Somo la 36
Naweza Kuwa Mfano Mwema
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuweka mfano mwema kwa wengine kwa kufuata mfano wa Yesu
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mathayo 4:19; Luka 19:1–10; Yohana 13:15; na 3 Nefi 17:11–24.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia na Kitabu cha Mormoni.
-
Nyayo kadhaa zilizokatwa kutoka kwenye karatasi.
-
Picha 1-3, Yesu Kristo (Picha za Sanaa za Injili 240; 62572); Zakayo juu Mtini; picha 1-64, Yesu Akiomba Pamoja na Wanefi (62542).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu duniani ili awe mfano kwetu
Onyesha picha 1-3, Yesu Kristo. Elezea kwamba mojawapo ya sababu Yesu alikuja duniani ilikuwa ni kuwa mfano kwetu na kutuonyesha sisi jinsi ya kuishi. Yesu alikuwa mkamilifu. Hii inamaanisha Yeye alifanya kila kitu katika njia sahihi. Jinsi Yeye alivyoishi wakati alipokuwa duniani ndiyo njia tunayopaswa kujaribu kuishi.
Fungua Biblia na uwasomee watoto Yohana 13:15. Waambie watoto kwamba haya ni maneno ya Yesu. Sisitiza kwamba tunataka kuwa kama Yesu na kufuata mfano wake.
Tunaweza kuwa mifano iliyo miema kwa wengine
Elezea kwamba kama tu vile watoto wanavyofuata mfano wa Yesu, watu wengine wanawatazama na kufuata mifano yao.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Tengeneza taji au kofia ya karatasi kwa kila mtoto. Kwenye kila taji au kofia, andika Naweza kuwa mfano mwema. Jadili njia ambazo watoto wanaweza kuwa mifano miema katikati ya wiki.
-
Imba “Jesus Once Was a Little Child” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 55, “Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 60), au “I Am Like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk,. 163).
-
Onyesha tochi au kitu kingine kidogo. Iwashe na ujadili jinsi mwanga kutoka kwenye tochi ambavyo huwasaidia watu inapomulika. Soma kwa sauti fungu la kwanza la maneno katika 3 Nefi 12:16. Waelezee watoto kwamba wao ni kama mianga midogo wanapoweka mfano mwema, kwa sababu watu wengine wanawatazama na kuwafuata. Acha kila mtoto ashike tochi na kuwaongoza wengine chumbani. Rudia hivi mpaka kila mtoto ambaye anataka kuongoza amepata nafasi.
-
Acha watoto wasimame na kufanya vitendo vya msitari shughuli ufuatao:
Yesu Anawapenda Watoto Wadogo
Baadhi ya watoto walikimbia kwenye mtaa wenye vumbi (kimbia katika sehemu hio),
Wakiharakisha mbio kwa miguu yao midogo (onyesha miguu)
Katikati ya umati wanapata sehemu (wajifanye wanapitapita katika umati)
Karibu na Yesu, kuona uso wake (simamia vidole na tazama huko na kule).
Baadhi ya watu wazima walisema, “Waondoeni” (fanya ishara kwa mkono kama unamaanisa “simameni”).
“Yeye ana shughuli nyingi hataki watoto leo” (kunja na utikise kichwa).
Lakini Yesu alisema, “Waacheni waje kwangu” (fanya ishara ya kuiita).
“Wao ni muhimu na nawapenda” (jikumbatie)
(Imetoholewa kutoka kwa Margaretta Harmon katika Bible Story Finger Plays and Action Rhymes [Cincinnati, Ohio: Standard Publishing Co., 1964], uk. 27.)
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Waombe watoto warudie neno mfano. Waambie kwamba mfano mwema ni mtu yule unayetaka kufanana naye utakapokuwa mkubwa. Wazazi wetu wanaweza kuwa mifano iliyo miema kwetu. Waombe watoto wataje mambo ambayo wazazi wao wanafanya ili kuwatunza wao au kuwafanya wawe na furaha.
-
Acha watoto waunganishe mikono yao na wakienda katika duara huku wakiimba au kusema maneno ya “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 198). Rudia wimbo mara nyingi utakavyo, ukibadilisha mama na baba, kaka, dada, bibi, au babu.
-
Cheza “Fuata Kiongozi” pamoja na watoto. Acha watoto wasimame katika mstari. Mtoto wa kwanza katika mstari akimbie, aruke, aruke kamba, au afanye kitendo upande mwingine wa chumba. Watoto wengine wamfuate mtoto wa kwanza, kwa kufanya kile anachofanya. Kisha mtoto wa kwanza aende mwisho wa mstari, na mtoto anayefuata anakuwa kiongozi mpya. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu ya kuwa kiongozi.