Somo la 7
Roho Mtakatifu Hunisaidia Mimi
Madhumuni
Kumsaidia kila mtoto kujua kuwa Yesu Kristo hutusaidia.
Maandalizi
-
Jifunze kwa maombi Yohana 14:16–17; 2 Nefi 32:5; Moroni 10:4–5; na Mafundisho na Maagano 39:23; 130:22. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 7.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia, na nakala ya Mafundisho na Maagano.
-
Kitu cha kawaida na mfuko wa kukiwekea ndani.
-
Picha 1-3, Yesu Kristo (Picha za Sanaa za Injili 240; 62572); picha 1-4, Ono la Kwanza (Picha za Sanaa za Injili 403; 62470);
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwaalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Roho Mtakatifu hutupa faraja na msaada
-
Unapoumia au kuhuzunika, mama au baba yako hukupa faraja vipi na kukufanya ujisikie vyema?
Onyesha picha 1-3, Yesu Kristo. Waambie watoto kwamba Yesu alijua kwamba wafuasi wake, wasaidizi wake, wangekuwa na huzuni wakati atakufa, kwa hiyo aliwaambia kwamba angemwomba Baba wa Mbinguni awatumie mfariji wa kuwasaidia wasjisikie vibaya (ona Yohana 14:16–17).
Waambie watoto kwamba mfariji huyu ni Roho Mtakatifu, na anaweza kutufariji sisi pia. Elezea kwamba tunapokuwa na huzuni au kukasirika, Baba wa Mbinguni atatusaidia kwa kumtuma Roho Mtakatifu kutufariji.
Roho Mtakatifu hutusaidia kujua kile kilicho sahihi
Elezea kwamba Roho Mtakatifu anatupenda na hutusaidia kuchagua kile kilicho sahihi. Acha watoto wafikirie vitu fulani ambavyo wamefanya ambavyo ni vyema, kama vile kuwatii wazazi, kuwasaidia wengine, na kusali.
-
Unahisi vipi unapofanya vitu ambavyo ni sahihi?
-
Unahisi vipi unapofanya vitu ambavyo ni makosa?
Elezea kwamba Roho Mtakatifu hutusaidia kujua tofauti kati uzuri na ubaya kwa kutupa hisia nzuri na za ukunjufu tunapofanya kitu sahihi na kuhisi huzuni tonapofanya kosa.
Acha watoto washiriki wakati walihisi hisia nzuri, za ukunjufu kwa sababu walifanya chaguo sahihi au walimsaidia mtu. Wasaidie kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu hutusaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni halisi
Elezea kwamba Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kutambua wakati jambo ni kweli au halisi. Waonyeshe watoto mfuko ulio na kitu ndani yake. Waambie watoto kwamba kuna kitu fulani ndani ya mfuko, lakini hauwaonyeshi kitu hicho.
-
Kuna kitu chochote katika mfuko huu?
Elezea kwamba ingawa watoto hawawezi kuona kitu ndani ya mfuko, wanajua kiko ndani kwa sababu uliwaambia kuwa kiko ndani hapo. Hata ingawa ni watu wachache ambao washamemwona Baba wa Mbinguni na Yesu, Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu ni halisi na kwamba wanatupenda. Elezea kwamba ufahamu huu unaitwa ushuhuda. Wakati fulani watu hutoa ushuhuda wao katika mikutano ya Kanisa na kutuambia kwamba wanajua Yesu yu hai. Roho Mtakatifu amewasaidia kujua ukweli huu.
Tunaweza kupokea karama za Roho Mtakatifu
Zungumzia kuhusu uzoefu wako katika kubatizwa na kuthibitishwa. Zungumzia kuhusu jinsi wanaume wanaoshikilia ukuhani waliweka mikono yao juu ya kichwa chako na kukupa karama ya Roho Mtakatifu.
Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 39:23 hadi Roho Mtakatifu. Elezea kwamba wakati watoto wanapofika miaka minane na kubatizwa na kuthibitishwa, wataweza kupokea karama ya Roho Mtakatifu. Karama ya Roho Mtakatifu itawasaidia kuweka ahadi walizofanya wakati walibatizwa.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo hilo.
-
Wasaidie watoto kuimba ua kusema maneno ya “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 106) au “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk.105).
-
Onyesha picha za watoto wakifanya vitu vizuri, kama vile kushiriki na kusaidiana. Waulize watoto jinsi wanahisi wakati wamefanya vitu vizuri. Waelezee watoto baadhi ya mazingira ya watu wakifanya vitu vizuri na vitu vibaya, kama vile kuwasaidia mama zao, kupigana na kaka zao, kushiriki wanasesere, na kutowatii wazazi wao. Acha watoto wasimame wakati kitendo ni kizuri na kuketi chini wakati ni kitendo si kizuri
-
Kwa sauti tulivu sema, “Mtu yeyote anayeweza kusikia sauti yangu, weka kidole chako kwenye pua lako. Mtu yeyote anayaweza kusikia sauti yangu, weka mikono yenu juu ya kichwa chako.” Endelea, ukitaja sehemu zingine za mwili, mpaka watoto wote wanaosikiliza sauti yako tulivu. Elezea kwamba hata ingawa wewe ulikuwa unasema kwa sauti ndogo, wakati watoto walisikiliza, wangeweza kusikia sauti yako na kutii maelekezo yako. Elezea kwamba Roho Mtakatifu wakati mwingine huzungumza nasi kwa sauti ndogo. Kama tutasikiliza kwa makini yeye atatwambia vitu muhimu.
-
Simulia kwa maneno yako mwenyewe, hadithi ya Rais Wilford Woodruff, Rais wa nne wa Kanisa.
Usiku mmoja Rais Woodruff, mkewe, na watoto wao wanne walipokuwa safarini, walisimama ili kulala katika nyumba ya rafiiki yao. Watatu kati ya watoto wao walilala katika nyumba hali Rais Woodruff, mkewe, na mtoto mmoja walilala nje katika gari. Rais Woodruff alisema: “Nilikuwa kitandani kwa muda mfupi niliposikia sauti ikiniambia: ‘amka na uondoe gari lako.’ Haikuwa radi, umeme au tetemeko la ardhi, lakini sauti tulivu, ndogo ya Roho wa Mungu—Roho Mtakatifu. … Niliamka na kusongeza gari langu … na kuliegesha kwenye upande wa nyumba. Nilipokuwa nikirudi kitandani Roho ile ile ikaniambia, ‘Nenda ukawaondoe nyumbu wako kutoka kwenye ule wa mti wa mwaloni.’ … Nikawaondoa hadi kwenye kijisitu cha migunga na kuwafunga hapo. Kisha nikaenda kulala. Katika mda wa dakika thelathini kimbunga kiliupiga ule mti ambao nilikuwa nimewafunga nyumbu wangu, kuung’oa kutoka mchangani na kuubeba yadi mia moja, kufagia ua mbili njiani mwake, na kuuangusha … karibu na pale gari langu lilipokuwa limesimama. … Kwa kutii ufunuo wa Roho wa Mungu kwangu niliokoa misha yangu na maisha ya mke wangu na mtoto, pia wanyama wangu” (“Leaves from My Journal,” Millennial Star, 12 Dec. 1881, pp. 790–91).
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wiki kabla ya somo hili, waombe wazazi wa kila mtoto wamruhusu mtoto alete “kitu cha faraja” darasani. Hii inaweza kuwa blangeti maalum au mwanasesere au wimbo maalum wa kuimba. Lete vitu vichache zaidi ikiwa mmoja atasahau kuleta kitu.
Darasani zungumza na watoto kuhusu jinsi vitu hivi huwafanya wahisi kuwa salama na kupendwa. Elezea kwamba mmoja wa wasaidizi wa Baba wa Mbinguni na Yesu anaweza kutufanya tuhisi kuwa salama na kupendwa. Mtu huyu wakati mwingine anaitwa Mfariji, kwa sababu Baba wa Mbinguni alimtuma kuwa nasi wakati tunahisi huzuni au hofu. Mtu huyu ni Roho Mtakatifu, rafiki wa ajabu!
-
Imbeni au mseme maneno ya mstari wa mwisho wa “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 106) na uwasaidie watoto kufanya vitendo vinavyoelezewa.
Sikiliza, sikiliza (kuja kiganja sikioni).
Roho Mtakatifu atanong’oneza (weka kidole cha shahada kwenye midomo).
Sikiliza, sikiliza (kuja kiganja sikioni).
Ile sauti ndogo tulivu (weka mikono pamoja juu ya moyo),