mafundisho ya Yesu yanayojadiliwa katika somo hili.

  2. Wasaidie watoto kukariri sehemu ya makala ya Imani ya nane: “Tunaamini kuwa Biblia ni neno la Mungu alimradi imetafsiriwa kwa usahihi; pia tunaamini Kitabu cha Mormoni kuwa ni neno la Mungu.”

  3. Tafuta picha za baadhi ya hadithi za Kitabu cha Mormoni kutoka katika picha ambazo zinaambatana na kitabu hiki cha kiada au kutoka kwenye maktaba ya tawi. Onyesha kila picha na kwa ufupi jadili hadithi inayoonyeshwa. Wakumbushe watoto kwamba maandiko yana hadithi za kweli. Waache watoto waimbe ”Book of Mormon Stories” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk.118).

  4. Wasimulie watoto juu ya wakati ambapo maandiko yalikuwa na maana maalumu katika maisha yako. Elezea jinsi maandiko yalivyokusadia wewe na jinsi yalivyokufanye ujisikie.

  5. Tafuta maandiko mafupi ambayo yana maneno ya Yesu, kama yale yaliyomo katika somo hili. Kariri kila andiko, ukianza na maneno Yesu alisema. Kwa mfano, Yesu alisema, ‘Nifuate.’” Rusha ama mpe mtoto kijifuko cha maharagwe au kitu laini kwa mtoto na muache arudie maandiko nyuma yako na kisha arushe kijifuko kwako tena. Endelea kurusha kijifuko cha maharagwe mpaka kila mtoto apata zamu.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Imba au sema maneno “Book of Mormon Stories” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 118, ukishikilia nakala ya Kitabu cha Mormoni au ”Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 57) ukishikilia Biblia.

  2. Kwa ufupi simulia hadithi ya watu kumi wenye ukoma (ona Luka 17;11–19), ufanye shughuli ya vidole pamoja na watoto:

    Watu kumi waliugua (inua vidole kumi juu);

    Kristo siku moja aliwaponya.

    Yeye kwa urahisi alisema, na maumivu yao yalitoweka (ishara ya kupunga mikono)!

    Je, haya sio maajabu? Na si mzaha (weka kidole upande mmoja wa kichwa na uonekane kushangaa).

    Kwamba mtu mmoja tu (inua kidole kimoja juu).

    Alimshukuru.

    Na akamsifu Mungu (inua mikono yote kuelekea juu)?

    (Imetoholewa kutoka kwa Jean Shannon katika Bible Story Finger Plays and Action Rhymes [Cincinnati, Ohio: Standard Publishing Co., 1964], uk. 27.)

    Waonyeshe watoto pale hii hadithi inapopatikana katika Biblia.

  3. Waulize watoto ni hadithi gani za maandiko wanazozipenda. Kama unaweza, waonyeshe pale hadithi hizi zinapatikana katika maandiko.

Chapisha