Kitengo 2: Siku 1
1 Nefi 1
Utangulizi
Kitabu cha Mormoni kinaanza na masimulizi ya Nefi ya baba yake, Lehi, akitimiza kwa uaminifu kazi yake kama nabii na kama kiongozi wa ukuhani wa familia yake. Kuelewa huduma ya Lehi, kunaweza kukusaidia kuelewa vyema kazi za manabii katika siku zetu. Alikuwa mmoja wa “manabii wengi, wakitoa unabii kwa [Wayahudi] kwamba lazima watubu” (1 Nefi 1:4). Kwa sababu Lehi alikuwa mtiifu kwa Mungu na kutoa unabii kuhusu maangamizo ya Yerusalemu, watu walimkejeli na wakataka kumuua. Hata hivyo, Lehi alifurahia katika huruma na nguvu za ukombozi. Unapojifunza 1 Nefi 1, fikiria jinsi huruma ya Mungu na ushiriki wako umeonyeshwa katika maisha yako.
1 Nefi 1:1–3
Nefi anaanza kumbukumbu yake
Soma 1 Nefi 1:1, na hutambue maneno muhimu na misemo inayotambua jinsi maisha ya Nefi yalivyokuwa.
-
Kutoka kwa yale uliyosoma katika mstari 1, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu aghalau njia moja ambayo unahisi maisha yako yanafanana na maisha ya Nefi.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Unafikiri ni vipi Nefi angeweza “kuona masumbuko mengi” na bado “kubarikiwa na Bwana maishani [mwake]”?
1 Nefi 1:4–20
Lehi alipokea ono na anawaonya watu kwamba Yerusalemu itaangamizwa.
Fikiria juu ya wakati ambapo wazazi wako au viongozi wa Kanisa walipokuonya kuhusu kitu hatari. Nia yao ya kukuonya ilikuwa ni nini?
Baba yetu wa Mbinguni anatupenda na anataka tuwe salama kutokana na dhambi, ambayo inatudhuru. Mojawapo wa njia ambayo Mungu anawaonya watoto Wake ni kupitia manabii. Manabii wanaonya dhidi ya dhambi na wanafundisha wokovu kupitia kwa Yesu Kristo. Unapojifunza 1 Nefi 1, tafuta ushahidi wa kanuni hii. Nefi alianza kumbukumbu yake kwa kutuambia kwamba manabii wengi walihubiri na kuonya watu juu ya kile kitakachotokea ikiwa hawatatubu (ona 1 Nefi 1:4). Soma 1 Nefi 1:5–7, na uweke alama maandiko yako jinsi Lehi alivyoomba na kitu alichoomba. Maombi ya Lehi kwa Bwana huonyesha kwamba aliamini kile manabii walikuwa wakisema.
Soma 1 Nefi 1:8–10, na uweke mviringo kwa yote ambayo Lehi aliona katika ono.
-
Mungu
-
Yesu Kristo
-
Malaika
-
Wengine Kumi na Wawili
Soma 1 Nefi 1:11–12, na uone kile kilichomtokea Lehi aliposoma kitabu alichopewa. Kupitia ono hili Bwana aliendelea kumtayarisha Lehi kuhudumu miongoni mwa watu wa Yerusalemu. Soma1 Nefi 1:13, na utambue kile Lehi alifundisha kuhusu Yerusalemu. Unaposoma, jiweke katika mahali pa Lehi na ufikirie jinsi unavyoweza kuhisi ikiwa Bwana amekuambia kuwa mambo haya yangefanyika nyumbani kwako na mji wako.
Kwa kuonywa juu ya maangamizo ya watu wake na mji ama kweli ingekuwa vigumu sana kwa Lehi. Bado, soma1 Nefi 1:14–15, na utambue kwa nini Lehi alifurahia ingawa aliona kwamba Yerusalemu ingeharibiwa.
-
Andika mawazo yako kuhusu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa njia gani uzoefu wa Lehi katika 1 Nefi 1:5–15unaweza kuvutia mapenzi yake ya kufundisha watu na kuwaalika kutubu?
Baada ya kuonywa dhidi ya maangamizo ya Yerusalemu, Lehi alishiriki pamoja na watu wa Yerusalemu kile alichojifunza. Aliwaonya kwamba wangeamizwa ikiwa hawatatubu. Soma 1 Nefi 1:18–20, na utambue jinsi watu wa Yerusalemu walifanya. Fikiria kuwa wewe ni mwandishi wa gazeti na ilikubidi kuandika kichwa cha habari kuhusu 1 Nefi 1:18–20. Kichwa chako kingekuwa nini?
Tafakari kauli ifuatayo:
“Kama vile manabii wa zamani, manabii leo wanashuhudia kuhusu Yesu Kristo na kufundisha Injili yake. Wanafunua mapenzi ya Mungu na maisha Yake. Wanaongea kwa ujasiri na wazi, wakishtumu dhambi na kuonya kuhusu matokeo yake. Wakati mwingine wanaweza kuongozwa kutoa unabii kuhusu matukio ya siku zijazo kwa manufaa yetu” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 129).
-
Katika maneno yako mwenyewe, andika sentensi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukieleza jukumu la nabii bila kujali upinzani anaoweza kupitia.
Nefi alivyoandika kuhusu uzoefu wa baba yake katika Yerusalemu, aliongezea ujumbe kwa msomaji kwa sehemu kupitia 1 Nefi 1:20, kuanzia kwa maneno “Lakini tazama, mimi, Nefi, nitawaonyesha nyinyi …”Kifungu hiki kinaleta mada ambayo Nefi alisisitiza kote katika maandishi yake. Piga mstari chini ya mada hii katika 1 Nefi 1:20, kisha usome Moroni 10:3 ukitafuta mada inayofanana. (Moroni alikuwa nabii wa mwisho wa manabii wa Kitabu cha Mormoni. Kipindi kati ya Nefi na Moroni kilikuwa karibu miaka 1000)
Tambua kwamba Nefi alitangaza katika mlango wa kwanza wa Kitabu cha Mormoni kwamba atatuonyesha “huruma nyororo ya Bwana” katika maandishi yake (1 Nefi 1:20). Katika mlango wa mwisho wa Kitabu cha Mormoni, Moroni alituambia tukumbuke “jinsi vile Bwana amekuwa na huruma” (Moroni 10:3).
Nefi alitaka tuelewe tokea mwanzo wa maandishi yake kwamba huruma nyororo ya Bwana hutolewa kwa wale wanaofanya imani katika Yeye. Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili alielezea maana ya huruma nyororo ya Bwana katika maisha yetu. Weka mviringo kwa maneno na vishazi ambavyo Mzee Bednar alitumia kueleza maana ya “huruma nyororo ya Bwana” unaposoma maelezo yake.
“Huruma nyororo za Bwana ni baraka za kibinafsi kabisa na za kipekee, nguvu, ulinzi, hakikisho, maongozi, ukarimu wa upendo, faraja, uhimili, na vipawa vya kiroho ambavyo sisi hupokea kutokana na kwa sababu ya na kupitia Bwana Yesu Kristo. …
“… Huruma nyororo za Bwana hazitokei hivi hivi au kwa sababu ya bahati. Uaminifu, utii, na unyenyekevu huleta huruma nyororo katika maisha yetu, na kila mara huwa ni wakati wa Bwana ndio hutusaidia sisi kuvitambua na kuthamini baraka hizi muhimu” (“The Tender Mercies of the Lord,” Ensign or Liahona, May 2005, 99–100).
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo: Ni mifano gani ya huruma nyororo ya Bwana ambayo umeona ikiletwa kwako au mtu mwingine unayemjua?
Anza au endelea kutafuta na kuandika katika shajara yako ya binafsi huruma nyororo ambazo Bwana ameleta kwako. Unapofanya hivi, utaona kwa haraka baraka ambazo Mungu ameleta kwako.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 1 Nefi 1na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: