Somo la 4
Mimi Ninaweza Kuomba kwa Baba wa Mbinguni
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kujifunza jinsi ya kuomba kwa Baba wa Mbinguni na kujua kwamba Yeye atasikiliza.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Danieli 6. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 8.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Picha 1-9, Maombi ya Asubuhi (62310); picha 1-10, Maombi ya Familia; picha 1-14, Danieli katika Tundu la Simba (Picha za Sanaa za Injili 117; 62096); picha 1-15, Kubariki Chakula.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zozote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Sisi tunaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni
Toa ushuhuda wako kwamba hata ingawa hatuwezi kumwona yeye, tunaweza kuomba kwa Baba wa mbinguni na Yeye atasikiliza maombi yetu.
Onyesha picha 1-9, Maombi ya Asubuhi.
-
Msichana huyu anafanya nini?
-
Anazungumza na nani?
-
Unafikiri anaweza kuwa anasema nini na Baba wa Mbinguni?
Tumia picha 1-9, Maombi ya Asubuhi; picha 1-10, Maombi ya Familia; picha 1-15, Kubariki Chakula, unapojadiliana na watoto nyakati ambazo tunaomba. Elezea kwamba tunaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni wakati wo wote tunapotaka; nyakati za kawaida sana ni wakati tunapoamka, tunapoenda kulala, wakati wa chakula, pamoja na familia zetu, na wakati tunapokuwa na mahitaji maalum. Acha watoto waonyeshe picha ifaayo unapojadiliana nao.
Yesu Kristo alitufundisha kuomba kwa Baba wa Mbinguni
Elezea kwamba Yesu ametufundisha kufanya mambo fulani wakati tunapoomba. Tunapojiandaa kuomba, tunafikiria juu ya Baba wa Mbinguni.
-
Tunafanya nini na mikono yetu wakati tunaomba?
-
Tunafanya nini na vichwa na macho yetu wakati tunapoomba?
Baba wa Mbinguni husikiliza wakati tunaomba
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Rusha kitu laini kama vile kijifuko cha maharagwe au mpira kwa watoto. Baada ya kila mtoto kushika kitu hicho, mwambie akamilishe sentensi hii “Ninapoomba, mimi humshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya.” Mtoto aweza kujibu, “Familia yangu.” Baada ya kila mtoto kupata zamu, rudia shughuli hii, watoto wakitaja vitu wanavyoweza kumwomba Baba wa Mbinguni wakati wanapoomba. Unaweza kuonyesha picha ili kuwasaidia wao kufikiri juu ya mawazo.
-
Imbeni au semeni maneno ya “A Song of Thanks” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20), mkifanya vitendo vinavyoelezwa hapa chini:
Tunakushukuru kwa ajili ya duniani nzuri (fanya umbo la duara kuashiria dunia);
Tunakushukuru kwa ajili ya chakula tunachokula (jifanye unaweka chakula mdomoni);
Tunakushukuru kwa ajili ya ndege waimbao (lete vidole na dole gumba pamoja mfano wa mdomo wa ndege.
Tunakushukuru, Mungu, kwa ajili ya kila kitu (nyoosha mikono kabisa)!
(Kutoka kwa First Year Music na Hollis and Dann. (© 1957 na D. C. Heath and Company. Imechapishwa tena kwa Idhini.)
-
Karirini mstari “Ninashukuru kwa ajili ya Macho Yangy,” mkiota kila sehemu ya mwili mnapoitaja:
Ninashukuru kwa ajili ya macho yangu,
Masikio yangu, mdomo wangu na pua;
Ninashukuru kwa ajili ya viganja vyangu na mikono yangu.
Miguu yangu na vidole vyangu
(Imetoholewa kutoka kwenye mstari wa Beverly Spencer.)
-
Acha watoto wafanye igizo la hadithi ya Danieli katika pango la simba. Unaweza kuleta mavazi ya kawadia. Kama hautaki kuigiza hadithi yote, acha watoto wajifanye simba wangurumao, na kisha waache wafunge midomo yao kana vile malaika wamefunga vinywa wao.
-
Imbeni au semeni maneno ya “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20) au “We Bow Our Heads” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.25).
-
Acha watoto wachore picha za vitu wanavyoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni wakati wanapoomba. Andika Ninapoomba, naweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya kile kilicho katika kila picha.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Wakumbushe watoto kwamba tunapoomba tunazungumza na Baba wa Mbinguni, ambaye anatupenda na hutusikia. Wasaidie watoto kusema mstari ufuatao:
Nampenda Baba yangu wa Mbinguni.
Mimi humshukuru ninapoomba.
Baba yangu wa Mbinguni ananipenda;
Yeye husikia mambo nisemayo.
-
Wasaidie watoto kusema mmoja au yote kati ya mistari ifuatayo, wakionyesha vitendo sahihi:
Mikono yetu tunakunja, vichwa vyetu tunainamisha.
Macho yetu twayafunga, tu tayari sasa.
Twakunja mikono yetu na twainamisha vichwa vyetu.
Na twasikiliza maombi yatolewapo.
-
Chora mikono ya kila mtoto kwenye kipande cha karatasi kwa kugandamizia mkono. Sema kuhusu kile tunachopaswa kufanya na mikono tunapoomba. Waache watoto wapake rangi michoro ya picha za kugandamiza mikono yao. Andika kila picha jina la mtoto.