Somo la 21
Mimi Nina Hisia
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa na kutambua hisia na kujifunza njia za kuwa na furaha.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Luka 15:11–32.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Mchoro wa Uso wa Tabasamu/Kununa (ona mpangilio mwisho wa somo).
-
Chaki na kifutio.
-
Picha 1-45, Kusafisha Vyombo; picha 1-46, Watoto Wakimpa Mama Maua; picha 1-47, Watoto Wakigombana; picha 1-48, Watoto Wakicheza na Vibao Mchemraba; picha 1-49, Mwana Mpotevu (Sanaa ya Picha za Injili 220; 62155).
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Hisia zetu huonekana katika nyuso zetu na katika vitendo vyetu
-
Unajisikiaje unapokuwa na tasabamu usoni mwako?
-
Unajisikiaje unapokuwa umenuna usoni mwako?
Elezea kwamba watu wanaweza kila mara kujua jinsi tunavyojisikia kwa kuangalia nyuso zetu. Acha watoto wakuonyeshe nyuso zao za furaha.
Tunaweza kujifunza kudhibiti hisia zetu
Elezea kwamba ni vyema kuonyesha hisia zote tofauti tulizonazo, lakini ni lazima tuzionyeshe katika njia sahihi, hasa tunapokasirika.
Onyesha picha 1-47, Watoto Wanagombana.
-
Wewe unafikiri watoto hawa wanajisikiaje?
-
Unafikiri wanasemezana vipi?
-
Unapaswa kufanya nini unapokuwa umekasirika?
Elezea kwamba ingawa tunaweza kujisikia kupiga mtu, kupiga kelele, au kumuumiza mtu tunapokuwa tumekasirika, tunaweza kujifunza kuonyeshe hisia zetu kwa upole na ukarimu. Tunapompiga mtu au kumpigia kelele, sisi tunakasirika tu zaidi, lakini kuwa wakarimu kunaweza kutusaidia kujisikia vyema.
Shughuli
Acha watoto wachuke zamu kuwa watoto walio kwenye picha. Wasaidie kufikiria mambo ambayo watoto katika picha hiyo wanaweza kusemezana badala ya kupiga kelele au kupigana, kama vile “Naomba nichukue zamu yangu sasa? “Acha tupeane zamu,” “Najisikia huzuni unaponiita majina mabaya,” au “Sipendi unapofanya hivyo.”
Onyesha picha 1-48, Watoto Wakicheza na Vibao Mchemraba. Elezea kwamba watoto hawa wanacheza vizuri pamoja na wana nyuzo za furaha kwa sababu wanashirikiana na kuzemezana kwa ukarimu.
-
Ni nani anaweza kukusaidia kujisikia vyema unapokuwa na huzuni, kukasirika, au kuogopa?
Elezea kwamba tunapoongea na mama zetu, baba zetu, na wengine wanaotupenda, wanaweza kutusaidia kuelewa kwa nini tunajisikia jinsi tunavyofanya. Ikiwa tutaomba kwa Baba wa Mbinguni, Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kujisikia vyema. Roho Mtakatifu atatusaidia kujua cha kufanya ili tuweze kuwa na furaha tena.
Shughuli
Acha watoto wasimame na kufanya kitendo cha msitari wa shughuli mara kadhaa:
Hisia Zangu
Wakati mwingine ninapokuwa na huzuni (fanya uso wa huzuni),
Mama hunikumbatia. Kisha ninafurahi (jikumbatie na ufanye uso wa furaha).
Wakati mwingine ninapokasirika sana (fanya uzo wa kukasirika).
Mimi huondoka na kuongea na Baba (tembea hapo na uitikie kwa kichwa, kana vile unazungumza).
Kama kitu kinaniogopesha (fanya uso wa kuogopa),
Mimi husali ili kujifariji (kunja mikono).
Halafu mimi niendapo nje kucheza,
Nitakuwa na furaha kila siku (fanya uso wa tabasamu).
Tunakuwa na furaha wakati tunapowasaidia wengine
Onyesha picha 1-48, Watoto Wakimpa Mama Maua.
-
Unafikiri hawa watu walio kwenye picha hii wanajisikia vipi?
-
Kwa nini unafikiri wanajisikia hivyo?
-
Unajisikiaje unapompa mtu mwengine kitu?
Onyesha picha 1-45, Kusafisha Vyombo.
-
Msichana huyu anafanya nini?
-
Unafikiri msichana huyu aliye katika picha anajisikiaje? Kwa nini?
-
Wewe unajisikiaje unapomsaidia mtu mwingine?
Shughuli
Wasaidie watoto kufanya kitendo cha shughuli kifuatacho:
Kusaidia Hunifanya Mimi niwe na Furaha
Mimi napenda kumsaidia mama yangu (jifanye unavaa aproni);
Yeye ana kazi nyingi sana za kufanya.
Mimi humsaidia kukausha vyombo (jifanye kukausha vyombo).
Na kumlisha mtoto pia (jifanye kumnyonyesha mtoto kwa chupa).
Mimi napenda kumsadia baba yangu (jifanye kuvaa glavu za shamba);
Yeye ana kazi nyingi sana za kufanya (jifanye unakatia miti au kuong’oa magugu).
Mimi humsaidia bustanini (jifanye unamwagilia maji mimea)
Mpaka kazi yake inapoisha.
Kusaidia hunifanya kuwa na furaha (onyesha uso wa tabasamu).
Hunifanya nijisikie vyema sana (weka mikono kupishana na mabega na ujikumbatie).
Kwani ninapowasaidia wengine (nyoosha mikono kabisa),
Mimi ninafanya kile ninachopaswa kufanya (inamisha kichwa na ukunje mikono)
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuwe na furaha
Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tuwe na furaha. Wao wanajua kwamba tunaweza kuwa na furaha tunapofanya kile wanachotaka sisi tufanye.
Hadithi
Onyesha picha 1-49, Mwana Mpotevu, na usimulie hadithi hiyo inavyopatikana katika Luka 15:11–32. Elezea hisia tofauti zilizoonyeshwa na baba na wanawe. Kila hisia inapoonyeshwa, unaweza kumwambia mtoto mmoja aonyeshe uso ufaao kwenye ubao. Kwa mfano, unaweza kusema: Mvulana anaondoka nyumbani kwenda nchi ya mbali sana. Wakati aliondoka, baba yake alikuwa na huzuni. Baada ya muda marafiki wakamuacha peke yake. Yeye alijisikia huzuni. Punde, hakuwa na hela yoyote. Yeye aliogopa kwa sababu alikuwa na njaa na hakuna mtu ye yote ambaye angempatia chakula … na mengineyo.
-
Je, unafikiri yule mwana alijisikia vipi alipokuja nyumbani?
-
Kwa nini baba alikuwa na furaha mwanawe aliporudi? (Ona Luka 15:24.)
-
Kwa nini kaka mkubwa alikasirika wakati yule kaka yake mdogo aliporudi? Ona Luka 15:28–30. Angefanya nini ili awe na furaha tena?
Ushuhuda
Wahakikishie watoto kwamba kila mtu hujisikia furaha, huzuni, kukasirika, au kuogopa wakati mwingine. Tunapaswa kujifunza kuonyesha hisia hizi katika njia iliyo sahihi. Wakumbushe watoto kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka sisi tuwe na furaha. Waambie watoto jinsi wewe unavyojisikia unapofanya kile ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu wanatuka tufanye.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Acha watoto wasimame katika duara. Waambie wafanye midomo yao kunyoka na wasitabasamu. Kisha waanze kutabasamu katika duara kwa kutabasamu na kusema maneno yafuatayo: “Nitatabasamu kwa (jina mtoto).” Mtoto uliyemtaja anapaswa kutabasamu na urudia maneno hayo, akiingiza jina la mtoto anayefuata. Endelea mpaka watoto wote katika duara wawe wanatabasamu.
Wakumbushe watoto kwamba tunapotabasamu kwa watu wengine, wao pia watarudisha tabasamu. Ni vigumu kuwa na huzuni, kukasirika, au kuogopa huku tukiwa tunatabasamu.
-
Imbeni “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 198 au ”Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 60).
-
Waombe watoto kufikiria kitu wanachoweza kufanya ili wawe na furaha. Tupa kijifuko cha maharagwe au chombo laini kwa mtoto na useme,” (Jina la mtoto ana furaha ____________.” Acha mtoto ajaze katika pengo kitu ambacho kinamfanya awe na furaha na kisha akurudishie kifuko hicho cha maharage. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu moja.
-
Simulia hadithi ya mtoto ambaye hufanya vitu vyema kwa mama yake, kama vile kazi za nyumbani. Mama haumjui yule aliyemsaidia, kwa hiyo akamuuliza kila mtoto katika familia ni nani aliyemsaidia. Wakati anapofika kwa yule mtoto aliyefanya kitendo cha ukarimu, yeye hujua kwamba ni huyu mtoto ndiye aliyefanya kazi kwa sababu ya tabasamu kubwa la huyu mtoto. Mtoto anajisikia furaha kwa sababu yeye amefanya kitu kizuri.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Unaposema mstari ufuatao, waongoze watoto katika vitendo. Rudia kama watoto wanataka.
Fanya Siku za Furaha
Macho mawili yanaona mambo mazuri ya kufanya (onyesha macho),
Midomo miwili ya kutabasamu siku nzima (tabasamu tabasamu pana).
Maskio mawili ya kusikia wasemayo wengine (kunja kiganja sikioni).
Mikono miwili ya kuweka wanasesere pembeni (jifanye kuokota wanasesere na kuwaweka pembeni).
Ulimi wa kusema maneno ya ukarimu kila siku (onyesha mdomo),
Moyo wa upendo wa kufanya kazi na kucheza (weka mkono juu moyo),
Miguu midogo miwili ikimbiayo kwa furaha (onyesha miguu)
Fanya siku za furaha kwa kila mmoja.
-
Imba “If you’re Happy” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 266), ukitumia vitendo vilivyoelezwa. Rudia vishazi vya maneno vya ziada kama vile ilivyopendekezwa chini ya ukurasa wa kitabu cha wimbo.
-
Acha watoto watengeneze uso wa furaha, uso wa huzuni, uso wa kukasirika, na uso uliochoka. Elezea kwamba wanaweza kusema kwa maneno jinsi wanavyojisikia badala ya kulia au kukasirika. Tunapoazungumza kuhusu hisia zetu kila mara tunajisikia vyema.