Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 8: Ninashukuru kwa ajili ya Mchana na Usiku


Somo la 8

Ninashukuru kwa ajili ya Mchana na Usiku

Madhumuni

Ni kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kulingana na mpango wa Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo aliumba mchana ili tuweze kufanya kazi na kucheza na usiku ili tuweze kupumzika.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mwanzo 1;1, 3–5, 14–18; Helamani 14:1–13; na 3 Nefi 1:15–23.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia na Kitabu cha Mormoni

    2. Mkato 1-1, jua; mkato 1-2, mwenzi; mkato 1-3, nyota (mikato kama hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha za Watoto wa Msingi seti 3).

    3. Picha 1-21, Samweli Mlamani Ukutani (Picha za Sanaa za Injili 314; 62370).

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Waambie watoto kwamba unafikiria kitu fulani ambacho Baba wa Mbinguni alikipanga na Yesu Kristo akakiumba. Waombe watoto wabahatishe ni kitu gani unachofikiria. Toa vidokezo vifuatavyo, kimoja baada ya kingine

  1. Hutufanya tujisikie joto.

  2. Ni cha duara na cha rangi ya njano.

  3. Kiko angani.

  4. Wakati mwingine huonekana kujificha nyuma ya mawingu au mlimani.

Baada ya watoto kubahatisha ni “jua” onyesha mkato wa umbo la jua.

  • Ni nani aliyeumba jua?

Tunafanya kazi na kucheza wakati wa mchana

Hadithi

Wasimulie watoto hadithi ya uumbaji mchana na usiku kutoka Mwanzo 1:1, 3–5 na uumbaji wa jua, mwezi, na nyota kutoka Mwanzo 1:14–18.

  • Ni nani aliyeumba mchana na usiku?

  • Ni nini Baba wa Mbinguni alimwambia Yesu Kristo aiweke angani ili kutuambia sisi kwamba sasa ni wakati wa mchana?

Waambie watoto kwamba jua hutupa mwanga ili tuweza kuona. Jua pia hutupa joto na husaidia mimea kuota. Hatungeweza kuishi duniani bila jua.

  • Tunauitaje muda ambao jua linakuwa limechomoza? (Mchana.)

Elezea kwamba tunaweza kufanya mambo mengi wakati wa mchana. Tunaweza kufanya kazi, kucheza, na kuwasaidia wengine.

Shughuli

Acha watoto wasimulie kuhusu vitu wanavyofanya wakati wa mchana, kama vile kula mlo, kucheza mchezo, au kufagia sakafu. Acha watoto wasimame na kuigiza baadhi ya mawazo yao. Unaweza kutaka kufanya baadhi ya vitendo pamoja nao.

  • Unaweza kufanya nini ili kumsaidia mtu wakati wa mchana? (Majibu yanaweza kujumuisha, kuokota wanasesere, kuosha vyombo, au kucheza na kaka au dada mdogo.)

Sisi tunapumzika wakati wa usiku

  • Je, tunaliona jua wakati wote?

Elezea kwamba kila jioni jua huzama na anga huwa giza. Hatuwezi kuliona jua usiku.

  • Tunauitaje muda ambao ni giza? (Usiku.)

  • Ni nini Baba wa Mbinguni alimwambia Yesu Kristo aviweke angani ili kutuambia sisi kuwa ni usiku? (Mwezi na nyota.)

Acha watoto waonyeshe maumbo ya mkato ya mwezi na nyota karibu na umbo la mkato la jua.

Shughuli

Acha watoto wazungumze kuhusu au wafanye igizo wa vitu wanavyofanya usiku, kama vile kusali wakati wa kulala, kusikiliza hadithi, kupiga mswaki, au kulala.

Elezea kwamba watu fulani, kama vile madaktari, manesi, na wazimamoto, hufanya kazi usiku, lakini wengi wetu hutumia usiku kulala. Wanyama wengi pia hulala usiku.

  • Kwa nini sisi tunalala?

Wasaidie watoto kuelewa kwamba usiku ni mzuri kwa miili yetu, na Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka sisi tuitunze miili yetu. Ikiwa tunapata usingizi wa kutosha, tutajisikia vyema na tutakuwa na afya zaidi. Ikiwa hatupati usingizi wa kutosha, tutachoka na kuwa wagomvi.

Ikiwa urefu wa michana unatofautina sana katika misimu katika eneo lako, elezea kwamba usiku unaweza kuwa mrefu wakati mwingine wa mwaka na mfupi nyakati zingine. Wazazi wanatusaidia kujua ni wakati gani wa kulala na ni wakati gani wa kuamka na kujishughulisha.

Shughuli

Acha watoto wasimame na kufanya mchezo ufuatao wa vidole:

Huyu Mdogo

Huyu mdogo ataenda kulala (inua kidole kimoja).

Kwenye mto yeye ulaza kichwa chake (laza kidole kwenye kingaja cha mkono mwingine)

Anajifunika kwa blangeti vyema (funga vidole juu ya kile cha kwanza),

Na hivi ndivyo anavyolala usiku mzima.

Asubuhi hufika naye hufungua macho yake.

Teke na matandiko yanaondoshwa (fungua mkono kuonyesha kidole kikipumzika).

Punde ameamka na akavaa na akaondoka (inua kidole).

Tayari kutabasamu na kufanya kazi na kucheza.

Baba wa Mbinguni alitumia mchana na usiku kutangaza kuzaliwa kwa Yesu

Hadithi

Waambie watoto kwamba Baba wa Mbinguni alitumia mchana na usiku kusaidia kuelezea kuzaliwa kwa Yesu. Onyesha picha 1-21, Samweli Mlamani Ukutani, na uelezee kile kichotendeka katika picha hiyo. Elezea kwamba Samweli Mlamani aliwaambia Wanefi nini kitatokea angani wakati wa Yesu kuzaliwa. Jua litazama, lakini anga halitakuwa na giza. Elezea kwamba watu wengi hawakumwamini Samweli, lakini kile alichosema kilitendeka (ona Helamani 14:1–13 na 3 Nephi 1:15-23).

Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa muhimu sana kwamba mbali sana katika Amerika, kule Wanefi na Walamani walikoishi, Baba wa Mbinguni aliufanya usiku ule uwe wa Yesu kuzaliwa kung’ara kama mchana.

  • Ni tukio gani muhimu ambalo Samweli Mlamani alikuwa anawaambia watu juu yake?

  • Wanefi waliona nini kikitokea angani usiku ule Yesu alipozaliwa?

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuumba mchana na usiku ili kutusaidia. Wahimize watoto kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya yote mchana na usiku.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.

  1. Pata karatasi nyeupe nzima na nusu karatasi ya rangi nyeusi au samawati kwa ajili ya kila mtoto. Gundisha ile nusu karatasi kwenye upande mmoja wa ile karatasi nyeupe kuashiria mandhari ya mchana na usiku. Kata duara ndogo ndogo kwenye karatasi kuashiria jua na mwezi, na wasaidie watoto kuzigundisha katika mahali sahihi. Tumia nyota au mikato ya nyota kuongezea katika mandhari ya usiku. Andika kwenye karatasi ya kila mtoto Ninashukuru kwa ajili ya Mchana na Usiku.

  2. Imbeni au semeni maneno “The World is So Lovely” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 233) au “Because God Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 234), au mstari wa pili wa The World is So Big” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 235). Fanya vitendo vya “Dunia ni Kubwa Sana” kama inavyoonyeshwa:

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Na ndani yake viumbe vya Mungu hupatikana;

    Nyota zing’aazo usiku kucha (nyosha na uchezeshe vidole),

    Jua mchana lina joto na linaangaza sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana.

    Mungu anatupenda sisi wote; baraka zetu ni nyingi (kunja mikono na ujikumbatie).

  3. Imba “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 253), ukitumia mapendekezo ya watoto kwa mistari hiyo. Kabla ya kuimba kila mstari, waulize watoto kama kitendo walichopendekeza kinafanywa mchana au usiku. Buni vitendo kama inavyopendezwa na maneno.

  4. Buni hadithi kuhusu kaka na dada ambao walikuwa wanacheza nje wakati wa mwisho wa siku. Tumia majina na hali ambazo watoto wa darasa lako wanazifahamu. Elezea kile ambacho watoto walifanya walipokuwa wakimaliza siku. Jumuisha maelezo ya kina kama vile jua lilianza kuzama, mama yao akiwaita waingie nyumbani, na watoto wakifanya kazi zilizohitajika, kusafisa, kujiandaa kwa mlo wa jioni, kusaidia kuosha vyombo, kujiandaa kulala, kusikiliza hadithi za wakati wa kulala, na kusali kando ya kitanda. Elezea jinsi kaka na dada, watu wengine, na ndege, wadudu, na wanyama wakijiandaa kwenda kulala.

    Wasaidie watoto kuelewa kwamba wakati wa usiku, tunapaswa kufunga macho yetu na kulala ili miili yetu iweze kukua na kuwa afya na nguvu. Hii ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu.

    Onyesha hadithi hii kwa maumbo ya mikato, au pangia sehemu kwa watoto na uwaache wafanye igizo la hadithi hii.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo zaidi

  1. Onyesha maumbo ya mikato ya jua, mwezi, na nyota. Uliza maswali yafuatayo:

    • Vitu hivi tunaviona wapi?

    • Tunaliona jua usiku?

    • Tunaona nyota wakati wa mchana?

    Elezea kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu aumbe jua ili kutupatia mwanga na kutupatia joto wakati wa mchana na mwezi na nyota kutupatia mwangaza usiku.

  2. Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari ufuatao huku ukisema maneno:

    Uumbaji wa Mungu

    Mungu aliumba mwezi (fanya duara kwa mikono).

    Na nyota za kumeremeta (fungua na ufunge mikono)

    Na akaziweka hewani (fikia juu)

    Aliumba jua (tengeneza duara kubwa juu ya kichwa)

    Na miti (nyoosha mikono kwa urefu)

    Na maua (weka mikono kama bakuli)

    Na ndege wadogo ambao huruka (punga mikono).

    (Kutoka Fascinating Finger Fun na Eleanor Doan. © 1951. Imetumika kwa Idhini.)

  3. Imbeni au semeni maneno “I Am like Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 163, au ”Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 60).

Chapisha