Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 17: Ninashukuru kwa ajili ya Mikono Yangu


Somo la 17

Ninashukuru kwa ajili ya Mikono Yangu

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuthamini mikono yake na kile inachoweza kufanya.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mathayo 19:13–15 na Mafundisho na Maagano 20:70; 35:6; 42:43–44.

  2. Andaa mfuko au sanduku lililo na vitu vya kawaida vilivyo na maumbo na sura tofauti, kama vile jiwe, jani, kipande cha kitambaa, kijiko, kichana na penseli. Jumuisha angalao kitu kimoja kwa kila mtoto katika darasa.

  3. Kama inawezekana, tengeneza nakala ya kitini cha ishara za lugha (kilichopo mwisho wa somo) kwa kila mtoto.

  4. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Kitu kidogo kama vile kifungo au sarafu.

    3. Picha 1-8, Kupitisha Sakramenti (62021); picha 1-11, Mvulana Akibatizwa (60018); picha 1-12 Msichana Akithibitishwa; na picha (62020); picha 1-39, Kubariki Mtoto Mchanga; picha 1-40, Kuhudumia Wagonjwa (62342).

  5. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Taarifa kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, wali si ulemavu wao.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Acha mtoto aingize mkono katika mfuko au sanduku ambalo umeandaa, bila kuangalia ndani. Mwambie mtoto aguse mojawapo ya vitu hivyo, na aelezee inavyosikika (nyororo, ngumu, laini, ya kukwaruza), na ajaribu kubahatisha kuwa ni kitu gani. Kisha uache mtoto huyo atoe kitu hicho kutoka kwenye mfuko au sanduku na kukionyesha kwa darasa. Acha watoto wengine wakiguse. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu moja.

  • Je, mlitumia nini kufikia ndani ya mfuko (boksi)?

  • Je, mlitumia nini kukihisi kitu hicho?

Sisitiza kwamba mikono yetu ni baraka kubwa kwetu. Tunaweza kutumia mikono yetu katika njia nyingi.

Tunaweza kufanya mambo mengi na mikono yetu

Acha watoto wainue mikono yao na kuiangalia. Zungumza kuhusu kile watoto wanaweza kufanya kwa mikono yao. Wanaweza kuokota kitu kwa vidole vyao pamoja na dole gumba, wanaweza kushikilia kitu katika viganja vyao, wanaweza kuipunga na kugeuza mikono yao kila upande.

Shughuli

Ukitumia kitu kidogo kama vile kifungo au sarafu, acha watoto wachukue zamu kujaribu kuokota kitu bila kutumia vidole gumba vyao. Wakumbushe watoto kwamba kila sehemu ya mwili wetu ni muhimu.

Shughuli

  • Mikono yako ilikusaidia vipi kujiandaa kuja kanisani?

Acha watoto wafanye igizo la shughuli za asubuhi, kama kuosha nyuso zao, kuvaa nguo, kuchana nywele zao, kula, na kupiga mswaki meno yao.

  • Mikono yako inakusaidia vipi kucheza?

Acha watoto wafanye igizo la njia wanazotumia mikono yao katika kucheza, kama vile kudundisha mpira, kumlisha mwanasesere, kujenga kwa tofali au mchanga, au kupiga ngoma.

  • Mikono yako inakusaidia vipi kufanya kazi?

Acha watoto wafanye igizo la njia wanazoweza kutumia mikono yao kufanya kazi, kama vile kuokota wanasesere, kupanga meza, kutandika kitanda, au kulisha mnyama wa nyumbani.

  • Mikono yako inakusaidiaje wakati unapokuja kanisani?

Acha watoto wafanye igizo la njia tunazotumia mkono yetu kanisani, kama vile kusamiliana, kuinua picha, kunyosha mkono ili kujibu swali, au kupokea sakramenti.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba mikono yetu ni baraka kubwa kwetu na kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tuitumie mikono yetu katika kujisaidia wenyewe na kuwasaidia wengine. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu hawataki tutumie mikono yetu kuwa jeuri kwa wengine—kupigana au kufinyana au kukwaruzana. Wanatutaka tujifunze kutumia mikono yetu kwa njia zilizo sahihi.

Watu wengine hutumia mikono yao katika kutusaidia sisi

  • Ni kwa namna gani wazazi na wana familia wengine hutumia mikono yao katika kutusaidia sisi?

Zungumzia kuhusu jinsi familia zetu wanavyoandaa chakula chetu, kusafisha nguo zetu, kufunga viatu vyetu, kucheza nasi, na kufanya mambo mengine mengi kwa ajili yetu.

Elezea kwamba wanaume ambao wenye ukuhani wanaweza kutubariki kwa kutuwekea mikono. Onyesha picha zilizoorodheshwa katika sehemu ya “Maandalizi,” moja kwa wakati, na waache watoto watambue aina tofauti za baraka tunazoweza kupokea kupitia mikono ya wenye ukuhani. Wasaidie wao kuelewa kwamba tunaweza kupewa baraka tukiwa watoto wachanga; tunaweza kubatizwa tunapofika umri wa miaka minane; tunaweza kuthibitishwa baada ya ubatizo na kupatiwa kipawa cha Roho Mtakatifu; tunaweza kupokea mkate na maji, ambavyo vimebarikiwa na kupitishwa na wenye ukuhani, wakati wa sakramenti kila wiki; na tunaweza kupokea baraka tunapokuwa wagonjwa.

Hadithi

Fungua Biblia yako katika Mathayo 19:13–15 na usimulie hadithi ya Yesu akiwabariki watoto. Soma kwa sauti sehemu ya kwanza ya mstari wa 13 (hadi kuwaombea). Zungumza kuhusu jinsi Yesu alivyoitumia mikono yake kuwabariki watoto.

Elezea kwamba Yesu pia alitumia mikono yake kuwasaidia watu wengine katika njia zingine, kama vile kuwabariki walipokuwa wagonjwa, vipofu, au viziwi.

Mikono yetu inaweza kuzungumza

Tumia mikono yako kupunga mkono au kuita. Waulize watoto kile unachosema kwa mikono yako.

Elezea kwamba watu fulani ambao ni viziwi na hawawezi kusikia na kusema hufanya ishara kwa mikono yao ambazo zinamaanisha kwa maneno. Wao huzungumza kwa mikono yao. Hii inaitwa lugha ya ishara.

Shughuli

Ukitumia kitini mwishoni mwa somo, wafundishe watoto jinsi ya kusema “baba,” “mama.” na “Mimi nakupenda” kwa lugha ya ishara. Kama inawezekana, mpe kila mtoto nakala ya kitini kuchukua nyumbani na kushirikiana na familia yake.

Ushuhuda

Inueni mikono yenu juu na mtoe shukrani zenu kwa ajili yake. Wahimize watoto kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya mikono yao na kuitumia mikono yao kujisaidia wenyewe na wengine.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.

  1. Chora kwa kukandamiza mikono wa kila mtoto kwenye kipande cha karatasi. Andika Mimi ninashukuru kwa ajili ya mikono yangu kwenye kipande cha karatasi, na waache watoto wapake rangi picha hii na waende nayo nyumbani.

  2. Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno ya “I Have Two Little Hands” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 272) au “My Hands” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.273). Buni vitendo kama inavyopendezwa na maneno.

  3. Kama eneo na hali ya hewa inaruhusu, wapeleke watoto kwa matembezi ya nje ili kugusa vitu tofauti tofauti, kama vile tofali, chokaa, mashina ya miti, na nyasi.

  4. Fanya shughuli ifuatayo ili kuwasaidia watoto kuhesabu vidole vyao pamoja na vidole gumba:

    Kuhesabu Vidole

    Inua mkono mmoja juu na utumie kidole cha mkono mwingine kuonyesha na kuhesabu, ukianzia na kidole kidogo.

    Kidole kimoja, vidole viwili, vidole vitatu, vinne.

    Sasa kidole gumba ili kuongeza kimoja zaidi.

    Viko vitano katika mkono mmoja,

    Kama vile tu Baba wa Mbinguni alivyopanga.

    Inua juu ule mkono mwingine na huonyeshee na kuhesabu kwa njia ile ile.

    Kidole kimoja, vidole viwili, vidole vitatu, vinne.

    Sasa kidole gumba ili kuongeza kimoja zaidi.

    Vitano viko katika mkono huu, pia.

    Naweza kuvifundisha cha kufanya.

    Inua mikono yote juu na ukunje vidole kila kidole kinapohesabiwa.

    Kumi vyote—acha tuhesbabu mara moja tena.

    Moja na mbili na tatu na nne,

    Tano, sita, saba, nane, tisa, kumi—vyote.

    (Kunjua vidole vyote kwa pamoja.)

    Vinaweza kusimama wima kabisa na ni virefu.

  5. Imbeni au semeni maneno ya “Fun to Do” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, p. 263) mara kadhaa. Kwa kila mstari, acha watoto wasimulie kitu ambacho mikono yao inaweza kufanya, kama vile kudundisha mpira, kuchuma maua, kumliwaza mwanasesere, kucheza piano, au kupunga mkono wa kwaheri.

  6. Wasaidie watoto kufanya mstari ufuatao wa shughuli, wakitumia vitendo vinavyopendekezwa na maneno:

    Mimi Nafikia Juu Sana

    Mimi nafikia juu sana

    Na nafikia chini sana

    Na ninatikisa mikono yote .

    Mimi natanua vidole vyangu kabisa,

    Na sasa nakunja ngumi.

    Nafikia mbele

    Na sasa nafikia nyuma;

    Mimi napiga makofi hivi.

    Kisha naketi na kuiweka mapajani.

    Ambapo itakaa tuli.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari ufuatao wa shughuli huku wakisema maneno:

    Mimi Napenda Mikono Yangu

    Mimi napenda mikono yangu; ni marafiki zangu (Inua mikono na uitazame).

    Inashughulika na kunisaidia mpaka siku iishe (fanya igizo la mikono ikifanya kazi).

    Inaweza kujikunja kimya kimya (kunja mikono) au piga makofi kwa nguvu (makofi)!

    Inapofanya kile kilicho sahihi, hunifanya nione fahara!

  2. Acha watoto wakae katika duara. Elezea hali na waache watoto wafanye igizo la kile ambacho mikono yao inapaswa kufanya katika hali hiyo.

    Mifano:

    Nionyeshe kile mikono yako inapaswa kufanya kabla ya wakati wa mlo.

    Nionyeshe kile mikono yako inapaswa kufanya wakati unasikiliza hadithi.

    Nionyeshe kile mikono yako inapaswa kufanya wakati umeombwa kuokota wanasesere wako.

    Nionyeshe kile mikono yako inapaswa kufanya wakati unaposali.

    Elezea kwamba sisi lazima tuisaidie mikono yetu ili daima ifanye yale inayopaswa kufanya.

  3. Kariri mstari ufuatao pamoja na watoto, mkifanya vitendo kama inavyopendekezwa na maneno:

    Pigeni Makofi

    Pigeni makofi, pigeni makofi,

    Pigeni makofi kama mimi.

    Gusa mabega yako, gusa mabega yako,

    Yaguse kama mimi.

    Piga magoti yako, piga magoti yako,

    Yapige kama mimi.

    Tingisha kichwa chako, tingisha kichwa chako,

    Kitingishe kama mimi.

    Pigeni makofi, pigeni makofi,

    Sasa tulieni

Picha
mikono yetu inaweza kuzungumza

Mikono yetu inaweza kuzungumza

Mimi

Nakupenda

Wewe

Baba

Mama

Chapisha