Somo la 23
Mimi nina Familia
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni alimpangia kila mmoja wetu kuwa na familia ambayo inatuhitaji na kutupenda.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Luka 1:26–35.
-
Fahamiana na familia za watoto wa darasa lako na ujiandae kusema kitu chanya ambacho kinatokea kwa kila mmoja wao, kama vile mtoto mchanga, kaka au dada akiwa misheni, au matembezi ya familia
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Chaki na kifutio.
-
Picha 1-5, Familia na Mtoto (62307); picha 1-7, Familia yenye Upendo; picha 1-16 Kuzaliwa kwa Yesu (Sanaa za picha za injili 201; 62495); picha 1-23, Kiota na Kinda; picha 1-51, Familia Ikifanya Kazi Pamoja (62313); Burudani ya Familia (62384).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Taarifa kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hali za familia za watoto katika darasa lako. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kitu cha muhimu kuhusu familia sio idadi ya watu katika familia, bali kwamba wana familia wanapendana na kutunzana.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Mimi nina Familia
-
Je, una familia?
-
Je, kwa nini unahitaji familia kukutunza wewe?
Onyesha picha 1-5, Familia na Mtoto Mchanga. Rejea jinsi Baba wa Mbinguni alipanga kila mmoja wetu kuja duniani na kuwa sehemu ya familia. Elezea kwamba wakati mtoto anapozaliwa, mtoto mchanga hawezi kujitunza mwenyewe. Mtoto mchanga hawezi kujilisha au kujivisha. Anahitaji familia ya kumtunza.
-
Ni nani alikutunza ulipokuwa mtoto mchanga?
-
Ni baadhi ya vitu gani ambavyo familia yako ilikufanyia ulipokuwa mtoto mchanga?
-
Ni baadhi ya vitu gani ambavyo familia yako inakufanyia kwa sasa?
-
Ni nani aliyekupangia wewe kuwa katika familia?
Wasaidie watoto kuelewa jinsi ya familia zao zilivyokuwa na furaha wakati walipozaliwa. Sisitiza ni kiasi gani wazazi wao na wana familia wengine wanavyowapenda na kutaka wawe na furaha.
Baba wa Mbinguni na Yesu Wanaipenda kila familia
Onyesha picha 1-7, Familia yenye Upendo. Elezea kwamba baadhi ya familia zina mama na baba, na familia zingine zina mzazi mmoja tu. Baadhi ya familia zina babu au bibi au mtu mwingine wa kusaidia kuwatunza watoto. Baadhi ya familia zina watoto, hali familia zingine zina mtoto mmoja au hazina mtoto kabisa. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kila familia ni tofauti na Baba wa Mbinguni na Yesu wanaipenda kila familia.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanataka wanafamilia kuonyeshana upendo
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Imba “A Happy Family” tena. Chagua watoto wanne wawe familia katika wimbo huu. Acha wao washikilie alama inayoonyesha ni mwana familia yupi kila mmoja anamwakilisha. Simama nyuma ya watoto wale wanne na uonyeshe kwa kidole kichwa cha mtoto husika unapoimba au kusema maneno pamoja na watoto. Rudia wimbo huu, ukiwaruhusu watoto wengine washiriki kama sehemu ya wana familia. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu.
-
Wasimulie watoto kuhusu maelekezo ya Mfalme Benyamini kwa familia, kama inavyopatikana katika Mosia 4:14–15. Soma nusu ya mwisho ya aya ya 15 kwa sauti. Acha watoto wapendekeze njia ambazo wana familia wanaweza kupendana na kutumikiana.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo vya mchezo wa vidole ufuatao:
Familia Yangu
Huyu hapa ni mama yangu mrembo (kionyeshe kidole cha shahada);
Huyu hapa ni baba yangu mrefu (onyesha kidole cha kati).
Huyu hapa dada yangu mkubwa (onyesha kidole cha pete),
Na hawa sio wote .
Huyu hapa ni kaka yangu mdogo (onyesha kidole kidogo),
Mdogo, kama mdogo alivyo.
Ni nani huyu mtu mwingine (onyesha kidole gumba)?
Kwa kweli mnajua ni mimi.
Moja, mbili, tatu, nne, tano, unaona (gusa kila kidole unapohesabu),
Ni familia nzuri sana!
Acha kila mtoto anyoshe idadi ifaayo ya vidole kuashiria idadi ya watu katika familia yake (ikiwa mtoto ana zaidi ya watu kumi, acha mtoto mwingine amsaidie). Acha kila mtoto arudie mistari miwili ya mwisho, akihesabu idadi ya watu katika familia yake kabla ya kusema “Ni familia nzuri sana!”
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Onyesha picha 1-23, Kiota na Kinda. Wasaidie watoto kufanya vitendo vya “Birds in the Tree” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 241) huku ukiimba au kusema maneno:
Tutapata kiota kidogo (kunja mikono)
Katika matawi ya mti (inua mikono juu ya kichwa)
Acha tuhesabu mayai hapa ndani.
Kuna moja, mbili, tatu (nyosha vidole, moja, mili, na tatu).
Mama ndege hukalia kiota (kunja mkono wa kushoto, weka mkono wa kulia juu).
Kuangua mayai, yote matatu (inua vidole vitatu juu).
Baba ndege hupaa raundi, raundi (fanya mikono kama vile mwendo wa kupaa),
Ili kulinda familia yake.
-
Imba “Here We Are Together” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 261), ukitumia baba, mama, dada, kaka pale wimbo unapoashiria uingize majina. Acha watoto wapige makofi au wacheze huku wakiimba.
Haya tuko pamoja, pamoja, pamoja
Ee, hapa tuko pamoja katika familia yetu.
Kuna baba na mama na dada na kaka.
Ee, haya tuko pamoja siku hii angavu ya jua.
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari ufuatao huku ukisema maneno:
Familia Yangu
Kama vile ndege huko juu mtini (fanya mikono kama mabawa),
Nina familia yangu mwenyewe (jionyeshe mweyewe);
Wao hunipa chakula (jifanye kama unakula).
Na wananifundisha kucheza (ruka)
Kwa hivyo ninaweza kuwa salama na kuwa na furaha siku nzima (tabasamu kwa tabasamu kubwa).
-
Sema maneno yafuatayo au yaiimbe kwa tuni yo yote inayoendana:
Mama anakupenda, Mama anakupenda.
Baba pia, Baba pia.
Watu katika familia yako, watu katika familia yako,
Wanakupenda kweli, wanakupenda kweli.