Somo la 20
Ninashukuru Kwamba Ninaweza Kunusa na Kuonja
Madhumuni
Ni kumsaidia kila mtoto kuthamini hisi za kunusa na kuonja.
Maandalizi
-
Kwa maombi jifunze Kutoka 16:11–15,31 na Mafundisho na Maagano 59:18-19.
-
Vifaa vinavyohitajika:
-
Biblia na nakala ya Mafundisho na Maagano.
-
Sampuli moja ndogo kwa ajili ya kila mtoto ya chakula kinachonukia vizuri (kama vile tunda, mkate, biskuti, au bisi). Weka sampuli kwenye mfuko. Zungumza na wazazi wa watoto ili kuhakikisha hakuna mtoto yoyote anaweza kudhurika na chakula unacholeta.
-
Sampuli za kitu kichachu kama vile (jusi ya limau), chenye chumvi (kama vile chumvi) na tamu (kama vile sukari) kwa ajili ya watoto kuonja. Zungumza na wazazi wa watoto ili kuhakikisha hakuna mtoto yoyote anaweza kudhurika na chakula unacholeta.
-
Onyesha picha 1-35, Kukusanya Mana.
-
-
Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.
Taarifa kwa mwalimu: Kuwa mwangalifu kwa hisia za watoto wo wote katika darasa lako ambao wana ulemavu wa kimwili. Zingatia mambo ambayo miili yao inaweza kufanya, siyo ulemavu wao.
Shughuli za Kujifunza
Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.
Kila mmoja wetu ana pua kwa hiyo tunaweza kunusa
-
Tunawezaje kunusa vitu?
Jadili pamoja na watoto baadhi ya vitu ambavyo wamevinusa katika wiki, kama vile chakula kikipikwa, hewa safi baada ya mvua au maua. Waambie watoto kwamba tunapaswa kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya hisi zetu za kunusa.
-
Unapenda kunusa vitu gani?
Kila mmoja wetu ana ulimi wa kuonja
Eleza kwamba Baba wa Mbinguni amembariki kila mmoja wetu kuwa na ulimi ili tuweze kuonja. Acha watoto waonje vitu chachu, vya chumvi, na vitamu kama wanataka.
-
Ni kipi kilicho chachu?
-
Ni kipi kilicho chumvi?
-
Ni kipi kilicho kitamu?
-
Unapendelea kuonja kitu gani?
Onyesha nakala ya Mafundisho na Maagano (au ukurasa wa jina wa Mafundisho na Maagano katika vitabu vitatu vya maandiko). Elezea kwamba sisi tunaambiwa katika kitabu hiki cha maandiko kwamba vitu vinavyonukia na kuonja ambavyo ni vizuri tunaweza kuvitumia na kuvifurahia (ona M&M 59:18–19).
Shughuli za Kuboresha
Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.
-
Lete vitu vingi ambavyo vina harufu ya kuvutia sana, kama vile sabuni, maua, limau, na baadhi ya vitu visivyo na harufu, kama vile kipande cha karatasi na mwanasesere. Acha watoto wachukue vitu ambavyo wanaweza kunusa. Acha mtoto mmoja kwa wakati afunge macho yake na kunusa mojawapo ya vitu hivi, na abahatishe ni nini? Acha kila mtoto apate zamu moja.
-
Acha watoto watazame ndimi zao kwenye kioo. Elezea kwamba ndimi zetu zina seli za kuonja ambazo hutusaidia kuonja vitu ambavyo ni vitamu, chachu, na vyenye chumvi. Acha watoto waonje maji. Elezea kwamba ndimi zetu pia zinatusaidia kujua kama kitu ni maji maji au baridi.
-
Acha mtoto achore picha ya chakula akipendacho. Acha watoto waonyeshe picha zao na kusema chakula wakipendacho ni kipi.
-
Weka kiasi kidogo cha vitu ambavyo vinafanana lakini vinaonja tofauti, kama vile chumvi na sukari au unga na wanga. Mpe kila mtoto kionjo kidogo cha kila kitu. Kisha waulize watoto jinsi kila kitu kinavyoonja. Jadili baadhi ya vitu jinsi vinavyofanana lakini vinaonja tofauti. Zungumza na wazazi wa watoto ili kuhakikisha hakuna mtoto yo yote anayeweza kudhurika na chakula unacholeta.
-
Imba “A Song of Thanks” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 20) au “For Health and Strength” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk.21).
Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo
-
Chora umbo la yai ubaoni ama kwenye kipande cha karatasi. Elezea kwamba hili umbo la yai ni picha ya uso.
-
Ni nini kinachokosekana?
Wakati watoto wanapotaja majina ya macho, masikio, pua, mdomo, chora kwenye picha. Kisha rejea kile kila kitu hufanya. Elezea jinsi ulivyo na shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya mwili wako.
-
-
Onyesha mdomo wako na useme, “Huu ni mdomo wangu.” Kisha uliza “Unaweza kunionyesha mdomo wako?” na wasaidie watoto kuonyesha midomo yao. Rudia macho, pua, masikio, mikono, na miguu. Kisha onyesha kila sehemu ya mwili bila kusema jina lake na uwaache watoto waitaje. Ikiwa watoto wanaweza kutaja sehemu hizi zote, unaweza pia kuwauliza majina ya sehemu za mwili zisizojulikana sana na watoto, kama vile viwiko, magoti, vifundo na visigino.
-
Wasaidie watoto kusimama na kusema mstari ufuatao, wakitumia vitendo kama inavyoonyeshwa na maneno haya:
Gusa Macho Yako
Gusa macho yako,
Gusa pua lako,
Gusa masikio yako,
Gusa vidole vyako,
Nyosha mikono yako,
Juu juu sana,
Hata juu sana,
Kuelekea angani,
Weka mikono yako,
Kwenye nywele zako;
Keti chini kimya kimya,
Juu ya kiti chako.