Somo la 14
Adamu na Hawa Waliumbwa katika Mfano wa Baba wa Mbinguni
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuelewa kwamba Adamu na Hawa waliumbwa katika mfano wa Baba wa Mbinguni.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Mwanzo 1; 2:15–25; na 3. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 5 na 6.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia.
-
Mikato 1-1 hadi 1-25 (mikato inayofanana na hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha vya Msingi seti ya 3, 4, na 5).
-
Picha 1-33, Adamu na Hawa (Picha za Sanaa za Injili 101; 62461); picha 1-34, Adamu na Hawa Wakifundisha Watoto Wao.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Dunia iliumbwa kulingana na mpango wa Baba wa Mbinguni
Adamu na Hawa walikuwa sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni
Acha watoto watazame maumbo ya mikato uliyoyabandika.
-
Ni kitu gani kingine kinachohitajika kuwa duniani?
Onyesha picha 1-33, Adamu na Hawa. Elezea kwamba baada ya vitu vingine kuumbwa, ndipo Adamu na Hawa waliumbwa. Simulia hadithi ya uumbaji wa watu, kama inavyopatikana katika Kutoka 1:26–28. Elezea kwamba Adamu na Hawa walikuwa watu wawili wa kwanza kuishi duniani. Walikuwa na miili ya nyama na mifupa ambayo ilifanana na mwili wa Baba wa Mbinguni.
-
Ni nani alikuwa mwanaume wa kwanza kuumbwa hapa duniani?
-
Ni nani aliyekuwa mwanamke wa kwanza?
-
Adamu na Hawa walikuwa na miili ya aina gani?
Acha watoto waguse mikono yao, na uwakumbushe kwamba miili yao inafanana na miili ya Adamu na Hawa.
Baba wa Mbinguni na Yesu Walisema dunia ilikuwa mzuri
Soma sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:31 kwa sauti. Acha watoto warudie sentensi hii pamoja na wewe. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka tuvione viumbe vyote kuwa ni vizuri. Cha muhimu sana, wao wanatuona sisi ni wazuri, na wanampenda sana kila mmoja wetu.
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Chagua shughuli kadhaa kutoka somo la 8 hadi 13 kama vile “Uumbaji wa Mungu,” au “Nuhu,” ili uzifanye pamoja na watoto.
-
Rejea kile kilichotendeka kila siku ya Uumbaji wakati watoto wakihesabu siku kwa vidole vyao.
-
Imba au sema maneno ya “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto , 228) pamoja na watoto.
-
Acha watoto wachore au wapake rangi picha ya kitu ambacho ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni, kama vile ua, mti, au jua. Andika juu ya karatasi ya kila mtoto Mimi nashukuru kwa ajili ya dunia.
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Imbeni au semeni maneno ya “The World Is So Big” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 235). Wasaidie watoto kufanya vitendo vilivyoandikwa hapo chini:.
Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),
Na ndani yake viumbe vya Mungu hupatikana;
Milima (weka kwa umbo la mlima juu ya kichwa)
Mabonde (weka viganja mbele ya mwili)
Na miti mirefu (nyoosha mikono kwa urefu)
Wanyama wakubwa (ishara ya ukubwa)
Na wanyama wadogo (ishara ya udogo)
Nyota zing’aazo usiku kucha (nyosha na uchezeshe vidole),
Jua mchana lina joto na linaangaza sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),
Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana.
Mungu anatupenda sisi wote; baraka zetu ni nyingi (kunja mikono na ujikumbatie).
-
Wasaidie watoto kufanya vitendo kwa mstari wa shughuli ufuatao huku ukisema maneno:
Uumbaji wa Mungu
Mungu aliumba mwezi (fanya duara kwa mikono).
Na nyota za kumetameta (fungua na ufunge mikono)
Na aliziweke hewani (fikia juu)
Aliumba jua (tengeneza duara kubwa juu ya kichwa)
Na miti (nyoosha mikono kwa urefu)
Na maua (weka mikono kama bakuli)
Na ndege wadogo ambao huruka (punga mikono).
(Kutoka Fascinating Finger Fun na Eleanor Doan. © 1951. Imetumika kwa Idhini.)