Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 18: Ninashukuru kwa ajili ya Masikio Yangu


Somo la 18

Ninashukuru kwa ajili ya Masikio Yangu

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuthamini masikio yake na kile yanachoweza kufanya.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Marko 7:32–35 na Joseph Smith—Historia 1:17.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia na Lulu ya Thamani Kuu.

    2. Picha 1-4, Ono la Kwanza (Picha za Sanaa za Injili 403; 62470); picha 1-41, Mtoto aliye Visaidizi vya Kusikia; picha ya nabii hai.

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote zenye Kuboresha unazotaka kutumia.

Angalizo kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wowote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, na si ulemavu wao.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Fanya yafuatayo kwa kunong’ona:

Msalimie kila mtoto. Waelekeze watoto wafanye mambo kadhaa, kama vile keti chini, nyosha mikono, shusha mikono, na nyoosha vidole viwili.

Kwa sauti yako ya kawaida, waulize watoto walijuaje cha kufanya wakati wewe ulipokuwa ukinong’ona.

  • Je, sehemu gani ya mwili wako ilikusaidia kujua kile nilichokisema?

Masikio yetu ni baraka kwetu

Wimbo

Pamoja na watoto, imbeni au mseme maneno ya mstari 1 na 2 wa “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20).

Shukrani kwa Baba yetu twaleta.

Kwani yeye hutupatia kila kitu.

Macho na masikio na mikono na miguu,

Nguo za kuvaa, na chakula cha kula.

  • Wimbo unasema Baba wa Mbinguni ametupatia nini?

  • Kipi kati ya vitu hivi hutusaidia kusikia? (Masikio.)

Waambie watoto kwa makini waguse masikio yao. Elezea kwamba sehemu za masikio zilizo nje ya vichwa vyao sio viungo watumiavyo kusikia. Sehemu hii husaidia sauti kwenda ndani ya sikio hata kwenye kiwambo cha sikio na sehemu nyinginezo za sikio ambazo hutusadia kusika.

  • Tunawezaje kuwa makini na masikio yetu?

Elezea kwamba tunapaswa kuyalinda masiko yetu kutokana na sauti kubwa na kutokana na vitu vinavyoweza kuyaharibu.

Elezea kwamba kuna sababu kadhaa, baadhi ya watu masikio yao hayafanyi kazi vyema, kwa hiyo hawawezi kusikia sauti zote ambazo watu wengi wanaweza kusikia. Kama kuna mtu ye yote ambaye watoto wanamjua ana mapungufu ya kusikia, unaweza kuelezea juu ya chombo kimsaidiacho mtu huyo kusikia. Onyesha picha 1-41, Mtoto Aliye na Kisaidizi cha Kusikia, unapoelezea. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kila mara watu ambao hawasikii vyema hawawezi kuongea vyema pia, kwa sababu watu hujifunza kwa kusikia na kuiga sauti wanazosikia.

Shughuli

Fanya ishara ya lugha ya ishara ya “Mimi nakupenda” (tazama somo la 17.)

  • Je, unakumbuka maana ya hii?

Acha watoto wafanye ishara hizi.

Wakumbushe watoto kwamba wiki iliyopita tulijadili jinsi mikono inavyoweza kuongea kupitia lugha ya ishara. Wasaidie watoto kuelewa kwamba watu ambao hawasikii wanaweza kuwasiliana kwa njia zingine, kama vile lugha ya ishara, maandishi, na kusoma midomo.

Hadithi

Simulia hadithi ya Yesu na mtu kiziwi, kama inavyopatikana katika Marko 7:32–35.

  • Je, unafikiri yule mtu kiziwi alijisikiaje wakati alipotambua kwamba sasa anaweza kusikia?

Sisitiza ni baraka iliyoje kuweza kusikia.

Tunaweza kusikia sauti kwa masikio yetu

Shughuli

Waambie watoto kwamba watafanya mazoezi ya kutumia masikio.

Acha kila mtoto achukue zamu kuja mbele ya chumba. Mnong’oneze mtoto sikioni jina la mnyama wa kawaida au kitu ambacho hutoa sauti. Acha mtoto huyu atoe sauti kwa darasa na uwaache wale wengine wabahatishe ni nini hutoa sauti hiyo. (Sauti inaweza kujumuisha mooo ya ng’ome, kubweka kwa mbwa, mlio wa simu, au honi ya gari.)

Jadili pamoja na watoto baadhi ya sauti muhimu wanazoweza kusikia kwa masikio yao, kama vile wazazi wakiitana na sauti ambayo inawaonya kwamba wanaweza kuumia.

  • Unapendelea kusikia sauti gani?

Tunaweza kusikiliza mafundisho ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Au acha watoto waketi kimya na kusikiliza.

  • Mmesikia nini ?

Jadili sauti tofauti wanaweza kusikia, kama vile milango ikifunguka na kufunga, watu wakizungumza ukumbuni, muziki wa kinanda, au upepo.

  • Ni sautii gani nyingine tunazosikia kanisani?

Elezea kwamba tunasikia walimu wetu, wazazi, viongozi wa watoto wa darasa la Msingi, askofu, na viongozi wengine kanisani.

  • Kwa nini ni muhimu kwetu kuwasikiliza watu hawa?

Elezea kwamba watu hawa hutusadia kujifunza kile Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanye.

Hadithi

Onyesha picha 1-4, Ono la Kwanza, na uwaache watoto waseme kile wanachokumbuka juu ya picha hii. Fungua maandiko katika Lulu ya Thamani Kuu na usome kwa sauti kitu ambacho Baba wa Mbinguni alimwambia Joseph Smith katika Joseph Smith—Historia 1:17, “Huyu Ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!”

Acha watoto warudie kauli hii pamoja nawe mara chache. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni anataka tusikilize kitu ambacho Yeye na Yesu wanasema. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu hawawezi kuongea na kila mtu moja kwa moja, lakini tunaweza kuwasikiliza wazazi wetu, walimu, na viongozi wa Kanisa. Wanaweza kutuambia kile ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu wanataka tujue. Roho Mtakatifu pia anaweza kutusaidia kujua kile ambacho Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanye.

Onyesha picha ya nabii aliye hai.

  • Je, huyu ni nani?”

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu husema nasi kupitia viongozi wetu wa Kanisa, hasa nabii wetu na askofu wetu. Viongozi hawa hutuambia kile Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tufanya. Tunapaswa kuwasililza wao kwa makini.

Ushuhuda

Elezea shukrani zako kwa ajili masikio yako na kwa kipawa cha kusikia.

Shughuli zenye Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Acha watoto wafunge macho yao, na kuyafunika na mikono yao. Gusa mtoto mmoja kichwani. Mtoto huyu anapaswa kusema, Mimi ninashukuru kwa ajili ya masikio yangu.” Acha watoto wengine wabahatishe hiyo ni sauti ya nani waliyoisikia. Endelea mpaka kila mtoto apate zamu ya kusema.

  2. Fanya mstari wa shughuli ifuatayo pamoja na watoto:

    Mimi Nina Mwili wa Ajabu

    Mimi nina mwili wa ajabu (gusisha mikono kwenye kufua)

    Baba wa Mbinguni aliipanga kwa ajili yangu.

    Yeye alinipa masikio ili niweze kusikia (kunja kiganja cha mkino sikioni)

    Na macho ili niweze kuona (onyesha macho).

    Mimi nina mikono miwili ambayo naweza kupiga makofi (piga makofi),

    Miguu miwili ambayo inaweza kugeuka (geuka).

    Wakati nikitaka, naweza kugusa.

    Vidole vyangu chini sakafuni (inama gusa vidole).

    Ninapofikiria kuhusu mwili wangu (weka kidole kichwani),

    Sehemu yake bora ni (keti chini kimya)

    Baba wa Mbinguni aliipanga kwa ajili yangu.

    Uweze kuonekana zaidi kama wake.

  3. Acha watoto waangalie upande mwingine huku wewe ukisimama nyuma yao. Fanya sauti kwa mikono yako au kitu kingine cha kutoa sauti, na waache watoto wabahatishe kile ambacho wewe unafanya ili kutoa sauti hiyo. Unaweza kupiga makofi, chezesha vidole vyako, au piga kengele. Waache watoto wajaribu kufanya sauti hizo wao wenyewe.

  4. Nasa sauti katika mtaa wako, kama vile mbwa akibweka, ndege wakiimba, au kicheko. Cheza sauti hizo darasani na waache watoto wasikilize na wabahatishe hizo sauti ni za nini.

  5. Wafundishe watoto wimbo rahisi au kipengele cha maneno katika lugha ya ishara. Kama unamjua mtu ambaye anaweza kufanya ishara vizuri, unaweza kumwalika kuja darasani na kufanya ishara ya “Mimi ni Mtoto wa Mungu” huku darasa likiimba.

  6. Keti pamoja na watoto katika duara. Nong’oneza ujumbe mfupi kwa mtoto aliye karibu nawe. Mtoto huyu naye kisha amnong’onezee mwingine, hivyo hivyo katika duara. Mtoto wa mwisho aseme ujumbe huo kwa sauti. Liambie darasa ujumbe ambao ulimpa mtoto wa kwanza ili kuona jinsi ulivyobadilika.

    Baada ya shughuli waulize watoto wametumia nini kusikia ujumbe huo. (Masikio.) Wakumbushe watoto kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya masikio yao.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Kama inawezakana wapeleke watoto huko nje. Wahimize wao wasikilize kwa makini kwa masikio yao. Ni sauti gani wao wanaweza kuzisikia? Mnaporudi tena darasani, rejea sauti walizosikia.

  2. Watoto wasimame na kusema mstari ufuatao, wakifanya vitendo kama inavyoashiriwa na maneno:

    Gusa Macho Yako

    Gusa macho yako,

    Gusa pua yako,

    Gusa masikio yako,

    Gusa vidole vyako,

    Nyosha mikono yako,

    Juu juu sana,

    Hata juu sana,

    Kuelekea angani,

    Weka mikono yako,

    Kwenye nywele zako;

    Keti chini pole pole,

    juu ya kiti chako.

Chapisha