Miitaala kwa ajili ya Msingi na Wakati wa Kushiriki
Somo la 37: Naweza kuwa Mwaminifu


Somo la 37

Naweza kuwa Mwaminifu

Madhumuni

Ni kuimarisha hamu ya kila mtoto ya kuwa mwaminifu.

Maandalizi

  1. Kwa maombi jifunze Kutoka 20:15–16; Alma 53:16–22; 56:44–57; na Makala ya Imani 1:13. Ona pia Kanuni za Injili (31110), sura ya 31.

  2. Tengeneza utepe wa kichwa kwa kila mtoto kutokana na upapi wa karatasi au kitambaa. Andika kila utepe wa kichwa Naweza kuwa mwaminifu.

  3. Vifaa vinavyohitajika:

    1. Biblia na Kitabu cha Mormoni

    2. Kifungo au kitu kingine kidogo.

    3. Picha 1-13, Joseph Smith (Picha za Sanaa za Injili 400; 62449); picha 1-65, Askari Vijana Elfu Mbili (Picha za Sanaa za Injili 313; 62050);

  4. Fanya maandalizi yanayohitajika kwa Shughuli zo zote za Kuboresha unazotaka kutumia.

Shughuli za Kujifunza

Mwalike mtoto atoe maombi ya kufungua.

Shughuli ya Usikivu

Alika mwanafunzi kuja mbele ya darasa. Gandamiza mikono yako pamoja ukiwa na kifungo au kitu kingine kidogo ndani yake. Acha watoto wengine wagandamize mikono yao pamoja. Nenda kutoka mtoto mmoja hado mwingine, ukipitisha mikono yako katikati ya mikono yao. Angusha kifungo katika mikono ya mtoto mmoja. Acha watoto waendelee kugandamiza mikono pamoja, wakijifanya wana kile kifungo. Sema, “Kifungo, kifungo, nani ana kifungo?” Acha mtoto aliye mbele ajaribu kubahatisha ni mtoto gani aliye na kifungo kwa kuuliza “(Jina), wewe una kifungo?” Waambie watoto kwamba wanapaswa kujibu kwa uaminifu, “La, sina kifungo” au “Ndio, nina kifungo.”

Cheza mchezo huu mara kadhaa, ukichagua watoto wengine kubahatisha na kupitisha kifungo. Wapongeze watoto kwa kuwa waaminifu.

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuwe waaminifu

Onyesha picha 1-13, Joseph Smith. Waambie watoto kwamba Nabii Joseph Smith aliandika, “Tunaamini katika kuwa waaminifu” katika makala ya Imani ya kumi na tatu. Wasaidie watoto kukariri maneno haya.

  • Inamaanisha nini kuwa mwaminifu?

Elezea kwamba kuwa mwaminifu inajumuisha kusema ukweli, kutochukua vitu vya mtu mwingine, kuwatendea watu wengine haki.

Onyesha Biblia na uwaambie watoto kwamba Musa aliwaletea watu wake Amri Kumi (ona Kutoka 20). Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu walimpa Musa amri mbili juu ya uaminifu: “Usiibe na Usishuhudie uongo.” Soma Kutoka 20:15–16 kwa sauti.

  • Kuiba humaanisha nini?

Elezea kwamba kushuhudia uongo humaanisha kusema kitu ambacho si cha kweli.

Wimbo

Imbeni au semeni maneno ya “I Believe in Being Honest” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto uk. 149).

Naamini katika kuwa mwaminifu;

Naamini katika kuwa mkweli,

Uaminifu huanza na mimi.

Katika vitu vyote ninavyosema, katika vitu vyote ninavyofanya.

Shughuli

Elezea a vitendo fulani kwa watoto. Acha watoto wasimame endapo kitendo ni cha uaminifu na kuketi chini wakati ni kitendo kisicho cha uaminifu. Tumia mifano ifuatayo au ubuni yako mwenyewe.

  • Kuchukua kitafunwa kama mama yako hajakuruhusu kufanya hivyo.

  • Kusema ukweli kuhusu kile unachofanya

  • Kuchukua kitu ambacho si chako.

  • Kukiri umefanya makosa.

  • Kusema mtu fulani amefanya kitu fulani hali kwa kweli hajafanya.

  • Kuokota hela au kitu fulani ambacho ni cha mtu mwingine na kumpa mwenyewe.

Waulize watoto washiriki uzoefu wa wakati ambapo wamekuwa waaminifu.

  • Unahisi vipi unapokuwa mwaninifu?

  • Unahisi vipi unapokuwa si mwaminifu?

  • Kwa nini wakati mwingine unaweza kuwa na uoga kuwa mwaminifu? (Unaweza kuadhibiwa au kumfanya mtu fulani asiwe na furaha.)

Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunaweza kujisikia vyema tunapokuwa waaminifu, hata ingawa wakati mwingine ni vigumu kufanya hivyo.

Tunabarikiwa tunapokuwa waaminifu

Hadithi

Onyesha picha 1-55, Askari Vijana Elfu Mbili. Simulia hadithi ya askari vijana elfu mbili, kama inavyopatikana katika Alma 53:16–22 na Alma 56:44–57, hasa Alma 53:20–21. Elezea kwamba sababu moja ya hawa wavulana kuwa bora sana ni kwamba walikuwa waaminifu. Soma kwa sauti sehemu ya mwisho ya Alma 53:20 (kutoka walikuwa wanaume wakweli). Elezea kwamba kuwa mkweli humaanisha kuwa mwaminifu. Kwa sababu hawa askari vijana walikuwa waaminifu, walilindwa vitani. Walibarikiwa kwa sababu ya uaminifu wao, imani na ujasiri. Sisi pia tutabarikiwa kama tutakuwa waaminifu.

  • Je, ni kwa namna gani askari hawa vijana elfu mbili walibarikiwa kwa sababu ya kuwa waaminifu? (Ona Alma 56:54–56.)

Shughuli

Wavishe watoto utepe wa kichwa. Acha wao wajifanye wao ni askari vijana elfu mbili na watembee chumbani huku ukipiga makofi kwa mpigo mmoja. Acha waache kutembea unapositisha kupiga makofi, na umuulize mtoto aelezee jinsi anavyoweza kuwa mwaminifu. Anza tena kupiga makofi, na urudie shughuli hii mpaka kila mtoto apate zamu ya kujibu swali.

Ushuhuda

Toa ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanatutaka sisi tuwe waaminifu na kwamba tunaweza kuwa na furaha tunapokuwa waaminifu.

Shughuli za Kuboresha

Chagua baadhi ya shughuli hizi ili uzitumie katika somo.

  1. Simulia hadithi ifuatayo ya Jacob Hamblin na mwanawe katika maneno yako mwenyewe:

    Jacob Hamblin alikuwa mmoja wa watangulizi wa kwanza kwenda Utah kusini. Aliwapenda Wahindi walioishi huko na alijifundisha kuongea lugha yao. Yeye alikuwa mwaminifu kwa Wahindi, nao wakajifunza kumwamini yeye. Siku moja Jacob alimtuma mwanawe kubadilishana mwana farasi na mablangeti kadhaa ya Kihindi. Mhindi alimtazama kwa makini mwana farasi na akaweka rundo la mablangeti. Mwanawe Jacob alisema, “Hayajatosha.” Mhindi aliendelea kuongeza mablangeti kwenye rundo lile. Wakati mwanawe Jacob alipofikiria kuwa amepata ya kutosha, akarudi nyumbani, akijivuna kwamba amepokea mablangeti mengi sana kwa mwana farasi. Wakati Jacob alipoona mablangeti yalivyokuwa mengi ambayo mwanawe ameleta nyumbani, hakufurahia. Mwana farasi hakuwa na thamani ya mablangeti mengi hivyo. Jacob alimwambia mwanawe arudishe nusu ya mablangeti kwa Mhindi. Wakati mvulana aliporudisha, Mhindi alicheka na kusema “Mimi nilijua kwamba Jacob atayarudisha” (ona Jacob Hamblin Jr., kama ilivyosimuliwa kwa Lousie Lee Udall, katika A Story to Tell [Salt Lake City: Deseret Book Co., 1945], 359–60).

    Elezea kwamba Mhindi alijua kwamba Jacob Hamblin alikuwa mtu mwaminifu na angeyarejesha mablangeti hayo yaliyozidi. Mhindi aliweza kumwamini Jacob kwa sababu siku zote yeye alikuwa mwaminifu. Acha watoto waigize au wasimulie tena hadithi hii.

  2. Imbeni ua mseme maneno ya “Jesus Loved the Little Children” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk. 59) au “Jesus Once Was a Little Child” (Kitabu cha Nyimbo cha Watoto, uk.55).

  3. Tumia vikaragosi, kama vile vikaragosi vya soksi au mifuko ya karatasi, muigize hali ambapo mtu anakuwa na nafasi ya kuchagua kuwa mwaminifu au kutokuwa mwaminifu. Tumia mifano ifuatayo au ubuni yako mwenyewe.

    • Umevunja sahani na mama yako anauliza ni nani aliyefanya hivyo.

    • Unasaidia kuokota hela zilizomwagika na kutawanyika chini, na wewe unajaribu kutwaa zingine.

    • Umekula biskuti mbili baada ya baba yako kukwambia usifanye hivyo. Baba yako anakuuliza kama ulikula biskuti hizo.

    Acha watoto wachukue zamu kutumia vikaragosi na kusema kile wanapaswa kufanya katika kila hali.

Shughuli za Ziada Kwa Watoto Wadogo

  1. Waulize watoto kama kulikuwa na farasi chumbani. Waambie kwamba hata wakitafuta kwa makini vipi, hawatampata farasi chumbani kwa sababu hakuwepo hata mmoja. Ingekuwa si uaminifu kusema kwamba kulikuwa na farasi chumbani. Waulize kama wanaweza kuona. (taja kitu ambacho watoto wanaweza kuona kwa urahisi). Elezea kwamba wanaweza kuwa waaminifu kwa kusema kitu hicho kiko humo chumbani. Waambie watoto kwamba wanaposema kuwa kitu ni kweli au halisi, wanakuwa waaminifu.

  2. Waombe watoto wanyoshe mikono yote unaposema kitu ambacho ni cha kweli na washushe mikono yote unaposema kitu ambacho si cha kweli. Tengeneza sentensi rahisi lakini za wazi, kama vile “mimi nina maua kwenye nywele zangu,” “mimi nimevaa gauni,” suruali ya John ni nyekundu,” au “wewe umekaa kwenye kiti.”

  3. Imbeni au mseme maneno ya “Sala” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 22, au ”Dare to Do Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, uk. 158).