Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Ninashukuru kwa ajili ya Ndege na Wadudu


Somo la 13

Ninashukuru kwa ajili ya Ndege na Wadudu

Madhumuni

Ni kumsaidia kila mtoto kuwa na shukrani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu kwa ajili ya ndege, wadudu, na viumbe vitambaavyo.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Mwanzo 1:20–25 na 1 Wafalme 16:29–17:6.

  2. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia.

    2. Kama inawezekana, tafuta picha za ndege, wadudu, na viumbe vitambaavyo vilivyo vya kawaidia katika eneo lenu.

    3. Mikato 1-20 hadi 1-25, ndege na wadudu (mikato inayofanana na hiyo pia inaweza kupatikana katika Mikato ya Vielelezo vya Picha za Watoto wa Msingi seti ya 4, na 5).

    4. Picha 1-31, Eliya Akilishwa na Kunguru; picha 1-32, Muujiza wa Shakwe wa Baharini (Picha za Sanaa za Injili 413; 62603).

  3. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Wape watoto vidokezo vifuatavyo na waache watoto wabahatishe jibu la swali “Mimi ni Nini?

  1. Mimi nina mdomo wenye ncha.

  2. Mini nina manyoya.

  3. Mimi nina mabawa.

  4. Mimi hupaa angani.

Watoto wanaposema “ndege,” acha wakufuatishe na kujifanya ndege wanapaa chumbani. Waongoze kurudi kwenye viti vyao.

Baba wa Mbinguni alimwomba Yesu Kristo awaumbe ndege

Elezea kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu kuumba ndege kwa ajili yetu na kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi. Onyesha Biblia na uwaambie watoto kwamba Biblia inatuambia kuhusu uumbaji wa ndege (ona Mwanzo 1:20–23).

Elezea kwamba aina tofauti za ndege huishi kote ulimwenguni. Onyesha picha za ndege ulizopata na maumbo ya mikato ya ndege, moja baada ya nyingine.

  • Je, huyu ni ndege?

  • Unawezaje kutambua? (Ana mabawa, manyoya, na mdomo wenye ncha.)

Acha watoto wazungumze kuhusu uzoefu wowote waliopata juu ya ndege.

Ndege wanaweza kutusaidia

Hadithi

Onyesha picha 1-31, Eliya Akilishwa na Kunguru, na usimulie hadithi ya kunguru wakimlisha Eliya nabii, kama inavyopatikana katika 1 Wafalme 17:1–6. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wana nguvu juu ya kila kitu, hata ndege. Yesu aliwaambia ndege wamtunze Eliya wakati alipoikuwa amejificha kutoka kwa mfalme Ahabu mwovu.

  • Je, kunguru walijuaje jinsi ya kumletea Eliya chakula? (Ona 1 Wafalme 17:4.)

  • Kunguru walileta chakula aina gani? (Mkate na nyama; ona 1 Wafalme 17:6.)

Shughuli

Chagua mtoto awe Eliya. Acha watoto wengine wajifanye kwamba wao ni kunguru wanaoleta chakula asubuhi na tena jioni.

Hadithi

Simulia hadithi ya shakwe wa baharini na nyenje kwa maneno yako mwenyewe:

Wakati watangulizi walipowasili katika Bonde la Salt Lake, walipanda ngano na nafaka zingine. Walikuwa wanahitaji nafaka kutengeneza mkate na mlo wa nafaka. Ngano ilikua kubwa na ndefu. Punde tu kabla ya wakati wa kuvuna ngano, wingu kubwa lilitanda angani. Halikuwa wingu la mvua, bali lilikuwa wingu la maelfu ya nyenje weusi wenye njaa. Nyenje walivamia ngano na kuanza kuila.

Watangulizi walifanya kila kitu walichoeweza ili kuwazuia nyenje kula ngano yao. Walitengeneza moto, wakapiga nyenje kwa fagio na mablangeti, na hata wakajaribu kuwamwagia nyenje maji. Lakini nyenje hawakukoma. Watangulizi walikuwa na hofu kwamba hawangekuwa na chakula msimu wa baridi. Walipiga magoti na kusali na wakamwomba Baba wa Mbinguni msaada.

Punde makundi mengi ya shakwe wa baharini wakaja na kuanza kuwala wale nyenje. (Onyesha picha 1-32, Muijiza wa Shakwe wa Baharini.) Muda mfupi, wengi wa nyenje walikuwa wameisha. Watangulizi walimshukuru Baba wa Mbinguni kwa kuwatuma shakwe wa baharini na kuokoa mavuno yao (ona William E. Berrett, The Restored Church [Salt Lake City: Deseret Book Co., 1961], pp. 283–85).

  • Je, shakwe wa baharini waliwasaidiaje watangulizi?

Baba wa Mbinguni alimuomba Yesu Kristo aumbe wadudu na viumbe vinavyotambaa

Waambie watoto kwamba pia Yesu Kristo iliumba wadudu na viumbe vinavyotambaa kama vile buibui na nyoka. Viumbe hawa walikuwa sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni.

Shughuli

Acha watoto wabahatishe wadudu na viumbe vinavyotambaa vinaoelezewa katika vitendawili vifuatavyo. Kila kitendawili kinapofumbuliwa, onyesha na zungumzia umbo la mkato husika.

  1. Mimi ni wa njano na huvuma.

    Tumbo langu limefunikwa na sufi.

    Mimi hutengeneza asali kwa ajili yangu na yako.

    Mimi ni asali. . (Nyuki; hutoa sauti ya kuvuma.)

  2. Mimi hufuma utando wa kunasa chakula.

    Nina miguu minane kama inavyonifaa.

    Watu hawanimpendi.

    Unaweza kubahatisha mimi ni nani? (Buibui; tembeza vidole kama miguu.)

  3. Siku moja nilikuwa kiwavi.

    Mimi hupaa angani.

    Nina mabawa maridadi.

    Mimi ni . (Kipepeo; tembeza vidole pole pole kama mabawa.)

  • Unajua nini kuhusu viumbe hawa?

Elezea kwamba wadudu waliumbwa kwa ajili ya sababu nyingi. Baadhi ya wadudu wanaweza kuliwa

na ndege, wanyama, na wadudu wengine; baadhi huwa mandhari maridadi na hutoa sauti za kupendeza. Nyuki hutengeneza asali kwa ajili yetu kula, na husaidia matunda na maua na mboga kukua.

Shughuli

Onyesha mkato wa nyuki na picha zo zote za nyuki au mzinga ambazo umepata. Elezea jinsi nyuki hukusanya nekta kutoka kwenye maua kuitumia katika kutengeneza asali, na kisha acha watoto wajifanye kuwa nyuki wakienda kutoka ua hadi ua ili kupata nekta ya kutengeneza asali.

  • Je, ni wadudu gani wewe unawapenda? Kwa nini?

Onyesha picha za wadudu ulizopata. Elezea kwamba wadudu wengi hutusumbua. Wao hula chakula chetu na wanaweza kung’ata au kutuuma. Wakumbushe watoto kuhusu hadithi ya shakwe wa baharini na nyenje. Nyenje walikuwa wanakula chakula chote cha watangulizi.

Elezea kwamba kwa kawaida wakati wadudu wanapotuumiza au kutusumbua, wao hujaribu tu kujikinga wenyewe.

Ushuhuda

Wakumbushe watoto ndege, wadudu, na viumbe vitambaavyo ni sehemu muhimu ya dunia yetu. Elezea hisia zako za shukrani kwa ajili ya viumbe hawa.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Cheza mchezo wa kipepeo. Acha watoto waketi katika duara. Chagua mtoto mmoja awe kipepeo. Mtoto huyu naye apunge kipepeo wa karatasi juu vichwa vya watoto wengine huku akitembea nje ya duara. Mtoto anapotembea nje ya duara, kariri mstari huu:

    Kipepeo mmoja mdogo aliruka

    Siku angavu sana, ya msimu wa joto.

    Alipaa juu kwenye anga ya samawati,

    Na alipotua, alitua juu yako!

    Anaposema, “Alitua juu yako,” mtoto yule ambaye ni kipepeo anaweka kipepeo wa karatasi kwenye paja la mtoto mwingine. Mtoto huyo sasa ndiye kipepeo. Rudia mstari huu mpaka kila mtoto apate zamu ya kuwa kipepeo.

  2. Elezea kwa maneno rahisi namna ambavyo kiwavi huwa kipepeo. Waache watoto wajifanye kuwa wao ni viwavi wanaosokota vifukofuko. Waache waketi chini kwenye viti vyao au kwenye sakafu na kukunja mikono yao karibu na miguu yao, wajifanye wanalala. Waambie wao kwamba wakati kiwavi kinabadilika kuwa kipepeo, mabawa yake hufanya kazi na kunyooka. Acha watoto wanyooshe mikono yao. Waambie watoto kwamba vipepeo ni watulivu sana, hata wakati wakiwa kwenye mwendo. Acha watoto wasimame na kujifanya wao wanaruka kimya kimya chumbani.

  3. Pamoja na watoto Imbeni au semeni maneno ya “In the Treetops” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 240) au “The World is So Big” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 235). Tumia vitendo vilivyo hapo chini “Dunia ni Kubwa Sana”:

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Na ndani yake viumbe vya Mungu hupatikana;

    Milima (weka kwa umbo la mlima juu ya kichwa)

    Mabonde (weka viganja mbele ya mwili)

    Na miti mirefu (nyoosha mikono kwa urefu)

    Wanyama wakubwa (ishara ya ukubwa)

    Na wanyama wadogo (ishara ya udogo)

    Dunia ni kubwa sana, ee, duara sana (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Mungu anatupenda sisi wote; baraka zetu ni nyingi (kunja mikono na ujikumbatie).

  4. Imbeni au mseme maneno ya “All Things Bright and Beautiful” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 231) mkitumia vitendo vinavyoelezewa hapo chini.

    Vitu vyote angavu na maridadi (tengenezeni duara kubwa kwa mikono),

    Viumbe wote wakubwa na wadogo (tanua mikono sana, kisha ilete pamoja),

    Vitu vyote wenye hekima na vya ajabu (ota kidole kwenye kichwa),

    Bwana Mungu aliviumba vyote (kunja mikono kana vile unasali).

    Kila ua dogo ambalo huchanuka (kunja mgumi, kisha ifungue),

    Kila ndege mdogo ambaye huimba (lete vidole na gumbu pamoja mfano wa mdomo wa ndege),

    Yeye alifanya rangi zao zing’aazo (fanya mikono kama umbo la upinde wa mvua);

    Yeye alitengeneza vijibawa vyao (fanya mikono kama mabawa).

  5. Lete kombe la asali ili watoto waone na kuonja. (Zungumza na wazazi wa watoto kuhakikisha hakuna mtoto anayedhuriwa na asali.)

  6. Wasaidie watoto kufanya mchezo ufuatao mmoja au yote ya vidole:

    Ndege Wawili Wadogo Wenye Mtwito

    Ndege wawili wadogo waliketi ukutani (weka kidole kwenye kila bega),

    Mmoja jina lake Petro (inua kidole kushoto)

    Na mmoja jina lake Paulo (inua kidole cha kulia).

    Ruka, Petro (weka kidole cha kushoto nyuma);

    Ruka, Paulo (weka kidole cha kulia nyuma).

    Rudi, Petro (weka kidole cha kushoto kwenye bega tena);

    Rudi, Paulo (Weka kidole cha kulia kwenye bega tena).

    Mzinga

    Hapa kuna mzinga (kunja kiganja cha kushoto kuelekea chini)

    Nyuki wako wapi?

    Wamejificha mbali sana hakuna wa kuwaona (ficha vidole vya kiganja cha kulia chini ya kiganja cha kushoto).

    Punde wakatoka wakiruka kutoka kwenye mzinga (lete mkono wa kulia nje na inue kidole kimoja kwa wakati watoto wakihesabu).

    Moja, mbili, tatu, nne, tano! BZZZ!

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Chora picha rahisi, umbo la mkato, au mchoro wa ndege. Waambie watoto kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo kuumba ndege (ona Mwanzo 1:20–23). Elezea shukrani zako kwa ajili ya ndege.

  2. Elezea kwamba ndege wana mdomo maalum ili kuwasaidia kudonadona chakula chao. Acha watoto waweke mikono yao kwenye midomo yao kama vile mdomo wa ndege na kujifanya kudonadona chakula. Elezea kwamba ndege pia wana mabawa ya kuwasaidia kuruka. Acha watoto wapunge mikono yao na kujifanya wanaruka.

  3. Imbeni au mseme maneno ya “Birds in the Tree” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 241), mkitumia vitendo vinavyoelezwa hapa chini:

    Tutapata kiota kidogo (kunja mikono)

    Katika matawi ya mti (inua mikono juu ya kichwa)

    Acha tuhesabu mayai hapa ndani.

    Kuna moja, mbili, tatu (nyosha vidole, moja, mili, na tatu).

    Mama ndege hukalia kiota (kunja mkono wa kushoto, weka mkono wa kulia juu).

    Kuangua mayai, yote matatu (inua vidole vitatu juu).

    Baba ndege hupaa kuzunguka, zunguka (fanya mikono kama vile mwendo wa kupaa),

    Kulinda familia yake.

  4. Wasaidie watoto kufanya mchezo wa vidole ufuatao:

    Eense, Weense, Buibui

    Eense, weense, buibui alienda kwenye tumba la maji (tumia vidole viwili vya mkono mmoja “kupanda” ule mkono mwingine).

    Mvua ikanyesha na kumfagilia buibui nje (inua mkono mmoja juu ya kichwa, kisha uteremshe ukichezesha chezesha vidole).

    Jua likachomoza na kukausha mvua yote (fanya duara juu ya kichwa ukitumia mikono).

    Eense, weense, buibui alienda kwenye tumba tena (rudia vitendo vya mstari wa kwanza).