Kitengo cha 18: Siku ya 4
Alma 32
Utangulizi
Baada ya kushuhudia mtindo wa ibada ya uasi ya Wazoramu, Alma na wenzake walihubiri neno la Mungu kwao. Walianza kuona baadhi ya mafanikio miongoni mwa watu waliokuwa maskini na kutupwa nje ya masinagogi ya Wazoramu. Kutumia mfano wa upandaji na ulishaji wa mbegu, Alma aliwafundisha yale wanapaswa kufanya ili kupokea na kuboresha imani katika neno la Mungu. Alma aliwaalika wao (na sisi) ili kufanya majaribio juu ya neno na kuboresha imani na ushuhuda wao kila siku.
Alma 32:1–16
Alma anafundisha Wazoramu ambao walinyenyekezwa kwa sababu ya umaskini wao.
-
Fikiria kwamba rafiki alikuuliza jinsi mtu anaweza kujua kama Kanisa ni la kweli. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika majibu yako kuhusu jinsi ya kupata ushahidi. Kisha andika Jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda juu ya mstari unaofuata wa shajara yako. Unapojifunza Alma 32, tengeneza orodha chini ya kichwa hiki cha umaizi unaogundua kuhusu jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda. Utaendelea kuongezea kwenye orodha hii kote katika somo, kwa hivyo, itakuwa na manufaa kuacha nafasi nyingine ya ziada kati ya kazi ya kwanza ya shajara hii ya kujifunza na zoezi 2.
Katika somo lililopita (Alma 31), ulisoma kuhusu jinsi Alma na ndugu zake waliona ibada ya uongo ya Wazoramu, kundi la Wanefi waliopotoka mbali na ukweli. Kufuatia maombi ya Alma ya imani, yeye na ndugu zake walianza kuhubiri injili miongoni mwa watu hawa. Soma Alma 32:1–3, na uangalie ni kundi gani la Wazoramu lilionyesha nia katika ujumbe wa wamisionari.
Soma Alma 32:4–6, na utambue jinsi madhara ya umaskini wao ulikuwa baraka.
Moja ya kanuni iliyonyeshwa katika aya hizi ni: Unyenyekevu hutuandaa kupokea neno la Mungu. Andika kuwa mnyenyekevu katika shajara yako ya kujifunza maandiko chini ya kichwa “Jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda.”
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri unyenyekevu ni muhimu kwa kupokea na kuimarisha ushuhuda.
Soma Alma 32:13–16, ukitafuta njia mbalimbali ambazo kwazo watu wanaweza kuwa wanyenyekevu. Kutokana na kile Alma alifundisha, je, ungechagua badala yake kuwa mnyenyekevu au kulazimishwa kuwa mnyenyekevu? Kwa nini?
Fikiria kile unafikiri inamaanisha kujinyenyekeza “kwa sababu ya neno” (Alma 32:14). Ni kwa jinsi gani inaweza kuathiri mtazamo wako juu ya shughuli za Kanisa, seminari, au jioni ya familia nyumbani?
Chagua kuwa mnyenyekevu kwa kutenda juu ya vishawishi vyovyote ulivyopokea kuhusu unyenyekevu wako mwenyewe.
Alma 32:17–43
Alma anawafundisha Wazoramu jinsi ya kuongeza imani yao.
Wakati akiwafundisha Wazoramu, Alma alitambua wazo moja la uongo watu wengi walikuwa nalo kuhusu kupata ushuhuda. Soma Alma 32:17–18, na utambue wazo hili la uongo.
Fikiria kwa muda jinsi kutarajia ishara kunaweza kuwa kikwazo kwa ajili ya kujenga imani na ushuhuda. (Unaweza kuandika M&M 63:9–11 katika pambizo la maandiko yako karibu na Alma 32:17–18 na uisome kwa ufahamu zaidi.)
Soma Alma 32:21, kifungu cha umahiri wa maandiko, na uangalie ufafanuzi wa Alma wa maana ya imani na kisichokuwa maana ya imani. (Unaweza kutaka kukiweka alama katika njia tofauti ili uweze kukipata katika siku zijazo.)
Soma Alma 32:22. Tafakari kile unaweza kufanya ili kukuza imani kubwa na ushuhuda wa kibinafsi.
Ongeza kumbuka rehema ya Mungu na chagua kuamini katika orodha ya shajara yako ya kujifunza maandiko ya “Jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda.”
Alma alifundisha Wazoramu jinsi wangeweza kuanza kuamini katika neno la Mungu kwa kujaribu majaribio. Fikiria juu ya baadhi ya majaribio uliyofanya katika madarasa ya sayansi au madarasa mengine na hatua uliyofuata. Kumbuka kwamba majaribio yanahitaji matendo kutoka kwa upande wa mtafiti. Aidha, mchakato wa kupokea au kuimarisha ushuhuda unahitaji matendo kutoka kwa upande wako. Soma Alma 32:27, na uangalie majaribio ambayo Alma aliwaalika Wazoramu kujaribu.
Inaweza kusaidia kujua kuwa neno akili ina maana mamlaka au uwezo tuliobarikiwa nao wa kujua na kuelewa ulimwengu ulio karibu nasi. Inajumuisha vitu kama vile hisia zetu za kusikia, kuona, na kugusa,; mawazo mantiki, na kumbukumbu.
Ongeza majaribio (au tenda) juu ya neno katika orodha ya shajara yako ya kujifunza maandiko la “Jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda.”
Unaposoma Alma 32:28, Unaweza kutaka kuweka alama vishazi katika maandiko yako kama vile “itaanza kuvimba,” “kukua ndani ya nafsi yangu,” “kuangaza kuelewa kwangu,” na “kunipendeza mimi.” Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha jinsi imani yetu hukua:
“Tunakua katika imani; tunakwenda hatua kwa hatua kutoka kiwango cha chini hadi kiwango cha juu. Tunaongeza neema kwa neema mpaka hatimaye tunafikia hali ambapo tumeboresha imani yetu, kufikia angalau ujumla wa haki, watu wa dunia wanaweza, na basi tunafikia mahali pa kuendelea hadi katika ukuaji wa milele. …
“Fanyia kazi miradi iliyo mbele na wakati umechukua hatua moja katika kupata imani, itakupatia uhakika katika nafsi yako kwamba unaweza kusonga mbele na kuchukua hatua inayofuata, na kwa viwango vya uwezo wako au ushawishi utaongezeka” (Lord, Increase Our Faith, Brigham Young University Speeches of the Year [Oct. 31, 1967], 9, 11).
-
Baada ya kusoma Alma 32:28, kamilisha mbili au zaidi ya kazi zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ni hatua gani ambazo ni lazima tuchukue ama tusichukue tunapofanya jaribio hili juu ya neno? (Orodha ya baadhi ya majibu imejumuishwa mwishoni mwa somo.)
-
Unafikiri inamaanisha nini “kutoa nafasi, ili [neno la Mungu] lipandwe ndani ya moyo wako”?
-
Ni lini uliwahi kuhisi neno la Mungu likivimbisha nafsi yako na kuangaza uelewa wako? Elezea kwa maneno yako mwenyewe jinsi ulivyohisi.
-
SomaAlma 32:29–34, na uweke alama kwenye maneno au vishazi vinavyoelezea kile mtu binafsi atajifunza kuhusu neno la Mungu wakati anapofanya majaribio. Neno kulisha lina maana ya kulisha, kudumisha, au kutunza.
Hebu fikiri kwa dakika jinsi mchakato wa kusaidia mti kukua ni sawa na ile ya kusaidia ushuhuda wako kukua. Pia fikiria ni kwa nini imani ya mtu na ushuhuda si kamili baada ya kufanya majaribio na neno la Mungu. Ni nini zaidi unafikiri inahitajika kufanywa ili kuwa na ushuhuda wa kudumu wa injili?
Soma Alma 32:35–40, ukiangalia kwa uangalifu kile ambacho Alma alisema ni lazima tufanye ili kukamilisha majaribio. Tafakari kile unachopaswa kufanya ili mti, au ushuhuda wako, ukue. Ni nini kitatokea ukishindwa kufanya mambo haya?
Funga maandiko yako, na uone ni mangapi ya maswali yafuatayo unaweza kujibu:
-
Tunapaswa kufanya nini ili imani yetu katika neno la Mungu ikue kuwa mti wa kuzaa matunda?
-
Unafikiri tunda linawakilisha nini?
-
Nini kinatokea wakati tunapotelekeza mti au kushindwa kuulisha?
-
Unafikiri ni vipi hiyo ni kama kile kinachotokea wakati tunapotelekeza au kushindwa kuulisha ushuhuda?
Kama ni muhimu, fungua maandiko yako na uchambueAlma 32:35–40 ili kukusaidia kujibu maswali. Ongeza kulisha kwa bidii katika orodha yako ya kujifunza maandiko ya “Jinsi ya kupokea na kuimarisha ushuhuda.”
Fanya muhtasari katika sentensi moja kile ulichojifunza kutoka Alma 32 kuhusu kile kinachotakiwa ili kupokea au kuimarisha ushuhuda, na uandike kanuni hii katika maandiko yako karibu naAlma 32:37–43.
Unaweza kuwa umeandika kitu kama: Tukilisha imani yetu kwa bidii katika neno la Mungu katika mioyo yetu, imani yetu na ushuhuda wetu wa Yesu Kristo na injili Yake utakua
Soma Alma 32:41–43, ukiangalia jinsi Alma alivyoelezea matokeo ambayo huja kwa wale ambao wanalisha shuhuda zao kwa uaminifu. Alma 32:42 inataja bidii na subira. Kwa nini unadhani inahitaji bidii na subira kwa mti —au ushuhuda wako —kukua?
Umahiri wa Maandiko—Alma 32:21
-
Soma Alma 32:21 tena. Jaribu kukariri aya hii, na kisha uisome kutoka kumbukumbu kwa rafiki au mwanafamilia. Andika sentensi chache katika shajara yako ya kujifunza ukielezea kile aya hii inafundisha kuhusu imani.
Majibu yanayowezekana kwa zoezi 3a: (a) toa nafasi kwa ajili ya neno (au mbegu) ili kupandwa katika moyo wako, (b) usitupe nje mbegu ya kutokuamini kwako, na (c) tambua ukuaji wa mbegu.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Alma 32na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: