Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 34: Mimi Naweza Kuwasamehe Wengine


Somo la 30

Mimi Naweza Kuwasamehe Wengine

Madhumuni

Ni kumhimiza kila mtoto awe mwenye kusamehe.

Maandalizi

  1. Kwa mombi jifunze Mwanzo 37:12–28; 41:38–43; 42:1–8; 45:1–15; Mathayo 18:21–22; na Luka 23:33–34.

  2. Andaa vipande vidogo vya karatasi na uandike kila kipande kauli kama vile moja ya zifuatazo:

    • Mtu fulani amekupiga na kukusukuma chini.

    • Mtu fulani hakuruhusu ucheze mchezo.

    • Mtu fulani amevunja kitu chako.

    • Mtu fulani amekuita jina baya.

    • Mtu fulani amechukua kitu ulichokuwa unachezea na anakataa kucheza na wewe.

    Andaa kipande cha karatasi kwa kila mtoto darasani (tengeneza hali zaidi kama inahitajika). Weka makaratasi katika kijisanduku kilichoandikwa “Sanduku la Msamaha”

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Picha 1-47, Watoto Wakigombana; picha 1-57, Yusufu Anauzwa na Kaka Zake (Sanaa ya Picha za Injili 109; 62525); picha 1-58, Yusufu Akijitambulisha kwa Kaka Zake; picha 1-58,Usulubisho (Sanaa ya Picha za Injili 230; 62505).

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Onyesha picha 1-47, Watoto Wakigombana.

  • Watoto hawa wanafanya nini?

  • Unafikiri wanagombania nini?

  • Unafikiri wanajisikiaje?

  • Watoto hawa wangeweza kuambiana nini ili kumaliza ugomvi na kuwafanya wajisikie vyema zaidi?

Rejea kutoka somo lililopita jinsi ilivyo muhimu kusema “Samahani.” Elezea kwamba baada ya watoto kusema samahani, wanapaswa kusemeheana. Hii humaanisha kwamba hawapaswi kukasirikiana tena na wanapaswa kuwa marafiki. Wakumbushe watoto kuhusu hadithi ya Matt na Travis kutoka somo lililopita. Matt alimsamehe Travis kwa kuchukua wanasesere wake. Walikuwa bado ni marafiki.

Yusufu aliwasamehe kaka zake

Hadithi

Onyesha picha 1-57, Yusufu Anauzwa na Kaka Zake. Simulia hadithi ya Yusufu akiuzwa Msiri, kama inavyopatikana katika Mwanzo 37:12–28.

  • Je, unafikiri Yusufu alijisikiaje wakati kaka zake walipomuuza awe mtumwa Msiri?

Elezea kwamba Yusufu alikuwa mtu mashuhuri huko Msiri (ona Mwanzo 41:38–43). Baada ya miaka mingi, kaka zake Yusufu walikuja Msiri kutafuta chakula kwa sababu hawakuwa na chakula cha kutosha katika nchi yao. Waligundua kuwa Yusufu alikuwa hai na kwamba alikuwa mtu mashuhuri katika Msiri (ona Mwanzo 42:1–8; 45:1–15).

Onyesha picha 1-58, Yusufu Akijitambulisha kwa Kaka Zake.

  • Je, unafikiri Yusufu alijisikiaje kuwa na kaka zake tena? (Ona Mwanzo 45:14–15.)

  • Je, Yusufu aliwakasirikia na kaka zake? (Ona Mwanzo 45:5.)

  • Unafikiri kaka zake Yusufu walijisikiaje kumhusu yeye?

  • Yusufu alionyeshaje kuwa alikuwa amewasamehe kaka zake? (Ona Mwanzo 45:5–15.)

Shughuli

Acha mtoto mmoja ajifanye kuwa Yusufu na wale wengine wajifanye kuwa kaka za Yusufu. Wasaidie watoto kuigiza hadithi ya Yusufu akiungana tena na kaka zake na kuwasamehe.

Yesu alituambia tusamehe

Inua nakala ya Biblia. Elezea kwamba katika Biblia, Yesu alituambia tuwe wenye kusamehe. Mmoja wa mitume wa Yesu alimuuliza kuhusu kusamehe wengine (ona Mathayo 18:21–22). Yesu alimwambia kwamba tunapaswa kusameheana kila mara. Elezea kwamba Biblia pia unatuambia kwamba Yesu alikuwa mwenye kusamehe.

Onyesha picha 1-59, Kusulubiwa. Elezea kwamba askari walikuwa wakatili sana kwa Yesu. Walimpiga na kumtemea mate. Askari walipigilia misumari katika mikono na miguu ya Yesu na kumtundika kwenye msalaba. Elezea kwamba Yesu aliwasamehe askari hao. Yeye hakukasirika na askari kwa yale waliyomfanyia. Kuwa mwangalifu usifanye igizo sana unaposimulia hadithi hii. Baadhi ya watoto wanaweza kuwa wepesi kudhuriwa na wazo la watu kumuumiza Yesu.)

Nenda katika Luka 23:34 na uwaambie watoto kile Yesu alichosema wakati alipoomba kwa Baba wa Mbinguni kabla tu ya kufa: “Baba, wasamehe hawa.” Acha watoto warudie kifungu cha maneno ya mstari huu kwa sauti mara kadhaa.

  • Hata kama askari walimuumiza Yesu, Yeye alifanya nini?

  • Yesu anataka sisi tufanye nini kama mtu anatufanya tukasirike au tukose furaha?

Shughuli

Waombe watoto wafanye kila kitu unachofanya. Acha wakuigize unaposimama, unapojinyosha, unapotabasamu, unapoketi chini, na unapokunja mikono. Elezea kwamba kwa sababu walifanya kila kitu ulichofanya, walikuwa wanakuigiza. Kama unamwigiza mtu, unafanya kitu kile kile anachofanya yule mtu. Tunaposamehe wengine, tunamwiga Yesu. Tunafanya kile ambacho Yeye alifanya. Yesu anataka tuwasamehe wale wanaotufanya tuwe na huzuni au kutukasirisha.

Tunaweza kuwasamehe wengine

Shughuli

Onyesha “Sanduku la Msamaha” na umwalike mtoto mmoja kwa wakati achukue kipande cha karatasi kutoka ndani yake.

Soma kila kauli na uliza maswali kama haya yafuatayo:

  • Haya yameshawahi kutokea kwako?

  • Yangekufanya ujisikie vipi?

  • Je, yule mtu anayekufanya ukose furaha au aliye kukasirisha anapaswa kusema nini kwako?

  • Wewe unapaswa kufanya nini au kusema nini kwa mtu ambaye amekuwa si mkarimu kwako au mtu anayekufanya ukose furaha au kukukasirisha?

Simulia juu ya wakati ambapo wewe ulimsamehe mtu na jinsi ulivyojisikia. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka sisi tuwe wenye kusamehe.

Wimbo

Wasaidie watoto kuimba au kusema maneno “Help Me, Dear Father” (Kitabu cha Nyimbo Watoto, uk. 99).

Nisaidie, Baba mpendwa, nisamehe kwa urahisi.

Wote wanaoweza kuonekana si wakarimu kwangu.

Nisaidie kila siku, Baba, naomba:

Nisaidie niishi karibu, karibu Nawe.

Ushuhuda

Toa ushuhuda kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tusamehe. Wahimize watoto wasali na kumuomba Baba wa Mbinguni ili awasaide kuwasamehe wengine.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Rejea hadithi ya mwana mpotevu, kama inavyopatikana katika Luka 15:11–12. Onyesha picha 1-49, Mwana Mpotevu. Wasaidie watoto kuelewa kwamba baba alimpenda mwanawe na alimsamehe.

  2. Cheza mchezo wa vidole ufuatao. Waalike watoto wafanye vitendo pamoja nawe.

    Marafiki wawili wadogo, mmoja kushoto na mmoja kulia (inua mikono yote kama ngumi imekunjwa),

    Walianza kuzozana na wakaanza kupigana (tishianeni ngumi).

    Sasa hawa marafiki wadogo hawakuwa na furaha siku hiyo.

    Kwani walikuwa wamefundishwa njia sahihi ya kucheza.

    Kisha rafiki mdogo mmoja aliinamisha kichwa kwa aibu (teremsha ngumi na ugeuke);

    Yule mwingine pia, kwani aliona aibu (teremsha ngumi na ugeuke pia).

    Yule rafiki mdogo wa kwanza akasema, “Najua kile nitakachofanya (piga makofi).

    Kukuonyesha kuwa najuta, nitakuomba msamaha.”

    “Mimi pia najuta,” yule mwingine akasema,

    “Acha tucheze na tuwe na furaha siku nzima (kunja mikono na ukae chini).

  3. Tengeneza beji rahisi kwa kila mtoto akavae nyumbani. Andika kila beji Mimi naweza kusamehe.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Rejea hadithi kutoka somo la 29 kuhusu watoto wawili wakicheza (ona Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo, shughuli ya 4). Elezea jinsi mtoto aliyeumizwa alivyomsamehe yule mwingine.

  2. Imbeni au semeni maneno “Jesus Said Love Everyone” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 61, au ”Jesus Wants Me for a Sunbeam” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 60).

  3. Imbeni au semeni maneno ya “If You’re Happy” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 266). Waeleze watoto kwamba tunaposamehe wale wasio wakarimu kwetu, tutajisikia furaha.