Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 34: Naweza Kuwapenda Wengine


Somo la 34

Naweza Kuwapenda Wengine

Madhumuni

Ni kumtia moyo kila mtoto kuonyesha upendo kwa wengine kwa njia ya maneno na matendo ya ukarimu.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mathayo 7:12; Marko 19:-16–10; Luke 10:30–37; na Yohana 13:34.

  2. Rejea hadithi kutoka kwenye somo la 10 kuhusu Yesu akimponya kipofu (ona Yohana 9:1–7).

  3. Tengeneza moyo wa karatasi kwa ajili ya kila mtoto katika darasa. Andika Nakupenda juu ya kila moyo.

  4. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Picha 1-3, Yesu Kristo (Sanaa ya Picha za Injili 240; 62572); picha 1-43, Yesu Akimponya Kipofu (Sanaa ya Picha za Injili 213; 62145); Picha 1-48, Watoto Wakicheza na Vibao Mchemraba; picha 1-62, Msamaria Mwema (Sanaa ya Picha za Injili 218; 62156).

  5. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote zenye Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Onyesha picha 1-48, Watoto Wakicheza na Vibao Mchemraba.

  • Watoto hawa wanafanya nini?

  • Unafikiri hawa watoto ni marafiki?

  • Je, marafiki hutendeana vipi?

Wakumbushe watoto kwamba marafiki hutendeana kwa ukarimu. Tunapokuwa wakarimu kwa wengine, tunawaonyesha wao upendo.

Wimbo

Pamoja na watoto imbeni au mseme maneno ya “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo zaa Watoto, uk. 61), mkitumia vitendo vinavyoelezwa hapa chini:

Yesu alisema mpende kila mtu (panua mikono wazi kabisa);

Watendee kwa ukarimu, pia (ishara ya kichwa ya kukubali),

Wakati moyo wako umejawa na upendo (weka mkono juu moyo),

Wengine watakupenda (jikumbatie [mwenyewe).

Yesu alionyesha upendo kwa wengine kwa kuwa mkarimu

Onyesha picha1-3, Yesu ndiye Kristo, na uwaelezee watoto kwamba Yesu alituambia tuwatendee wengine jinsi vile ambavyo tungependa wengine watutendee sisi. Onyesha Biblia na usome Mathayo 7:12 hata nanyi watendee vivyo hivyo. Elezea kwamba maandiko haya humaanisha kwamba kama tunataka wengine wawe wakarimu kwetu, tunapaswa tuwe wakarimu kwao.

Hadithi

Onyesha picha 1-43, Yesu Akimponya Mtu Kipofu. Acha watoto wakusaidie kusimulia hadithi inayoonyeshwa katika picha hii (ona Yohana 9:1–7

  • Yesu alikuwaje mkarimu kwa mtu kipofu?

Hadithi

Simulia hadithi ya Yesu akiwabariki watoto wadogo, kama inavyopatikana katika Marko 10:13–16.

  • Yesu alikuwaje mkarimu kwa watoto?

Sisitiza kwamba Yesu alitumia maisha Yake akiwasaidia watu wengine. Kwa kuwa mkarimu, Yesu alionyesha upendo kwa wengine. Elezea kwamba Yesu alituamuru tupendane. Soma Yohana 13:34 kwa watoto. Acha watoto warudie “Pendaneni; kama nilivyowapenda ninyi” mara kadhaa.

Wimbo

Pamoja na watoto imbeni au mseme maneno “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, p. 136).

Kama nilivyowapenda ninyi.

Pendaneni.

Hii amri mpya:

Pendaneni.

Kwa hilo watu watajua.

Nyinyi ni wanafunzi wangu,

Kama ninyi

Mtapendana

(© 1961, 1989 by Luacine C. Fox. Imetumika kwa Idhini.)

Tunaweza kuwaonyesha wengine upendo kwa kuwa wakarimu

Hadithi

Onyesha picha 1-62, Msamaria Mwema, na usimulie hadithi ya Msamaria Mwema, kama inavyopatikana katika Luka 10:30–37.

  • Ni nani katika hadithi hii alikuwa mkarimu?

  • Msamaria alifanya nini ili kumsaidia mtu aliyejeruhiwa?

Waulize watoto wafikirie njia wanazoweza kuwa wakarimu kwa wengine. Acha wao washirikiane mawazo yao na washiriki wengine wa darasa.

Elezea kwamba wakati mwingine ni vigumu kuwa mkarimu kwa mtu mwingine kwa sababu mtu huyo anaweza kuonekana kuwa jeuri au tofauti nasi. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kila mtu huhitaji kutendewa kwa ukarimu. Hata kama watu wanaoneka kuwa jeuri au tofauti nasi (kwa mfano, kama wana rangi ya ngozi tofauti au wana ulemavu), tunapaswa kuwatendea wao kwa ukarimu.

Zungumzia kuhusu umuhimu wa kuonyesha upendo na ukarimu katika familia zetu.

  • Unawezaje kuonyesha upendo kwa baba yako? Mama yako? Kaka zako na dada zako?

Sisitiza kwamba tunapokuwa wakarimu kwa familia zetu, sio tu familia zetu zitakuwa na furaha, bali Baba wa Mbinguni na Yesu watakuwa na furaha, pia.

Elezea kwamba wakati mwingine watoto wachanga au wadogo huchukua au kuvunja vitu vyetu. Wasaidie watoto kuelewa kwamba watoto wadogo wengi kwa kawaida hawaelewi wanachofanya. Tunahitaji kuwatendea kwa ukarimu na tusiwakasirikie wao. Kama tuna vitu ambavyo vinaweza kuvunjwa, tunapaswa kuviweka mbali na watoto wadogo.

  • Je, tunawezaje kuonyesha upendo kwa Baba wa Mbinguni na Yesu.

Sisitiza kwamba tunaweza kuonyesha upendo kwa Baba wa Mbinguni na Yesu kwa kutii amri, kuwa na staha kanisani, na kuwa wakarimu na kuwasaidia walio karibu nasi.

Tunaweza kuonyesha upendo kwa kusema kwa upole

Shughuli

Waombe watoto wafuate maelekezo yaliyopo hapo chini. Baada ya watoto kufanya kila kitendo, washukuru kwa kufuata maelekezo hayo.

  1. Tafadhali simama.

  2. Tafadhali keti chini.

  3. Tafadhali simama na ugeuke. Tafadhali keti chini. Tafadhali simama tena.

  4. Nyoosha mikono yako juu ya kichwa chako, tafadhali.

  5. Tafadhali keti chini pole pole.

  • Ni maneno gani ya upole na ukarimu niliyosema?

  • Je, Unajisikiaje mtu anaposema “tafadhali” na “asante” kwako?

Wasaidie watoto kuelewa kwamba kama tunataka wengine waseme nasi kwa ukarimu, tunapaswa kuongea nao kwa ukarimu.

Wakumbushe watoto kuhusu maneno mengine ya upole, kama vile “Samahani” na “Naomba radhi, tafadhali,” na katika hali ambayo sentensi hizo zinapaswa kutumika. Uliza maswali yafuatayo au yale yanayofanana nayo katika desturi yenu.

  • Unawezaje kuomba maji kwa upole?

  • Unapaswa kusema nini kama mtu amekuletea zawadi?

  • Unaweza kusema nini kama umemfanya mtu ahuzunike?

  • Unaweza kusema nini kwa upole ili mtu akupatie usikivu wake?

Elezea kwamba hata kama watu wengine wanasema nasi kwa ukatili, tunapaswa kujibu kwa upole.

Wimbo

Imba tena pamoja na watoto “Jesus Said Love Everyone.”

Ushuhuda

Wapongeze watoto kutokana na namna ambavyo umewaona wakiwa wakarimu. Elezea kwamba kwa sababu Baba wa Mbinguni na Yesu wanampenda kila mtu, wanafurahia wanapotuona tukitendeana kwa ukarimu. Toa ushuhuda kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka tuwe wakarimu. Mpe kila mtoto karatasi ya moyo. Waambie watoto kwamba maneno yaliyo kwenye moyo yanasemaje, na elezea upendo wako kwa watoto.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Soma mifano ifuatayo (au buni yako mwenyewe), na uwaache watoto wainue juu mioyo ya karatasi kama kitendo kinachoelezwa ni cha ukarimu au kinaonyesha upendo. Acha waweke mioyo ya karatasi yao kwenye mapaja kama kitendo hicho si cha ukarimu au hakionyeshi upendo.

    • Wakichukua zamu wanapocheza mchezo huu.

    • Kuwa mnung’unikaji.

    • Kumsaidia mtoto aliyeumia.

    • Kumpiga mtu ambaye amekukasirisha.

    • Kutembea kwa staha katika jumba la mikutano.

    • Kusema “tafadhali” na “asante.”

    • Kumshikia mtu mlango ili apite.

    • Kupiga kelele kanisani.

    • Kusaidia kufanya usafi.

    Wakumbushe watoto kwamba tunapokuwa wakarimu, tunaonyesha upendo, na Baba wa Mbinguni na Yesu wanafurahishwa nasi.

  2. Fikiria hali kadhaa ambazo watoto wanazo za kuwa wakarimu na kuonyesha upendo kwa wengine. Andika hali hizi kwenye kipande cha karatasi na uache kila mtoto achague kipande cha karatasi. Soma kila hali na uache mtoto ambaye aliichukua aelezee kitendo cha hali hiyo. Unaweza kutaka kuuliza mifano ifuatayo:

    • Wewe na rafiki yao mnacheza pamoja, na mtoto anaingia chumbani. Mnapaswa kufanya nini?

    • Wewe na dada yako mnataka kuchezea mwanasesere mmoja. Mnapaswa kufanya nini?

    • Kaka yako mdogo amechukua kitu chako. Mnapaswa kufanya nini?

  3. Ukitumia mifano hii kutoka katika kata yako, au eneo, jadili jinsi ya kuonyesha ukarimu na upendo kwa watu walio na ulemavu. Wasaidie watoto wafikirie juu ya njia mahususi wanazoweza kumsadia mtu yule mwenye ulemavu.

    • Unawezaje kuonyesha upendo kwa mtu ambaye hawezi kuona.

    • Unawezaje kuonyesha upendo kwa mtu ambaye hawezi kusikia?

    • Unawezaje kuonyesha upendo kwa mtu ambaye anatumia kitimwendo au mikongojo?

  4. Wasaidie watoto kuelewa ingawa watu fulani waweza kuwa wanaongea lugha tofauti au wana rangi tofauti au wana ngozi ya rangi tofauti na yetu, sisi wote tu watoto wa Baba wa Mbinguni. Tunapaswa kuwa wakarimu mmoja na mwingine. Tunapaswa kumtendea kila mtu jinsi sisi tungependa kutendewa. Mnaweza kuimba au kusema maneno ya “We Are Different” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 263, au ”Every Star Is Different” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 142). Eleza kuwa kila mtu ni tofauti na wengine kwa njia fulani.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Imbeni au mseme maneno ya “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 145, au ”A Special Gift Is Kindness” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 145).

  2. Wasaidie watoto kufanya shughuli ya mstari ufuatao:

    Tabasamu hugusa sana (panua pembe za mdomo iwe tabasamu),

    Na hivyo ninapohisi huzuni (kunja mdomo ile unune),

    Mimi napenda kutoa tabasamu (panua pembe za mdomo iwe tabasamu),

    Na punde nahisi furaha (weka mikono juu ya moyo)!

    Imetoholewa kutoka kwa Pat Gratam, “Feeling Glad,” Friend, Mar 1990, uk 21.)