Somo la 38
Naweza kuwa na Staha
Madhumuni
Ni kumtia moyo kila mtoto kuonyesha upendo kwa Baba wa Mbinguni na Yesu kwa kuwa na staha.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Kutoka 3:1–10.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Picha 1-19, Kristo na Watoto (Sanaa ya Picha za Injili 216; 62467); Picha 1-66, Musa na Kichaka Kinachoteketea kwa Moto (Sanaa ya Picha za Injili 107; 62239);Picha 1-67, Darasa lenye Staha.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Tunaweza kuwa na staha kanisani.
Onyesha picha 1-67, Darasa Lenye Staha.
-
Watoto hawa wako wapi?
-
Wanafanya nini?
-
Unafikiri wanafikiria kuhusu nini?
-
Utafanya nini unapokuja katika Msingi?
Eleza kuwa tunapokuja kanisani tunapaswa kutenda kwa njia fulani. Hii inaitwa kuwa na staha.
Acha watoto warudie neno staha mara kadhaa.
-
Unafikiri inamaanisha nini kuwa na staha?
Elezea kwamba kuwa na staha ni kufanya mambo ambayo yanaonyesha upendo wetu na heshima yetu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu. Tunaweza kuonyesha upendo wetu kwao katika njia zifuatazo (acha watoto waonyeshe baadhi ya njia hizo unapozungumza juu yake):
-
Kutembea kwa utulivu na kuongee kwa sauti ndogo.
-
Kukaa kwa utulivu na kusikiliza sala na masomo.
-
Kunyosha mikono yetu wakati tunapotaka kusema kitu.
-
Kukunja mikono yetu
-
Kuliweka safi jumba letu la mikutano.
Elezea kwamba tunapofanya mambo haya, Baba wa Mbinguni na Yesu wanajua kwamba tunawapenda na kwamba tunafurahia kuwa kanisani.
Tunaweza kuwa na hisia za kuwa na staha
Onyesha picha 1-19, Kristo na Watoto, na uelezee jinsi unavyojisikia unapofikiria kuhusu Yesu Kristo na jinsi Yeye anavyotupenda. Elezea kwamba hizi ni hisia za staha. Waalike watoto waonyeshe hisia zao kuhusu Yesu.
Tunaweza kuwa na staha nyumbani
Waambie watoto kwamba jumba la mikutano si mahali pekee tunapopaswa kuwa na staha.
-
Je, wewe hufanya nini wakati mtu anasali?
-
Je, wewe hufanya nini wakati wa jioni ya familia nyumbani?
Elezea kwamba wakati tunaposikiliza kwa utulivu wakati wa maombi na masomo nyumbani, pia tunakuwa wenye staha. Hii humwonyesha Baba wa Mbinguni na Yesu kwamba tunawapenda.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie wakati wa somo.
-
Wapeleke watoto matembezi ya staha katika kumbi za jumba la mikutano. Kama inawezekana, nendeni katika kanisa. Mnaporudi darasani, wapongeze watoto kwa kuwa na tabia ya staha na jadili jinsi staha yao ilivyowasaidia watu wengine katika jengo kuwa na staha katika madarasa yao.
-
Imba au useme maneno ya “I Will Try to Be Reverent” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 28, “Father, I Will Reverent Be” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 29), au “Our Chapel Is a Sacred Place” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 30).
-
Chora nyayo za kila mtoto kwenye karatasi ambayo ina mstari “Two Happy Feet” ulioandikwa juu yake (ona uk 126). Acha kila mtoto apake rangi mchoro wa mguu wake na kuuchukua nyumbani.
-
Acha kila mtoto achukue zamu kuonyesha njia anayoweza kuwa na staha darasani, kama vile kuketi kwa utulivu, kukunja mikono, na kunyosha mkono anapotaka kusema kitu. Zungumzia kuhusu kwa nini tunapaswa kuwa na staha katika nyumba ya Baba wa Mbinguni.
-
Wasaidie watoto kusema maneno ya mstari mmoja au yote miwili katika mistari ifuatayo. Buni vitendo kama inavyopendezwa na maneno.
Ifungue, Ifunge [Mikono]
Ifungue, Ifunge;
Ifungue, Ifunge;
Piga makofi kidogo.
Ifungue, Ifunge;
Ifungue, Ifunge;
Iweke kwenye mapaja yako.
Mimi natikisa mikono yangu.
Mimi natikisa mikono yangu.
Mimi nabingirisha mikono yangu.
Mimi napiga makofi.
Mimi nainua mikono yangu,
Kisha naishusha chini.
Na naikunja mapajani.
Mimi naituliza miguu yangu.
Mimi naipumzisha miguu yangu.
Mimi naketi wima kwenye kiti changu.
Mimi nainamisha kichwa changu.
Mimi nafunga macho yangu.
Mimi ni tayari kusali.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Imbeni au semeni maneno ya “The Chapel Doors” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 156). Acha watoto waweke kidole kwenye midomo yao kila mara kifungu cha maneno “Sh, tulia kimya” kinaposemwa.
-
Acha watoto wafunge macho yao. Waambie wao wanyoshe mikono yao kama wanaweza kukusikia ukiangusha sarafu au kifungo. Angusha sarafu au kifungo sakafuni au mezani. Kisha funga kifungo au sarafu na kitambaa cha mkono au kipande cha nguo. Waombe watoto wafunge macho yao, na wanyoshe mikono yao kama wakisikia sarafu au kifungo wakati huu. Angusha kifungo au sarafu iliyofungwa katika kitambaa sakafuni au mezani. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuna mengi ya kusikia kama watasikiliza kwa makini.