Seminari
Kitengo cha 32: Siku ya 3, Moroni 10:1–7, 27–29


Kitengo cha 32: Siku ya 3

Moroni 10:1–7, 27–29

Utangulizi

Moroni aliwahimiza Walamani, na wengine wote ambao wangesoma ushuhuda wake, kujifunza kwa ajili yao wenyewe ukweli wa maneno yake kwa kumwuliza Mungu. Alifundisha kwamba ushahidi wa Kitabu cha Mormoni na wa Yesu Kristo ungekuja kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Moroni alitangaza kwa ujasiri kwamba angekutana na wasomaji wake mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, ambapo Mungu angethibitisha ukweli wa maneno yake.

Moroni 10:1–7

Moroni atuhimiza tupate ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni na wa Yesu Kristo

Reje masomo ya utangulizi wa Kitabu cha Mormoni katika kitengo cha 1 cha mwongozo huu. Je, unakumbuka lengo la jiwe la katikati katika tao na jinsi jiwe kuu la msingi linahusiana na Kitabu cha Mormoni? Rejelea utangulizi wa Kitabu cha Mormoni (unaopatikana katika mwanzo wa kitabu ), na usome kauli kutoka kwa Nabii Joseph Smith katika aya ya sita.

Picha
tao na jiwe la katikati

Nabii Joseph Smith alikieleza Kitabu cha Mormoni kama “jiwe la katikati ” la dini yetu, maana ya kwamba ushuhuda wetu wa Kitabu cha Mormoni unabeba na kuimarisha ushuhuda wetu wa kweli zote za injili ya urejesho. Soma aya ya mwisho ya utangulizi kwa Kitabu cha Mormoni, na utafute kweli mtu anaweza kujua kwa kupata ushahuda wa Kitabu cha Mormoni. Kama vile tu jiwe la katikati linashikilia tao pamoja, ni jinsi gani ushuhuda wako umeshikiliwa pamoja na kuimarishwa na Kitabu cha Mormoni?

Takribani miaka 1,400 kabla ya Joseph Smith kupokea mabamba ya dhahabu, Moroni alihitimisha kumbukumbu ya baba yake kwa kuandika ushauri wake wa mwisho kwa wale ambao watapokea Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho (ona Moroni 10:1–2). Neno ushauri linamaanisha kumhamasisha mtu kwa nguvu. Moroni alitumia neno hili mara nane katika sura ya mwisho ya Kitabu cha Mormoni. Aliwahimiza wote watakaopokea Kitabu cha Mormoni kutafuta ushuhuda wa ukweli wake na utukufu.

Soma Moroni 10:3–4, na utambue vitu Moroni alisema tunapaswa tufanye ili kupata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni. Huenda ukataka kualamisha vitu hivi katika maandiko yako. Soma taarifa zifuatazo kuhusu kila kitu Moroni alisema tunapaswa kufanya:

“Soma vitu hivi”

Hatua ya kwanza katika kupata ushahidi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli ni kikusoma. Mzee Tad R. Callister wa Urais wa Sabini alishiriki jinsi msichana mmoja alinufaika kutokana na kusoma Kitabu cha Mormoni chote:

“Msichana wa umri wa miaka 14 alisema kwamba alikuwa akijadili dini na mmoja wa marafiki zake shuleni. Rafiki yake alimwambia, ‘Je, wewe ni wa dini gani ?’

“Alijibu, ‘Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, ama Wamormoni.’

Rafikiye alijibu, ‘Ninajua kanisa hilo, na ninajua si la kweli.’

“Je, unajuaje?’ jibu likaja.

“ Kwa sababu.’ Alisema rafikiye, ‘Nime fanya utafiti juu yake.’

“Je, umesoma Kitabu cha Mormoni?’

“Hapana, jibu likaja. ‘Sijakisoma.’

Kisha msichana huyu mwema akajibu, ‘Basi haujafanya utafiti juu ya kanisa langu, kwa sababu nimesoma kila kurasa ya Kitabu cha Mormoni na ninajua ni cha kweli’” (“The Book of Mormon—a Book from God,” Ensign ama Liahona, Nov. 2011, 76).

Kwa nini unafikiria kusoma Kitabu cha Mormoni ni muhimu ili kupata ushuhuda wa ukweli wake?

“Kumbuka jinsi vile Bwana amekuwa na huruma”

Hatua ya pili katika mchakato ni “Kukumbuka jinsi vile Bwana amekuwa na huruma.” Kukumbuka huruma za Bwana katika maisha yetu kunaweza kulainishe mioyo yetu na kututayarisha kupokea Roho Mtakatifu. Tafakari wakati ambapo umehisi huruma yake Bwana katika maisha yako.

Katika mwanzo wa Kitabu cha Mormoni, Nefi alitangaza kwamba kupitia maandiko yake angetuonyesha mifano ya huruma nyororo za Bwana (ona 1 Nefi 1:20). Mwishoni mwa Kitabu cha Mormoni, Moroni ametuomba tukumbuke huruma za Bwana kwetu (ona Moroni 10:3). Huenda ukataka kuandika marejeo-mtambuko 1 Nefi 1:20 kando ya Moroni 10:3.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Ni ushuhuda gani wa huruma ya Bwana umeona katika maisha yako?

    2. Unadhani kukumbuka huruma za Bwana kunasaidia vipi mtu kupokea ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni?

Kukumbuka huruma za Bwana kwa wengine na kwetu sisi wenyewe kunaweza kututayarisha kutafakari ujumbe wa Kitabu cha Mormoni kwa ajili yetu.

“Kuitafakari katika mioyo yenu”

Hatua inayofuata Moroni alifundisha ni “kuitafakari katika mioyo yenu Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza jinsi kutafakari kunaweza kutusaidia kupokea Roho Mtakatifu maishani mwetu:

Picha
Mzee Marvin J. Ashton

Ninaposoma maandiko, mimi hutiwa moyo na kuvutiwa na neno kutafakari linalotumika mara kwa mara katika Kitabu cha Mormoni. Kamusi husema kwamba kutafakarikunamaanisha kupima kwa fikira, kufikiria kwa kina kuhusu, kujadili, kuwaza. Moroni alitumia neno hili alipofunga kumbukumbu yake [ona Moroni 10:3].

Kwa kutafakari, tunampa Roho nafasi kutia msukumo na kuongoza. Kutafakari ni kiungo kilicho na nguvu kati ya moyo na akili. Tunaposoma maandiko, mioyo yetu na akili huguswa. Tukitumia karama ya kutafakari, tunaweza kuchukua kweli za milele na kutambua jinsi tunaweza kuzitumia katika matendo yetu ya kila siku. 

Kutafakari ni harakati ya kuendelea ya akili. Ni karama kuu kwa wale ambao wamejifunza kuitumia. Tunapata kuelewa, ufahamu, na matumizi ya vitendo tukitumia karama ya kutafakari (There Are Many Gifts, Ensign, Nov. 1987, 20).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu moja la maswali yafuatayo ama yote mawili:

    1. Kutafakari ukijifunza Kitabu cha Mormoni kumekusaidia vipi kuhisi Roho Mtakatifu?

    2. Ungeweza kufanya nini ili kutafakari kila mara na kwa ufanisi unapojifunza maandiko?

Picha
kijana akisoma

“Uliza kwa moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo”

Watu wanapoomba “na moyo wa kweli na kusudi halisi,” inamaanisha kwamba wanakusudia “kutendea jibu wanalopata kutoka kwa Mungu” ( Hubiri Injili Yangu [2004], 111).

Mtu mmoja aliyeitwa Rodolfo Armando Pérez Bonilla alijifunza umuhimu wa kuomba na kusudi halisi. Alibatizwa katika umri wa miaka tisa lakini familia yake haikushiriki kikamilifu Kanisani. Alipokuwa kijana, alianza kufikiria kuhusu Injili na alikuwa na tukio lifuatalo:

“Mara kwa mara niliomba ili kujua kile kilichokuwa sahihi, lakini ilikuwa zaidi wazo la juu juu kushinda swali la moyoni la kweli. Kisha usiku mmoja niliamua kuomba na kusudi halisi.

“Nilimwambia Baba wa Mbinguni kwamba nilitaka kumjua Yeye na kwa muumini wa Kanisa Lake la kweli. Niliahidi: ‘Kama Wewe utaniacha nijue kama Joseph Smith ni nabii wa kweli na kama Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, nitafanya chochote Wewe ungetaka nifanye. Kama Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ndilo Kanisa la Kweli, nitalifuata na kamwe sitawahi kuliacha.

“Sikuwa na udhihirisho wowote wa maajabu, lakini nilihisi amani na kwenda kulala. Masaa kadhaa baadaye niliamka na wazo la kina: ‘Joseph Smith ni nabii wa kweli, na Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.’ Wazo hilo liliambatana na amani ya ajabu sana. Nililala tena, tu kuamuka baadaye na wazo lile lile na hisia

“Tangu wakati huo, sijawahi kuwa na shaka kwamba Joseph Smith ni nabii wa kweli. Ninajua kwamba hii ni kazi ya Mwokozi na kwamba Baba wa Mbinguni atajibu maombi yetu ya kweli ” (“How I Know,” Ensign, Oct. 2011, 64).

  1. Fikiria jinsi gani unataka kuwa na ushuhuda wa nguvu wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko baadhi ya vitu tayari umefanya ili kupata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni. Kisha andika nini ungeweza kufanya ili kupata ushahuda wa nguvu zaidi wa Kitabu cha Mormoni.

Picha
msichana akiomba

Soma Moroni 10:4, na utambue kile Moroni alishuhudia Mungu angewafanyia wale ambao wanafuata mchakato huu wa kusoma, kukumbuka, kutafakari, na kuuliza. Huenda ukataka kualamisha ahadi hii katika maandiko yako. (Moroni 10:4–5 ni kifungu cha umahiri wa maandiko.)

Soma Moroni 10:5–7, na utafute ni nini kingine Moroni aliahidi tunaweza kujua kupitia Roho Mtakatifu.

Kanuni moja tunaweza kujifunza kutoka kwa Moroni 10:3–7 ni: Tukitafuta kwa imani, tunaweza kupokea ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni na wa Yesu Kristo kupitia Roho Mtakatifu.Huenda ukataka kuandika haya katika maandiko yako kando ya mistari hii.

  1. Fanya yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Andika jinsi kusoma, kukumbuka, kutafakari, na kuomba mwaka huu kumeimarisha ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni na kweli kinafundisha ama kimekusaidia kupata ushahuda wake.

    2. Fikiria kuhusu wakati umehisi Roho Mtakatifu akikushuhudia juu ya ukweli wa Kitabu cha Mormoni ama ukweli mwingine wa injili. Ni muhimu kukumbuka kwamba ufunuo mwingi huwa hauji katika njia ya ajabu. Watu wengi watasikia uvutio tulivu na mgumu kutambua kutoka kwa Roho Mtakatifu, kama vile hisia ya joto, hisia ya amani ama uhakika wa kweli. Roho anaweza pia kushuhudia kweli za injili mstari juu ya mstari, akitusaidia kujifunza kweli hatua kwa hatua baada ya muda. Andika kuhusu wakati umehisi ushahidi wa kuthibitisha wa Roho Mtakatifu.

Moroni 10:27–29

Moroni alishuhudia kwamba angekutana nasi kwenye baraza la hukumu la Mungu.

Soma Moroni 10:27–29, na uzingatie jinsi mistari hii inatufunza kanuni ifuatayo: Wale ambao wamepokea Kitabu cha Mormoni watawajibika kwake Mungu kwa jinsi walivyokichukulia. Fikiria kwamba una nafasi ya kukutana na Moroni katika baraza la hukumu la Mungu. Tafakari kile ungemwambia kuhusu Kitabu cha Mormoni na jinsi kimeathiri maisha yako.

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko —Moroni 10:4–5

Kukariri Moroni 10:4–5 kunaweza kuwa na manufaa makubwa kwako katika kushiriki ujumbe wa Kitabu cha Mormoni na wengine. Zingatia kuchukua muda sasa kuikariri neno kwa neno. Njia moja ya kufanya hivi ni kusoma kifungu hicho kwa sauti kubwa mara kadhaa. Kisha ukiandike neno kwa neno mara tatu kwenye kipande cha karatasi ama katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Ukisha maliza, ona kama unaweza kukariri mistari hii kutoka akilini.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Moroni 10:1–7, 27–29 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha